kwa furaha na masikitiko napenda kuwaaga wanablogu kwa picha hii ya waziri mkuu wa sasa edward lowassa na wa zamani cleopa david msuya ya hivi karibuni. nawaaga kwa sababu mapigo yote nahamishia kwenye www.mbongo.com ili kutii amri ya edita wangu wa mtandao huo wenye nia ya kuleta vitu vingi na vizuri zaidi kwa picha na maandishi. siku moja moja tutaonana...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

 1. kila la kheri Michuzi! tutakutana huko! napendekeza feyaweli pati ifanyike kibarazani kwa Ndesanjo!

  ReplyDelete
 2. Michuzi,

  Nakuomba usituache kwa sababu ya kuhamia mtaa mwingine. Blog yako imekuwa kiburudisho kikubwa sana kwa walio wengi.

  Nakuomba sana ufikirie tena uamuzi wako halafu usikilize mapendekezo ya mashabiki wengine.

  Halafu samahani hapa katikati sikuwa mchangiaji kwa sababu ya ratiba kubanwa sana na majukumu.

  Mshabiki wako,

  F MtiMkubwa Tungaraza.

  ReplyDelete
 3. Nakubaliana na Tungaraza,fikiria tena uamuzi wako.Kama sikosei kule mbongo.com lugha ni zile ngumu.Burudani ya picha zako tulishaizoea.

  ReplyDelete
 4. Nenda mwalimu, haya ni maamuzi yako. Ulikuja na sasa unajiondoa bila shaka umefanikiwa sana au huko kuna vijimalipo kiasi tofauti na hapa. Tunafanya uchunguzi na tukigundua kuwa unafuata maslahi kama wabunge tunakufuta kabisa katika wananchi wanaojali haki ya habari kwa umma.

  ReplyDelete
 5. Wewe umeona kule MBONGO hapatembelewi kwa hiyo unataka kutulazimisha tupatembelee kwa nguvu. Poa nimeshaongea na wapiga picha wengine wa serikali watajiunga as soon as possible.

  ReplyDelete
 6. Michuzi kama itawezekana hii safu iendelee kwani imekuwa ya kuelimisha mno kuliko hata magazeti yetu ya Tanzania.Je kuna namna ya kusaidia kuendeleza hii safu.

  ReplyDelete
 7. usimlilie huyu tuna jibu jipya na bado siku chache tunafunika hapa. Aende kwani yeye nani hadi atishe watu wazima waliomfundisha kufungua bilogi. Haya kazi kwenu wanablogu hai, sasa picha jhuko huko kwenu mtindo mmoja.

  ReplyDelete
 8. Ni vizuri kwa bwana Michuzi kukaa chini na kufikiria maana mtu kuwa na website yako na kuonesha kazi zako ni vizuri zaidi kwasababu baada ya miaka michache unaweza ukawa mbali zaidi, mfano wa google au wikipedia.com ni watu walio anzisha website ambazo sasa ni respect.

  Itakuwa mpaka lini mtu uwe unaajiliwa au kutengeneza partnership na watu wengine ambao wanachukua credit kwa talent uliyo nayo wewe? Sasa fikiria na uweze kuonesha kazi yako peke yako hasa hasa fikiria kuwa na website itakayo wafikia watanzania walio wengi kwa upande wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kama ikiwezekana tengeneza ya kwako itayokuwa na na space kubwa yaani sio kama blogs maana siku hizi web hosting ni bei rahisi sana na nyingi.

  Ungekuwa unajua jinsi gani hii forum inavyo fika mbali ktk ulimwengu huu na kiasi cha watu wanavyo ipenda usinge fikiria ata kwenda mbongo.com sasa rafiki fikiria eidha kuweka website hii online au mbongo au kesho na keshokutwa wengine wapate faida zaidi yako kutokana na kipaji chako. Kalaga bao - Kazi kwako.

