mh. jakaya mrisho kikwete rais wa awamu ya nne

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. aaaaaaaaaaaaaaaaaaaah!brazameni,mzee wa tripu,yanga africa kwa sana,hongera zake kwa kutekeleza ilani ya CCM kuhusu michezo ila halahala hizo tripu wadau wemeanza kuzishikia bango

    ReplyDelete
  2. mmmm,huyo ni bwana msafiri hakai nyumbani na kuwatemebelea hao anaosema wamempa kura hatimaye yeyena nje ya nchi laa balaah kama antaka akae nje ya nchi na kuwa rahisi kwanini asimtume bwana mdogo lowassa huko nje au watumie simu kwenye mikutano badala ya kwenda na kuhifadhi hizo hela za kodi za masikini

    ReplyDelete
  3. mzee wa kasi mpya na nguvu ya soda. Maneno mengi tu hakuna policy making zozote. Kutwa kuomba misaada.

    ReplyDelete
  4. Yaani huyu jamaa kakaa ki bishoo bishoo! kama mcheza sinema vile! purukushani nyiiiingi, lakini matokeo hatuyaoni. janja hili!

    ReplyDelete
  5. huyu bwana kwa misifa! kazi kwelikweli!

    ReplyDelete
  6. Jamaa ni safari na yeye kasahau kuwa anatakiwa akae na kubuni mipango imara.Ni kweli misaada tu ndio suluhisho la matatizo yetu inashangaza.Jamaa yeye anawa win tu wale watu wa uswazi ambao ndio walimchagua.Hao ndio wakisikia anawaleta Real Madrid wanamfurahia sana,hapa anawakuna.
    Lakini hajafanya lolote kwa uchumi mkuu.
    Pia hata miradi yote inayotekelezwa ni matunda ya Benny jamaa yeye bado anapaa sijui kama hangekuwa Waziri wa mambo ya nye ingekuwaje.
    Pia ananitia wasiwasi na uhusiano wake na wanahabari inaelekea anapenda sana kusifiwa japokuwa nadai hapendi lakini ninawasiwasi.
    NAONA BADO HATUKUMTARAJIA KUFANYA HAYA TUNAYOYAONA.
    Pia hata maisha yamekuwa magumu kila kunvyokucha kunanini hapa Je amafeli
    UTAONA PIA MAAMUZI YAKE MENGI NI YA KUWA WIN WATU
    TUSUBIRI

    ReplyDelete
  7. Huyu Jamaa ni MTALII, kila kukicha ni TRIPU....
    Policy ambazo zitahakikisha hayo Maisha Bora sijaziona bado...

    ReplyDelete
  8. WACHUMI NISAIDIENI SIELEWI MBONA....!!?
    MIMI SIYO MCHUMI LAKINI NASHINDWA KUELEWA MTU MWENYE AKILI TIMAMU MSOMI ANAWEZAJE KUKUBALI MASHARTI YA REAL MADRID YA KUKODIWA NDEGE two WAY SPAIN DAR, DAR SPAIN HALAFU ANAAMBIWA ALIPE MISHAHARA YA TIMU YA WEEK MOJA AMBAYO NI KATI YA POUND MIL.50 HADI POUND MIL.100 AKAKUBALI? WADAU WENZANGU HATA KAMA NIKUITANGAZA NCHI HII GHARAMA NI NYINGI MNO BADO WANATAKA WAFIKIE 5 STAR HOTEL? UJIO NIWA WATU 80? WALIMU HAWALIPWI MISHAHARA, DARAJA LA KIGAMBONI IMEBAKIA NI MYSTERY,ELIMU IMEPANDA,MISHAHARA KIDUCHU, SASA WACHUMI MNAONA HII NI GOOD MOVE YA KASI MPYA? HAWA WATU WANAKUJA KUCHEZA DAKIKA 90 HICHO KIINGILIO HAKITA FIKISHA HIZO ZAIDI YA POUND MILIONI 100 TUTAZIRUDISHA VIPI? MIMI NAONA HII NI MISIFA TU YA KIONGOZI WETU, MKAPA KAKUSANYA MIHELA TELE JAMAA ANA TUMBUA!

