mh. benjamin william mkapa rais wa awamu ya tatu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Kafanikiwa on major economic fundamentals ila the guy was not sensitive on hisia za wananchi. Never made any efforts to tajirisha wazawa na kuwa bize kuwauzia makampuni wageni. Huyu kama Dick Cheney, hajali hisia za wananchi na hajali kuuza idea zake ili zikubalike.Wakulima ndio kabisa aliwasahau na kubaki kuwakumbatia wawekezaji, kununua ma dege na ma rada!!!

    ReplyDelete
  2. Mzee wa Utandawazi au mzee wa uwazi na ukweli

    ReplyDelete
  3. Mkapa alikuwa na kibri na alijifanya too much know. angeendelea na uongozi basi angeweza kuwa dikteta wa demokrasia. Aliwafungia HAki Elimu baada ya kuona namna kweli inavyouma.
    Mkapa aliwapa kibri viongozi wa Zanzibar na kufanya watakavyo. Mkapa alipeleka majeshi na polisi Zanzibar kudhibiti wapinzani ili wasifurukute.
    Vifo vilivyotokea Pemba mwaka 2001 vilitokea kwenye mamlaka yake. Kwahiyo ana damu mikononi mwake. Hakughasika hata kidogo kutokana na vifo na mateso waliyoyapata watu wasio na hatia.
    Japokuwa hivi sasa anajifanya mcha Mungu sana lakini damu iliyomwagika Pemba wakati wa utawala wake atakwenda kuulizwa mbele ya Hakimu wa Haki.

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  6. alikuwa mkweli sana kama ujuavyo nabii haheshimiki kwake lakini jamaa alikuwa anapiga sana mzigo

    ReplyDelete
  7. Mkapa yeye ndiye ambaye ametufanya kuonekana watu katika Dunia ya leo. Amefanya Mengi. Amerithi Mfumko wa Bei kutoka 48% na akaudhibiti mpaka 4%. alirudisha heshima iliyokuwa imepotea serikali ya kila mtu kujiamulia mambo. alionekana ni dikteta kwa kuwa watu mlishazoe kubembelezwa kufanya kazi.

    Watanzania wamezoea kulalamika serikali serikali haitufanyii hili wala lile.
    Alihakikisha kwamba Muafaka kati ya CUF na CCM unarudishwa ambayo ni matokeo ya wazanzibari wenyewe kujichanganya kwa kupenda madaraka kuliko utu. Pia muafaka haukufanikiwa kwa sababu ya wanzanzibar wameweka maslahi yao mbele ya taifa lao,

    Mkapa aliweka mazingira bora ya uwekezaji, na watanzania walishindwa kuchangamkia tenda. Mnabaki kusema kwamba jamaa kauza nchi. alipokuwa anauza nyie mlikuwa wapi? Mbona hamsemi jinsi Mwinyi alivyouza sehemu yetu ya wamasai kule Loliondo?

    Kwangu mie Mkapa ni nambari wani katika Marais Wote, labda akifutiwa JK, akifatiwa na Mwl na mwisho kabisa ni Mwinyi...mie hata sikumbuki alichofanya.

    ReplyDelete
  8. Mkapa aliongoza nchi ikia kwenye kipindi kizuri kuliko wenzake. Lakini aliongeza rushwa zaidi. Wasomi walikuwa wengi zaidi na uelewa wa watu kwa ujumla ulikuwa umeongezeka. Lakini hakutumia mwanya huo kwa manufaa ya wananchi. Hata kiburi chake kilikuwa kimezidi saaana. Hakuchukua ushauri wa wenzake. Angekuwa makini na mwangalifu, angeheshimika zaidi ya anavyoheshimika sasa. Kipindi chake watu walipenda rushwa zaidi. Rushwa imeongezeka kwa sababu hatukuona akiikemea

    ReplyDelete
  9. Kaiuza Tanzania kwa so the called Wawezekaji, mimi huwaita wachukuaji maana sioni Watanzania wengi waliobenefit na sera za uwekezaji ukiondoa wachache sana ambao hawafiki hata 10,000.

