julius kambarage nyerere rais wa awamu ya kwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Huyu jamaa alikuwa "KICHWA" sana kwa hali ya siasa ya ya wakati ule japo kuna wanaombeza kuwa alikuwa aina ya akina 'BOKASA"

    ReplyDelete
  2. Mungu akupe pumziko la milele,Mengi mazuri uliyoyafanya kwa wakati huo,watu hawayakumbuki,wanalinganisha na maisha ya sasa.wenye akili wanajua ila waliochanganyikiwa wala hawakumbuki.

    ReplyDelete
  3. Baba yetu wa Taifa Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi siku zote kwenye maamuzi yake aliweka mbele nini athari ya maamuzi yake kwa Watanzania. He was the best president ever, as human being he was not perfect but he always had good intentions to Tanzania and Tanzanians. Rest in peace my friend. We still miss you a lot.

    ReplyDelete
  4. Mwaminifu, muunganishaji wa watu, si mbaguzi ila kiuchumi he was probably one of the worst leaders on the face of the earth!!

    ReplyDelete
  5. Mchonga au haambiliki.

    ReplyDelete
  6. Nadhani ni baada ya miaka hamsini au hata mia watanzania watakapoangalia nyuma na kutambua ni jinsi gani Mwalimu alikuwa na uwezo wa kuona mbali sana. Ni miongoni mwa viongozi wachache ambao walikuwa wakichukua maamuzi kwa ajili ya manufaa ya TAIFA, WAAFRIKA na BINADAMU kwa ujumla

    ReplyDelete
  7. Zama zake hakuna hakuna dawa za meno.hakuna sabuni hakuna Tv,etc kila kitu kwa foleni,nchi nzima shule 300 za sec,chuo kikuu kimoja,kila kitu kwa kibali,mwenye ruhusa ya na kuwa na benz ni ikulu,ukiw nae mtu binafsi bi bepari,kuwa duka kubwa ni bebari,kuwa na kiwanda ni bepari,kuvaa suti ni bepari,watu walivaa majunia ya mbolea kama nguo.
    Ukimatwa na dozen moja ya sabuni ni mhujumu uchumi,hakuna ruhusa kukosoa serikai yake,
    Ameruhusu mfumo wa vyama vingi baada ya kungatuka,ukimkosoa ndaaani

    Huyo ndiye Nyerere

    ReplyDelete
  8. 1.Serikali ilikuwa ni ya "one man" show yeye ndiye alikuwa kila kitu.Aliendesha nchi kama kampuni binafsi ambayo ni mwenye kampuni tu ndie inabidi asikilizwe na atoe mwelekeo na mustakabali wa kampuni.

    2.Alikuwa haheshimu uhuru wa Dini.Mfano aliburuza na kuwatesa wasabato na walokole waliogoma kulima tumbaku kwenye vijiji vya ujamaa kinyume na imani yao inayokataa matumizi ya tumbaku.

    Dini alizojua yeye na kuzitambua ni zile zilizoletwa na wakoloni tu toka mataifa mengine mfano Uislamu toka Uarabuni,Uanglikana toka Uingereza,Ukatoliki toka Roma,na Ulutheri toka Ujerumani.Lakini Imani zingine zote zilizoanzishwa na wazawa ndani ya nchi aliziponda na kuziona takataka na kuwatesa na kuwasumbua wenye imani hizo.Alikuwa haamini Mzawa kuwa na yeye ana uwezo wa kuanzisha dini zaidi ya hao wakoloni.

    ReplyDelete
  9. Jomo Kenyatta wa Kenya aliwahi kuulizwa tofauti ya Tanzania na Kenya ni nini akajibu kuwa "kama unataka watendaji wazuri katika sekta ya mbalimbali njoo Kenya na kama unataka wahutubiaji wazuri kila eneo liwe la sisa,uchumi,biashara,kilimo n.k nenda Tanzania kamwambie Nyerere akupe anao tele.

    Tatizo la Raisi Nyerere ni kuwa alitengeneza wahutubiaji wazuri si watendaji na wachapa kazi wazuri.Alipenda sana watu ambao kazi yao ni kuimba kwa nguvu hadi kufoka mate mdomoni kwa kusema "Zidumu fikra za mwalimu Nyerere" kiutendaji ni sifuri.

    Hadi leo Wengi wanaiga tabia ya Nyerere ya kuwa wahutubiaji wazuri kuliko kuwa watendaji na wachapa kazi.Mwalimu Nyerere alikuwa mwalimu zaidi wa hotuba kuliko kuwa mwalimu wa utendaji.

