Na Ripota Wetu, Misenyi

MBUNGE wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera Balozi ,Dk. Kamala amempongeza kijana Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.

Kijana Omary wakati Rais Dk.John Magufuli akiwa kwenye ziara katika mkoa huo Novemba mwaka jana alitoa kilio chake kwa Rais kuwa kuna moja ya maofisa mifugo alifika kwenye shamba lake na kufyeka mazao yake.

Hata hivyo kijana huyo bado anaendelea na kilimo hicho baada ya Rais kutaka asisumbuliwe bali aachwe.

Hivyo Dk.Kamala ameamua kwenda kwenye shamba la kijana Omary kuona shughuli anazofanya, ambapo ametumia nafasi hiyo kumpongeza kwa jitihada zake kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda.

Dk.Kamala ameona haja ya kutembelea shamba hilo na alipofika akavutiwa na ubunifu wa kijana huyo na hivyo ameshauri ni vema vijana wakaanzisha kikundi ambacho kitajikita kwenye aina hiyo ya kilimo.Amesema yeye ameahidi kutoa vitendea kazi ikiwamo mashine za umwagiliaji.
 Sehemu ya shamba la Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera Balozi ,Dkt. Kamala akikagua shamba la kijana Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge mkoani Kagera Balozi ,Dkt. Kamala akiungumza jambo na kijana Rosh Omary ambaye ameamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na matunda kando ya mto Nkenge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...