wapi hapa?
kama kawa hili ni shindano la walio ughaibuni tu na masharti ni:
1. uwe ughaibuni
2. kudesa hairuhusiwi (itajulikana tu)
3. usilete ufundi kwenye kujibu (jibu swali kwa ufasaha)
4. uamuzi wa jaji ni wa mwisho
5. zawadi ni picha yoyote utakayo
6. mstari mfu ni saa sita usiku (za bongo) alhamisi ijayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Hapo ni Kariakoo, barabara ya msimbazi na morogoro zinapokutana. Picha ninayoomba kama nikipata ushindi ni ya Zay B.

    ReplyDelete
  2. Michuzi. Mimi sidhani kama ni haki kwa watu walioko ughaibuni kwa hili shindano. Hili jengo linaonekana limeanzwa kujengwa miezi michache au mwaka uliopita. Sidhani kama ni rahisi kulifahamu. Labda kudesa kama unavyosema!! Watu wengi ughaibuni ni hurudi yumbani kwa likizo au wengine hawajarudi kwa muda mrefu.

    ReplyDelete
  3. HAPA NI CORNER YA KUINGILA BARABARA YA UMOJA WA VIJANA KUTOKEA BARABARA YA UWT.

    ReplyDelete
  4. Hilo jengo Issa ni la NHC kama sikosei,lipo karibu na jengo la Extelecom,along samora avenue,mkabala na Twiga bank,TIB yaani benki ya rasilimali,wale madenti wa enzi zile secondary miaka ya 90's karibu na Tahafifu ile ya posta. Na hapo chini huwa kuna chinga walikuwa wanauza pamba, upande wa extelecom kuna jamaa walikuwa wanauza vifaa vya magari,sijui kama bado wapo hapo.Natoa hoja Issa,kazi kwako.

    ReplyDelete
  5. hapa ni arusha sanawari kona ya kuelekea chini nbc na safari hoteli kupitia aicc. jengo hili ni la tajiri mmoja ambaye alisumbuliwa kidogo ila sasa linaendelea kujemngwa. picha ninahitaji maana nimeshashinda. Picha uniwekee kanisa la lutheran azania front hapa.

    ReplyDelete
  6. Hapo pale faya inatazamana na trafiki lights kama unaenda upanga mbele unaenda kariakoo. opposite kuna gas station moja ya mafuta. Kulikuwa na kituo cha mabasi hapo kulia.

    ReplyDelete
  7. Hapo ni corner ya mtaa wa livingston na msimbazi. Opposite na hio jengo ni BP gas station. mbeleni, morogoro road.
    -Songo Mbingo

    ReplyDelete
  8. jamani michuzi unawaonea hao walioko majuu,yaani hapa nilipo nasuuzika na roho yangu kujua hakuna hata mmoja hapo juu aliopatia ,masikini sio faya,sio kariakoo,sio arusha na wala sio NHC......Jamani nisemeee,aku nisije nikawakosesha zawadi zenu maana mie niko BONGO DAR ES SALAAM,na hapo ni.....pale GONGOLA NYOKA alipouliwa MBOTO....[hahaha sio GONGOLAMBOTO ALIPOULIWA NYOKA}
    changamkeni bathiiiii

    ReplyDelete
  9. nyie wote ndo hamnazo kweli! yaani mnashindwa kujua hapo wapi! si uwanja mpya wa taifa huo! embu nipe zawadi yangu michuzi!

    ReplyDelete
  10. ama kweli wabongo noma..hapo ni Jengo la nasaco...si liliungua ndio wakaanza kulijenga tena....ebana zawadi yangu nataka picha...ya wema sepetu na Tid..

    ReplyDelete
  11. livingstone str na msimbazi,hayo magari ni kituo cha taxi

    ReplyDelete
  12. easy!!
    hapo ni ikuru, wanajenga banda la kuku wa kikwete.

    ReplyDelete
  13. Ilo jengo lipo posta samora kwenye kona ya mtaa wa India

    ReplyDelete
  14. ...Hapo jengo lilipo ni kona ya mtaa wa libya na morogoro karibu na kituo cha mabasi cha za zamani ya kwenda arusha, moshi nk.Mbele ya hizo taxi kuna kituo cha mafuta zamani sana kilijulikana kama Agip.

    ReplyDelete
  15. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  16. ...Hapo jengo lilipo ni kona ya mtaa wa libya na morogoro karibu na kituo cha mabasi cha za zamani ya kwenda arusha, moshi nk.Mbele ya hizo taxi kuna kituo cha mafuta zamani sana kilijulikana kama Agip.

    ReplyDelete
  17. Pungwani wote nyie hiyo ni nyumba ya baba yangu ipo kwenye makutano ya Good time na Feel Good. Upande wa kulia kuna nyumba ya the late Greet Taste na kushoto ni kwa mzee Envy. Can't wait for my gift, na ninataka picha yako Michuzi bila shati.

    ReplyDelete
  18. Jengo lipo kwenye makutano ya Livingstone na Msimbazi, karibu na kituo cha Bakhressa

    ReplyDelete
  19. Hii chemsha bongo yako leo wallah haina clue....kama ni corner lot yapo mengi tu hapo Dar...Sasa hiyo miti kila mahali Dar si ipo...jamani dar sio jangwa...Sasa sijui tuangalie mawingu tupate clue au aina ya magari yaliyopark hapo.

    Mimi nipo na huyo aliyesema aliyesema hili jengo kama hukuwa Dar mwezi uliopita hutajua ni wapi shurti kudesa tu hapa.
    Mimi jibu langu .....he he he he na miye nijibu ...ni maeneo ya Morogoro road...Nikiangalia hayo mawingu yananifanania kama pale vile.

    ReplyDelete
  20. Bwan' 'Supu, kama kibao kinavyoonesha hapo ni India Street. Nipe zawadi ya picha ya sekondari ya Mzizima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...