    ReplyDelete
  10. Positive:
    -Alitutoka mikononi mwa wa koloni.
    Hali ya nchi kiuchumi ilikuwa mbaya sana ilifanya kazi yake iwe ngumu pia, wakoloni walijua ni "kichwa" walifanya kila njia asifanikiwe hata kuwachochea wagombane na rafiki yake mkubwa kambona. Wasomi walikuwa wachache wakati huo.
    -Alipenda watanzani wa moyo mmoja, kwake hakuna ukabila wala ubaguzi wa dini kiswahili kiwe lugha ya taifa kutuunganisha, alihuribi upendo kati yetu (ndoo maana watanzania hadi leo hata tukigombana bado tunapendana hasa tukiwa nje)
    - Alitaifisha mabiashara makubwa kwa manufaa ya watanzania, alitoa elimu bure, usipopeleka mtoto shuleni unafungwa, alisisitiza elimu ya watu wazima,
    -Hakujilimbikiza mali, watoto wake wenyewe walikuwa kama watoto wote wakitanzania, alipenda vijana, hata Kawawa alipopinga vi-mini alisema "waacheni vijana yatapita hayo...." kuwapeleka jkt ilikuwa ni njia mojawapo ya kuwafanya vijana wawe wakakamavu.
    -Siasi yake ya ujamaa ilikuwa ni njia yakufanya kugawane sawa mali ya nchi (ilipigwa vita na wazungu)

    -Alifanya kazi kwa uhuru na ubaguzi wa rangi SA
    -Alikuwa mshauri mkubwa kwa ma Raisi wengine wa kiaafrika nakuwa rafiki mzuri kwa wengine ka vile Kaunda kama kuna raisi haangalii "well being" ya wananchi wake hawa kusikilizana kama vile hayati Mobutu.
    -Hata akiwa mgonjwa alifanya kazi kusuluhisha waafrika wagombanao Burundi/Ruwanda.
    -Alipiga vita ukimwi

    Negative:
    -Alisema sana
    -Akisha kuwa na msimamo wake humtoi uwe mzungu au nani
    -Alikuwa Conservative
    - Kheri uwe maskini lkn huru kuliko kuwa tajiri na mtumwa
    -Too simple for a president hata uvaaji wake yeye chuenilai tu!

    All the same nilimpenda sana, Rest in peace baba yetu wa taifa
    Aurely

    ReplyDelete
  11. Mzee wetu maskini,hakuwa na watendaji.Alikuwa akiwaamini watendaji wake lakini wakamwangusha.Hakuwa na pakuiga,yeye ndio alikuwa mwanzo.hapaswi kulaumiwa,wakoloni walimtega!

    ReplyDelete
  12. 1-Alituunganisha watanzania kuwa kitu kimojo
    2- hakuwa mlaruswa
    3- alisaidia sana bara la Africa
    4- hakukubali kuburuzwa na wanene
    5- alihamasisha sana kilimo na elimu

    mabaya.
    1- alisahau sana mambo ya ndani ya nchi na kusaidia sana majirani
    2- aliwabeba watendaji wake wabovu kwa kuwabadilisha badilisha hao hao tu wakiendelea kuharibu
    3-Alikuwa dikteta kiani lakini wakati ule ilifaa
    4-alikuwa na huruma kwa watendaji wake wabovu ambao ndio walikuwa waharibifu wakubwa wa nji

    ReplyDelete
  13. Nyerere mzalendo wa Tanzania
    Mazuri aliyoyatenda
    1.Kupinga rushwa kwa njia zote,ndio maana alikuwa na mashariti sana katika importations.
    2.Alipigana kwa dhati na adui ujinga,maradhi na hata umaskini.
    3.Alijitahidi kuweka uchumi kwa wazawa kupitia azimio la arusha.
    4.Aliweka misingi ya amani tanzania hasa baada ya kuongoza mapambano ya kutafuta uhuru
    5. Alithamini usawa kwakila mtanzania.
    6.Alipinga watu kujilimbikizia mali,na hata yeye hakujilimbikizia.
    7.Alithubutu kupiga marufuku kutumika kwa baadhi ya maliasili kama madini,akisema watanzania walikuwa hawana elimu yakutosha,ivo viachwe kwaajili ya vizazi vya baadae.
    8.Wenye elimu ya kusoma na kuandika walikuwa zaidi ya 97% wakati wa utawala wake.
    9.Pato la mtazania lilikuwa zaidi dolla 700 enzi zake.
    10.Kiwango cha kubadilishia dolla kilikuwa chini ya shillingi 50,kwa dolla enzi zake.
    11.Alikuwa hana ukabila wala undugu wakati wa utawala wake,alithubutu kumuweka jela hata kaka yake,watoto wake walipanda daladala kwenda shule.
    12.Ni Rais pekee aliyeamua kwenda kuishi kijini kwake baada ya kustaafu na kulima.
    13.Aliendela kupigania haki za wa africa wote hata baada ya kustaafu
    14.Mtu wa kwanza kuwa na masters education level kwa tanzania.
    15.Viwanda vingi vilijengwa wakati wa utawala wake.
    16.Alipenda michezo,utamaduni na kutembelea sehemu nyingi za tanzania hasa vijijini.
    17. Alikuwa na miiko ya uongozi wakati wa utawala wake.
    18.Viongozi wa ngazi za juu walikuwa wanaheshimu wananchi.
    19. Kiongozi wa Tanzania aliyeheshimika sana kimataifa,na aliweza kusimama na kuwakosoa viongozi wa mataifa makubwa.
    20. Vitendo vya uharifu vilikuwa chini sana wakati wa utawala wake.

