jamaa akipokea barua posta mpya. je, wa ughaibuni, haya mambo bado yapo ama mambo ya kuletewa hadi mlangoni. sie tufanyeje tufikie huko?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Masanduki kama hayo yapo kama kawaida lakini ni kwa matumizi binafsi mfano mtu una vitu vya thamani (jewels, makaratasi ya ulithi, contracts za thamani, n.k) unataka kuifadhi basi inakuwa ni kwa ajili yako tu.

    Karibia asilimia 99.99 za barua zote uletwa mpaka nyumbani yaani mlangoni, Milango inakuwa kama ina sehemu ya kupenyezea barua bila ya kusumbua watu mida ya hasubui.

    Tanzania kufikia hatua hii inabidi mitaa na nyumba ziwe ndani ya ramani ili isiwe vigumu kwa kusambaza barua, Pia milango yetu iwe na nafasi za kupenyezea barua.

    Usalama inabidi uwe zaidi maana bila hii itafanya watu wawe wakipotezewa barua zao (wizi), Postal offices wawe na uwezo wa kusambaza barua kwa muda muafaka na wa haraka yaani watuma leo kesho hasubui wapata.

    Kama Postal Office wakitaka haya wanaweza kuja huku au popote(nchi yoyote) penye huduma kama hizi ili wajifunze zaidi.

    ReplyDelete
  2. Ili kufikia huko, kwanza kabisa ni lazima wenye nyumba wabadili tabia ya kufukuza fukuza wapangaji, halafu ndio mengine yatafuatia.

    ReplyDelete
  3. Kabla ya yote hayo wenye nyumba kufukuza wapangaji au kutengeneza sehemu za kupenyeza barua kwenye nyumba namaofisa wa posta kuwa waaminifu, cha kwanza kabisa ambacho ni muhimu kila mtaa au sehemu ambayo kuna nyumba zipewe majina na yaandike na kila nyumba iwe na namba kwa nchi nzima kuanzia mijini mpaka vijijini. je mtaweza?

    ReplyDelete
  4. duh hii kali! lakini sijui ni kwa nini, nadhani kwa sababu ya maisha ambayo labda hayatabiriki sana au!! cha ajabu sana huku kwenye nchi za wenzetu, ukienda benki yoyote, bima yoyote, idata yoyote, iwe polisi au afya.....yaani wana historia yako, tangu siku ulipovuka mpaka, gari ulilotumia, nyumba zote ulizoishi, na kazi zote ulizofanya!!!!!! hakuna ubabaishaji wana data base system nzuri sana, na nafasi za kufanya utapeli ni finyu sana- kwa kweli Tanzania kufika huko inabidi kudevelop sana system ya IT..samahani nilitoka nje kidogo ya topic! -

    ReplyDelete
  5. As we say in Texas, Why fix something that ain't broke? Kwani upatikanaji wa barua posta sasa hivi una matatizo gani? Don't fix something that ain't broken!

    ReplyDelete
  6. mmh ndugu mliavukana kufuata barua posta kuna matatizo mengi sana,siku hizi the trafic is so busy in dar so to get to the center is a head ache.ni vyema tukaidefine mitaa yetu na nyumba zitu ili tuweze kuletewa barua hadi maskani.Imani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...