mola atupe nini zaidi kama si hii amani tuliyonayo inayotokana na siasa za wapinzania kukaa meza moja na chama tawala na kubishana kisera bila kelele wala mikwaruzo tofauti na ilivyo kwingineko...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2007

    Mwalimu wangu huyo ( Chuo kikuu 83/84). I think he was a good professor. Niliondoka kabla ya multi party system kwa hiyo sikupata nafasi ya kuona performance yake as a politician. Lakini nasikia chama chake kina mwelekeo wa kidini; that combination (politics + religion ) does not work very well in most counties.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2007

    Anon wa kwanza hapo juu,

    Na wewe umetekwa na "sumu" za CCM? Wanachofanya CCM ni ku-supress and kill any "strong" opposition; "give a dog a bad name and then kill it"! Hoja yao kubwa ni "idadi kubwa" ya waislamu ktk chama cha Lipumba.

    Lakini kwa chama ambacho kimeasisiwa na watu wa Tabora (Masobi Mageni, Mapalala,n.k) na wanzanzibari (Shaaban Mloo, Seif Shariff, Juma Duni, Hamad Rashid, n.k) kuwa na waislamu wengi kwangu si ajabu maana mara nyingi mtu anaungwa mkono nyumbani kwao.

    Mfano mtu akisema TLP (Mrema, Ngawaiya-enzi zile), CHADEMA (Mbowe, Makani, Mtei, Slaa,n.), NCCR (Mbatia, Mvungi, Tenga) au TPP (Peter Mziray, Anna Senkoro, n.k) ni chama cha "kikristu" au "kichaga" au "kipare" NITAMSHANGAA SANA. Katiba ya chama husika inasemaje? Utendaji wa kila siku wa chama ukoje? Mbona msajili (ambae anateuliwa na Rais-mwenyekiti wa CCM) hakifuti?

    Sasa hivi vyama vya upinzani vinataka "kuungana" ili kupata nguvu kubwa dhidi ya CCM (wataweza?). Sidhani kama kina Mbatia, Dr Mvungi, Mbowe, Dr Slaa (former priest), Mrema,n.k wanaweza kuruhusu kungana na "chama chake chenye mwelekeo wa kidini" (kama kweli kipo).

    Hii mbinu ya CCM itakuja ku-backfire siku moja vibaya sana. Maana ukisema "kile" ni chama cha waislamu kuna siku waislamu "wanaweza" kuamua kujiunga na chama "chao". Sasa ikitokea hivyo CCM nayo haitakuwa "chama cha kikristo"?

    Kama tukifuatilia sana kuna maeneo ambayo CCM inapungua umaarufu na inapoteza wanachama na imani ya watu inapotea kwa hiki chama chetu kikongwe! Tufikiri kabla ya kusema tusije tukagawanyika eti "dini, dini" kumbe ni mradi wa wajanja kuendelea kutunyonya daima! Lengo lao watu wasiungane ili "tusiwahoji"!

    HOJA JUU YA HOJA, SIO MATUSI JUU YA MTU!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2007

    Chama hiki ni Chama Cha Wapemba walioko Tanzania Bara na Visiwani ambacho kimemweka mwenyekiti toka Tanzania bara.

    Chama hicho kina Profesa mmoja tu nchi nzima.Wasomi hawataki kujiunga nacho sababu kimejaa Upemba na Udini wa kiislamu kwani hata katika mikutano yao ya hadhara wasikilizaji hukaa tofauti kama wako msikitini,wanawake hukaa upande wao na wanaume huwa upande wao.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 12, 2007

    Anon wa 8:37:00 AM,

    Acha "U-CCM" (uwongo na uzushi). Hivi unajua jamaa walipata kura nyingi zaidi za urais na ubunge nchi nzima baada ya CCM? Hivi unajua kuwa idadi ya wazanzibar wote ni milioni moja tu (watu wa Pemba ni kama 40% ya wazanzibar wote)? Tafuta ktk mitandao data hizo halafu uje utuambie kama hao mamilioni ya watu waliowapigia kura Lipumba na wagombea wake wa ubenge ni wapemba!

    Bahati nzuri nimekuwa mhudhuriaji mzuri wa mikutano ya kampeni ya vyama karibu vyote vya TZ na ktk mikoa mbalimbali ila SIJAWAHI KUONA eti wanawake wanakaa mbalimbali na wanaume. Inawezekana umeona picha ya Zanzibar ambako ni CULTURE yao wanawake kutochanganyika na wanaume. Lakini kutochanganyika kwa wanawake na wanaume na wanaume ni udini?

    Au tuseme majaji na mawakili wanavyovaa kama MAASKARI ya Roman Empire (RC) ni udini (wa kikristo) pia? Hilo suala la wasomi sijui kama una ushahidi nalo;leta ushahidi. Msomi ni nani? Mtu mwenye elimu gani? Fafanua, hii sio blogu ya kijijini ambako CCM inawaambia tu vitu vya uwongo wanakijiji nao wanakubali NDIYOO!

    Kama una chuki na wapemba au waislamu tafadhali usizilete ktk siasa. Hata TANU nayo iliitwa (na watu wa makanisa) chama cha waislamu kwasababu hadi baada ya uhuru (hata kesho) idadi ya waislamu ktk TANU ilikuwa ni KUBWA mno toka Kigoma hadi Unguja, Mwanza hadi Mtwara.

