hili ndilo basi la bufallo lililopata ajali na kusababisha vifo vya watu wengi na majeruhi kibao. habari zake zaidi bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hizi ajali hazitaisha wala kupungua kwa jinsi mambo yalivyo Tanzania.Jinsi barabara zetu zinavyojengwa ajali lazima ziwepo kwa wingi,hivyo serikali ijifunze jinsi barabara zinavyopaswa kuwa-designed.
    Kwa sasa serikali ifanye lifuatalo - ipitishe sheria kwamba basi lolote la abiria linapopata ajali lazima mwenye kampuni awe accountable na kwa maana hiyo itabidi walioathirika walipwe fidia kisheria na vilivile dereva kama atapona ashitakiwe ipasavyo.Bima ya gari hailindi gari tu bali hata waliomo ndani.Haya yafanyike iwapo makosa ni ya dereva,wenye mabasi wakijikuta wanalipa fidia za mamilioni kwa kila ajali nadhani watahakikisha madereva wao wanakuwa makini kazini.Kuhimiza madereva wawe waangalifu tu bila wao kujua fika nini kitawapata wakiwa wazembe hakutapunguza ajali.

    ReplyDelete
  2. Tatizo la matajiri wa mabasi Tanzania wote ni watu wa vijiweni. Ni wale ambao walifanikiwa kulipua mizigo ya madawa ya kulevya na kununu hayo magari, hawana uelewa wa biashara nzima ya usafirishaji. Mbona makampuni kama Scandnavia yametulia ingawa (mara chache sana kupata ajali). Vile vile askari wa usalama barabarani nao michosho tu.

    ReplyDelete
  3. duuuuuuu! dereva mjanja kweli alivyoona khali mbaya akabidi aliingize side ya kondakta.. cheki ubavuni kwake hakujapata jelaha lolote

    ReplyDelete
  4. Michuzi, asante kwa kutuwekea picha híi. Juhudi zako nazikubali.

    ReplyDelete
  5. Annoy wa Thursday, April 19, 2007 6:23:00 PM, Nakubaliana nawe kuhusu paragraph yako ya pili ya maoni, lakini hiyo ajali ya buffalo design imefanyaje?

    ReplyDelete
  6. HIVI ZILE 'SPIDI GAVANA' ZILIISHIA WAPI?... AU ULIKUWA MRADI WA MTU, STOCK ILIPOKWISHA BASI BATI CHINI? MAANA BUFFALO HILO HUWA LINARUKA CHINI CHINI... SERIKALI yetu huwa inaanzisha jambo then ufuatiliaji ZERO, au ndio mpaka siku za 'wiki ya kwenda kwa usalama'???. Kama funzo basi lingeanzia wakati ule miaka ya 80's mabasi ya Mzalendo na Kamata yalivyoteketeza watu pale Morogoro. WANANCHI nasi tungejenga utaratibu wa kuyanusuru maisha yetu kwa kutoyapanda mabasi haya 'yanayoruka chini kwa chini'. ~mwiba~

    ReplyDelete
  7. Naona aina ya mabodi ya basi ya kisasa hayafanani na hali halisi ya barabara na tabia za madereva wa Tz

    ReplyDelete
  8. Kuna tatizo la kiufundi kati, mfumo mzima wa usafirishaji (kwa ujumla) hapa nchini Tanzania. Jeshi la polisi lisafishwe, waajiri wahakikishe kuwa madereva wao wapo 'qualified', barabara zitenganishwe kulingana na matumizi na muda ufuatwe kwa kuzingatiwa ipasavyo.

    Naomba kuwasilisha.

    Kaka Mkubwa

    ReplyDelete
  9. Misoup, asante kwa kutuwekea hii picha ya ajali ya buffalo a.k.a mnyama iliyotokea j2 eneo la Kisangara, Mwanga. Inasikitisha sana watu 22 wamepoteza maisha kutokana na uzembe wa madereva kutozingatia sheria za barabarani. Nadhani ni wakati muafaka serikali kutunga sheria kali za usalama barabarani na kuzipa meno makali ziweze kufanya kazi kupunguza ajali zisizo za lazima. Ila basi za kampuni ya mnyama zilijenga jina kwa kukimbia sana kwenye hiyo njia ya Dar-Arusha.

    ReplyDelete
  10. Mimi nina mawazo tofauti kuhusu hizi ajali. Mara nyingi zinapotokea ajali visingizio/lawama huwa kwa madereva ambao huitwa wazembe na hapo basi huisha, ila haianagaliwi kwa kina kweli vyanzo hivi vya ajali ni uzembe wa madereva? sikatai kuwa kuna madereva wazembe ambao husababisha ajali kwa ulevi, kwa kutokuwa wangalifu kwa kuwapa k.m.utingo wa maroli au Day Worker kuendesha magali kwa niaba yao.
    Kwa mtazamo wangu vyanzo vingi vya ajali hapa nchini husababishwa Kwanza na ubovu wa barabara, ubovu wa barabara sina maana kutokuwa na lami la hasha barabara nyingi zina lami siku hizi ila sasa barbara hizo ni nyembamba mno "single lane" sio za two way traffic magari hupishana uso kwa uso kwa karibu kwa usiku huwa ni vigumu sana kwa dereva kulimudu gari huku akipishana uso kwa uso na mwenzie ambaye wakati huwa amemwashia taa, Pili barabara nyingi hata za mjini hazina taa ni giza totolo taa ama zimegongwa au zimeungua hazibadilishwi wala kurekebishwa Tatu barabara nyingi zimemegeka kingo zake za pembeni yani lami imeliewa kiasi ambacho dereva anawajibika kukwepa pembeni nakuingia "site' ya mwenzie anaekuja kwa mbele chukulia kwamba barabara hiyo ni "single lane"
    hii ni hatari sana Nne hakuna 'alternative roads' hasa kwa barabar ziendazo mikoani ni moja moja tu karibu kila uelekeo kiasi kwamba barabara hizi hichoka zinapitiwa na magari kukuki kwa wakati mmoja matokeo yake lami za barabara hizi hutelezaa kutokan na na mafuta yaliyomwagika pia zina mabuja/manundu manundu. Nne alama za barbarani nyingi zimeharibika na hazijatengenezwa k.m zebra cross, alama zinazoashiria kuna kona kali, mtelemko mkali, punguza mwendo, kuna daraja mbele, kuna kivuko cha wanyama n.k. Barabara nyingi zina kona kali na mitelemko mikali inawezekana hii ikapunguzwa hasa katika sehemu zenye kusababisha ajali mara kwa mara. Tano madaraja mengi ni zamani yamechoka k.m Ruvu, Wami, Kitonga n.k . Mambo ni mengi ila nafikiri wahusikia hawajajua bado vyanzo halisi vya hizi ajali .

    ReplyDelete
  11. JE MWENYE BASI AMEWAFIDIA WAFIWA? KAMA HAPANA, FAMILIA ZA WAFIWA ZINAFIDIWA NA NANI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...