THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

ulinzi kibao


polisi akilinda benki. nji sasa imetulia na kuleta wasi wasi kuwa labda kweli hawa jamaa hushirikiana na jamaa. unaambiwa hata loba hamna siku hizi bongo!


Kuna Maoni 8 mpaka sasa.

 1. majaliwa Anasema:

  hilo ndio tatizo. Polisi amekaa kizembe kama anacheza chakacha.

 2. mark msaki Anasema:

  huruma! - pia inategemea jana alikuwa lini, nani na nani wanamdai na kama jamaa atakatiza amgalau kama alivyoahidi ili jioni unga wa ugali upatikane la sivyo kimbembe itabidi kumuachia mama Kayaii jukumu la kusolicite milo...na ikifika hapo ujihadhari usirudi na bunduki nyumbani...utaua tuu kwa vyovyote!

 3. Anonymous Anasema:

  Muhidin,

  hiyo "unaambiwa hata loba hamna siku hizi bongo!" ina maanisha siku ngapi? Mbili, tatu, nne, wiki, mwezi, au mwaka? Na askari kulinda benki hawakuanza "siku hizi" wanazilinda tangu zamani lakini wakifika "mabwana fanya" wanalamba mishahara na akiba zingine kama zao. Jinginewe, askari analinda kuzuia majambazi lakini benki haziibiwi na majambazi tu kuna wezi wa kalamu na matapeli pia! Hao wanalindwa na nani? Fraud officers?

  Nimekumbuka nyimbo moja iliyoimbwa sana radioni kwenye tukio fulani kubwa la kitaifa, Nyimbo hiyo ilikuwa ikisema "Bunduki, risasi wala hatuzijali..." Kama utakumbuka nyimbo hiyo na tukio hilo utaupata ujumbe wangu kwa ufasaha zaidi.

  F MtiMkubwa Tungarza.

 4. Anonymous Anasema:

  Tisha toto watu wa kazi wanakuja kumi na huyu bwana hapo pichani huenda akawa wa kwanza kuokoa maisha yake kabla ya raia anaowalinda

 5. John Mwaipopo Anasema:

  Just imagine ni mdogo wako huyo aliamua kwenda jeshi la polisi baada ya kukosa ajira zingine. Roho yako nahisi inakuwa juu juu kila wakati aendapo kazini. Itakuwaje maisha yake pale wazee wa kazi watakapoamua kuja kufanyiza.

  Vile vile just imagine wakubwa wake wa kazi wanamuamuru awatungue watu wasio na hatia risasi za midomoni. Kesho yeye ndiye atakayeandikwa kwenye tume na yule kibosile aliyemtuma kutoandikwa na kuepushwa na zahma nzima.

 6. Anonymous Anasema:

  jama,polisi wana maisha magumu,wanapewa mishahara midogo,hivyo kama huyu inaonekana yupo kazini lakini anawaza pengine!!!!!!!
  ni matatizo ya kisaikolojia pamoja na hali halisi ya undata bongo.

 7. Anonymous Anasema:

  Jamani huu ndio ulinzi gani? Mbona mkono upo kiuononi? Au analinda mauno?

 8. Anonymous Anasema:

  Tena hawa wanaolinda mabenki ndio wenye njaa kinoma, kazi kukamata wahindi usiku wa manane, kisa, wamepita ktk njia in a wrong direction, sasa analinda benki au anafukuzia shilingi?