damija. hawa ndo sis tambala ya sasa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Kuna uwezekano wa vikundi kama hivi kuja kufanya maonyesho hapa Canada kila mwaka wakati wa majira ya joto.Naomba tuwasiliane ili nikupe "mchongo" huu.

    ReplyDelete
  2. Jeff ukishauita mchongo umekosea. Kumbuka kasi ya Kikwete kwa wala rushwa na ametangaza anawafahamu kwa majina sasa isije na wewe ukawekwa kwa kutangaza sera za chajuu. Natania tena hapa lakini neno mchongo na cha juu huko bongo lina maana ya kirushwa rushwa hivi katika dhana ya kupokea na kutoa yaani unatoa kazi halafu unapata kapasenti fulani. sijui nimeeleweka!

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu Michuzi,

    Sisi tambala hususani Kalulu a.k.a 'Faza', amenifundisha jambo moja kubwa sana katika maisha yangu, kwamba unapoyavulia maji nguo, basi yaoge.. tena yaoge hasa uhakikishe umetakata na sio kujimwagia kichwani na tumboni kama watoto wanavyofanya. Kufanya kitu kwa ukamilifu ndiyo kanuni anayoitumia Kalulu katika kuiendesha Sisi Tambala, mtu huyu havumilii hata kajikosa kaduuuchu kwenye sauti au katika ala za muziki mnapokuwa mazoezini na kwenye onesho,.. mtasikia ghafla muziki umezimwa vaaap!!!! sauti ikitokea nyuma.." Kasembe nini bwana wewe??...au wee Mija hukula??..anza upyaa..." basi mnaanza tena, na kama vikosa vitaendelea basi mtarudia wimbo hata mara kumi. Hadi wimbo utoke.., kazi iliyofanyika hapo huwa si lelemama.

    Na kuanzia hapo nilijifunza kwamba unapofanya jambo lako, fanya kwa ukamilifu, usikubali hata kidogo makosa ya bila sababu, usiwe na haraka ya kukimbilia kulimaliza kwani kwa kufanya hivyo utayapa mwanya makosa. Lakini pia usizembee mno kwa madai kwamba huna haraka ya kulimaliza jambo lako.

    Michuzi asante sana kwa picha, naomba unipitishie salamu zangu.

    ReplyDelete
  4. sawa kabisa da mija! ushauri hata mimi naumeza kama ulivyo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...