HIVI KARIBUNI KULIKUWEPO NA MAONI YALIYOTUMWA NA WADAU ‘ANONYMOUS’ KWENYE BLOGU HII YALIYOJAA UJUMBE WENYE RANGI YA KASHFA DHIHI YA FAMILIA YA MPENDWA WAZIRI WETU MKUU MH. EDWARD LOWASSA, HUSUSAN BINTI YAKE PAMELLA NA NDUGU ZAKE.
HAKIKA UJUMBE HUO HAUKUWA WA KUPENDEZA NA ULIKIUKA MAADILI YETU NA KULETA USUMBUFU NA MAJERAHA YA NAFSI KWA WAAHUSIKA.

NACHUKUA NAFASI HII KUOMBA MSAMAHA KWA FAMILIA YA MH. LOWASSA KWA YOTE YALIYOSEMWA NA PIA KUWAPA POLE WAHUSIKA KWA USUMBUFU WALIOUPATA NA MAJERAHA YAKE. PIA NAMLAANI KWA NGUVU ZOTE YEYOTE ALIYETUMA UJUMBE KAMA HUO NA KUMUOMBEA KWA MUNGU APATE NGUVU YA KUJENGA MIOYO YA UPENDO KWA WENZAKE. NAAMINI NI WATU WACHACHE WENYE CHUKI BINAFSI DHIDI YA MAFANIKIO YA WENZAO KADHALIKA NA YA BLOGU HII.

NACHUKUA NAFASI HII PIA KUWATAKA RADHI WADAU WENGINE AMBAO NAO WAMEKUMBWA KAMA YA HAWA NDUGU ZETU WAPENDWA. KWA KWELI INAKATISHA TAMAA KUONA JINSI WATANZANIA WANAVYOWAFANYIA WATANZANIA WENZAO, NA WAKIELEZWA JUU YA UBAYA WA UDHAIFU WAO HUO, WANAKUJA JUU. NDO MAANA NAMUWEKA MUNGU MBELE ATUSAIDIE WATANZANIA TUONDOKE HAPA TULIPO NA TUWE NA MAWAZO/MAONI YA MAANA NA UPENDO KWA WATANZANIA WENZETU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Naunga mkono tamko hili. Naongeza kuwa tusikilize wimbo wa Jabali la Muziki, Marijani Rajab, anasema: Katika watu kumi binadamu mmoja.

    Endelea. Wako watu wengi makini wanaofuatilia na kufaidika na blogu yako.

    ReplyDelete
  2. OOOPS! Kuna familia nyingi za Watanzania ambazo zimewahi kutukanwa katika blog hii, usiku na mchana!

    ReplyDelete
  3. Pole michuzi.Lakini inabidi watu wakomae.

    Mwalimu wangu aliwahi kuniuliza swali wewe kama mwandishi wa habari kikao kikikosa maelewano hadi mwenyekiti akashindwa kukidhibiti na wajumbe wakawa wanatukanana matusi ya nguoni kwenye kikao na kikao kikavunjika utaandikaje kwenye gazeti lako?Nikamjibu sijui.Akasema ina inabidi uandike kuwa Kikao kilikuwa cha uhuru Sana ambapo kila upande ulitoa mawazo yake kwa uwazi bila kuingiliwa na upande mwingine na mwishowe kikao kiliahirishwa hadi itakapotangazwa tena.

    Kwenye blog yako kuna watu wanaandika kwa uhuru waachwe na upande wa pili kama unalo jibu nao utoe kwa uhuru.Familia ya Lowasa nayo ingejibu badala ya wewe kuwa msemaji wao.Mwenyekiti michuzi ungekaa kimya maana hii blog huwezi kuidhibiti.Na si sahihi uidhibiti.Huo ndio uhuru wa habari.

    ReplyDelete
  4. Kosa ni lako bwana michuzi,
    siku hizi kila tukiweka maoni tunaambiwa kuwa "your posting will appear after owner's approval" sasa ilikuwaje ukaruhusu hayo mawazo??
    Pia kwa kuangalia haraka haraka bado naona matusi yamejaa kwenye hii blog. Hivi ni kweli una muda wa kusoma kila maoni?? Kama hausomi maoni-mie nashauri uondoe hiyo sentensi "your comments will appear after owener's approval" las sivyo utajikuta unapelekwa kwa wanasheria. Bahati nzuri wabongo hatuna hizo tabia, lakini huwezi kujua bwana. Watu wanaweza kuku"sue".
    Over to you

