wadau. kwa kutambua kiu yenu ya kujadili uongozi wa sasa na uliopita, kwa idhini yenu napenda kufungua mjadala wa uchambuzi yakinifu wa viongozi wetu hao hapo chini wanne ambapo nitatoa zawadi kwa yeyote atakaye wachambua vyema.
waama, ningeshukuru kwamba kila mtoa hoja atoe vipengele kumi vya sifa na mapungufu kumi ya kila mmoja wao chini ya picha husika bila kujumuisha lugha isiyofaa.
mdau mwenye lugha isiyofaa asijisumbue kwani haitochapishwa. kinachotakiwa hapa ni nguvu ya hoja, na sio hoja ya nguvu. isisahaulike kwamba kiongozi aliye madarakani hivi sasa ana umri wa takriban mwaka mmojakitini, wakati waliomtangulia walikuwa ikulu kwa miaka kumi ama zaidi.
asante kwa ushirikiano wenu.
mstari mfu wa zoezi hili ni jumanne ijayo saa sita usiku (saa za bongo).
karibuni...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mwl alikuwa ni ngumu kumlinganisha na hawa wengine kwani yeye alichukua nchi kutoka kwa wakoloni. Alikuwa na wasomi wachache!

    Sifa zake ni kama ifuatavyo kufuatana na ninavyoona!

    1. Alijenga Utaifa na kuwafanya watanzania kama Ndugu..ukilinganisha na nchi za jirani kama kenya..ukabila bado unawasumbua hata katika chaguzi, utoaji wa kazi serikalini, na mengine ukabila unazingatiwa, kitu ambacho kwetu hakipo kwenye kamusi zetu neno (ukabila)
    2. Mwalimu aliweza kutobabaishwa na Wakoloni Mamboleo kama akina IMF na World Bank. aliziamini juu ya utu (dignity) kuliko kupewa misaada
    3.Mwl alikuwa Jasiri, hawezi tu kuitwa na Mtu kama Blair na kukimbiakimbia eti kwa ajili ya misaada, kama anavyofanya Rais wenu.
    4.Mwl. alipigania usawa wa binadamu wote. Ingawa hakufanikiwa ila alijaribu kwa kutumia mifumo aliyoiamini
    5. Mwl. alifanikiwa kwa swala la kufuta ujinga kwa kutumia elimu ya watu wazima
    6. Mwl.Pia aliipa kipaumbele elimu
    7.Mwl.Alikuwa na upeo wa kuona mbali
    8. Mwl. Hakula Rushwa
    9. Mwl.alimini juu ya uhuru wa tanzania na africa kwa ujumla
    10. Mwl. aliwaanda wote hawa wanaosahau principles zake

    Mapungufu yake ni haya yafuatayo
    1. Mwl. alikuwa na kachembe ka-udictator, ila alikuwa kwa sababu ya hali halisi ya nchi.
    2.alikuwa ni conservative, hata alipooona kwamba mfumo aliofuta wa ukomunist umeshindwa, yeye alishindwa kukiri hivyo na badala yake aliachia uongozi ili asije akajikuta, anapiga magoti kwa bwana wakubwa.
    3.Alimwingilia sana Bwana Ruksa wakati wa uongozi wake
    4.Mwenge-mimi niliona kwamba ulikuwa unatupotezea tu wakati na kumaliza hela za wananchi
    5. watu walikamatwa kamatwa hovyo kwa misingi ya magendo na vitu kama hivyo.
    6. Viongozi mimangi meza ilijitokeza wakati wa mwl.
    7.Mwl. alipenda sana sifa na aliimbwa sana kila mahali, na sidhani kama kuna mtu ataimbiwa tena kama yeye
    RUKSA
    Mazuri yake ni kwamba
    1. alianzisha ujenzi wa miundombinu dar es salaam
    2. aliruhusu soko huria hivyo kufanya
    3. Uhuru wa vyombo vya habari ulianza kuwa mkubwa wakati wa Ruksa

    Mabaya yake
    Kwanza serikali yake ilikuwa inabadilishwa badilishwa
    Pili aliuza sehemu ya loliondo Gate kwa misingi ambayo mpaka leo siifahamu
    Tatu alikuwa hana ubavu wa kuongoza hivyo kaamua kuwa uongozi huria (kila mtu ni bosi)