    ReplyDelete
  9. mpaka miaka 10 iishe atakuwa ameiweka tanzania kwenye madeni makubwa saaaaannaaaa, mikopo ndugu zangu wa amerika wabongo simnaijua issue yake na interest kibao? jamaa kila msaada anaukubali na masharti yake anayakubali hata kama ni magumu kama ya real madrid hii ni aibu hata kwa anaye kupa msaada. utakuwaje unashinda unasafiri hata kama unaomba omba mbona maraisi wengine siyo omba omba kama wetu, nakuanza kushtaki maraisi wengine kwa bush?

    ReplyDelete
  10. msanii nambari wani bongo.

    ReplyDelete
  11. Huyu msafiri kafika na cheap popularity. Kusafiri kwa kisingizio cha kuomba misaada, jana Norway kakosa cha kuomba kaanza kusingizia wataalamu wa kibongo eti kutoelewa ndo maana wanaingia mikataba kibwegebwege. Hapa bwanaa kakosa cha kusema sababu mikataba mingi siasa ndo inatawala zaidi ya utaalamu. Rejea IPTL, katibu wa wizara alikataa, lakini hao wenyewe wanasiasa wakaweka mikwara na kupitisha sababu walishapata 10 percent. Asituzuge, Tz kuna wataalamu wengi wazuri tu, lakini siasa inawekwa mbele.

    Yaani katalii, na kukosa cha kusema kaanza kuomba eti tupewe wataalamu watusaidie kwenye mikataba, huo ni uwongo mtupu. Na hii Rais mzima anajishushia hadhi yake kwani kudharau wataalamu wa kitz ndo maana tunaletewa wataalamu wa ovyo kama wezi wa TTCL na Tanesco. Shame shame shame kama huna cha kuomba rudi home ukapambane na majanga ya kitaifa-- Leo m-treni wako umeua watu kibao wewe unatangatanga.

    LAkini wajinga ni watz waliokupa kura nyingi kumbe ni mtalii.

    ReplyDelete
  12. Tusi panic na safari zake he is just taking contact mwaka mmoja on business it is too early to say something kuongoza nchi si rahisi. He sounds promising, young, active and simple (like all tanzanias)
    I have confedience he will do good work maana kitu kimoja anapenda wananchi. Tukutane hapa after three yrs ya uongozi wake then we can say something.

    Mungu ibariki Tanzania, Viongozi na hasa Watu wake!
    Aurely

    ReplyDelete
  13. Kukujibu shwali lako wewe ambaye umeuliza kuhusu Real Madrid ni kwamba, JK hakufanya maamuzi hayi kichwa kichwa. HAwa watu wa nchi ambako hii timu inatoka wanakuja kwa kiasi kidogo sana kwenye mbuga zetu hapa bongo au hata kutembelea maeneo mengine ya utalii.

    Ukumbuke pia kwamba watalii wako wa aina nyingi sana. Kuna watalii wanaitwa VISHUKA. Hawa huwa wanakuja na mabegi makubwa sana na wanataka kulala kwenye guuest house za kawaida na kula ugali. HAwa mchango wao huwa ni mdogo sana kwenye utalii. Wengi wa hawa ni Wataliano na baadhi ya Waingereza.

    Pia kuna watalii wanaitwa BIG PACKERS. Wenyewe wanakuja kukaa kwenye hotel kubvwa kubwa na kulipa ma-fedha kibao. Pia wanunuzi wazuri wa vitu vya kibango. Hawa ni kama wale wa US, UK, Scandinavia, Germany, Spain and Japan. Kwa TZ hatupati watu wa Spain kwa wingi.

    Ujio wa Real Madrid ni moja ya mikakati ya kuufanya utalii Tanzania uchangie asilimia kuwa ya kipato cha taifa. Kwa sababu ni majina makubwa, hawa jamaa watatangazwa kila kona ya Dunia kuwa wamekuja bongo na picha zao zitaonekana kwenye websites zao pia za club ambazo watu wengi wanazitembelea.