    Kajilimbikizia mali na wale walio karibu naye.

    Katika miaka 10 aliyokaa madarakani ameshindwa kuongeza uzalishaji wa umeme, kuboresha maisha ya Watanzania na kuinua kiwango cha elimu kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari.

    Ameingiza Tanzania kwenye mkenge katika mikataba ya uchimbaji wa madini. Kwa kifupi ameiacha Tanzania pabaya kuliko alivyoikuta. Kamwe hakustahili kuwa Kiongozi wa Watanzania.

    ReplyDelete
  10. Kama idadi ya maoni ingekuwa ni kura ,hiyo ni reflection ya jinsi watanzania wanavyo rate carisma za viongozi hao wa serekali zilizopita !

    ReplyDelete
  11. Nampongeza sana kwa maamuzi yake ya kuacha "kubabysit" watanzania.

    ReplyDelete
  12. MAZURI
    1) uchumi-(kwenye makaratasi)
    2) uwekezaji
    3) alirudihsa heshima na umuhimu wa kwenda shule-kwa kuongeza mishahara ya wasomi
    5)sio mwizi

    MABAYA
    1)mbishi/kichwa ngumu-wananchi wa kawaida wanaweza kuona hakuwajali

    ReplyDelete
  13. BWM anastahili heshima kubwa kutoka kwa watz walioko nje ya nchi na ndani ya Tz,kuliko hivyo sasa kila mtu anamponda wengine wanamuita mzee wa Rada,mara ndege ya Rais!!! nchi hii ukiwaambia watu ukweli utachukiwa sana,utaambiwa una kiburi,unajidai,unadharau wanyonge n.k bado tulio wengi tuna mawazo ya enzi zile za ujamaa na kujitegemea,wakati mambo hayo yalizikwa kule zenji,kwenye azimio la zanzibar!!!! BMW alikuwa msema kweli na alikuwa na mapungufu yake kama alivyo mwanadamu yeyote.Amerudishia heshima nchi iliyokuwa imetoweka,misheni tangu wakapungua kwa kazi kwa ofisi zao za mifukoni!!wanasiasa uchwara akawapasha ukweli wao!!! Kuna PM mstaafu aliwaambia watz "kila mtu atabeba mzigo wake" watz wakapiga kelele sana kuwa wamedharauliwa!! sasa imekuwaje baada ya hapo si kila mtu na maisha yake???? au alisema uongo
    Tuache ushabiki!!! tupiganie mambo ya msingi ya nchi yetu,la sivyo hili kundi ya " wapambe" wa waheshimiwa litaendelea kukua kwa kasi ya ajabu
    MUNGU IBARIKI TZ

    ReplyDelete
  14. hUYU NDIO KICHWA CHA NCHI,HAKUNA RAIS KAMA HUYU,ENZI ZA NYERERE WANASIASA WALIKUWA KAMA MIUNGU INGAWA NDIO WALIHARIBU NCHI,ENZI ZA MWINYI WASANII NA MATAPELI NDIO WALIKUWA NYOTA LAKINI WATANZANIA WENGI WALISOTA KAMA VILE WAFANYAKAZI KUKOSA MISHAHARA. hUYU BWM AMEWEZA KUONYESHA KUWA HAKUNA SHORT-CUT KWENYE LIFE,JUST WORK HARD NA NENDA SHULE

    ReplyDelete
  15. Mkapa is a great man. As a student in Economics and Bussiness what I can say Mkapa raised the GDP of Tanzania economy, you have to be proud of him, you better off today in Economy because of him. I know many people have been talking about Globalization, people, people, you have to understand that your living in Global world now, you cannot escape that. I lived in your country for 3 years it was the time of Mwinyi president, many people said that Mwinyi was great, because many people had everything they needed, but what about your economy? remember when Mwinyi was a president Tanzania was one of the poorest country after Sudan, and now your better than Uganda and even Ethiopia,

    ReplyDelete
  16. Nyerere katuunganisha Watanzania kwa kuona umuhimu wa kuwa na lugha moja, leo hii tunajivunia umoja wetu. Sidhani kama huyu angweza kutuunganisha kwa kuwa aliwapa kipaumbele wazungu na wale walio karibu naye.

