hapana, hawa si intarahamwe ama banyamulenge bali ni askari mgambo wa jiji la dar wakiwa kwenye doria. ni hodari sana hawa kuvamia wauza nyanya na mchicha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hii picha na ujumbe uliouambatanisha umenikumbusha hoja niliyoisoma katika kitabu Wretched of the Earth cha Hayati Franza Fanon. Hoja yenyewe ni kwamba umasikini ukisakini na kutamakani humpunguzia masikini uwezo wa kufikiri. Moja ya matokeo ya kupungua uwezo wa kufikiri ni kwamba masikini badala ya kupigana dhidi ya adui yake wa kweli ambaye ni mkandamizaji masikini huanza kugeukiana na kupigana wao kwa wao.

    Hii tabia ya kuwanyanyasa, kuwaonea, na kuwadhulumu wafanya biashara ndogo ndogo imejikita sana katika utamaduni wa Tanzania. Nakumbuka zamani pale Kisutu, kona ya mtaa wa Libya na mtaa wa Zanaki baraza zinazotazamana na Zanzibar Hotel palikuwa ndiyo uwanja wa fujo kati ya wanamgambo wa halmashauri ya jiji na wauza mboga na matunda. Mahali pengine ilikuwa ni soko Mjinga, Kisutu. Ninakumbuka kama ninatazama sinema jinsi malori ya halmashauri ya jiji yalivyokuwa yanawavamia wafanyabiashara na kuanza kusambaratisha bidhaa zao huku wakiwapiga virungu, magumi, mateke, na vichwa kama wana ugomvi nao.

    Waliokuwa na bahati mbaya walikuwa wanakamatwa na kutupwa nyuma ya malori ya site na kupelekwa sentro polisi kuandikiwa stetimenti na baadaye kupelekwa rumande Keko kusubiri mashitaka ya uzururaji. Walionusurika ni wale waliokuwa na mbio kumpita Filbert Bayi. Au waliokuwa na vijipesa vya kuhonga.

    Wengi wa wafanyabiashara hawa walikuwa ni walalahoi kwa hiyo pesa ya kumuhonga prosekyuta ili wapate bondi (dhamana) walikuwa hawana. Na hata ndugu zao wenyewe hawakuwa na pesa za kuwawekea bondi (dhamana). Nyingi ya kesi hizi zilikuwa zinachukua muda mrefu kusikilizwa na hatima yake waliokuwa wanaleta mlundikano katika mahabusu walikuwa ni "wazururaji" na siyo wavunja sheria kama wauaji na wafilisi wa mashirika na makampuni ya umma, viongozi wabadhilifu wa chama na serikali, majambazi, na wezi.

    Baada ya kuwakamata na kuwapeleka rumande askari wa site walikuwa wanagawana vidhibiti vya kesi na kuwapelekea wake zao vitoweo vya mchicha, kabechi, maharage, njegere, na kunde. Viungo vya nazi, nyanya, vitunguu, mabilinganya, karoti,pilipili hoho, mbuzi na kichaa. Na kuongeza vitamini kwa maembe dodo, machungwa, ndizi, mananasi, mapeasi, matunda damu, mabungo nk ya unyang'anyi!

    Haya yote yalikuwa yanafanyika na yanaendelea kufanyika kwa amri,ruhusa, na baraka za chama na serikali tawala.

    Kuna swali huwa napenda kumuuliza swahiba wangu Dennis Londo kwamba "..Ikitokea siku omba omba wakafanya mgomo wa kuomba watafanya nini?.." Dennis hunijibu kwamba "..Watanyang'anya.." Naomba niulize ikifika siku hawa wafanyabiashara ndogo ndogo wakagoma kukimbia itatokea nini?

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  2. Mkulu MtiMkubwa Tungaraza, Nimekupata. hapa nilipoiona hii picha wazo lililonijia kichwani ni kukushtua uiangalie tuijadili.
    Tuendelee kuombea, hawa vijana waendelee tu na jitihada zao za kujitafutia riziki zao kwa njia halali kama hii.
    Iwapo utatokea "Mgomo wa ombaomba" basi tutakuwa na hali ngumu mnoo.Sina hakika lakini kwa hali hii "Kadogoo" hayupo mbali.
    Mkulu si umeshasikia wale waliouawa hawakuwa majambazi? Unakumbuka tulipokuwa tuaongelea hili suala, kuwa wanaporushiana risasi mbona ni majambazi tu wanaouawa na sio polisi kujeruhiwa?
    Tuna safari ndefu.
    Dennis Londo

    ReplyDelete
  3. na walikuwa wana milioni 75 za mauzo ya madini si milioni tano kama ilivyoripotiwa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...