    Mapungufu yake
    1.Aliamini kuwa viongozi wengi walikuwa na mtizamo kama wake katika kusimamia maendeleo ya nchi.
    2. Alishindwa kusimamia ujamaa,kwaani mataifa ya kibepari yalikuwa yanatumia kila njia kuharibu mafanikio yake.
    3.Alibana sana uhuru wa vyombo habari,kwahofu ya usalama wa nchi kuwa hatarini.
    4.Watu walishindwa kuwa wabunifu na kuwa wajasiriamali wakati wake kwa hofu ya kuhujumu uchumi,ingawaje kwayeye dhamira yake ilikuwa ni kupambana na rushwa.
    5.Alishindwa kusimamia uchumi baada ya vita na Iddi amini.

    Maoni yangu binafsi kuhusu yeye
    Nyerere analaumiwa sana kwa kushindwa kusimamia uchumi,nadhani watu wengi wanasahau kuwa sera zake zilipingwa sana na World bank,pia IMF na mataifa mengi tajiri, unaweza ona kinachomkuta Mgabe saivi.
    Udhibiti wake wa uingizaji bidhaa nje,pamoja na kuzia watu kujilimbikiza mali,ulikuwa na nia ya kwabana watu wasije hatarisha usalama wa raia,hasa kipindi kile cha mapema tangu kupata uhuru.
    Kwahio aina ile ya utawala kwa usalama wa nchi,ila matatizo mengine ni ya watu wengi kutokuwa na professiona education kwa wakati ule na utalaamu wa uchumi.

    ReplyDelete
  14. Nyerere hakuwa mzuri kwenye mipango ya uchumi.Wakoloni walikuwa bora kuliko Nyerere kwa mipango ya uchumi mizuri kwa ajili ya nchi hii.Wakoloni walileta mazao kama pamba,chai,kahawa, ili kutegemeza uchumi wa nchi hii, na waliona mamia ya miaka kuwa mazao hayo yatasaidia nchi hii na mamilioni ya wananchi wa nchi hii.Hadi leo Uchumi wa Tanzania unategemea mazao hayo.Bado unategemea mipango uchumi ya wakoloni ambao wachumi wao wa miaka hiyo walipanga.


    Miaka ya utawala wa Nyerere kwa ufupi tunaweza kusema ilikuwa ni miaka ya kushindwa kuendesha uchumi wa nchi.Alianzisha Azimio la Arusha kama njia ya uendeshaji uchumi Azimio hilo likamfia mikononi kabla hata hajafariki.Akaanzisha siasa ya Ujamaa na kujitegemea aliopanga na wachumi wake uchwara.Siasa hii ikamfia mikononi hata kabla hajafariki.Kwa hasira akaamua kiutu uzima kiujanja ujanja kutoroka uraisi na kumtupia Mwinyi kwa kusingizia anan`gatuka mapema(ile ilikuwa janja ya nyani. Alitoroka kwa kuona ameshindwa kuendesha uchumi na kila aalichoanzisha cha kiuchumi kinakufa kifo cha mende).

    Mazao yaliyoletwa na wakoloni bado ni tegemeo kuu la uchumi hadi leo.Wakoloni walikuwa na mipango bora ya maisha yetu na ya kiuchumi kuliko Wachovu wachovu wa leo walioelimishwa na Nyerere maana mazao ya kiuchumi waliyoyapanga na waliyoleta ndio tegemeo la uchumi wa nchi hii ya Tanzania hadi leo.Wakoloni na wachumi wenu hoyee!!!!!Asanteni sana kutuletea zao la chai,kahawa na pamba na kwa mipango yenu ya kiuchumi iliyozingatia kuwasaidia watanzania kwa miaka mingi.

    Mungu wasaidie viongozi na wachumi koko (bush economists)waliolelewa na Nyerere na maprofesa uchwara wa uchumi wa Tanzania wawe na huruma kama wakoloni kwa kuanzisha mipango ya uchumi itakayosaidia vizazi vingi vya miaka ijayo ili vizazi vijavyo visije kuendelea kusema wakoloni hoyeee!!!!

    ReplyDelete
  15. Michuzi umetupa mtihani mkubwa ambao uchambuzi wetu hautakidhi haja; upeo wake mkubwa sana. Labda ungeweka mizani za kuwapima hao viongozi wetu, thematically, kwa mfano, elimu, afya au kilimo.

    Niruhusi nizungumzie machache juu ya Mwalimu katika mapinduzi ya elimu na uongozi, kwa ujumla.

    Mwalimu alikuwa “mwalimu mwenye maono” katika fani ya elimu nchini:

    Nikiwa Darasa la 7, katoa ubaguzi wa rangi na dini mashuleni kabla ya uhuru. La sivyo, wengi wetu tusingeweza kujiunga na shule kama za wakina Agakhan na St. Michael and St. George.

    Karuhusu wanafunzi wa Darasa la 7 kuandika Mtihani wa Darasa la 8 washindapo, waende sekondari.

    Katoa kikwazo cha Mtihani wa Darasa la 8 (Territorial Standard Eight) nikiwa Darasa la 7 ili kuongeza hesabu ya kujiunga na sekondari.