  ReplyDelete
 9. Ni vizuri kwa bwana Michuzi kukaa chini na kufikiria maana mtu kuwa na website yako na kuonesha kazi zako ni vizuri zaidi kwasababu baada ya miaka michache unaweza ukawa mbali zaidi, mfano wa google au wikipedia.com ni watu walio anzisha website ambazo sasa ni respect. Itakuwa mpaka lini mtu uwe unaajiliwa au kutengeneza partnership na watu wengine ambao wanachukua credit kwa talent uliyo nayo wewe? Sasa fikiria na uweze kuonesha kazi yako peke yako hasa hasa fikiria kuwa na website itakayo wafikia watanzania walio wengi kwa upande wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kama ikiwezekana tengeneza ya kwako itayokuwa na na space kubwa yaani sio kama blogs maana siku hizi web hosting ni bei rahisi sana na nyingi. Ungekuwa unajua jinsi gani hii forum inavyo fika mbali ktk ulimwengu huu na kiasi cha watu wanavyo ipenda usinge fikiria ata kwenda mbongo.com sasa rafiki fikiria eidha kuweka website hii online au mbongo au kesho na keshokutwa wengine wapate faida zaidi yako kutokana na kipaji chako. Kalaga bao - Kazi kwako.

  MK

  ReplyDelete
 10. Ni vizuri kwa bwana Michuzi kukaa chini na kufikiria maana mtu kuwa na website yako na kuonesha kazi zako ni vizuri zaidi kwasababu baada ya miaka michache unaweza ukawa mbali zaidi, mfano wa google au wikipedia.com ni watu walio anzisha website ambazo sasa ni respect.

  Itakuwa mpaka lini mtu uwe unaajiliwa au kutengeneza partnership na watu wengine ambao wanachukua credit kwa talent uliyo nayo wewe? Sasa fikiria na uweze kuonesha kazi yako peke yako hasa hasa fikiria kuwa na website itakayo wafikia watanzania walio wengi kwa upande wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kama ikiwezekana tengeneza ya kwako itayokuwa na na space kubwa yaani sio kama blogs maana siku hizi web hosting ni bei rahisi sana na nyingi.

  Ungekuwa unajua jinsi gani hii forum inavyo fika mbali ktk ulimwengu huu na kiasi cha watu wanavyo ipenda usinge fikiria ata kwenda mbongo.com sasa rafiki fikiria eidha kuweka website hii online au mbongo au kesho na keshokutwa wengine wapate faida zaidi yako kutokana na kipaji chako. Kalaga bao - Kazi kwako.

  Bakari

  ReplyDelete
 11. huyu bwana ameonyesha msisitizo kutuma maoni yake mara tatu....nilifikiria kumshauri michuzi hivyo hivyo kuwa na uwanja mpana zaidi wa kudisplay mavitus lakini kwa kuwa sikujua nature ya arrangement zake katika mbongo, nikahisi nitakuwa nimeingilia indivijo za mtu....

  hata hivyo kaka michuzi, kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza....kuhusika katika mbongo au jarida lingine kwa jinsi utavyoonelea wewe haina potential ya kukufukuza kwenye blogu....actual kuwa na blogu kutakusaidia zaidi kukua na kuongeza mtandao! mfano unaweka chachandu ya mjadala hapa, au picha moja kati ya kadhaa za matukio unayopiga, na unaweza hata kujumuisha reference na maoni toka hapa globuni kwenye jarida lako....ninachosema ni hiviii blogu ni blogu na jarida ni jarida!

  cheers

  ReplyDelete
 12. nashukuru kwa michango yote. ila kuna mtu ambaye sijamsikia. ndesanjo nasubiri kauli yako - ndiyo ya mwisho.

  ReplyDelete
 13. unamtega Ndesanjo?

  ReplyDelete
 14. Masuala ya blogu yamekuwa
  yakinifurahisha mno. Toka nianze kublogu sijawahi kupata huzuni kutokana na blogu. Ni furaha tupu. Ila leo ndio mara ya kwanza nimepata huzuni kubwa sana. Niliposoma habari hii ya kutuaga, nilinyanyuka, nikaenda jikoni. Nikatengeneza chai. Nikaketi, nikanywa. Wakati wote huo ninajiuliza kwanini?