    ReplyDelete
  5. Michuzi
    Mimi ni mmoja wa wasomaji wa hii blog yako na huwa nafurahishwa sana na maoni ya wote ambao wanachangia humu. Kitu kimoja lazima ukubali dunia ya sasa hivi ni ya mtandao wazi na siyo ile enzi ya CCM kushika hatamu tena. Popote pale kutokana na wingi wa mawasiliano lazima watu wataongea tuu na kutukana na ndiyo sifa kubwa ya utanzania hiyo. Binafsi sijafurahia matusi aliyotukanwa mtoto wa PM hasa ukizingatia ilikuwa nje ya topic, ila kuna moja lakujifunza hapo. Kwa jinsi ilivyokuwa rahisi kwako kutoa hiyo topic yenye matusi ( kwa mtotot wa PM), basi tunakuomba uwe fair across the board. tumejionea ni watu wengi sana wamekuwa wakitukanwa huku kwenye blog yako na umekuwa ukikaa kimya, sasa hii ya PM umeitoa katika masaa 24 na kuomba radhi. Kwa mtaji huo basi, ili tukuelewe tunakuomba uombe radhi kwa wote waliotukanwa katika blog hii yako, since umekubali kuwa responsible na kuapologize kwa pamela Lowassa, basi fanya hivyo kwa akina Cynthia na wengineo wengi waliokwisha tukanwa katika blog hii. Pili nakuomba basi moving forward uset standard ya kuandika na ikiwa mtu akitukanwa basi usipost hiyo topic kutokana na standard ulizoweka na sisi tutafata utaratibu huo na mwongozo huo bila kukiuka maadili ya mtandawazi. Ninasema hivi kwa kukusaidia wewe mwenyewe na kuondoa hisia tofauti za watu walizoanza au watakaoanza kukuhisi wewe pamoja na hii serikali ya JK na sasa tunaonana hata familia zako zinavyokueffect kwenye shughuli zako. Wape watu uhuru wao wa kusema ila tuu, tuwe na standard ya acceptable maoni na unacceptable ones.
    Shukrani Mkuu.

    ReplyDelete
  6. Nakubaliana na Anon wa 6:34:37 PM wa hapo juu yangu. Michuzi ndugu yetu watu wengi sana humu kwenye blog yako wanatukaniwa mpaka mabibi na mababu zao lakini hakuna hata siku mmoja ulishawahi kuomba msamaha familia na hao wahusika. Iweje leo kwasababu ni mtoto wa PM ndio uombe msamaha?? Unaona kama hili jambo liko fair?? Unaelewa fika ukitoa picha humu watu wataongea mengi sana na kuna wengi sana sana wametukanawa hata recently kwenye msiba wa ndugu zetu Walter na Vonetha ila hakuna mahali uliomba msamaha. Kuwa fair kwa wote usijali huyu ni mtoto wa PM au huyu ni mtoto wa mtu mwingine, kama unaweka masharati kwenye blog yako basi yafuatwa kisawa sawa kwa wote na sio kwa baadhi. Kwa kifupi sioni nimesikitishwa na msahama uliitoa na umenifanya nikuone kwamba unayumba yumba na hauko imara inawezekana unalinda sembe yako ila kuwa na ubinadamu kwa wote na usawa. Nimesikitika sana.

    ReplyDelete
  7. Bwana Anonymous, you could not write it better than his....let the facts of the matter be spoken.

    ReplyDelete
  8. MICHUZI HII BLOG SASA IMEKUWA NA SIASA NA STORY NYINGI KULIKO PICHA....KUMBUKA PICHA ZAKO NDIO ZIMEFANYA HII BLOG IWE MAARUFU SANA..SIO VINGINEVYO,NAOMBA TURUDI KWENYE PICHA NA STORY ZIWE KIDOGO NA ACHIA WATU WAKOMENT WANAVYOTAKA...UHURU WANANCHI NA SIJUI KWANINI UMEOMBA MSAMAHA? ANATUKANWA BUSH ALL OVER THE INTERNET ITAKUWA HUYO BINT WA LOWASSA...WE DONT EVEN KNOW HER..WATU TUNA HAVE FUN TUU NA HAKUNA WIVU WALA CHUKI HAPO

    ReplyDelete
  9. Thingz Rnt gonna get any better!, leo hii Tony Blairz income is 5th from the top, sasa kuna watu ma manager wanaingiza kuliko yeye ktk gov. companies within. tell me Tanzania kukoje, who earn s more??, LOL. Sioni problem kwa nini kuwe na tatizo hapa. we talked a lot about Blair & co, hakuna problem, leo hii ije kuwa huyo binti!?, tell em 2 get on & live. no criticism no life, thatz it. Ule muda wa kutishana umekwisha, the global is shrinking we all 2gether, she has 2 liver her life. We heard a lot about Royal family, Clinton , Bush etc. Let em learn this world! Aaargh. Big up democracyyy! Jimmy K

