kila ijumaa kuna onesho la ngoma nyumba ya sanaa ambapo sisi tambala, simba theatre na kyandu music hupokezana kwa zamu. na sheria ni kwamba wimbo wa mwisho kabla ya pazia kushuka, lazima kundi likaribishe watazamaji kucheza kama mnavyoona wenyewe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Macho hayo michuzi! Yapeleke kwingine basi.

    ReplyDelete
  2. Kulalek! Sikujua Michuzi nawe unajua kucheza ngwashala. Nakubaliana na Mwaipopo kuhusu jicho lako. Unatazama nini? Halafu huyo jamaa aliyeko mkono wako wa kulia hiyo staili ni ngwashala nayo?

    Kingine ni hao wanawake nyuma yako. Nimependa sana mavazi yao. Ukikutana nao tena waambie.

    ReplyDelete
  3. wizara iwasaidie zaidi wasikate tamaa kudumisha mila setu!

    ReplyDelete
  4. huu ndio mwanzo wa kupeana virusi, baada ya ngoma,,,,,,eeehhh! jj

    ReplyDelete
  5. Acha upuuzi wewe unamanisha nini virusi? Mawazo yako yasiwe negative tu.

    Jamaa ameamua kutuwekea picha wewe watoa matusi. Jalibu kuwaza na kutumia lugha nzuri.

    ReplyDelete
  6. mambo ya virusi yametoka wapi?

    ReplyDelete
  7. Ukisikia ujinga ndio huo wa kujadili yasiyotakikana hapa.

    ReplyDelete
  8. sasa naona bloguni kunaanza kuibuka mamluki kutuharibia mwelekeo wetu.
    Ngoma na virusi vinahusiana kivipi?????Watu wenye fikra kama hawa hawatufai katika uwanja wetu huu mtukufu wa kulishana fikra!!!

    ReplyDelete
  9. Picha hii inanikumbusha Cho cha Sanaa Bagamoyo enzi hizo wakati wakihitimisha onyesho:

    Mwalimu Luiza Maganga: Kokoliikoo koX2 Kajogoo kalia koko

    Wanachuo: Alialia ko ko alialia koko weX2

    Baadaye lilipoingia chuoni 1988 kundi la wendawazimu (Marehemu Basil Jia mtaalamu wa kupiga ala zote za kiasili na uchezaji ngoma zote za kiasili, Gasper Tumaini sasa katibu wa TOT, Stephen Ndibalema, Selemani Rehani mara ya mwisho kuwasiliana naye alikuwa chuo kikuu cha Edinburgh, Dennis Mango, Solomon Mwasokwa wicked lead guitarist Chuo cha Sanaa to ever produced, John Shogholo mchoraji wa kimataifa, F MtiMkubwa Tungaraza, Marehemu Valentina Kiondo mwimbaji aliyetambuliwa kitaifa, Marehemu Grace Kassege, Marehemu Avina Mkapa, Graceana Kambanyuma, Mwanaima Sharif, na Joyce Fisoo) wakaona wimbo wa kokoliko umepooza wakabadilisha na kuingiza wimbo wa Askari Melimee. Wimbo ulitoholewa kutoka kwa Mganga wa asili Mwalimu Hassan wa Mlingotini Bagamoyo ambapo wanafunzi wa Chuo cha Sanaa walikwenda kushuhudia uganga wa jadi unavyoendeshwa siku ya waganga kufunga kitabu.

    Siamini uchawi lakini nguvu ya wimbo huu wa Mganga Mwalimu Hassan kuwavuta watu jukwaani ilikuwa siyo ya kawaida.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...