machinga wakiwa chini ya ulinzi wa mgambo wa site kwa kosa la kuuza nyanya barabarani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Sasa hapa ndipo ninapopachukia kuliko upeo. Hkauna vitambulisho vya uraia na kuna kesi za kikoloni za uzururaji nadhani Baragumu anaweza kulifafanua hili vema. Tazama kuna Machinga wachina hakuna hata mmoja hapo aliyeshikwa lakini sisi kwa sisi tukilana jeb lazima safari iendelee? Alihoji Prof Kezilahabi katika Karibu Ndani

    ReplyDelete
  2. amiri jeshi mkuu hayaoni haya manyanyaso au hawa sio askari wake?

    ReplyDelete
  3. Mkulu MtiMkubwa Tungaraza, kama nakuona vile unaoona picha hiyo na hasira ulizonazo. Tujipe pole ndugu yangu, huyo muuza nyanya akija Ulaya anaitwa "Illegal Immigrants" na akikaa nyumbani anaitwa "Mzeruraji" waende wapi hao? Yana mwisho haya.

    Dennis

    ReplyDelete
  4. Hilo la uzurulaji Kasri amenikumbusha ilhali nilikuwa nimeanza kulisahau. Ilikuwa tarehe 20/6/1997.Jioni ile nikisubiri siku zipite-pite ili nikaanze kidato cha tano Malangali nikaamua nitembee mtaani walau kusabahiana na washikaji.

    Afanaleki! muda si muda yapata saa 1:45 'vizombe' na 'vimahita' kama 50 vikatuzunguka na kutuvamia pale tulipokuwa tunaangalia video. Kumbuka video sie wakina pangu pakavu tulikuwa tunalipia hata miaka ya 1990.

    Virungu walitubamiza magotini, viwikoni, vichwani, ugokoni ilimradi sehemu zile ngumungumu na zenye kimbelembele cha kuchomoza. Damu chururururururu kama jambazi, nikarundikwa ndani ya karandinga na watu wengine. Yawezekana kulikuwa na wahalifu lakini ujio wa vimahita na vizombe vile ulikuja kwa gia ya uzururaji. Sijawahi kusikia hata kwenye nchi zenye machafuko kuwa na vizuizi(curfew) saa mbili kasorobo. Mara nyingi huanzia saa 4 usiku. Pia sijawahi kusikia Bongo kuwa muda wa kazi ni saa mbili kasorobo usiku. Kazi nyingi huwa ni mchana na wala si vinginevyo.Sura na umbile langu lilitosha kuwafanya waniachililee lakini la. Kwa mara ya kwanza na ya mwisho nililala rupango hata nilipotolewa na baba yangu kesho yake.

    Hata nakwenda shule magoti yangu hayafanyi kazi. Nalijatribu kucheza mpira shuleni lakini usingaliwaza kuwa mie ndiye yule tuliyekuwa timu moja na Emmanuel Gabriel Mwakasagule (wa Simba kwa sasa). Tangu hapo mpira sikuutamani tena kwani ulikuwa ni maumivu badala ya furaha na hamasa kwangu. Nani anajua pengine leo ningalikuwa nagombea namba nakina Thiery Henry na Didier Drogba isingalikuwa virungu au kama wanavyoviita kule Iringa 'visonzo' vya polisi wale makatili kwa sie tusiokuwa na hatia.

    ReplyDelete
  5. Muhidin,

    Naomba maoni yako juu ya haya mambo ya askari na raia. Umetuletea picha kadhaa tangu za FFU katikati ya umma, wanamgambo wa jiji wakiwavurumisha wafanya biashara ndogo ndogo, wanamgambo wa jiji wakiwa katika doria, polisi wakimpa raia 'no smoking', polisi na vibaka, na hii ya hapa ja wanamgambo wa jiji na vibaka. Naomba kusikia maoni yako wewe binafsi unafikiri nini juu ya hili.

    Natanguliza shukrani zangu za dhati,

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  6. Muhidin,

    Samahani hii picha si mgambo wa site na vibaka bali na matching guys ambao tumewabadili kwa Kiswahili kuwaita machinga.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  7. 'Marching guys' sio 'matching guys'

    ReplyDelete
  8. Samahani kwa kukosea na asante kwa kunisahihisha sarufi.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  9. na si marching guys wala maching guys. jina limetokana na kikiji cha mchinga kilichoko mkoani lindi ambako waanzilishi wa biashara hii inasemekana wametoka. hivyo wakaitwa wa-mchinga na kisha wa-machinga. hakuna aliekosea kati yenu kwa nadharia ya kisasa ambayo hata mie nilidhania hivyo mpaka nilipoelimishwa...

    ReplyDelete
  10. Asante kwa maelezo yako. Biashara hizi za kutembeza barabarani bidhaa zinazopatikana madukani ipo katika nchi duniani hususani nchi zinazoendelea.

    Lakini hujanijibu bado: wewe binafsi unafikiri nini juu ya hao Wamachinga na mgambo wa site?

    Kwa heshima na taadhima,

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  11. mtimkubwa nenda www.mbongo.com soma 'a day in a life of a machinga' upate jibu lako..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...