    Nyerere baada ya kujitawala aliona umuhimu wa kuwa na viongozi wa Kitanzania katika sehemu mbali mbali za mashirika yetu na mawizara yetu. Hivyo akaona umuhimu wa kila Mtanzania bila kujali uwezo wa wazazi wake, apate elimu ya uhakika ili mradi ana unwezo wa kucharika na vitabu. Leo tunaona matunda ya sera za mwalimu siyo Tanzania tu bali ulimwengini kote utawakuta wabongo ambao hawaoni aibu kutamka kwamba elimu zao ni matunda ya sera za Baba wa Taifa, vinginevyo wasingeweza kwenda shule maana wazazi wao walikuwa hawana uwezo.

    Jamaa mmoja kaandika Mkapa aliacha kuwababy sit wabongo, je sera hiyo iliwasaidia nini Watanzania? Kiongozi ni lazima unyanyue kiwango cha maisha ya wale unawaongoza kielimu, kimapato, kilimo cha mazao ya biashara na chakula n.k. Nyerere aliliweza hili ingawaje matatizo ya mafua duniani mwaka 1973/74, ukame wa 1974/75 na vita dhidi ya nduli vilimrudisha nyuma. Lakini siku zote alitoa kipaumbele katika kujenga maisha bora kwa Watanzania wote bila kujali rangi, dini au uwezo.

    Hili Mkapa hakulifanya na sidhani kama kuna chochote ambacho Watanzania wanaweza kupinpoint kwamba kiliwanufaisha kutokana na sera za Mkapa, Lakini Nyerere ni miaka 22 tangu ang'atuke lakini matunda yake bado yanang'ara siyo Tanzania tu bali uliwenguni kote. Mkapa kamaliza awamu yake less than 18 months ago, nenda nchi yoyote kama wanamkumbuka au wanajua hata kama alikuwa kiongozi Wa Tanzania, lakini Nyerere bado anakumbukwa si Tanzania tu bali nchi nyingi za Afrika, Asia na ulaya mashariki na magharibi na hata North America. Kwa kifupi Nyerere alikuwa ni kiongozi wa watu ambapo hata siku moja hakuwabeza Watanzania na siku zote alisema ukweli bila kuogopa, lakini Mkapa alikuwa ni kiongozi aliyejali maslahi yake na wale walio karibu naye na wachukuaji (yeye anawaita wawekezaji}

    Rest in peace Mwalimu.

    ReplyDelete
  17. Huyu bwana BWM alifanya vizuri miaka mitano ya mwanzo baada ya hapo na mwalimu kufa akaanza jifanyia kama chama chake yaani Chukua Chako Mapema(CCM) kwani aliwamilikisha Tanesco shemeji zake kwa kutumia FFU na aliona matatizo ya umeme,wakatumia maji yote kupata kamisheni kubwa na kumpa JK mtihani wa nchi isiyo na power,laiti kama sio JK kutoka Bagamoyo ingechukua miaka kujaza Mtera,Huyu bwana BWM mkewe kajilimikizia mali nyingi sana,zaidi hata ya mama Siti

    ReplyDelete
  18. Napenda kusema kuwa duniani hakuna mtu atafanikiwa kila idara katika maisha.Jamabo la msingi ni kujenga juu ya msingi imara wa mazuri ya yaliyojengwa na kuyaendeleza.Tunarudi kuangalia mabaya pale ambapo tunahitaji kurekebisha jambo.Marais wote waliopita walileta neema katika upande mmoja na kuharibu katika sehemu nyingine.Lakini tukumbuke huyu ndo yule binadamu ambaye njia zake siku zote ni matatizo.Hawezi kufanya jambo bila kosa.hata wewe ungelipewa urais ungefanya mazuri na ungelifanya makosa.

    kati ya mambo mimi ninayochukia ni pale wasomi wanapotumia elimu kuila nchi na kuimaliza.Elimu ni nzuri ikitumika vizuri lakini elimu ikitumika kuiibia nchi hii ni hatari.

