KUNA MDAU KATULETEA PICHA NA HABARI HII. SOMA KWA MAKINI


Kuna kundi la watoto wa pale Majengo, Moshi, kwenye kituo cha watoto yatima cha TUNAHAKI, na bahati wamepata msamaria mwema na wapo ziarani marekani kutafuta wafadhili.

kwenye ziara hii waliweza kuonyesha umahiri wao wa sarakasi kwenye gemu ya basketball (NBA) mapumzikoni wakati L.A Lakers walipopambana na Detroit Pistons tarehe 10/11/06; na siku iliyofuatia kwenda kufunzwa sarakasi za kisasa nakundi maarufu la sarakasi duniani Cirque du Soleil,kwenye shule yao iliopo Las Vegas.

Kabla ya kupata fursa ya kufunzwa sarakasi na magwiji wa Cirque du Soleil watoto hao wenye umri kati ya miaka 10 na 16 waliweza kukutana na wadau mbali mbali toka Tanzania na kupata 'breakfast' kwenye hotel ya stratosphere, ambapo picha hizi zimechukuliwa.

Pia watoto hawa waliweza kukutana na makamu wa rais wa kampuni ya bima ya afya Nevada, ijulikanayo kama Sierra Health Choices na pia kuwa na fundraising kwenye ukumbi ujulikano kama Gymfest siku ya jumapili 12/11/06.

Kama kuna mdau ambaye angependa kujua zaidi juu ya watoto hawa na namna ya kuwasaidia kufikia malengo yao tafadhali tembelea tovuti hizi:

www.tunahaki.com
www.tunahakithefilm.com
http://www.tunahaki.org/

hapo juu kwenye snepu huyo mwenye nyekundu mbele hayupo kwenye msafara wa watoto wa Tunahaki, ila ana mahusiano na mdau aliyetuletea picha hii. dogo yupo katika kujichanganya na dogo wenzake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Shule itakuwaje? Au ndo basi? Kama kusaidiwa ni ktk shule na sitoi pesa zangu kwa wao kucheza sarakasi.

    ReplyDelete
  2. Shule itakuwaje? Au ndo basi? Kama kusaidiwa ni ktk shule na sitoi pesa zangu kwa wao kucheza sarakasi.

    ReplyDelete
  3. Shule itakuwaje? Au ndo basi? Kama kusaidiwa ni ktk shule na sitoi pesa zangu kwa wao kucheza sarakasi.

    ReplyDelete
  4. Nadhani watu wengine ni wepesi wa kukosoa na kuuliza maswali kabla ya kufanya ka-utafiti kidogo. Ukienda kwenye mtandao wa hawa watoto, utaona kuna picha zinazoonesha shughuli mbali mbali wanazofanya hawa watoto,ikiwemo shule.

    I can't imagine how it is to live without a supporting father and a mother, but living without one of my parents around taught me a lesson. So if you are lucky enough to have never lived in poverty or in a socially devastating situation, please be respectful of kids who are trying their best.

    If there were not involved in creative activities, kama sarakasi, they would have just ended up on the streets.

    I am sure they didn't buy their own tickets to the USA, giving the indication that they are under good hands.

    Kutoa ni moyo na ni haki yako binafsi. But a negative spirit is not required for kids who are trying to gain our support.

    ReplyDelete
  5. Ero kamano, Jaduong!

    ReplyDelete
  6. Kweli kabisa Jaduong huyo anon hapo juu sidhani kama anatumia busara au ndio wale wale waropokaji ... jambo usilolijua... ni muhimu kufanya utafiti kidogo kabla ya kuanza kuingilia issues. Sarakasi ni moja ya changamoto na fani pia sio lazima uwe na degree uishi vizuri. Hivyo hao waliowafikisha hapo wanaelewa fika programme zao za kila siku na kama watoto ni nini wanafanya ili na wao wawe na maisha bora badae.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...