    Ukijumlisha, utana kuwa mapato yatazidi mara kadhaa hiyo gharama ya kuwaleta hapa nchini. Biashara ni matangazo. Sisi tulilala sana na ndo muda wa kuamka sasa.


    Nadhani umeelewa.

    ReplyDelete
  14. Anajitahidi kuvutia wawekezaji toka nchi nyingine.Lakini ni vizuri akakaa na wataalamu na ahimize wananchi na wataalamu wajadili na waangalie ni jinsi gani watanzania nao wanaweza kuwa wawekezaji kwenye mataifa mengine pia.It should not only be a one way traffic ambapo wawekezaji toka nchi zingine tu ndio wanaalikwa bila wa kwetu kutafutiwa namna ya kuwa wawekezaji kwenye mataifa mengine.Tunaweza hamasisha watu wetu kuwa wawekezaji mfano hata katika nchi kama Msumbiji,Zambia,malawi,Zimbabwe,n.k kwa kuanzia.Hili ni juu ya raisi na wataalamu wake kukuna vichwa kuona lifanyikeje.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  15. wadau wa nchi,
    this is very crazy tena balaa, how can we spend that much kwa hao real madrid, its true we re going to make them know of all that we have but jamani tuna shida nyingi mno kujiingiza kwenye ushenzi kama huo. hizo simple interests za mtu mmoja jamani hazifai imagine wanafunzi hawajui watapata wapi 40% ya elimu yao ya juu halafu we re paying for 80 pax for just a tourist trip this is crzy eti walale kempinzki na mashaku shaku kibao mie naogopa kama kuna kasi mpya ... hii ni dalili tosha ya kasi sana kwa mambo yasiyo na msingi, ari kwa yasiyo na maendeleo na nguvu ya kufaidisha wachache, jakaya should take things serious, but anyway nitasema sitamaliza the world is for the benefits of the ruling class ....thats it. inauma saaaana!

    ReplyDelete
  16. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  17. Anon wengine bwana,issue zote hizi wanakalia Real Madrid tu.Kwani mmeambiwa hela zote wanalipa serikali?Hata hao Siemens wamejitokeza kudhamini part ya gharama.au unafikiri siemens hawataki kujitangaza Africa?Isitoshe angalia na upande wa pili wa hii ziara,Sidhani hata kama unajua hao watu 80 ina include na wakina nani,we makelele tu.Wewe unafikiri kuitangaza nchi duniani ni mpaka upeleke tangazo CNN tu?
    Chukua mfano,Mali miaka ya mwisho ya Tisini waliandaa African cup of Nations,unadhani Mali ni tajiri sana,au hujui hata viwanja vingine walijengewa na S.Africa?Nia yao ilikuwa ni kuitangaza nchi na kuinua ari ya vijana ktk soka,hivyo kufungua ajira za nje kwa wachezaji wao.Au hujaona wachezaji wangapi wa Mali wamepata timu Europe baada ya kuandaa mashindano yale?
    Eti mimi sio mchumi,kwani mpaka uwe mchumi ndio uangalie vitu kwa sides zote halafu upime?KMB

    ReplyDelete
  18. Huyu JK kwa kweli hakuna kitu. No hope. Nchi itabaki pabaya kuliko awamu zote. Kwa sababu hana data na mawaziri wake kedekede hakuna hata mmoja anayesikika akifanya kazi ya uhakiki. Huyu mtu alituahidi mengi kiujanjaujanja tu:
    1. Mapinduzi ya kilimo halafu anampa kazi Mungai?
    2. Maisha bora kwa kila mtanzania-umaskini wazidi kila siku hasa mfumuko wa bei na kushuka thamani kwa DAFU zetu
    3. Ajira milioni moja - bila interviews, walimu waandaliwa kisiasa UPE warudi kwa kasi, nguvu na ari mpya.
    4.Mikataba mibovu ya uwekezaji imemshinda kuifanyia marekebisho- ubabaishaji wa Richmond na TTCL mapema kabisa.
    5.Aliahidi upendeleo maalum kwa mikoa iliyoduni- Hakuna kinachofanyika Rukwa hakupitiki huko.
    6.Aliahidi kutoa maamuzi mazito Machi mwaka jana kumbe mazingira na hakuna kinachofanyika. RAMBO ziko mtaani kibao tu.
    7.Aliahidi kutatua migogoro ya ARDHI- Hakuna kitu
    8. PM wake alisema atakagua maghorofa nchi nzima- Hakuna kitu
    9.Aliwashikilia kwa muda magwiji wa UJAMBAZI na hatujui waliachiwa vipi?
    10. Ni Kweli Babu SEYA na wanawe walibaka kwa kushirikiana? Siamini-hajamsamehe

