Home
Unlabelled
msikiti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Msikiti huu unaenda kwa jina lake na upo karibu na Bwawani Hotel.
ReplyDeleteMsikiti mabuluu (blue Mosque)... pale pembezoni ya Hoteli ya Bwawani, ulijengwa enzi hizo za Sheikh Amaan Abeid Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar, au sio?!. ~MchongomaMwiba~.
ReplyDeleteMichuzi umenirudisha home kabisa huo unaitwa msikiti Mabluu.
ReplyDeleteKAKA MICHUZI WIKI HII UMEBOA KWELI AAAGHH!
ReplyDeleteHuu ni Msikiti wa Buluu wa kisasa uliojengwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dr Salmin Amour mwaka 1996 katika jitihada zake za kurejesha na kuenzi historia ya Zanzibar. Hapo kale katika karne za nyuma kulikuwa na Msikiti Mabuluu wenyewe wa asili uliokuwa ukitumiwa sana na wenye merikebu za pepo za siku hizo za kusi na kaskazi. Wakiingia hapo na merikebu zao na kutia nanga na kusali kila wakifika na kuondoka. Msikiti Mabuluu wa asili ulipotea kabisa na umri na kuzeeka pamoja na shughuli za ujenzi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar za miaka ya 1960 na 1970. Dr. Salmin aliamua kukusanya kumbukumbu za msikiti huo na hatimaye kuurejesha upya kwa asilimia kubwa.
ReplyDeleteMichuzi kuwa makini sana na masuala ya imani za kidini, utazua vita humu na wewe ukakufuru pia, utaachiaje maoni negative?
ReplyDeletemdau hapo juu asante kwa ujumbe. ila nashindwa kuelewa ulichosema. labda unifafanulie ni maoni yapi negativu niliyoachia?
ReplyDeleteMsikiti wa Mabluu, nimefenay baadhi ya swala hapa. Huu msikiti una mvuto mkubwa sana. Unaleta hisia chanya kwa vile ni wa kipekee kujengwa katika madhari kama hii, ya kuelea baharini. Mimi sioni utata kuweka picha kama hii na kuomba maoni ya wasomaji. Sijui kwa nini kila jambo liwe la tahadhari kubwa? Nadhani mhusika angefafanua zaidi...
ReplyDelete