    Katoa Darasa la 8 ili Elimu ya Msingi iwe miaka saba badala ya minane kufupisha muda wa kujiunga na sekondari.

    Kaongeza streams mbili Darasa la 9 kuongeza idadi ya wanafunzi sekondari nikiwa Darasa la 8.

    Nikiwa Darasa la 9, katoa Mtihani wa Darasa la 10 (Territorial Standard Ten) kikwazo kikubwa kwa wengi kutomaliza elimu ya sekondari

    Kapunguza kwanza kima cha kutoa karo kwa elimu ya sekondari kwa watoto wa walalahoi nikiwa Darasa la 9.

    Nikiwa Darasa la 10, katoa karo yote kwa elimu nchini toka Darasa la 1 hadi Chuo Kikuu.

    Karuhusu wanafunzi wa Darasa la 11 kujaribu Mtihani wa Cambridge School Certificate “O” Level ili washindapo waingie Darasa la 13 hadi 14.

    Karuhusu wanafunzi wenye ujuzi wajiunge na Darasa la 13 mwezi wa Januari kuliko kungoja wajiunge baada ya matokeo kutoka Cambridge mwezi wa Februari. Wanafunzi wa Darasa la 12 la mwaka wetu tukawa wa kwanza ku-enjoy na ku-benefit kutoka mpango huo mpya.

    Katoa masharti ya kuingia Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki kutoka ushindi wa principals zote hadi principal moja na subsidiary moja ili kuongeza nafasi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu. Darasa la 14 letu tukawa wa kwanza ku-enjoy na ku-benefit kutoka mpango huo mpya.

    Kaleta mapinduzi katika elimu, Elimu ya Kujitegemea, yaliyojaribu kurekebisha mfumo wa elimu ya kikoloni tuliyorithi, kwamba elimu yetu kwa miaka mingi ilikuwa ni kwa wachache wenye kupata ajira ya chini katika mfumo wa kikoloni; elimu ili-produce wasomi ambao wanadharau kazi ya mikono; wanafunzi wakariri na ku-regurgitate facts za vitabuni; na wasomi waliojitenga na jamii vijijini.


    Azimio la Musoma empowered wenye elimu ya Darasa la 12 kujiunga na Chuo Kikuu wenye ujuzi wa kikazi wa miaka miwili.


    Katika uongozi wa taifa:


    Mwalimu was contradicting himself: Aliamini kuwa hakuna cha trickle-down effects katika global economic relations (ambapo matajiri wanasaidia walalahoi); na huku aling’ang’ania trickle-down effects on a national level katika elimu ya post-Azimio la Arusha!

    Mwalimu alikuwa “mwalimu”, hata katika uongozi wake wa taifa. Lakini alikuwa ni a bit “dikteta”. Hakuvumilia kukosolewa (ingawa alikihimiza kukosolewa) mithili ya hedimasta mkali kwa walimu na wanafunzi wake au baba mkali kwa watoto wake. Aliwatimua waliomkosoa, kwa mfano katika Mkutano Mkuu wa Chama mjini Tanga: wakina Masha na wenzake walitimuliwa.

    Mwalimu alifuata falsafa ya tangu enzi za wakina Aristotle, Plato, John Locke, Thomas Hobbes, Jean-Jacques Rousseau, E. L. Thorndike, Alfred Binet, Jean Piaget) kwa kuamini kuwa elimu inatokana na “experientialism or empiricism.” Mwalimu kasomea ualimu pale Chuo cha Makerere wakati falsafa ya ualimu ilikuwa imejengwa kwa misingi ya imani ya kundi hili kuwa kichwa cha mtoto ni sawa na ukurasa mpya usio na maandishi au clean plate (tabula rasa); lazima ubongo ujazwe, kama nyuki anayotafuta poleni na nectar na kuileta mzingani.

    Mwalimu, katika Elimu ya Kujitegemea, alizingatia falsafa hiyo hiyo ku-criticise elimu ya mfumo wa kikoloni iliyolenga wachache wenye kupata ajira ya chini katika mfumo huo; elimu ili-produce wasomi ambao walidharau kazi ya mikono; wanafunzi wakariri na wenye ku-regurgitate facts za vitabuni bila kuwa na “inquiring mind”; na wasomi waliojitenga na jamii vijijini.

    Lakini katika uongozi wa kujenga taifa jipya, Mwalimu alijikuta akitumia that falsafa na methodologies za “didactic”: kujaza bongo za watoto, na kujaza bongo za taifa kuinda taifa jipya. Shule na Chama vikawa kama “a factory”. Wanafunzi na wananchi wakawa “malighafi” isindikwayo na kutoa bidhaa, ingawa kuhusu bidhaa za kawaida, nyingine hutoka kama “rejects.”

    ReplyDelete
  16. Yaani humu kunawakereketwa wa chama sana. Mnaandika maneno yote haya mnategemea tutasoma yote hii au michuzi anakusanya survey?
    Andikeni basi in brief

    ReplyDelete
  17. MAZURI
    1) "alijaribu" kumfanya kila mtanzania awe na maisha bora
    2) kiongozi wa nchi zilizokuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa bara la Africa
    3)kung'atuka
    4)kutoiba
    5)kukubali kuwa siasa zake zilishindwa.

