huyu ndiye halima shariff ambaye sasa ni kamishna
kwenye kamisheni ya ukimwi (TACAIDS) akitoa mada kwenye semina ya ukimwi dodoma juzi. yeye, rose kalemela ambaye ni mkurugenzi wa swissaid, khadija riyami anayetangaza voa, ichikaeli maro aliyeko benki ya dunia, dar, ni kinadada waandishi waandamizi wakali wa bongo ambao niliwakuta daily news nilipojiunga na gazeti hilo januari 1, 1990.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Michuzi kajina kako tumekaona-ona kwenye magazeti tokea tunapata-ga vijiakili miaka ya themanini na kadhaa. Vipi, kama hujali, ulikuwa-ga kagazeti gani kabla ya Daily Noise?

    ReplyDelete
  2. Namkumbuka mentor wangu Halima Shariff. Nishafanya chini ya supervision yake pale Tanzania AIDS Project (TAP) miaka ile ya early 1990s.

    ReplyDelete
  3. "Sisi tuna masihara mabaya" huo ndiyo msemo aliyozoea kusema rafiki yangu mmoja pale anapokuwa ameishiwa na la kusema kufuatia uborongaji wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii unaofanyika mara kwa mara nchini Tanzania.

    Nimekuwa nikifuatilia sana jinsi Tanzania inavyopambana na UKIMWI kwa kulinganisha na nchi zingine za Afrika kama Uganda na Afrika ya Kusini. Na kwa kulinganisha na nchi zingine nje ya Afrika kama Brazil na India.

    Katika ufuatiliaji wangu nimepata kupata fursa ya kujadili suala la UKIMWI na Watanzania mbali mbali wakiwemo mhadhiri mkuu mmoja wa Chuo Kikuu cha Tiba, Muhimbili. Pamoja na viongozi wa juu wa kisiasa wa Tanzania ambao nilikutana nao walipokuwa ziarani ughaibuni kujinoa kuhusu mfumo wa vyama vingi.

    Jibu ninalolipata kuhusu harakati za kitaifa za kupambana na UKIMWI ni kwamba harakati hizo hazijafikia kiwango kinachohitajika au kinachopaswa. UKIMWI umekuwa kama alivyotabiri muandishi Ibrahim Ngozi aliyeandika tamthiliya ya Ushuhuda wa Mifupa kwamba UKIMWI utakuwa ni kithibitisho cha methali ya 'Kufa Kufaana'

    Kwa kifupi tu, nawaombeni tuangalie tena jinsi serikali yetu inavyolichukulia suala la kupambana na UKIMWI aidha kwa kinga au tiba. Wahusika wakuu wa kiserikali wanaohusishwa na suala UKIMWI. Idara na serikali zinazohusika na suala la UKIMWI, ambapo serikali ya awamu ya nne imeliongezea suala la UKIMWI "nguvu mpya" ambapo Rais Kikwete alimtaja Naibu waziri Dk. Luka Siyame wa Ofisi ya Waziri Mkuu atashughulikia Maafa na kampeni dhidi ya Ukimwi. Na pia kumteua Profesa David Mwakyusa ambaye ana taaluma ya tiba, kuwa Waziri wa Afya. Huko TACAIDS napo natumaini patafanyiwa mabadiliko makubwa ili kuingiza wataalamu wenye kila uwezo wa kukabiliana na na suala la UKIMWI kuanzia kampeni za kitaifa hadi za kimataifa kama zilizofanywa na zinazofanywa na wenzetu wa Uganda, Afrika ya Kusini, Brazil, na India.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  4. Kuna mwingine sidhani kama jina lake nalikumbuka vyema,anaitwa Yasmin Aloo kama sikosei,yuko wapi siku hizi?

    ReplyDelete
  5. Michuzi, nilikukosea nini jamani! Si nilikukaribisha vizuri Daily News. Unakubumbuka ile pic ya ZNB iliyoleta mgogogoro?

    Asante kwa picha ya Dada Halima. Keep it up. I feel so at home.

    ReplyDelete
  6. That's my mother right there!!! I'm so proud of her!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...