    ReplyDelete
  10. Nilivyomuelewa ndugu Michuzi ni kwamba licha ya kuiomba radhi familia ya Mweshimiwa PM kwa yale yaliyotokea pia amewaomba radhi wale wote ambao wamekutwa na matatizo kama hayo kwa maneno yafuatayo,

    NACHUKUA NAFASI HII PIA KUWATAKA RADHI WADAU WENGINE AMBAO NAO WAMEKUMBWA KAMA YA HAWA NDUGU ZETU WAPENDWA. KWA KWELI INAKATISHA TAMAA KUONA JINSI WATANZANIA WANAVYOWAFANYIA WATANZANIA WENZAO, NA WAKIELEZWA JUU YA UBAYA WA UDHAIFU WAO HUO, WANAKUJA JUU. NDO MAANA NAMUWEKA MUNGU MBELE ATUSAIDIE WATANZANIA TUONDOKE HAPA TULIPO NA TUWE NA MAWAZO/MAONI YA MAANA NA UPENDO KWA WATANZANIA WENZETU.

    ReplyDelete
  11. WE MICHUZI ACHA HIZO WAMETUKANWA WANGAPI HAPA LEO KUTUKANWA MTOTO WA LOWASSA NDIO UNAJIFANYA MISAMAHA MINGI. ACHA KUJIGONGA NA WAKUBWA, JUZI ULIWEKA YA MTOTO WA KIKWETE LEO LOWASSA UNADHANI WATAKUFAGILIA KWA BABA ZAO SIO!!

    ReplyDelete
  12. WEWE ANONY HAPO JUU MSHAMBA SANA. UNADHANI MICHUZI ANA SHIDA YA KUFAGILIWA WAKATI KAZI YAKE INAMFAGILIA NA IMEKUWA IKIMFAGILIA HATA KABLA YA WEWE KUJA MJINI NA MWENGE MWAKA JUZI? ACHA HIZO. INAONESHA WEWE NI WALE, KAMA SIO YULE, AMBAYE NI KIRANJA WA MATUSI. WE KAMA UNAPENDA MATUSI BASI JITOKEZE UONA RAHA YAKE, EBO! MICHUZI ACHANA NA WASHAMBA KAMA HAWA. ENDELEZA KAZI, MAANA NASIKIA ULITAKA KUIFUNGA BLOGU HII. WE USIIFUNGE WALA NINI. NAKUSHAURI IFUNGUE NA URUHUSU MEMBA TU KUTOA MAONI, ACHANA NA WASHAMBA KAMA HUYO HAPO JUU. ANAKERA KWERI KKKKHHHHHHHAAAAA

    ReplyDelete
  13. We anonymous unakuwa FALA

    ReplyDelete
  14. Sio siri watu wanapenda kupata habari za watu mashuhuri au waliotoka kwenye familia za jinsi hiyo. Sasa ili kuweza kuwapatia watu habari hizo, mradi sio za kizushi, nashauri ianzishwe blog au website yenye nyepesi nyepesi za namna hiyo. Ndio utandawazi wenyewe huo, mradi isiwe na majungu tu. Wenzetu ughaibuni wanazo, haya ajitolee mtu basi kuianzisha ili hii ya michuzi ibaki kuwa nahsusi kwa picha

    ReplyDelete
  15. MICHUZI UNGEONA JAY LENO NA DAVID LEATHERMAN KILA USIKU BASI UNGEOMBA MSAMAAHA KILA SIKU...MTU UKISHAKUWA KWENYE PUBLIC MEANS YOUR LIFE IS NOT SO PRIVATE ANYMORE. MBONA WANAVYOSEMWA WATOTO WA KICHAKA NA MSAIDIZI WAKE KILA SIKU HAMNA ANAYEOMBA MSAMAAAAAAA. HIYO NI FREEDOM OF SPEECH NA WATU WANAVYOONA. NDUGU YANGU WANASEMA TEMBEA UONE. NADHANI UNATEMBEA KILA SIKU NA UNAONA....KUMBE HUFUNGUI MACHO???

    ReplyDelete
  16. Naheshimu mawazo na utashi wa kila mtu katika kila jambo ili mradi havunji sheria, taratibu na ustaarabu wetu kama watanzania. Lakini cha msingi wachangia waeleze facts ambazo zinaweza kuwa na ushahidi. Japo atatajwa mtu lakini bado itakuwepo issue ambayo public inalazimika kuifahamu, kwa mfano anatajwa mtu, lakini issue ni corruption au anatajwa mtu ambaye anaonekana kuhimiza mema jukwaani lakini nje ya jukwaa hafai, mbovu hawezi hata kuelekeza familia yake nk nk nk. TUKEMEEE KWA SANA TU!!!!

