asha baraka na kaka yake baraka msiilwa, wamiliki wa africa stars entertainment inayoendesha bendi za african stars 'twanga pepeta' na african chipolopolo (zamani african revolution) wakitete jambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Yaani....nimefurahi saana kwa Chock kurudi TWANGA...

    ReplyDelete
  2. Muhidin,

    Amini usiamini, umeniwahi kidogo nilikuwa nataka nikutumie ombi la picha ya timu ya netiboli ya BIMA kufuatia msululu ulioutoa wa picha za zama za kandanda.

    Una picha yoyote ya Asha Baraka na kina Marehemu Amina Mohamed, Aziza Fataki, Beti Ndolezi, Suma Mwaisaka, na wengineo wakiwa bado katika timu ya netiboli ya BIMA. Kama unayo tafadhali naomba utuletee ili tukumbuke enzi za netiboli uwanja wa Reli, Gerezani.

    Msishangae sana kwa sababu enzi hizo ushabiki wa netiboli kwa wanaume ulikuwa unakwenda sambamba na ushabiki wa soka. Hali kadhalika ushabiki wa soka kwa wanawake.

    Jamani, Tanzania ilikuwa ina wakati wa karaha iliyokuwa imejaa raha.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  3. F MtiMkubwa Tungaraza nimekuvulia kofia kwa kumbukumbu nzuri. Hatuitaji kusoma kitabu tujue yale yaliyotukia wengine tukiwa makinda. All we have to do ni kukualika na kukupa tu-bia (kama watumia)halafu lete stori.Ntakutafuta ntakakapokuwa nakamilisha kuandika kitu fulani.

    ReplyDelete
  4. nayule alikwa mwenyekiti wao ni nani Chiku? du ilikuwa raha sana enzi hizo kweli raha ndani ya karaha... Michuzi unawakumbuka vijana wa maghorofani, MK group na MK nani wale..mambo ya Ngulupa tupa tupa....huwezi amini zile bendi mbili zilikuwa za huyu mama..kweli katoka mbali1 je unapicha zao?

    ReplyDelete
  5. Mk Beats. Unawakumbuka wakina Sem Karenga? Siku hizi ana kibendi chake kinapiga Sugar Ray Sokota Temeke Ijumaa na Jumamosi

    ReplyDelete
  6. Msimsahau Neddy nombo pale maghorofani, raha tupu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...