    Michuzi nitaendelea na wengine kesho nimechoka...naomba mtu asinipinge mpaka nimalize. Naitwa Ole lengesera

    ReplyDelete
  2. Michuzi mi naomba kuuliza. Hilo shindano lipo katika vipengele 4 au kimoja tu. Yaani mtu akitoa hoja nzuri kwa Raisi Nyerere na kwa Raisi Mwinyi akachemcha itakuaje? Amepoteza ushindi ....duh

    ReplyDelete
  3. Mimi naona ungemuondoa kikwete katika shindano hili.
    1. Kikwete yupo kazini just one tenth compare to others. This is not fair
    2. Bado kikwete yupo kwenye atleast tutasema probation period. Bado anaenjoy, bado nguvu ya soda haijaisha na bado hajaanza kuwa mwenyewe na kutoa makucha yake
    3. You can't make a piece of history yet from him. Hata leo Marekani bado hawajaweza kuandika history ya Gerge Bush Junior kwasababu bado yupo kazini ingawaje ana less than two years kwenye kazi lakini anything can happen btn now and then...anaweza kufanya just ordinary thing or extra ordinary kuichange history kabisa.


    Ndio maana kwa ushauri wangu ungemuengua kikwete kwenye malumbano haya.....

    ReplyDelete
  4. Michuzi: Pongezi kwa kukusanya haya maoni nyeti. Hata hivyo nimeona matatizo mawili katika zoezi zima.
    1. watu wanachanganya sifa za mtu na matokeo ya sifa zake. Mfano kusema kuwa wakati wa Nyerere hakukuwa na TV hayo ni matokeo au mapungufu ya nchi sio ya mtu.
    2. Sioni haja, kwa nini useme vipengele 10 vya sifa na mapungufu 10, je nikiwa na mbili tu? Maana hata sifa inaweza kuwa nzuri au mbaya, na kwamba sifa mbaya inaweza kusimama kama mapungufu ya mwanadamu. Na pia sifa moja mbaya mfano. kutokuwa na maamuzi au maelekezo thabiti yaweza kumeza sifa nyingine mbaya nyingi au mapungufu.
    3. Ungetoa angalau mwelekeo wa maeneo ya kuzungumzia (mf. elimu, kiuchumi, kiuongozi, haiba, kifamilia, kidini, kisera n.k ili iwe rahisi kulinganisha au hata kutoa majumuisho ya uchambuzi wa maoni mwishoni. Ilivyo sasa ni ngumu sana maana wengi wetu wamejikita katika kakona fulani tu ambako wanakafahamu zaidi. Hapa chini mimi natoa sifa moja moja kubwa na pungufu kubwa moja moja tu.
    NYERERE:
    1. Rais alijitambulisha (identified with) na maisha ya kawaida na ya kikabwela. Mfano. mavazi yake (Chuenilai) na vyakula vyake (karanga, mgagani/kisamvu,ugali wa ulezi na mchezo wa bao sio golf)n.k
    2.Rais huyu alikuwa hakubali (kiulahisi) kupokea ushauri unaotofautiana na maono yake.

    MWINYI:
    1.Rais aliyekuwa baba mwenye huruma, mpole hadi kukubali kuwa jalala na kuchorwa / kuandikwa ovyo lakini akawasamehe hao wapinzani wake kwa kuelewa mzigo wa kuwa Ikulu.
    2.Kuruhusu uchumi huria usio na mipaka wala mifumo ya uthibiti (checks and balances).

    MKAPA:
    1.Rais aliyejitahi sana kudumisha mahusiano mema ya kimataifa na kuendana na masharti ya kiutandawazi ya asasi za kiblitonihudi.
    2. Rais aliyekuwa msiri kupita kiasi juu ya namna ya uongozi wake na hata maisha yake.(waulizeni hata jamaa zake!!)

    KIKWETE:
    1.Pamoja na haiba nzuri na utanashati pia ni rais aliyewakumbuka sana akina mama katika nyadhifa za juu.
    2.Rais asiyeonyesha umakini(seriousness) katika hotuba zake. Apunguze kuonekana kwenye vyombo vya habari na aache Mawaziri wake na Makatibu wakuu wa wizara ndio wawe wasemaji wa mara kwa mara ili Ikulu itulie!

    Ni mimi Jicho la Mamba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...