  Nikarudi tena kuja kusoma vizuri. Halafu nikasoma mawazo ya wengine. Nikafunga mtandao nikasema ngoja nije baadaye labda nimesoma vibaya. Nimerudi nikakuta yale yale. Eti Michuzi unatuaga!

  Kuingia kwa Michuzi kwenye blogu kumeleta uhai fulani kwasababu kadhaa. Inafahamika kuwa kutokana na uwezo wako wa kupiga picha na kuwa na "jicho la picha" wewe sio mpiga picha tu bali ni kama taasisi ya picha Tanzania. Picha zako wengi tumekuwa tukizifuatilia kwa miaka mingi. Sasa blogu imetupa ukumbi wa kuweza kuzipata picha zako (iwe uko Tanzania au nje ya Tanzania. Iwe unasoma Daily News/Sunday News au husomi.)

  Binafsi nimekuwa nikitazama ukuaji wa blogu yako kwa kutazama mbali sana. Sifikirii leo wala kesho. Nimekuwa niiona blogu yako kama vile ni makumbusho pepe ya taifa. Unatumia picha kujenga kumbukumbu zetu kama taifa. Badala ya kwenda jumba la makumbusho, naweza kuja kwenye blogu yako. Kupitia blogu yako nina picha za baraza la kwanza la mawaziri, nina picha ya marais wa kwanza wa Afrika, picha ya Mwalimu akiwa na JFK, helikopta la Chadema, kampeni za uchaguzi, wanamuziki wa Tanzania, mbuzi wanaosubiri basi kituoni!, picha ya vazi la taifa, picha ya yule ustaadhi akiingia na wanyama wake uwanja wa taifa, mwanao Alihassan, mtunzi wa kitabu cha Kuli na Kasri ya Mwinyi Fuad, Kawawa, mji wa Moshi nyumbani kwa Mwalimu Butiama, muhogo ambao uko kama mbuyu, n.k.

  Historia ya karne zijazo haitatunzwa kwenye makaratasi au njia nyingine za zamani bali zitatunzwa kwa teknolojia pepe. Teknolojia pepe ndio njia bora kabisa ya kutunza kumbukumbu, hasa kumbukumbu muhimu kama za taifa. Teknolojia hii inatuepusha na hatari za wizi, moto, mapanya, uchakavu, vumbi, kupotea, n.k. Maktaba ya Daily News ikiungua moto leo hii (mungu pitilishia mbali...ni mfano tu ninatoa), rekodi ya kumbukumbu za taifa letu kupitia picha itatokomea kwa kuwa kumbukumbu hiyo imehifadhiwa kwa kutumia teknolojia ya karatasi ambayo haina umilele. Uhifadhi wa kumbukumbu kwa njia za elektoniki/pepe unaipa historia uzima wa milele.

  Nimesikitika sana Michuzi kuwa unatuaga. Nimesikitika pia kuona kuwa unaondoka katika teknolojia ambayo inakufanya wewe uwe ndio mhariri (baadhi ya watu wanaiita teknolojia hii kwa kimombo: me, the editor)ili kutii amri ya mhariri wako. Vyombo vya habari vyenye mfumo wa uhariri...yaani vyombo vyenye mfumo wa utawala wa ngazi (kuna mkubwa na mdogo, mfano: mhariri mkuu, mhariri mtendai, mhariri wa makala, maripota, n.k) vina kazi na wajibu wake kwenye jamii. Ila pia vyombo hivi vyetu kama blogu vina kazi na wajibu wake. Hasa tunapoongelea blogu za Kiswahili ambazo zinatumika kujenga kumbukumbu na historia ya nchi yetu kama hii yako.

