Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Kagera Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Azam FC na kufikisha 34 sawa na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi.
Kagera Sugar yenyewe inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi 18 na sasa inajinasua mkiani ikirudi nafasi ya 15 kwa wastani wa mabao tu baada ya kulingana kwa pointi na Njombe Mji FC. 
Katika mchezo wa leo, Kagera Sugar walitangulia kwa bao la beki Eladslaus Mfulebe dakika ya 50, kabla ya Iddi Kipagwile kuisawazishia Azam FC dakika ya 53.


Kikosi cha Kagera Sugar kilikuwa: Ramadhani Mohammed, Mwaita Gereza, Eladslaus Mfulebe, Juma Shemvuni, Mohammed Faki, George Kavila/Peter Mwalyanzi dk57, Suleiman Mangoma, Ally Nasoro ‘Ufudu’, Japhary Kibaya/Edward Christopher dk79, Ally Ramadhani na Venance Ludovic/Atupele Green dk69.
Kikosi cha Azam FC: Kipa Razack Abalora, Saleh Abdallah/Iddi Kipagwile dk46, Bruce Kangwa, David Mwantika, Yakub Mohammed, Abdallah Kheri, Stephan Kingue/Paul Peter dk74, Frank Domayo, Salmin Hoza, Mbaraka Yussuph/Ennok Atta Agyei dk46 na Shaaban Idd.

Shangwe kwa Kagera Sugar, wameumaliza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Timu ya jijini Dar es salaam Azam Fc.
Kikosi cha Timu ya Azam Fc kilichoanza leo dhidi ya Kagera Sugar.


Mshambuliaji wa Azam Fc Mbaraka Yusuph akigombea mpira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...