mdau wa bulyanhulu katuletea picha hii mwanana ya alfajiri huko machimboni. nakaribisha picha tamu kama hizi toka popote pale ili sie wapenzi wa picha tuzijadili. kwa maoni yangu kajua haka kangekuwa katikati ya miti, ingekuwa shega zaidi. hata hivyo namsifu mdau kwa jicho lake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2007

    Michuzi, ulichosema kuwa ingekuwa katikati ya miti ingekuwa bora zaidi ni sawa...lakini kwa kuongezea, mimi naona ingekuwa katikati ya miti halafu hicho kijumba na hiyo milingoti ya umeme isingekuwepo ndiyo ingekuwa marudufu...ingelikuwa asilia full kujiachia hapo, waonaje?!
    SteveD.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2007

    Michuzi,
    Nakupongeza kwa ubunifu wako ktk hii globu yako.

    hii Idea ya wadau kutuma picha ni bomba sana.
    mimi nashauri ili kuipeleka hii idea ktk level ya juu, nashauri picha zitumwazo ziwe ni picha zenye theme ya mazingira. tuna mandhari na mazingira mazuri sana ktk nchi yetu. Ni ngumu sana kwako michuzi kwenda mikoa yote na kupata picha za huko, lakini kwa hii 'programm' yako itatusaidia sote kupata habari ktk picha za mandhari za sehemu mbali mbali za nchi yetu.

    Ukiruhusu picha za watu, basi kubali pia kupata picha za viatu - watu na viatu.

    Nampongeza sana huyo mdau wa Bulyanhulu kwa hiyo picha nzuri. Atakuwa ni mtu mwenye feeling na mazingira na mandhari.

    nina hamu sana ya picha za Mandhari ya Lushoto na Maporomoko ya maji ya huko Soni - Tanga, achia mbali picha za wanyama ktk mbuga zetu za wanyama pori. mdau mwenye picha za Mandhari ya hayo maeneo naomba azirushe kwa michuzi.

    Michuzi,
    toa maelezo ya jinsi wadau watakavyotuma picha walizonazo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2007

    mnayoyasema hapo juu yote yangewezekana iwapo mpiga picha huyu angecheza na angle ya camera yake, lakini hata hivyo nampa hongera kwa kuwa na jicho la kutambua

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2007

    Mamboz misupu!
    katika swala la picha umenikumbusha jambo moja la muhimu sana,pliz michu tunaomba uweke picha za maliasili ya huko kwetu TANZANIA zaidi za kuutangaza mlima kilimanjaro.
    inasikitisha sana michu huku ughaibuni kila mzungu unayemuuliza mlima Kilimanjaro ukwapi anakwambia Kenya,hivi sisi watanzania Tumelala wapi mpaka tunapokonywa kila kituuuuuuuuuu.
    Tanzanite wanabeba jamani hata kilimanjaro nao tunauachia hivihivi tene kwa hao majirani zetu wakenya,pliz michu naomba uiamshe Tourism industry ya Bongo,wautangaze kwamba uko kwetu na sio kenya.
    yaani mpaka aibu jamani,kila mzungu uanyemuuliza about mt kilimanjaro anakwambia anaujua vizuri sana na ameshaupanda na cha mwisho kukwambia ni kwamba uko Kenya. Wadau mlio ughaibuni try to do a research,ulizeni mzungu yeyote abt this then mtaniambia!
    michu chonde chonde waambie idara ya utalii iamke na ifanye matangazo zaidi about huo mlima!

    yours,
    frm.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...