  Kuna raha fulani ya kupata picha hapa kwako, kwanza hakuna matangazo matangazo. Ukurasa haujaa matangazo ya nunua hiki, nunua kile. Ni picha ya maelezo yako. Hili unaweza kuona kuwa ni jambo dogo, kumbe sio. NI furaha iliyoje ninapotembelea mahali kwenye mtandao wa tarakilishi bila bugudha ya matangazo ambayo ninajaribu kuyakwepa. Ndio moja ya sababu kubwa inayonifanya nisiwe na luninga nyumbani siku hizi(baadhi huwa wanashangaa sana kumbe ni uamuzi rahisi sana!)ni matangazo na uchafu uliojaa kwenye luninga. Sipendi matangazo. Napenda habari. Napenda maarifa. Siku hizi vyombo vya habari vinatusukumia matangazo na luninga zimejaa vipindi vya ushenzi ushenzi kuliko habari au maarifa. Kwahiyo ninapokuja kwako nakutana na ukurasa ambao haujajaa matangazo ninafarijika. Nakuja ili nitazame picha. Na ninachokuta ni picha, na sio nunua hiki, pata huduma hii, n.k.

  Halafu kuna suala la lugha. Nimesema tayari kuwa blogu hii ni kama jumba la makumbusho ya taifa kwa picha. Kitendo cha makumbusho haya ya taifa letu kuwa katika lugha yetu ya taifa kimekuwa kikinigusa sana. Tusipopenda na kuenzi lugha yetu, nani atafanya hivyo? Baadhi ya watu wanasema kuwa tukitumia lugha yetu tutashindwa kunadi nchi yetu na kukuza utalii. Sina muda kwa sasa kuingia ndani kuchambua hoja hii, ila mtazamo wa kuja utalii ni shughuli inayofanywa na wazungu au watu toka nje ya nchi ni mtazamo ambao sikubaliani nao. Kabla hatujaanza kutangaza nchi yetu kwa watu toka nyika za mbali, ni vyema tukaitangaza kwa watu wetu kwanza. Kwa mfano, hivi hakuna umuhimu kwa Mtanzania kutembelea mapango ya Amboni? Kwanini tunapenda sana kutaka kunadi nchi yetu na uzuri wake kwa watu wengine zaidi yetu sisi wenyewe? Nikiambiwa nani awe wa kwanza kutembelea soko la watumwa pale Bwagamoyo, kati ya mzungu na Mtanzania , nitasema Mtanzania. Lazima tujenge tabia ya kwenda sehemu hizi ili kujua tulikotoka, tulikopitia. Ili kujijua.

  Utu wetu, historia yetu, utamaduni wetu ndio unaotufanya sisi kuwa sisi. Uzuri ni kuwa mambo haya hayahitaji "misaada" toka nje. Kinachohitajika ni kile ambacho Bob Marley ameimba kwenye Wimbo wa Ukombozi (redemption son),"...hakuna wa kutukomboa bali sisi wenyewe." Kwahiyo ninaposikia kuwa unahama, sio tu unahama toka kwenye blogu, ila pia unahama kilugha, yaani unahama toka kwenye lugha ambayo mimi na wewe tukikutana huwa ndio tunaongea unakwenda kwenye lugha ya kuazima. Ninasikitika sana. Tena sana.

  Tunafurahia picha zako Michuzi. Bado tunapenda kuziona kupitia blogu yako. Pia tunapenda blogu yako kuwa ni ya Kiswahili. Tuna jukumu la kuenzi na kuheshimu lugha yetu. Tuna kila sababu ya kutunza kumbumbuku zetu kwa ajili ya vijukuu vya akina Alihassan (mwanao). Ndio ninaposema kuwa blogu hii ni jumba pepe la makumbusho ya taifa la Tanzania la kwanza la kwenye mtandao wa tarakilishi.

  Nimekuwa ninafurahia pia jinsi ambavyo picha zako zinachochea mazungumzo na mijadala. Hiyo ni moja ya kazi ya mwandishi. MOja ya faida za teknolojia ya blogu. Nipe, nikupe. Nasema hivi, anasema vile. Kiti moto. Gumzo.