    MABAYA
    1) uchumi
    2)kutufanya watanzania tufikirie kuwa vitu hugawiwa bure-au kuwa kila kitu tutapewa na serikali
    3) kuifunga nchi-kiasi cha kutojua nini kinaendelea duniani.
    4)kuwaona wasomi wenye mtazamo tofauti kama maadui/tishio

    ReplyDelete
  18. Hakuwa sahihi kuchukua mashule ya mashirika ya dini ambayo yalijengwa kwa sadaka za waumini wa dini kwa ajili ya watoto wao na kuyafanya mali ya serikali.Hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana.Huwezi kuchukua religious property ukaitaifisha wakati wewe si mdau au mwanachama na mtoa sadaka za ujenzi wake.Huu ulikuwa uonevu wa hali ya juu na ndio uliomfanya Nyerere ajulikana kama Mkomunisti Nyerere kwa taasisi za dini na nchi za magharibi.Maana aliingilia moja kwa moja taasisi za dini na kujifanya Raisi pia wa taasisi hizo na kufanya chochote katika taasisi hizo ikiwemo kuchukua mashule na kuzisimamia uendeshaji wake ikiwemo kuamuru ipi isajiliwe na ipi isisajiliwe na nini kifanyike kuhusu mali zao.

    Alipenda kuwa Raisi wa mashirika ya dini pia ambapo dini zinawajibika kwake moja kwa moja pamoja na waumini na mali zao zote akawa kama kamungu fulani hivi

    ReplyDelete
  19. mazuri:
    1.alipiga vita mgawanyiko kwa misingi ya ukabila.
    2.hakujilimbikizia mali kwa kuwadhulumu wananchi.
    3.alijitahidi kufundisha uzalendo mashuleni kwa nyimbo nk.
    4.alisaidia ukombozi wa nchi zingine za afrika na kupiga vita ubaguzi wa rangi afrika kusini.
    5.alisimamia hoja zake na kuzitetea kwa nguvu zake zote.
    6.baada ya kustaafu aliendelea kufuatilia kwa karibu jinsi nchi inavyoongozwa ikiwa ni pamoja na kuwashauri viongozi.
    7.aliingilia kati katika kampeni za rais mkapa ili kuhakikisha kuwa Mrema ashindi uchaguzi mwaka 1995,mrema ngashinda sijui nchi ingekuwa wapi sasa hivi!
    8.aliweka mfumo unaowezesha watoto wanaotoka kweny familia za kimasikini kupata fursa ya kusoma.
    9.alikubali kuhatarisha kazi yake ya ualimu kwa kujiunga na TAA kinyume na circular no.6 iliyokuwa inakataza watumishi wa serikali kufanya hivyo.
    10.alitoa wazo zuri kuwa makao makuu ya serikali yawe katikati ya nchi kwa manufaa ya mote na usalama.

    alipokosea:
    1.alishindwa kutekeleza kuhamia kwa makao makuu ya serikali Dodoma.
    2.alitawala kwa miaka mingi mno.mpaka alipomaliza yeye kutawala ndio akachombeza katiba ikataze marais wanaofuata kuongoza zaidi ya miaka 10.
    3.aliwahukumu wale wanaopinga hoja zake hata kama walifanya hivyo kwa malengo mazuri.
    4.alikuwa anachukua jukumu la mahakama kutoa hukumu mbalimbli ambazo katiba haikumruhusu kuzitoa.
    5.aliwahamisha watu kwenda kwenye vijiji vya ujamaa na akaacha swala la ardhi walizozimiliki mwanzoni likiwa halijafanyiwa maamuzi,ardhi hizi zilichukuliwa na watu wengine baadae,hili limesababisha matatizo yanayodumu mpaka sasa hasa mkoani Arusha.
    6.alikuwa na tabia ya kuyakimbia matatizo fulani na kuyaacha tu ingawa yalikuwa ni masuala ya msingi kutatuliwa.mfano,ameng'atuka bila kufanya jitihada za kutatua mgogoro wa mpaka wa Tanzania na malawi na kile kinachoitwa kero za muungano kati ya tanganyika na zanzibar.
    7.hakuwatumia wataalam ipasavyo.kuna maamuzi aliyoyafanya alipaswa kuchukua mawazo ya wataalam lakini hakufanya hivyo mfano,wakati wautekelezaji wa sera ya uanzishwaji wavijiji vya ujamaa ilipaswa wanasheria wahusishwe ipaswavyo.
    8.alifanya maamuzi makubwa kinyume cha katiba mfano,alisaini mkataba wa kuunganisha tanganyika na zanzibar bila kuhusisha wananchi kinyuma na katiba ilivyokuwa inasema kuwa maamuzi yote ambayo yatapelekea kubalika kwa zaidi ya asilimia 75 ya katiba ni lazima yahusishe wananchi wote.
    9.amepindisha historia ya nchi.mfano,chief marelle aliyefariki wiki iliyopita na jamaa mmoja anaitwa Fred Mchauri ni watanzania wa kwanza kwenda kusoma nchini uingereza.nyerere amekaa kimya juu ya maandishi mengi yanayosema kuwa yeye ndio wa kwanza ingawa kulikuwa na malalamiko kadhaa.katika hili pia Nyerere kama Rais wa kwanza hakuhakikisha kuwa historia ya nchi inaenzi wale wote walioshiriki katika harakati.
    10.wakati akipinga harakati za G55 alitamka "wazungu Ulaya wanaungana nyinyi hapa mnajadili kutengana" sentensi hii kutoka kwa kiongozi wa taifa ina madhara kwa jamaa.somo analotoa hapa ni kwamba sisi tunatakiwa kufuata wanachofanya wazungu,ilitegemewa mtu kama yeye awe mstari wa mbele kuwapa moyo wananchi kuwa wanaweza kuwa wabunifu wa mambo yanayowafaa na sio lazima wawe wanaiga tu toka kwa wengine.kuungana kwa wazungu hakumaanishi kuwa sisi pia muungano unatufaa,hivyo basi tulipaswa kuchambua umuhimu wa muungano kwetu na muundo wake na sio kukemea wanaotaka kuujadili kwa sababu wazungu wanaungana!