    R.I.P TZ!

    ReplyDelete
  19. Sidhani kama tunahitaji miaka kumi kujua ya kuwa nchi yetu inaelekea pabaya ! JK alianza kazi kwa sifa kwa kukimbilia kila wizara na kuwaaimbia wafanye nini hili likuwa katika lengo tuu la kujitakia sifa . Haikuishia hapo akaenda Tanesco na kamera za TV mbali mbali na kuwaambia wasipandishe bei ,wenye akili tukaona mwisho wetu umefika kwani tunajua ya kuwa ni soko na gharama za uzalishaji ndizo zinazopanga bei bei za bidhaa .Nini kilitokea baada ya miezi nane bei ya umeme ilipanda na hakuwa na lakusema.

    Swala lingine ni suala la Richmond , hili sula limexpose kikwete vibaya sana . Mbali ya kuwa mpaka leo hatuna majibu sahihi kuhusu ni nini hasa kilichotokea lakini tunajua jambo moja RUSHWA ilitembea. Kampuni hii ilishindwa kuzalisha umeme katika muda uliokusudiwa mpaka mvua zilipotunusuru !

    ReplyDelete
  20. -JK punguza safari unakosa mengi nyumbani ambayo ungeweza kusaidia
    -Nchi inakufa kwa rushwa
    -hatuoni any major policy making ya kutuondolea umaskini mpaka sasa
    -nina wasiwasi kama una chochote kwa wanannchi maana ni mwaka sasa lakini ni story tuu... hayo mambo ya kupanga bei za Tanesco au kujidai kutoa mikopo kila mkoa, kwa wajanja tunajua that is just BS na hakuna kitu kitafanikiwa hapo ila ni kutafuta umaarufu tuu...this guy better be serious kupigana na rushwa na kujenga miundo mbinu

    ReplyDelete
  21. Nimesoma maoni hapo juu, kaaazi kwili kwili. Nimedokezwa na watu wengi huko TZ wamepigiwa simu wawe mashushu? Ina maanaa mambo ya Nyerere yamerudi tena. Kaazi Kwili kwili.

    ReplyDelete
  22. Real Madrid watalii gani wanataka kuja kwa masharti? Hao mastaa hata insurance haiwaruhusu kucheza huku maana season imekwisha

    ReplyDelete
  23. Safari za huyu bwana naziunga mkono saaana tena saana. Kusema kweli kaanza vizuri JK. Safari ya real madrid pia naiunga mkono saaaaana tena mara elufu kumi. Kama mnajua Kenya iko mbele kwa sababu ya kujitangaza. Tanzania tunatumia less than 5 % ya hela ambayo Kenya inatumia kujitangaza. Kwa hiyo safari ya real madrid ina faida sana si kwa michezo lakini pia kwa kujitangaza. Real madrid ni timu kubwa. Na pale Real kuna wachezaji kibao hata hawajui kama kuna nchi inaitwa Tanzania, huenda Kenya wanaifahamu.
    JK kaanza vizuri. Mpaka sasa sijaona kosa lake kubwa zaidi ya lile la kutoweza kukaa kimia kwa masuala asiyotakiwa kuongelea. Kama la nightmaire asingeongelea kabisaaaa. Angekaa kimya kabisaaa.

