Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KIONGOZI Chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Kabwe ameendelea kusota mahabusu baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro.

Zitto anashikiliwa kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko isivyo halali baada ya ziara ya Chama cha ACT -Wazalendo kutembelea madiwani wao katika kata mbalimbali katika mikoa 8 nchini kuwa ni kosa kisheria.

Akizungumza leo asubuhi, Wakili wa Zitto,Emmanuel Mvula amesema hadi sasa Zitto bado anashikiliwa na haijafahamika kama ataachiwa,atapa dhamana au atapelekwa mahakamani.

Mvula amesema Zitto alifikishwa Polisi jana usiku na baada ya kuandika maelezo hakuachiwa,hivyo amelala Kituo cha Polisi.

"Tunasubiri tuone nini konafuata baada ya kuendelea kumshikilia ndugu yetu Zitto.Hivyo kitachoendelea tutaufahamisha umma," amesema Wakili Mvula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...