    ReplyDelete
  20. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  21. Kunirahini, Michuzi na wana-Blog, naomba mtundiko wangu hapo juu uondolewe, au usahaulike. Na badala yake, unitundikie na msome huu ufuatao:

    Nampambia Nyerere kwa kuwa "mwalimu mwenye maono” katika fani ya elimu nchini:

    1. Katoa ubaguzi wa rangi na dini mashuleni kabla ya uhuru. La sivyo, wengi wetu tusingeweza kujiunga na shule kama za wakina Agakhan na St. Michael and St. George.
    2. Karuhusu wanafunzi wa Darasa la 7 kuandika Mtihani wa Darasa la 8 washindapo, waende sekondari.
    3. Katoa kikwazo cha Mtihani wa Darasa la 8 (Territorial Standard Eight) ili kuongeza hesabu ya kujiunga na sekondari, na katoa Darasa la 8 ili Elimu ya Msingi iwe miaka saba badala ya minane kufupisha muda wa kujiunga na sekondari.
    4. Kaongeza streams mbili Darasa la 9 kuongeza idadi ya wanafunzi sekondari, na Katia Mtihani wa Darasa la 10 (Territorial Standard Ten) kikwazo kikubwa kwa wengi kutomaliza elimu ya sekondari.
    5. Kapunguza kwanza kima cha kutoa karo kwa elimu ya sekondari kwa watoto wa walalahoi, katoa karo yote kwa elimu nchini toka Darasa la 1 hadi Chuo Kikuu.
    6. Karuhusu wanafunzi wa Darasa la 11 kujaribu Mtihani wa Cambridge School Certificate “O” Level ili washindapo waingie Darasa la 13 hadi 14.
    7. Karuhusu wanafunzi wenye ujuzi wajiunge na Darasa la 13 mwezi wa Januari kuliko kungoja wajiunge baada ya matokeo kutoka Cambridge mwezi wa Februari.
    8. Katoa masharti ya kuingia Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki kutoka ushindi wa principals na subsidiary zote hadi principal moja na subsidiary moja ili kuongeza nafasi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu.
    9. Kaleta mapinduzi katika elimu, Elimu ya Kujitegemea, yaliyojaribu kurekebisha mfumo wa elimu ya kikoloni tuliyorithi, kwamba elimu yetu kwa miaka mingi ilikuwa ni kwa wachache wenye kupata ajira ya chini katika mfumo wa kikoloni; elimu ili-produce wasomi ambao wanadharau kazi ya mikono; wanafunzi wakariri na waku-regurgitate facts za vitabuni; na wasomi waliojitenga na jamii vijijini.
    10. Azimio la Musoma empowered wenye elimu ya Darasa la 12 kujiunga na Chuo Kikuu wenye ujuzi wa kikazi wa miaka miwili.

    Katika uongozi, kidogo alitetereka. Alikuwa na ka-udikteta dikiteta (alikuwa kichwa ngumu; vigumu kumbadilisha mawazo (to compromise), kama M-7 wa Uganda).