    ReplyDelete
  17. Michuzi usifanye kazi na woga.Huna haja ya kuomba radhi.Wakikuambia ufunge Blog utakubali?

    ReplyDelete
  18. Michuzi,
    Pole sana Kaka lakini mimi nitakua tofauti kidogo na Watoa maoni wengi hapo juu. Kuna anony mmoja hapo juu amsekariribaadhi ya blogu ambazo kwake yeye amesema ni kiboko kwa Malumbano kama hayo. (Katoa mfano wa JAY LENO NA DAVID LEATHERMAN). Mi nadhani tunapotoka tunavozitumia hizi teknolojia na Huu "utandawazi" wetu tunao uita.Sio lazima kila kitu tuige kutoka nje ndo tuwe tumetumia teknolojia vizuri. Tunaweza kutumia teknolojia hizi lakini tukalinda Utamaduni wettu wa Kuheshimiana, Kulumbana kifikra bila kutukanana(Natoa mfano imefikia kipindi ETI hata hawa jamaa wa Bongo fleva nao wanaweka block zao yaahn East coast na West coast na mara nyingine kuiga yale makuzi ya Kigenster kama ya American hip hop. TUNAWEZA KUIGA AU KUADDOPT HAYA MAENDELEO BILA KUHARIBU UTAMADUNI WETU.
    Kublog sio lazima kutukanana kama wewe ulivoona zile za Kimagharibi. Yawezekana kwao ni sahihi lakini si HAPA. si kwa blog hii ya KITANZANIA.

    ReplyDelete
  19. Michuzi,
    Pole sana Kaka lakini mimi nitakua tofauti kidogo na Watoa maoni wengi hapo juu. Kuna anony mmoja hapo juu amsekariribaadhi ya blogu ambazo kwake yeye amesema ni kiboko kwa Malumbano kama hayo. (Katoa mfano wa JAY LENO NA DAVID LEATHERMAN). Mi nadhani tunapotoka tunavozitumia hizi teknolojia na Huu "utandawazi" wetu tunao uita.Sio lazima kila kitu tuige kutoka nje ndo tuwe tumetumia teknolojia vizuri. Tunaweza kutumia teknolojia hizi lakini tukalinda Utamaduni wettu wa Kuheshimiana, Kulumbana kifikra bila kutukanana(Natoa mfano imefikia kipindi ETI hata hawa jamaa wa Bongo fleva nao wanaweka block zao yaahn East coast na West coast na mara nyingine kuiga yale makuzi ya Kigenster kama ya American hip hop. TUNAWEZA KUIGA AU KUADDOPT HAYA MAENDELEO BILA KUHARIBU UTAMADUNI WETU.
    Kublog sio lazima kutukanana kama wewe ulivoona zile za Kimagharibi. Yawezekana kwao ni sahihi lakini si HAPA. si kwa blog hii ya KITANZANIA.

    ReplyDelete
  20. samahani narudi tena kukazia hayo niliyosema hapo juu.
    Hebu tembelea tovuti hii kwa habari zaidi. (TAfadhali kuena makini na Uhuru wa Maoni)


    http://www.sfgate.com/cgi-bin/article.cgi?file=/chronicle/archive/2006/08/03/EDG0RK9T7T1.DTL

    ReplyDelete
  21. We Michuzi ukiomba radhi maana yake umekosa na unastahili adhabu. Basi mlipe huyo uliyemkosea.Nani kakuambia mkonoa mtupu unalambwa?
    Basi acha woga usianzishe blogu kisha unabembeleza kaisari. Na rafiki yako Mzuzuri kaua dereva huko Dar .Tangu Jumapili anakunya kwenye debe.

    ReplyDelete
  22. Tatizo la viongozi wengi waafrika wengi ni wasafi wakiwa mbele ya Public Lakini maisha binafsi ni wa hovyo sana.Ukiwavamia kwenye private life wanasema umewatukana,umevunja sheria uchwara walizojiwekea kujilinda uchafu wao kwenye private life.Kwenye utandawazi huwezi kuficha private life hata ukitaka.Ukikataa zisiandikwe kwenye blog ya michuzi utazikuta kwenye blog ingine au wakitaka kukukomesha wanazituma magazetini au kuzianika kwa wagomvi wako kisiasa au hata kuwapelekea wabunge ili kukumaliza.Watu wanajua mengi kuhusu maisha binafsi ya viongozi iwe mali zao walivyopata n.k Ni vizuri wasiandame wanablog ,wanablog kama walivyo wana mtandao wa CCM wanayo mengi tu na ni nguvu yenye uwezo wa hali ya juu mno duniani sasa hivi.Ni heri kuwa na amani nao kuliko kuwa na ugomvi nao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...