    ReplyDelete
  24. Unajua nini ndugu zangu,kila kitu kinahitaji mmuda ili ukitolee maamuzi.
    Rais wetu hafanyi kosa kutembelea nchi mbali mbali kwani tutajitangaza vipi na asikudandanye mtu kwamba kuna nchi haswa Afrika inayojitegemea kwa uchumi,hakuna. Ila sema akisafiri huwa anaandamana na watu wengi sana kwa ajili ya ulinzi hali inayosababisha kutumika kwa kiasi kikubwa cha pesa.Inatisha sana kwa kweli.
    Akienda na Mkewe naye anahitaji wa kuwa nao karibu na hakuna kupingwa. Ukiyachambua sana mambo unaweza kulia kwani ni balaa kwenye suala la matumizi. Wakati wengine wanatanua huku wengine tunaendelea kudumaa kiuchumi hasa wa kifamilia.
    Hata huko serikalini wafanyakazi wake wenyewe wanalipwa vimshahara hata kati kati ya mwezi havifiki,halafu ndio sera eti!!!!!lol. Itafikia wakati Tanzania itakuwa haitoshi jamani,maana mabo mengine sio kwamba hatuyaoni na sio kwamba hayatuumizi ila tumeamua kukaa kimya kwanza tukisikilizia zali. Ila siku ya kuibuka ni moja tu halafu kitaeleweka.
    Haya bwana aliye juu mngoje chini maana baada ya kufilisika ndio tutajua wapi pa kuegemea.

    ReplyDelete
  25. Jamani Wabongo wenzangu najua kuna watu mna machungu, lakini yahusu nini kumjaji Jakaya Kikwete wakati ndio kwanza ana kamwaka??? Wazungu wanasema "The Jury is still out ".... bwana Michuzi usingemuweka Jk kwenye Ligi moja na Viongozi waliomaliza muda wao, bado mchanga wee unafikiri Urais mchezo si lelemama, baba wa watu uzuri woote unamuisha ..........Lets give him time. Ila kweli huo msafara wa Rais noooma .....!!!!!!

    ReplyDelete
  26. inaonekana wote mliotoa mawazo hapo juu mnakaa nje ya nchi-hamjaenda nyumbani hivi karibuni. JK ni kipenzi cha wananchi bwana,
    mazuri yake ni haya
    1) amerudisha swala la utaifa "symbolism" mie nafikiri hiki ni kitu kizuri
    2)amejua kuwa nchi haiwezi kuendelea bila "biashara". Huwezi kuuza bidhaa bila kujitangaza-ndio maana anafanya hizo safari. Wote mnaopinga safari za JK-bado mnaishi katika enzi za Nyerere, mnataka kupata pesa bila kuweka mtaji (investement)! Biashara sio lelemama!!!!!!Hivi wabongo mtajua lini juu ya haya maswala??
    3)Nchi nyingi duniani kwa sasa zinataka kuacha maswala ya kutoa misaada (aid), badala yake zinataka kufanya biashara kama njia ya kusaidia nchi inazoendelea kama Tanzania.

    MABAYA
    1) Elimu inazidi kudidimia sioni kama JK anafanya juhudi kukomboa elimu-mie nashauri sambaba na shule za kulipia shule za serikali nazo zipewe vitendea kazi.

    KWA UFUPI MIE NAFIKIRI SIO VYEMA KUWALINGANISHA HAWA MARAISI-KILA MMOJA AMESAIDIA KUIFIKIKISHA NCHI YETU HAPA ILIPO. LAZIMA TUJIVUNIE KUWA NA MARAISI WANNE WASTAAFU-SIDHANI KAMA KUNA NCHI NYINGINE YA AFRICA AMBAYO INA HISTORIA YA NAMNA HII.
    MUNGU IBARIKIA BONGO !

    ReplyDelete
  27. Anajitahidi sana.Gharama za kusaka vitu vizuri ni kubwa.Huwezi zuia gharama za safari.

