mzee mathias kisa akipokea tuzo ya 'mchezaji wa karne' wa tanzania kutoka kwa katibu mkuu wa tff mwakalebela kwa niaba ya fifa leo. kushoto ni mchezaji mkongwe wa simba arthur mwambeta akishuhudia. mzee kisa amechezea timu ya taifa kwa miaka 13 na vilabu mbalimbali. tuzo hii ilikuwa apewe 1994, lakini uongozi wa wakati huo ulizembea na kufanya fifa watume tena zawadi hiyo ambayo hutolewa kwa nchi wanachama ambazo zinapendekeza jina la m chezaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kweli kina Ndolanga walikuwa wanawazibia watu riziki zao. Sasa huyu mzee zawadi yake mpaka leo? Yaani kina Ndolanaga na Rage wao walichokuwa wanakijua ni kula mipesa tu. Nasikia walikuwa wanawazibia hata wachezaji kwenda kujaribu bahati zao nje ya nchi maskini!!! Ndio wao walichangia kuifanya Tz tuwe kichwa cha Mwendowazimu. Halafu madarakani walikuwa hawataki kutoka kujifanaya Madikteta. Pongezi sana huongozi mpya angalau sasa tanz. tumeanza kuamka kidogo kimichezo, hasa soka

    ReplyDelete
  2. tuache wakina ndo langa na mwenzie maha rage ambao waliamua kuangusha soka yetu chini, mimi nina ono moja ambalo nataka nijue.

    timu yetu imekuwa inaangahika kutafuta nembo ya taifa. huyu mzee anaonekana amevaa suti ambayo nahisi ina nembo ya tff.....wadau kama hamjaona.

    je ni vipi tukiamua kuendelea kutumia hii nembo ili tuondoe aibu ya timu ya taifa kutumia bendera kama alama yao .tuangalie simba watatu wa england na logo kwa brazil.

    AKSANTENI

    ReplyDelete
  3. Michuzi nikusahihishe huyo mchezaji wa zamani wa Simba anaitwa Arthur MAMBETA na sio Mwambeta.Ni watu tu walivyozoea kumuitwa kwa kuona linatamkina Mwa,kumbe anaitwa Mambeta.
    Ni mchezaji pekee aliyekuwa akiruhusiwa na kocha kunywa bia mbili kabla ya kuingia uwanjani na vitu alivyokuwa akifanya huwezi kuamini.

    ReplyDelete
  4. Michuzi nakusahihisha hiyo zawadi alitakiwa kupewa mwaka 2004 na sio 1994 kama ulivyoandika..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...