Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

NAIBU Waziri wa Viwanda, Uwekezaji na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema uwepo wa viwanda nchini utachangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa bidhaa za kilimo kwa kuwahakikishia wakulima wanakuwa na soko la uhakika.

Mhandisi Manyanya ameyasema hayo leo jijijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza viwanda nchini lililoandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA).

Amesema ili kufikia malengo hayo kunahitajika ushirikiano mkubwa kati ya sekta binafsi na Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara."Tasisi za fedha mnatakiwa kuhakikisha mnatatua changamoto za wajasiriamali za ukosaji wa mitaji jambo ambalo limekuwa likiwasumbua wengi wao, ili kuhakikisha tunafikia Tanzania ya viwanda" amesema.

Mhandisi Manyama, amesisitiza ikiwa taasisi za fedha zitasaidia kukuza uchumi kupitia viwanda maana yake itakuwa chachu ya kukuza kipato cha wawekezaji na kuongeza mnyororo wa thamani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhandisi Stela Manyanya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) kuhusu wajibu wa taasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Nchini na Mwenyekiti wa jumuiya ya Mabenki , Charles Kimei akichokoza mada wakati wa Kongamano kuhusu wajibu wa Tasisi za fedha katika kuendeleza Viwanda Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tasisi ya Sekta Binafsi Nchini(TPSF),Geoffrey Simbeye, akichokoza mada wakati wa kongamano la kujadili umuhimu wa mabenki na sekta binafsi katika maenedeleo ya Viwanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...