  Mmoja wa watoa maoni ametaka kujua kama unahamia Mbongo kama njia ya kupeleka wasomaji. Wahariri wengi siku hizi wanatumia blogu ili kupeleka wasomaji wengi zaidi kwenye magazeti pepe yao. Ukijua jinsi ya kuitumia, blogu ni zana nzuri sana ya kutangaza jambo. Kwahiyo kama nia ni hii sidhani kama wewe kuwa na blogu kutaharibu jambo zaidi ya kufanikisha na kuongeza wasomaji wa Mbongo. Suala muhimu ni kujua jini ya kutumia blogu kuitangaza. Ni sayansi.

  Kumbuka pale Helsinki Michuzi...nakusihi...

  Tafadhali....

  ReplyDelete
 15. Michuzi,

  Sijui kwa wenzangu kama wameshaligundua hili,...kila nikienda 'mbongo.com', nakutana na 'mzungu.com''
  , labda ndio maana watu wanakuwa wanarudi hapa...maana ndiko mbongo tunapomkuta.

  ReplyDelete
 16. Mbongo.com ni mbongo kumaanisha Tanzania au kumaanisha Ulaya yaani mzungu.com?
  Sasa nikienda pale nakuta mambo ya online dating na mambo mengine nisiyoelewa hadi niwasiliane na kamusi.

  ReplyDelete
 17. Michuzi, ninajilazimisha kuamini kuwa uamuzi huu umeuchukua bila kufikiria vyema. Kuna tatizo gani la wewe kuendelea kuwa na blogu na kuwa huko mbongo kwa wakati mmoja. Ukikimbia, huko mbongo hatuji. tutakugomea.

  ReplyDelete
 18. Muhidin,

  Mzee mwenziyo nakuita kwa jina la kwanza.

  Natumaini umemsoma na kuyaheshimu maoni ya mashabiki wako.

  Nikirejea mawazo ya Ndesanjo kuhusu blog yako kwamba imekuwa kama makumbusho. Utakumbuka nilivyokushauri kuhusu kuturudisha nyuma katika mafaili ya historia. Nilikushukuru sana kwa kukubali kufanya hilo na wewe mwenyewe ukanijibu kwa text message ambayo naomba niinukuu "..Vipi blog imenoga?.." Ilikuwa nusura nikujibu kwamba imenoga sana kupita hata tovuti ya mwajiri wako TSN. Ombi langu lile lilikuwa lina maana kubwa sana tena mno. Wewe mwenyewe utaafiki kwamba lilileta chachu iliyonogesha ki aina yake blog yako. Kama alivyosema Ndesanjo blog yako ilianza kugeuka kuwa makumbusho nzuri sana ya historia katika picha.

  Kabla ya miaka ya 1990 nchi yetu haikuwahi kuwa televisheni kama chombo cha habari. Kwa hiyo kumbukumbu zote za picha ni za kupiga (photographes). Wewe ni mmoja kati waliobahatika kuweka rekodi mbali mbali katika picha kabla ya kuingia televisheni nchini Tanganyika kwa sababu Zanzibar ilikuwa na televisheni. Naomba nirejee kanuni za mwana TANU kwamba "..Nitatumia elimu yangu kwa manufaa ya taifa langu.." Sasa ninakuomba tena utumie elimu yako kwa manufaa ya taifa lako kwa kurudi kwenye blog na kuendelea kutuletea picha mbali mbali za kuelimisha na kuburudisha umma.

  Natumaini utaheshimu na kuyathamini maombi yalio wengi kwamba badili uamuzi wako na kuendelea kuwepo kwenye blog.

  Mtu mzima mwenziyo,

  F MtiMkubwa Tungaraza.