    Anachotakiwa ni kusaidiwa sasa na watanzania walioko nje na wasomi kujenga jina la Tanzania na uchumi wake.Watu mlioko nje ya nchi Kusema tu nyumbani kuchafu hakuna maji,safi,hakuna ajira,n.k hakusaidii kitu huko nje ya watawacheka kama mtaendelea kuzungumzia hilo.

    Watanzania tunahitaji "Solution providers" na siyo "Proffessors wajuaao kuelezea matatizo ya Tanzania kwa undani,na uchungu na data juu za ku-support wanachosema" au "maprofessa wa kuuliza maswali magumu ya kusumbua kichwa cha Raisi kujibu"

    Nyie wasomi na wataalamu na wasomi mlioko nje kama kazi yenu itakuwa tu kutwa kuelezea matatizo ya nchi tutawachoka na hatuwahitaji mrudi heri mbaki na kufia huko huko.Unganeni na Raisi Kikwete kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo ya nchi myajuayo miaka nenda rudi.Kama maji hamna ,umeme hakuna,barabara hakuna,Elimu duni,n.k Solution ni nini? Pesa zitoke wapi? Be part of solution na msiwe sehemu ya kundi la wauliza maswali au watu wambeya wa kulaumu tu.Toeni practical solution na siyo academic solution.

    Kazi kubwa ya wataalamu si kuuliza maswali kama mlalahoi wa kijijini wanapokutana na Raisi.Wasomi mkikutana na Raisi huko nje siku ingine mtoe solution badala ya kuuliza maswali.Nimefuatilia kwa karibu ziara za Raisi huko alikoenda ni aibu tupu.Wasomi walikuwa wakimmiminia maswali Rais ajibu.Nilitegemea wakinyoosha vidole kama wasomi waseme Raisi hapa tuna ufumbuzi wa kueleweka wa Tatizo mOja, mbili, tatu.Hivi msomi wa Ulaya na Marekani akiwa hana solution ana swali,na mchovu wa kijijini ambaye hakusoma kabisa naye hana solution ana swali hivi nchi nani atatoa majibu ya matatizo?

    Wasomi anzeni kutoa practical solution.Unganeni na Juhudi za Raisi za kutafuta majibu ya matatizo na maswali ya nchi.Msiishie kujibu vizuri maswali ya darasani tu jibuni maswali ya matatizo ya nchi with practical solution.Ubabe wenu wa fani uonyeshe kwenye ufumbuzi wa matatizo na siyo kwenye maswali complicated yasiyo na solution au magumu kuyajibu.

    Keep it Up Kikwete.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  28. Ni nani alimpa rais ushauri aialike real madrid na walitumia vigezo gani kuchagua madrid badala ya timu nyingine kubwa kama,
    1. bayern munich,
    2. arsena
    3. chelsea
    4. Juventus
    5. AC/Inter Milan
    6. Liverpool
    7. Man Utd n.k.

    Waliweka mbele maslahi ya nani au ni upenzi binafsi wa Rais kwa gharama za watanzania?

    Kwanini waalike timu kutoka Spain ambao hali yao ya hewa ni more or less the same as TZ. Unadhani waspanish wana haja kuja kwenye jua letu wakati na wao wana jua karibu mwaka mzima? Washauri wa rais hawakuzingatia climate na mandhari ya Spain ktk kualika madrid kwa sababu hao ni rivals wetu ktk kuvutia utalii, sana sana madrid watajitangaza wao na spain badala ya kuitangaza TZ.

