wanachama wa cuf wameandamana kushinikiza igp mahita apigwe chini baada ya kuwatuhumu ujambazi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kwa mara ya kwanza katika historia
    wananchi wameruhusiwa kuandamana kupinga vitendo vya unyanyaswaji hayo ni maendeleo yanayoleta matumaini kuwa serikali ya sasa inaelekea kwenye demokrasia.Ni vyema tabia hii iheshimiwekwa sababu tumejionea wenyewe kuwa watanzania ni wastaarabu hakuna fujo yoyote iliyotokea mbona siku zote uhuru huo kwa nini ulikuwa unanyimwa wananchi imefika mahali wananchi wapewe haki zao za msingi.
    Rais amsitafishe Mahita kwa kujenga heshima yake ila kama anataka kumlipa fadhila za kuvuruga uchaguzi kama Mrema anavyodai basi amwache.

    ReplyDelete
  2. tuhuma alizotoa bwana mahita ni kubwa sana,kweli inasikitisha kuona serikali ya ccm inakaa kimya bila ya kutoa tamko lao.sijui ingekuwaje kama angetuhumu ccm, haya JK mpenda demokrasia anafikiria nini? jamjuah.

    ReplyDelete
  3. JK mpige chini Mahita ndio mchochezi wa vurugu zote Tanzania tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi!! watanzania tangu lini wanarusha mabomu na kutia vinyesi visima wanavyokunywa maji wenyewe! ni huyu huyu mtu! na saa hizi kakaa kimya pengine anadhani anaweza kupindua nchi!- karibuni kwangu nimemjadili mahita!

    Michuzi blogu zinafanya kazi! teyari suala la utata wa CV ya Mahita limejionyesha hapo kwenye picha ya Michuzi kama tulivyomjadili humu mabloguni! ni KIHIYO! na si graduate wa Ontario!

    ReplyDelete
  4. huyu bwana ni kada na itamchukua muda rais kumfukuza kazi unless bunge liingilie kati zaidi ya hapo ataachwa tuu kwa kusubiri wingi la kasheshe za kisiasa lipungue,amekisaidia chama kumzibiti Mrema kule Moshi alipokuwa RCP na ndio zawadi yake kuwa IGP

    ReplyDelete
  5. Mnamkumbuka mbuge Derefa wa Shinyanga? Mnamkumbuka mbuge nanhii...the name escapes... wa Njombe huko. Mwaka fulani walimjia juu Mahita na kuhoji ulipukaji wake holela wa hoja. Wakati ule tuliwaona kama wajinga vile. Tukalitunza na kulikumbatia yai viza sasa limetupasukia na linanuka mmmhhhffff!

    ReplyDelete
  6. je kikwete si ni moto wa kuotea mbali? au naye anamuogopa?

    ReplyDelete
  7. Huyu Mahita ni mmoja kati ya waheshimiwa wachache wanaoishi kwa kujipendekeza kwa wakubwa na kwa sababu alipata cheo kwa kujipendekeza inaelekea anaendeleza KUJIKOMBA huko huko lakini naamini JK ni tofauti, alishasema mwenyewe hao wa kujikomba kwake noma. Eti sasa kapata aibu anajifanya kuondoa selikarini. Bila shaka yeye ni jambazi namba moja. Aeleze hayo majumba aliyonayo kayapata wapi. Hivi ndiyo sababu ana support kuua watu bila makosa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...