    1. Kajiuzulu ualimu huko Pugu kuliko ku-compromise msimamo wake.
    2. Kataka kujiuzulu akiwa kiongozi wa wateuliwa katika Legico, wakati Gavana Twining alipokataa kuharakisha uhuru wetu. Gavana Twining katamka, “He is a stubborn guy; he thinks by making too much noise Babel would come down collapsing!”
    3. Wabunge walipohoji uongozi wake kuhusu wazungu na wahindi kupewa uraia ki urahisi, kuliko Waafrika wa nchi za Kiafrika, na Mbuge wa kwao Richard Wambura kumwambia kuwa “kama huwezi kuongoza, tuachie sisi”, Nyerere kwa hasira alijiuzulu baada ya kuwa Waziri Mkuu wetu kwa muda wa siku elfu moja.
    4. Kazozana na Kwame Nkurumah over makao makuu ya vyama vya wapigania uhuru Barani Afrika.
    5. Wanafunzi wa vyuo vikuu (1966) walikataa ku-jitoa kafara kwa madhambi ya wakati huo (madhambi ya matabaka kama yanayojitokeza sasa), kawafukuza, eti, kwa sababu walisema “Afadhali wakati wa mkoloni’. Nyerere alijua wazi kuwa ni mwanafunzi mmoja tu aliyebeba kibango hicho kidogo chenye kauli hiyo!
    6. Alipokuwa Rais, wa-Bunge wetu walihoji kwa nini serikali iwape Wakuu wa Mikoa - baada ya mwisho wa Bunge - kiinua mgongo (gratuity) na hali walikuwa ni civil servants, Nyerere alifukuza Bunge lote, na kuliita tena ku-rubber stamp muswada huo.
    7. Mwalimu hakuvumilia kukosolewa (ingawa alikihimiza kukosolewa) mithili ya hedimasta mkali kwa walimu na wanafunzi wake au baba mkali kwa watoto wake. Aliwatimua waliomkosoa, kwa mfano katika Mkutano Mkuu wa Chama mjini Tanga, wakina wa-Bunge Fortunatus L. Masha, Choge na wenzao walitimuliwa.
    8. Kavunja uhusiano na Wajerumani kuonyesha alivyokuwa na msimamo mkali: “Nanajua hawa Wajerumani ni Maasai wa Ulaya. Mara mbili wameitingisha Ulaya. Lakini mimi sitingishiki," ikiwa ni pamoja na kuvunja uhusiano na Waingereza kwa kushindwa to decolonize Rhodesia following Smith na wazungu wachache wa Rhodesia kujitangazia uhuru kwa nguvu.
    9. Mwalimu was contradicting himself: Aliamini kuwa hakuna cha trickle-down effects katika global economic relations (ambapo matajiri wanasaidia walalahoi); na huku aling’ang’ania trickle-down effects on a national level katika elimu ya post-Azimio la Arusha!
    10. Mwalimu alijikuta akitumia falsafa ya tangu enzi za wakina Aristotle, Plato, John Locke, Thomas Hobbes, Jean-Jacques Rousseau, E. L. Thorndike, Alfred Binet, Jean Piaget ya kuamini kuwa elimu inatokana na “experientialism or empiricism” na kwamba ubongo wa mtoto, kama lilivyo taifa changa, ni tabula rasa (a clean plate). Katumia falsafa na methodologies za “didactic”: kujaza bongo za watoto, na kujaza bongo za taifa katika kuunda taifa letu jipya. Shule na Chama vikawa kama “a factory”. Wanafunzi na wananchi wakawa “malighafi” isindikwayo na kutoa bidhaa, ingawa kuhusu bidhaa za kawaida, nyingine hutoka kama “rejects.”

    ReplyDelete
  22. Nyerere alitutosa watanzania kupigana vita ziliozotufilisi na zisizo na maana yoyote kwa uroho wake wa kupenda misifa wakati nchi yake ni ya malofa watupu.

    Tulichangia damu zetu,pesa na wanajeshi kumsaidia Mandela. Wakina Mandela walipokuwa wakimbizi wa kisiasa tuliwapokea kwa wingi bila kinyongo kwa mikono miwili,leo hii vijana wetu wa kitanzania ambao ni wakimbizi wa kiuchumi wanaokimbilia Afrika ya kusini,wakikimbia hali mbaya ya uchumi wa Tanzania ulioharibika sababu pesa zetu nyingi za kigeni tulizitumia kupigania uhuru wa akina Mandela,Vijana wetu hutimuliwa na kukimbizwa mitaani kama wanga na serikali ya Mandela na akina Mbeki na kurudishwa na pingu.Mbona wakimbizi wa kwenu hatukuwakimbiza barabarani na kuwarudisha kwao?

    Mandela na Mbeki muturudishie damu tulizochangia,Pesa tulizochangia namtulipe na riba juu na mutulipe fidia kwa vijana wetu waliofia Afrika ya kusini wakiwasaidia kupigana.

    ReplyDelete
  23. Nyerere Alikosea kuanzisha vijiji vya ujamaa.

    Profesa Wa uchumu wa kilimo anayeheshimika duniani Profesa RENE Durmond Mfaransa aliyeandika kitabu maarufu cha "Africa Inakwenda Kombo" alipotembelea Tanzania walimuuliza wakataka asifie ile "Operation vijiji vya Ujamaa ya Nyerere" Yeye operation ile bila kuogopa wala kumeza maneno akajibu kuwa hiyo siyo "operation vijiji" bali ni "operation hamishia watu kandokando ya barabara yenye lengo la kuanzisha vimiji vidogo vitakavyokuwa miji baadaye".Akasema kijiji maana yake ni "nyumba ya kila mwanakijiji kuzungukwa na mashamba ya kutosha eneo la mifugo kabla ya kumkuta mwanakijiji mwingine mwenye vitu kama hivyo".

    Nyerere hakusikiliza ushauri huo Wa profesa Durmon kama kawaida yake alikuwa Haambiliki kila kitu anajua yeye kama vile Dunia nzima wote wajinga akachukulia kuwa huyo profesa kama ni beberu tu aliyetumwa mabepari na makabaila wa ili apinge Fikra zinazotakiwa zidumu milele za Mwenyekiti Wa CCM.