    ReplyDelete
  29. mazuri:
    1.amekuwa mvumilivu kwa muda mrefu bila kusababisha mgawanyiko kwenye chama kwa tamaa za uongozi.
    2.ameanzisha taratibu za kuipitia mikataba ya uchimbaji madini ambayo ilikuwa inayanufaisha kwa wingi makampuni ya nje kuliko Tanzania.
    3.anajitahidi kuitangaza Tanzania nje.kitendo cha kuileta real ni kizuri sana na ningemshauri next time amlete Tiger Wood msafara wake hautakuwa mkubwa sana.
    4.ametoa maagizo kwa sekretariet ya CCM kujihusisha sana na shughuli za uwekezaji kwa ajili ya chama badala ya kutegemea misaada toka kwa vibopa,misaada hii huwa iko attached na strings.
    5.amekuwa akikutana na viongozi wa upinzani na ameanzisha tena mjadala wa kero za muungano.
    6.ameanza vizuri katika kupiga vita rushwa.
    7.Mkakati wa kujenga shule za sekondari umewezesha wanafunzi wengi kujiunga form 1 mwaka huu.
    8.mkakati wa kuleta kocha toka brazil umeiwezesha stars kuwa kileleni katika kundi lake mpaka sasa.
    9.ameongeza mishahara ya wafanyakazi wa serikali,ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho ya mishahara hiyo.
    10.wakati wa ukame mwaka jana alisimama kidete kuhakikisha kuwa hakuna anayekufa kwa njaa.

    makosa:
    1.anashikilia bango swala la shirikisho la afrika mashariki,hii ni kutoa mwanya wa majuto kwa watanzania.
    2.hatoi ufafanuzi juu ya malalamiko ya wananchi juu ya safari zake.safari hizi zinaweza kuwa na manufaa makubwa sana na ninaamini zinayo ila ni vyema rais anaposikia malalamiko atoe ufafanuzi.
    3.ameendeleza utamaduni wa kuwahamisha mawaziri toka wizara moja kwenda nyingine kama ishara ya kuleana.
    4.anaingiza mkono katika mfumo wa habari nchini.RAI siku hizi halitemi tena nondo zake(Mjengwa upo?)

    ReplyDelete
  30. Kwa wale mnaodhani Kikwete amesahau nyumbani mnajidanganya. Kikwete anapendwa Bwana kwa sababu anawajali walalahoi pia. Hebu soma hii http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=2444

    ReplyDelete
  31. Nimesoma malalamiko mengi juu ya rais, mtu ambaye inasemekana is the most popular president in africa according to the percentage of votes. Watu wanashindwa kuelewa kikwete is leading the beginning of a new administration so, he needs to familirise himself, inform and familiarise partner states about his administrations policies and solicit aid and investment from abroad.

    Watu lazima muelewe, hali ya nchi yetu ni mbaya, tuko nyuma sana kimaendeleo, tunahitaji foreign investment sana pamoja na technical assistance sana, if we are to achieve any meaningful economic growth which I think rais anajaribu ku achieve.

    Vilevile rais hafanyi maamuzi hivi hivi tu wa kusafiri, mara nyingi anapata mialiko, it is very undiplomatic kukataa mualiko especially when you are undeveloped and need assitance. Waziri mkuu alisha fafanua kuhusu masuala haya and I fully support statement yake.

    Nje kikwete amekua viewed has a nationalist, mtu ambaye anajali maslahi ya wananchi na kuyaweka mbele kuliko kitu chochote. Ushahidi unaonekana, tume zinaundwa kila wakati kuchunguza maovu, au ufujaji wa pesa na ukiukwaji wa utaratibu, mambo ya simu 2000, mauaji ya raia na polisi , wizi benki kuu, upitiaji wa mikataba na kadhalika. Kikwete ameweza ku prove he is truly a nationalist.

    Administration yake imeweza kusimama kidete and actually go against the odds. Muda mfupi baada ya kushika madaraka kikwete akiri kitu ambacho only nyerere peke yake alishawahi kusema.....nchi lina tatizo tena tatizo kubwa la uongozi, tatizo ambalo haliwezi kuondoka leo au kesho. Tunaona uongozi wa mkoa na wilaya unashindwa kuchukua maamuzi na kusimamia sheria paka rais au waziri mkuu afuatilye mfano lile suala la wanafanya biashara wa korosho, inspite of all this jamaa hasa lowasa ameweza kusimamia expansion of secndary education na ufualitiaji wa hali ya juu wa utekelezaji wa sera mbali mbali.

