haya ndo madhara watu kama jeff msangi wanayokumbana nayo mara baada ya kuruka ukuta kuingia neshno...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jeff acha hizo. Si ulipe tu kiingilio?

    ReplyDelete
  2. Maisha huwa yanaendana na maamuzi magumu.Hela ya kiingilio sina,soka liko kwenye damu na isitoshe wanangu wa Jangwani wapo dimbani.Nifanyeje??ahahah!

    ReplyDelete
  3. hahahaha michuzi! sasa kama kaka Jeff na hivi kidogo kalamba lamba chumvi hiyo mashine ikitua kwenye goti atapona kweli?

    mark

    ReplyDelete
  4. sio kosa la jamaa, kwanini wao wanatengeneza uwanja mbovu, ukuta unarukika, hii ndio ukandamizaji wa police wa bongo, anaweza hata kumvunja mbavu huyu mlala hoi ,hii inaitwa tocha. hakuna haki huko, noma,unyamaunyama tu, bora kubaki ughaibuni. jj

    ReplyDelete
  5. Michuzi sijui sasa Jeff ana mpango gani wa kuingia uwanjani mathalani baada ya kujengwa hilo jiwanja jipya la kimataifa. Sijui anapanga kuchimba handaki ili awe analitumia kupitia chini ili aingie uwanjani bila kulipa. Urukaji ukuta samahani hilo neno nilotumia sina maana ile ya kule Mombasa au Tanga bali kitendo cha kukwea na kuingia neshino strediumu bila kulipa kitaisha kama tuna viwanja vyenye viwango. Picha nzuri maana hapo kuna haja gani ya kutoa kipigo, kwa nini asikamatwe tu na kupelekwa kunako sheria? Polisi wa Bongo akili zao zilishawatuma kuwa kazi yao inaendana na kupiga. Jeff ni mwanasheria wakimvamia hana haja ya kusubiri tume, atawafunga hata kupitia mahakama za kimataifa.

    ReplyDelete
  6. Kweli nimekumbuka mbali sana. Mwenyewe nimetoroka Mbeya Secondary School, madaftari mfuko wa suruali (siku hiyo unakuja na madaftari mawaili au matatu kwani unajua Yanga wapo mjini), mfukoni una shilingi mia mbili (kiingilio mwanafunzi mia tano, ambayo huna) halafu unaruka ukuta. Polisi anaanza kuwaruhusu mmoja baada ya mwingine (bosi wake kamtuma afanye hivyo kisha baadaye wagawane). Nani yuko radhi awakose wanagu mwenyewe wa Jangwani siku wakija Mbeya?

    Enzi hizo walichukua Kombe la Afrika ya mashariki Nakivubo Stadium. Kilichoumua hamasa ni baada ya Uganda waliingia ligi daraja la kwanza kwa nguvu ya kushinda mechi kumi bila droo. Marehemu Abbas Gulamali aliwapa TV mojamoja.

    Golini alikuwa Stephen Nemes, ambaye aliumia fainali na nafasi yake kuchukuliwa na marehemu Rifat Said, Mrundi Ngado Ramadhani alikuwa namba mbili. Sentahafu alikuwa Mrundi mwingine Costantin Kimanda. Winga ya Kushota kama kawa Eddy Lunyamila. Wengine walikuwa marehemu Issa Athumani, Marehemu Method Mogella, wengine mbona wananitoka ....

    ReplyDelete
  7. Mimi hapo natoa tafsiri ya ugumu wa kimasiha zaidi.Huyu bwana hakupenda kwenda kudhalilika bali hali ngumu inawezekana ikawa inachangia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...