Baraza la Mawaziri jipya. Toka shot mbele Dr Asha Rose Migiro (mambo ya nje), Margareth Sitta (elimu) Mizengo pinda (tawala za mikoa), Kingunge ngombale mwiru (ofisi ys rais- siasa na mahusiano na jamii), John Chiligati (mambo ya ndani, Dr Juma Ngasongwa (mipango), Prof,. Juma Kapuya (ulinzi), Mramba (miuondombinu), Bakari Mwapachu (usalama wa raia), zakhia meghji (fedha), mary nagu (sheria), Joh magufuli (ardhi), Jumanne Maghembe (kazi), na Prof. David Mwakyusa (afya). Nyuma toka shoto Dr Hussein Ali Hassan Mwinyi (masuala ya muungano), stephen wassira "Tyson" (Maji) prof mwandosya (mazingira), andrew chenge (afrika mashariki), Seif Khatib (habari,k utamaduni na michezo) Dr Ibrahim Msabaha (nishati na madini), joseph mungai (kilimo), Anthony diallo (utalii), juma akukweti (masuala ya bunge), Philip marmo (utawala bora), sofia simba (wanawake na watoto), peter msola (elimu ya juu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Vipi hamna picha ambayo wamepiga Mhe. JMK? Michuzi kweli mambo yako siyawezi we get the update by the minute

    ReplyDelete
  2. Mavazi ya mawaziri wetu yanasema mengi kuhusu fikra zao, athari za elimu (maana sio unaona kuna madokta na maprofesa?), athari za msukumo wa utamaduni-maarufu wa magharibi na mustakabali wa utamaduni utaifa wetu.

    Hata waziri wa utamaduni naye pia?? Lakini sijui nashangaa nini wakati jina lake (Seif Khatib) linaonyesha amevaa begani mwake utamaduni wa akina nani.

    ReplyDelete
  3. Nesanjo Macha,
    Wewe katika majina yote kwanini umeamua kutaja jina la Seif Khatib??????

    Hii picha ya mzee Kingunge na wajukuu zake imetoka poa.

    ReplyDelete
  4. Mawaziri hawana mpangilio katika kupiga picha, sijui hiyo ni taswira ya jinsi watakavyofanya kazi?

    Hamna umoja wa kuangalia kamera, kila mmoja annangalia kwake kama wamekurupushwa vile.Michuzi vipi bwana,au wazee walikuwa too daunting kuwaambia "Haya sasa sema cheese"!

    ReplyDelete
  5. michuzi mbona hujamtaja mheshimiwa waziri Hawa Ghasia yule pale nyuma amefunga hijabu?

    ReplyDelete
  6. Nimemtaja Seif Khatib maana yeye ni waziri wa utamaduni. Ni waziri wa historia yetu, utaifa wetu, dini zetu, mila zetu, majina yetu, jadi zetu, desturi zetu, n.k. Sasa kama waziri wa mambo hayo ameshindwa kabisa kupata jina katika utamaduni anaotakiwa kuulinda na kuundeleza kupitia wizara yake, kiasi cha kusafiri hadi Uarabuni kuazima jina...maana yake nini? Ndio maana nikamtaja yeye maana yeye alipaswa kuwa mfano wa huo utamaduni anaotakiwa kuulinda na kuuendeleza.

    Tabia hii ni sawa na ile ya waziri wa elimu kutopeleka watoto wake katika shule za serikali ambazo ziko chini ya wizara yake. Hii inaashiria nini? Anaongoza elimu ambayo hataki watoto wake "waifaidi"??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...