    Nyerere akaanzisha vimiji midogo (Vijiji vya Ujamaa) ambapo watu wanalundikana pamoja kama mijini wakisafiri mbali kwenda kulima ambako mtu anachoka hata kabla hajafika shamba matokeo yake wengi wakageuka machinga,wauza maandazi na wapika chips,na chapati kwenye hivyo vimiji vidogo alivyovianzisha Nyerere.

    Mpaka leo wengi wanakimbilia mjini sababu Nyerere mwenyewe alichochea watu kupenda vimji badala ya vijiji.Nyerere ni chanzo kikubwa cha watu kupenda mijini kuliko vijijini.

    Vijiji vya ujamaa havikuleta maendeleo bali viliua maendeleo ya vijijini na ndio mwanzo wa kuua kilimo kabisa.Machinga wengi waliorundikana mijini ni wale walionzia kwenye vimji hivi alivyoanzisha Nyerere wakiuza vipipi na karanga badala ya kulima. Vilileta mfumuko wa watu kupenda miji na vimiji vidogo(Vijiji vilivyoanzishwa na Nyerere)ambako watu walikuwa wakiishi kwenye nyumba za hovyo zilizosongamana karibu bila hata mpangilio wa mitaa utafikiri vijumba vya wavuta bangi na machangudoa.

    ReplyDelete
  24. Ninyi wa-Tanzania wengine, what is this: Profesa Wa uchumu wa kilimo anayeheshimika duniani Profesa RENE Durmond?

    Jina la Profesa huyo wa "agronomy" na "sociology" ni René Dumont! Huyu Profesa aliandika kitabu kiitwacho False Start in Africa.

    Aliyeandika kitabu cha Afrika Inakwenda Kombo ni Profesa Gabriel Ruhumbika (kwa kutafsiri kitabu hicho hicho cha René Dumont)!

    Ukitafuta kitabu cha Afrika Inakwenda Kombo, utakikuta kwa jina la Gabriel Ruhumbika.

    The two are different contexts.

    ReplyDelete
  25. Ninampongeza Gabriel Ruhumbika alipoona kakosa kitu cha kuandika cha kwake akaona atafsiri alichoandika mwenzie.Na ukitafsiri cha mwenzio basi hicho ulichotafsiri kinakuwa chako na si cha yule uliyemtafsiria.(Hapo ndipo napendea Tanzania iko tofauti na nchi nyingine duniani ambako ukitafsiri bado kila kitu ulichotafsiri kinakuwa cha yule unayemtafsiria)

    Na hongera Walimu na Maprofesa wa Tanzania kila mnapooana hamna cha kwenu original cha kufundisha au kuandika hamkawii kunukuu vilivyoandikwa na wenzenu walioko Ulaya na Marekani.Hongera kwa kuwa macopy-cats.Nchi hii inahitaji wakalimani zaidi wanaotafsiri vya wenzao ili iendelee?!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Na ndiyo maana hata serikali imekuwa ikihimiza elimu ya kufundishia shule zote kuanzia msingi hadi chuo kikuu iwe kiswahili .

    Kitakachofanyika ni kutafsiri vitabu vyote vya chuo kikuu kwa kiswahili na kutangaza kuwa hiyo ni elimu yetu ambayo ni (original work made in Tanzania for Tanzanians).Yaani unatafsiri hivi

    GEOGRAPHY-jiografia
    SCIENCE-sayansi

    Halafu unajitangaza kuwa umegundua elimu original ya kufundishia watanzania itakayowasaidia watanzania waelewe haraka na unawapa medali ya utumishi uliotukuka waliotafsiri.

    ReplyDelete
  26. Jamani kitabu hicho cha AFRIKA INAKWENDA KOMBO kinapatikana wapi? Ni kitabu kizuri mno nakumbuka kukisoma zamani.Ni moja ya vitabu abavyo vyafaa msomi yeyote awe nacho.Vinapatikana wapi? nataka kununua.Nimezunguka maduka yote sijapata hapa Dar es salaam.Ila naambiwa kilikuwepo miaka ya nyuma.

    ReplyDelete
  27. Popote pale katika academia, mabingwa wanaojua lugha hutafsiri vitabu vya lugha nyingine. Hii ni njia mojawapo ya democratising knowledge! Hakuna ubaya!

    Ingawa vinaonekana kana kwamba vimeandikwa na hao watafsiri wapya, huwa vinaambatana na kiru kama "Translated from (jina la lugha mama) into (jina la lugha mpya) by (jina la mtafsiri).

    ReplyDelete
  28. Prof. Gabriel Ruhumbika alifanya kazi kubwa ya kutafsiri kitabu hicho.

    Ka-co-translate kitabu kingine, chenye ujumbe mzito, cha Frantz Fanon, The Wretched of the Earth, kama, Viumbe Waliolaaniwa!

    ReplyDelete
  29. huyu ni babu gani tena jamani nifafanulieni manake mi simtambui lakini anaanana na ngoya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...