  ReplyDelete
 19. Uwamuzi ni wako bwana michuzi wewe ndiye unayejua ni kwa nini unataka uhamie mbongo.com sisi ni wasomaji tu wa hii blog, lakini matatizo yote ni wewe unaeyajua kwa hiyo bwana jiangalie kwanza wewe na maslahi yako, maisha ya sasa kwanza unajijari wewe mwenyewe, kama unaona hakuna chochote kinachozidi ukiifunga hii blog na kuhamia mbongo.com bora usiifunge lakini kama kuna chochote kidogo kitaongezeka upande wako wewe fanya ulivyofikiria, au kama hiyo mbongo.com ni yakwako au uko patna na mtu bora uhamie huko kuliko kufanya kazi mbilimbili kuandika kwenye blog na kuandika kwenye mbongo wakati unaweza kuifanya kazi hiyo pamoja, kama kweli mtu anapenda kukusoma kwenye blog atakufuata kwenye mbongo.

  Mkongo

  ReplyDelete
 20. Natumaini Michuzi hukutumia jambo hili kama mbinu ya kufahamu idadi ya watu wanaotembelea blogu yako. Hata hivyo maoni yaliyotolewa yanakupa uhalisia wa idadi ya washabiki wako. Blogu hii imekuongezea umaarufu na kukujengea heshima pengine kuliko kazi nyingine. Hii ni Blogu ia Muhidin Issa Michuzi na sio mali ya shirika fulani. Unamiliki hisa kwa asilimia 100% na una nafasi ya kuwa maarufu zaidi ya hapo. Si umeanza siku si nyingi? Kumbuka ulikopotoshwa, angalia ulikotoka, angalia uendako na Tanzania inakokwenda, fanya uamuzi binafsi na songa mbele. Huu uamuzi unaotaka kuchukua sio wa kwako, ila umeshinikizwa.

  H.J.M

  ReplyDelete
 21. Ni vizuri kwa bwana Michuzi kukaa chini na kufikiria maana mtu kuwa na website yako na kuonesha kazi zako ni vizuri zaidi kwasababu baada ya miaka michache unaweza ukawa mbali zaidi, mfano wa google au wikipedia.com ni watu walio anzisha website ambazo sasa ni respect.

  Itakuwa mpaka lini mtu uwe unaajiliwa au kutengeneza partnership na watu wengine ambao wanachukua credit kwa talent uliyo nayo wewe? Sasa fikiria na uweze kuonesha kazi yako peke yako hasa hasa fikiria kuwa na website itakayo wafikia watanzania walio wengi kwa upande wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kama ikiwezekana tengeneza ya kwako itayokuwa na na space kubwa yaani sio kama blogs maana siku hizi web hosting ni bei rahisi sana na nyingi.

  Ungekuwa unajua jinsi gani hii forum inavyo fika mbali ktk ulimwengu huu na kiasi cha watu wanavyo ipenda usinge fikiria ata kwenda mbongo.com sasa rafiki fikiria eidha kuweka website hii online au mbongo au kesho na keshokutwa wengine wapate faida zaidi yako kutokana na kipaji chako. Kalaga bao - Kazi kwako.

  Msomaji

  ReplyDelete
 22. Jamani utani nao umo, Michuzi anatutania tu katika kuzidi kutia hamasa na shamrashara katika blogu yake. Nampongeza kwa kuwa ni mwanablogu wa kwanza kuweza kutikisa kibiriti na kikatikisika hasa. Naomba Mungu Ndesanjo asijethubutu kututania kwa mtindo huu.

  Nina ombi, kama ukiweza kupata picha za msiba wa Edward Moringe Sokoine, naomba tubandikie unajua 1984 wengi wetu tulikuwa si watu wazima hivyo.

  Asante.

  ReplyDelete
 23. Michuzi ningekushauri ufungue website yako mwenyewe www.issamichuzi.com or www.michuzi.com .Hii blog ilikuwa burudisho tosha na kama ingekuwa chini ya site yako nina uhakika hata makampuni yangeshaanza kuleta matangazo humu.Nafikiri hii blogu inapata hits nyingi kuliko website yoyote ya Tanzania.

  Kila la kheri na tuta miss sana hii blog.