    People dont realise that what they want kikwete to do, lowassa tayari anafanya tena kwa ufanisi na ustadi wa hali ya ju. This is why kikwete ni kiongozi mzuri because he is able to delegate authority to the right people and focus on the big issues, namely foreign investment, and economic management.

    I think the kikwete administration he done a lot through the difficult times of drought, power shortages, education deficits, inflation and high oil prices all in one year.

    I think in ten years kutakuwa na tremendous changes. This is my assesment, even though mimi ni mwana chama hai wa mageuzi na mpinzani mkubwa wa ccm.

    ReplyDelete
  32. Wewe, Koloboi (sijui nikuite, Koroboi), si "koroboi" ni taa ya kandali ukiwa njiani kuwa karabai njiani kuwa taa ya umeme!

    Ni rahisi sana kuwa "expert" baada ya "event"! Mbona X hakumpasia Y mpira, na Y akampasia Z kufunga goli!

    Experts wa namna hiyo wanajidhihirisha kuwa hawana walijualo; hawana solution yeyote!

    Mimi ningekuwa Kikwete, ningebadili mkakati wa hotuba zangu. badala ya kuwataka watu waniulize maswali, ningewauliza mwenyewe maswali nisikie wanashauri kama ufumbuzi wa matatizo ya Tanzania!

    ReplyDelete
  33. Kitu alichonifurahisha Kikwete pia ni uwezo wa kuchagua watu wenye uwezo toka kwenye sekta binafsi na waliojiajiri na kuwaingiza katika utawala rasmi wa serikali na kuwapa Vyeo na kuvunja ile tabia iliyojengeka kuwa utawala wa serikali ni wa watu fulani tu miaka nenda rudi.

    Watu wengine aliowateua wasingeweza pata nafasi ya kuingizwa serikalini pamoja na michango yao mikubwa katika jamii kupitia sekta binafsi,kujiajiri au kupitia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali n.k

    Nchi kubwa kama Marekani inapoteua viongozi hutizama kote kuanzia serikalini,mashirika ya dini,mashirika binafsi,Mashirika yasiyo ya kiserikali,watu binafsi walioko mitaani,nje ya nchi,wakulima,wafanyabiashara,wafugaji,wastaafu n.k ili kutafuta watu wenye potential ya uongozi na kuwateua kushika vyeo katika serikali badala ya kutizama walioko serikalini na kwenye chama tu.

    Raisi Kikwete kaanza vizuri ameanza kuingiza damu mpya toka kila kona katika utawala wa serikali.

    Ninachomwomba Raisi aangalie watanzania walioko nje ya Nchi pia ambao wanaonyesha uwezo mkubwa huko katika maeneo wanayoyafanyia kazi na wale wanaotoa mchango mkubwa kwa jamii ya watanzania iwe wamejiajiri au wameajiriwa awateue nao kushika nafasi anazodhani waweza zimudu ili utawala na utendaji wa serikali uzidi kuchangamka na kushika kasi zaidi.

    Naomba ikiwezekana Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kupitia Balozi za Tanzania zilizoko nje ya nchi wakusanye CV za watanzania wote walioko nje ya nchi na kuwa nazo na kumkabidhi mheshimiwa Raisi baada ya kuzihakiki ili azitumie kwa uteuzi baadaye akiona kuna haja.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  34. Guys, Real Madrid is the richest team in the world, by visiting Tanzania your country will be well known more in tourist bussiness. Last year South Africa invited Manchester United, ofcourse you cannot compare your country and South Africa, dont complain about money, money.... From William in South Africa, I love Tanzania...

    ReplyDelete
  35. Watanzania fumbueni macho, huyu Rais wetu hizo trip anazofanya anawanawake kila kona.

    ReplyDelete
  36. JK amefanya kazi kubwa sana tangu aingie madarakani,ni MAJAMBAZI tulikuwa hatulali,uwezi kwenda pub kuanzia saa 1 jioni lakni sasa shwari hata wizi wa magari umepungua karibia kuisha kabisa,uteuzi wa New IGP was perfect choice. BIG Up JK kwa hilo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...