THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

utamu wa sindimba


kila ijumaa kuna onesho la ngoma nyumba ya sanaa ambapo sisi tambala, simba theatre na kyandu music hupokezana kwa zamu. na sheria ni kwamba wimbo wa mwisho kabla ya pazia kushuka, lazima kundi likaribishe watazamaji kucheza kama mnavyoona wenyewe


Kuna Maoni 9 mpaka sasa.

 1. John Mwaipopo Anasema:

  Macho hayo michuzi! Yapeleke kwingine basi.

 2. ndesanjo Anasema:

  Kulalek! Sikujua Michuzi nawe unajua kucheza ngwashala. Nakubaliana na Mwaipopo kuhusu jicho lako. Unatazama nini? Halafu huyo jamaa aliyeko mkono wako wa kulia hiyo staili ni ngwashala nayo?

  Kingine ni hao wanawake nyuma yako. Nimependa sana mavazi yao. Ukikutana nao tena waambie.

 3. mark msaki Anasema:

  wizara iwasaidie zaidi wasikate tamaa kudumisha mila setu!

 4. Anonymous Anasema:

  huu ndio mwanzo wa kupeana virusi, baada ya ngoma,,,,,,eeehhh! jj

 5. Anonymous Anasema:

  Acha upuuzi wewe unamanisha nini virusi? Mawazo yako yasiwe negative tu.

  Jamaa ameamua kutuwekea picha wewe watoa matusi. Jalibu kuwaza na kutumia lugha nzuri.

 6. mudi Anasema:

  mambo ya virusi yametoka wapi?

 7. John Mwaipopo Anasema:

  Ukisikia ujinga ndio huo wa kujadili yasiyotakikana hapa.

 8. Fikrathabiti Anasema:

  sasa naona bloguni kunaanza kuibuka mamluki kutuharibia mwelekeo wetu.
  Ngoma na virusi vinahusiana kivipi?????Watu wenye fikra kama hawa hawatufai katika uwanja wetu huu mtukufu wa kulishana fikra!!!

 9. Anonymous Anasema:

  Picha hii inanikumbusha Cho cha Sanaa Bagamoyo enzi hizo wakati wakihitimisha onyesho:

  Mwalimu Luiza Maganga: Kokoliikoo koX2 Kajogoo kalia koko

  Wanachuo: Alialia ko ko alialia koko weX2

  Baadaye lilipoingia chuoni 1988 kundi la wendawazimu (Marehemu Basil Jia mtaalamu wa kupiga ala zote za kiasili na uchezaji ngoma zote za kiasili, Gasper Tumaini sasa katibu wa TOT, Stephen Ndibalema, Selemani Rehani mara ya mwisho kuwasiliana naye alikuwa chuo kikuu cha Edinburgh, Dennis Mango, Solomon Mwasokwa wicked lead guitarist Chuo cha Sanaa to ever produced, John Shogholo mchoraji wa kimataifa, F MtiMkubwa Tungaraza, Marehemu Valentina Kiondo mwimbaji aliyetambuliwa kitaifa, Marehemu Grace Kassege, Marehemu Avina Mkapa, Graceana Kambanyuma, Mwanaima Sharif, na Joyce Fisoo) wakaona wimbo wa kokoliko umepooza wakabadilisha na kuingiza wimbo wa Askari Melimee. Wimbo ulitoholewa kutoka kwa Mganga wa asili Mwalimu Hassan wa Mlingotini Bagamoyo ambapo wanafunzi wa Chuo cha Sanaa walikwenda kushuhudia uganga wa jadi unavyoendeshwa siku ya waganga kufunga kitabu.

  Siamini uchawi lakini nguvu ya wimbo huu wa Mganga Mwalimu Hassan kuwavuta watu jukwaani ilikuwa siyo ya kawaida.

  F MtiMkubwa Tungaraza.