  Chief Nyamranga
  Columbus, Ohio

  ReplyDelete
 24. kwa vile umesema uamuzi wa Ndesanjo ndo wa mwisho, basi naamini umessitisha uamuzi wako wa kuachana na blogu kwenda Mbongo.com. Mbongo nenda, lakini na blogu usiondoke. Mimi sitakufuata huko kwako Mbongo.com.

  ReplyDelete
 25. Tunashukuru kwa kubadili mawazo yako

  ReplyDelete
 26. Michuzi alikuwa anatania kama anavyosema Da'mija. Maoni yote haya yanaonyesha namna alivyo na hadhira kubwa. Halafu inamkubali.

  Kimsingi, nadhani Michuzi hahami tena amegundua kuwa watu tunakubali kazi zake. Haiwezekaqni ahame wakati anajua kabisa watanzania wengi sasa wanajiunga na Blogu kila siku. Itakuwa ajabu yeye kufanya kimyume chake, aishie.

  Michuzi hongera kwa kutikisa kibiriti, nadhani umeona kilivyojaa.

  ReplyDelete
 27. nimezidi kukupenda kwa usikivu wako, wewe ni mwema.

  ReplyDelete
 28. Haki ya Nani, Michuzi unajua nini, niliposoma tangazo lako la kutaka kuondoka katika uwanja huu nilipatwa na Shock na hivi jana tu ndio nimetoka Hosptali baada ya Saimon kupatia taarifa kuwa umekubali kurudi tena, welcome back brother, tunaipenda kazi yako usitukatili, cheers!!!!!!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 29. Michuzi,
  suala hili nilikuwa ninalipeleka mbele kwa wakubwa. Nimekuja nikakuta umebadili uamuzi. Basi itabidi niwape taarifa hizi.

  ReplyDelete
 30. Watu mmelilia weeeeeee mpaka Michuzi kabadilisha mawazo. Haya nawaombeni basi mtembelee kule mbongo.com even if it is just to see what the fuss was all about.

  ReplyDelete
 31. Tunashukuru kwa uamzi huo,wapo baadhi yetu ambao hatuoni umuhimu wa blog yako na kwa wale ambao mnaona umuhimu ni wakati muafaka wa kumpa support Muhidini katika kazi hii.Hiki ni kipaji siyo tu kwamba ni kila mwandishi anaweza kuwa mubunifu na kuelimisha umma kwa jinsi hii.Watu wengi ambao tumenufaika na hii blog waliowengi tuko huku nje ya nchi yetu tuna soma habari kwenye magazeti yetu ya huko lakini habari zenyewe huwa ni fupi mno huelewi kinacho endelea lakini blog yako bwana michuzi hata baada ya maswali yaliyotutatiza ulijitahidi kuyatafutia majibu.Mimi nafikiri umefanya vyema kubadili huo msimamo.Sasa tunaomba uanze kutuletea hata taarifa za viongozi mabomu huko ili tuchangie maoni ya kuwang'oa.Tupigie picha za wabunge wanaoingia bungeni kwenda kulala usingizi kwa vile usiku wote hawakulala sababu ya ......unajua mwenyewe wazee hao wakifika Dodoma watoto wote wa kondoa wanashuka hapo idodomya na wazee wetu wakisha tandika maji wao wanawaona ni machotara kwani mnajua watoto wa kondoa walivyo weupe.Sasa tupigie picha hao wazee wanapokuwa wamelala,bila kujali kilichowapeleka huko.

  ReplyDelete
 32. Michipix waweza kutupatia tupicha twa Nelson Mandela na Papa Yohanne wa Pili walipotembelea-ga Bongo mwaka 1990.

  ReplyDelete
 33. michuzi weka counter ujue ni watu wangapi kwa siku wanatembelea blogu yako ni wengi mno ingawaje hawaachi maoni

  ReplyDelete
 34. Walter MachaFebruary 15, 2006

  Sijui nilie kichaga:KELEUWIIIIIII!!!Usiondoke tafadhali.Mimi ni mmoja wa watu wanaopenda sana kukutembelea kwenye blogu hii.