    ReplyDelete
  19. Benjamin Mkapa is probably the best leader east africa has ever had. Aliingia madarakani wakati nchi ikiwa katika hali mbaya kiuchumi, na kijamii. Mashirika ya fedha ya kimataifa yote yalikuwa yame acha kufanya biashara na serikali, infact serikali ilikuwa imefilisika. Utawala wa sheria ulikua dhaifu, mfumuko wa bei ulikua mkubwa , huduma za jamii zilikuwa hoi, mashirika ya umma yalikuwa yamesambaratika, na mbaya zaidi serikali ilikua inashindwa kukusanya kodi.

    Mkapa a technocrat had two choices. One kufuatilia na kuwa adhibu watu waliokuwa wana hujumu uchumi kupitia rushwa, kusamehe kodi na matumizi mabaya ya fedha za umma, kupitia judicial system ambayo ilikuwa corrupt and almost non existant. Matokeo yake angeweza kuonenkana dikteta kwa kuwaweka watu ndani ovyo, bila ushaidi wa kueleweka angeshindwa kutawala kwasababu hata nguvu yake kisiasa ilikuwa ndogo mno. Kingetokea yaliyotekea malawi na zambia, badala ya kutawala nakufocus kwenye pressing issues muda unatumika in endless political wrangles, for sure at that time ccm ingekufa, hasa kwasababu watuhumiwa wakubwa walikuwa na nguvu kubwa kisiasa, maengo ya mzee benja yasingefikiwa.

    Au mzee wetu ange concentrate on bringing the econmic back on its foot, kukusanya kodi, kulipa madeni, ku re structure idara ya mahakama, and overhaul the judical process, control inflation and ulitimatly bring back economic stability. Huyu mzee alikua technocract hasa, na kusimama kwake kidete ndo kumeweza kututoa katika hali yetu huku nyuma amabayo it was hopeless , it is because of him that now at least tanzania has hope.

    For one, he made a good decison though it wasnt the best, maamuzi yake ndo yametuwezesha kufika tulipo leo. Sidhani kama kuna kiongozi kama yeye in the past 20 years, labda museveni lakini museveni ameshindwa kujizuia na tamaa ya madaraka, kama mkapa angepata muda zaidi in ten years I believe tungefikia double digit growth rate in the economy, ila kikwete anaelekea huko thanks to mkapa.

    ReplyDelete
  20. I do like the guy and everything but am really concerned about his healthy,anakula tuuuuuuuuuu,kufanya mazoezi kwake mwiko?

    ReplyDelete
  21. Kaka Michu,
    Nashukuru sana kwa topick hii nzuri. Nina sekunde chache tu kabla ya mstari mfu... hivyo nitatoa maoni ya wote kwa pamoja nikianza na bwj
    Huyu jamaa kichwa kiko fiti kwa kweli. Alipambana sana na kuweka sera imara na kurudisha heshima ya nchi. Kwa kufanya hivyo ikawa vigumu kuwapendeza wote. Aliharibu kwenye utawala wa sheria. Kakumbatia Mapuri weeee mpaka ikawa aibu katika jumuia ya kimataifa. Waziri wa mambo ya ndani kuwa active CCM player asiyejua ku strike balance ilimharibia sana huyu jamaa yetu. Hata JK inamwia vigumu kutatua migogoro zenji kwa kuwa bwm ali halalisha kila kitu.

    Mzee Mwinyi sina cha kuongeza, wadau wamesema mengi. JK anahitaji kufanya kazi ya ziada kuboresha maisha ya watanzania. Kwa sasa hali haiendani na kauli mbiu. Maisha kwa ujumla ni magumu sana na wawekezaji wana zidi kuwanyanyasa wazawa. Akhsante.

    ReplyDelete
  22. Mkapa alijenga Tanzania lakini akawatupa na kuwadharau Watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...