  ReplyDelete
 35. Blog site yako ina mambo yanayofundisha na imenipa changamoto ya kuiboresha site yangu pia.

  nitembelee kwangu http://vizoh.blogspot.com

  ReplyDelete
 36. Mi naamini, jasiri haachi asili,
  Bali siamini,Michuzi kuacha hili,
  Kaziye ya thamani,hako wa kuihimili,
  Michuzi Chonde kwa hili, bakia Bloguni.

  Bakia Bloguni,Kaziyo twaithamini,
  Mengi twayatamani,yaonwe na wajivuni,
  Bin Issa kulikoni, wataka tutia majonzini,
  Michuzi Chonde kwa hili, Bakia Bloguni.

  ReplyDelete
 37. Michuzi nafikiri ulikumbuka msemo usemao "WENGI WAPE,USIPOWAPA WATACHUKUA KWA NGUVU" ni vizuri uliogopa mapinduzi baridi maana wanyonge wakiungana wanakuwa na nguvu kuliko vifaru vinavyoshambulia Gaza,Lebanon,Baghdad,Karbala au Kabul.Asante sana ulithamini mawazo ya wengi,kwani "KWA UMOJA WALIVYOSIMAMA,KWA KUGAWANYIKA WANGEANGUKA"

  ReplyDelete
 38. Sielewi unakwenda wapi yaani hatutakupata tena kwenye issamichuzi.blogspot.com au una maanisha nini? na hiyo Mbongo ndo nini sasa. mmmh

  ReplyDelete
 39. Mimi nimsomaji wa blog yako ya zamani yaani michuzi-blog, kilaasiku,lakini nikasema ngoja nitembelee blog yako mpya ya mbongo.com, ukweli sijaipenda kabisa.Kwanini,Blog yako ilikuwa inafurahisha jamii nakuona wanajamii wanavyochangia na kuonyesha matukio mbalimbali yanayotokea kila siku,alafu nadhani uliianzisha kwa madhumuni ya watanzania na wana africa mashariki, kwakuwa ulihamua kutumia kiswahili,na matukio yalitoka africa mashariki.Sasa leo Jumapili 4, nikasema ngoja nikatembelee mbongo.com,"hamuna kitu".Kama umeamua kuhama, endeleza polojo ulizokuwa nazo mwanzo,akika tutaangalia blog yako mpya.Kuna tofauti kubwa mno kati ya matukio uliyokuwa ukionyesha blog yako ya kwanza na ya sasa.Nilivoona blog yako mpya tutakosa mambo mengi (maoni,picha na matukio mbalimbali) ambayo hayapatikani kwenye vyombo ya habari,nadhani umenielewa.blog yako mpya imeonyesha matukio ambayo mara nyingi tunayaona kwenye vyombo vya habari.Unajua wengine hatuna muda wakuangalia TV (local channels),kwahiyo tulitegemea blog yako itufikishie ma-ujumbe na tupate matukio mbalimbali.
  Asante
  Tindamanyile-Tegamaisho
  Mbarika-Misungwi,Mwanza

  ReplyDelete
 40. AnonymousMay 31, 2009

  Nimerudi kazini, nafungua Michu ola. vipi Mzee mwenzangu, Mwinyi Mpeku.

  ReplyDelete
 41. AnonymousJune 26, 2009

  poa nenda mwalimu

  ReplyDelete
 42. daaaaah najuta kwa nini unataka kutuacha nachotaka kusema blog yako imekuwa chachu ya mimi kufanya kipindi changu vizuri,yani matukio mengi huwa nayapata hapa na ndio nafanyia kipindi changu cha mambo ya jamii cha kusema ni kwamba nyuma yako kuna jeshi kubwa sana japo hulioni ila mbali na waandishi watangazaji pia tafadhali sana usije toka huku nakuomba bw mkubwa

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...