    Katika nchi kama Tanzania ambayo Waislamu ni majority ,wako 35% wakati wakristo ni 30%,(TAZAMA C.I.A FACT BOOK 2003) sio ajabu chama fulani kuwa na waislamu wengi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 12, 2007

    Angekuwa Raisi Lipumba huyo. Alikuwa mwanauchumi mzuri huyo Economist kabla ya kuingia kwenye siasa. Lakini naona kama udini ulimwingia nikaanza kuogopa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 12, 2007

    Mpe fact huyo mzushi anaeongelea udini na usomi kama limbukeni. He/she is neither critical nor nlytical...uninformed consumer of information.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 12, 2007

    Jamani tutumie hoja zaidi ya ushabiki. Wewe unaesema CUF ni chama cha kidini, Una ushahidi gani kwa uyasemayo au ndio nyie mlinyweshwa maji ya kijani, basi kila siku hamtaki kukubali ukweli?

    Hoja zilizokuwa zinatolewa na watu wa jembe na nyundo(CCM)japo hiyo alama kwa sasa inatia mashaka ni kwamba kwa nini CUF mwenyekiti na katibu wake ni Waislam??, wakati wao kipindi hicho Mkapa na Mangula walikuwa ni wapagani?? au sasa hivi Kikwete na Makamba ni wapagani?. Mi ninavyojua karibu watanzania wengi wana dini zao, na tusiangalie dini za viongozi au wanachama tuangalie katiba ya Chama.

    Ni wapi katiba ya CUF inasema kuwa chama chao kitaongozwa kwa misingi ya uislam?. Hizi mbegu mbaya zinazopandizwa masikioni mwa watanzania kwa ajili ya wajanja wachache kuendelea kula nchi zina tu cost siku moja wakati wao wakiwa makaburini ama hai.

    Huu ni wakati wa hoja na si wakati wa fitina na majungu katika siasa kwani mara zote fitina ni chanzo cha kuvurugika kwa amani.

    Na watanzania wenzangu hii imani mnayosema ipo haipo bali uwoga umetutawala watanzania, siku watanzania watakapo kata tamaa na ndio uwoga utaifa na CCM na "Polisi na Jeshi" lao watatumia mizinga kuwanyamazisha watanzania lakini itakuwa vigumu ku-win "hearts and mind" of the citizens.

    Hebu tuache kejeli na dharau katika siasa kama kweli tunalipenda taifa letu kwani kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote halali cha siasa anachoona kinaweza kumbadilishia mwelekeo wa maisha yake bila kujali dini au kabila lake.

    Huu ni wakati wa ISSUE sio wakati wa kuimbia watu kwaya nzuri na magita huku hawana matumaini na maisha bora.

    Strong opposition ni chachu ya kuwafanya wanaotawala kukaa mkao wa kwa heri pale wanaposhindwa kutetea au kutekeleza waliyoyaahidi.

    Tu invest kwenye research za kuleta maendeleo sio za "KUSHINDA KWA VYOYOTE", Kushinda kwa vyovyote maanaake ni kuiba kura, na kuiba kura maanaake ni kwenda na matakwa ya wengi, na ndicho tunachoshuhudia leo watu wanakaa katika miafaka isiyo na tija badala ya miafaka ya kuwaendeleza watu.

    "SOONER OR LATER" The country will be under the leadership of other part.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2007

    majority ya hao cuf walikuwa ccm halafu wakafuja watatueleza nini.hampati kitu cuf

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 13, 2007

    Anon wa 12:28:00,

    Walifuja nini na lini? Tupe basi ushahidi ili tuwashughulikie mara moja. Maana ktk kumbukumbu zetu hatuajaona jina lolote la hao CUF ktk ufujaji wowote ktk nchi ya Tanzania.

    Lakini ulete na jina lako kamili na anuani ili utusaidie baadae ktk upelelezi na ushahidi. Tunaamini hii sio HEARSAY STORY!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2007

    Unabisha nini hicho ni chama cha kidini pale ofisi ya CUF bugurunni yaliko makao makuu ya CUF ukiingia Ofisi ya Huyo Menyekiti wa Taifa Profesa Lipumba lazima Uvue viatu nje kama wafanyavyo uingiapo msikitini.

    Chama hicho si cha upinzani.Seif Sharif Hamad Katibu mkuu anakaa nyumba ya serikali hadi leo ana walinzi wanaolipwa na serikali na anapewewa pensheni yake kama waziri kiongozi mstaafu wa serikali kila mwezi.Utasema huyo ni mpinzani?

    Ukimgusa utapambana na walinzi wake ambao ni wa dola! Hivi Hawa waliotoka CCM Watatuzuga hadi lini?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 14, 2007

    Anon wa June 13, 2007 4:13:00 PM EAT inaelekea umefilisika kiakilia au ndiyo wale wavivu wa kufikiria. Hivi kuvua viatu ofisini kwa mtu au nyumbani kwa mtu ni udini? Kuna nyumba nyingi tu marekani ukiingia unavua viatu kwa sababu za ki afya au wanazojua wenye nyumba.

    Kuhusu ulinzi wa dola, Seif Sharif Hamad alikuwa waziri kiongozi wa Zanzibar. Waziri kiongozi kama waziri mkuu anahaki kikatiba ya kupata ulinzi akiwa kazini na hata anapo staafu kazi hiyo. Hivyo usishangae kumuona maalim Seif anaulinzi wa dola...ni haki yake kisheria.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 14, 2007

    UPINZANI HAUWEZI KUUNGANA KWA SIASA ZA ".KIDINI." NI ".NDOTO." WANANCHI HATUNA UDINI MNATULAZIMISHA, NAFIKIRI HII NI MBINU YA CCM YA KUUA UPINZANI.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 14, 2007

    Anon wa 7:52:00 AM,

    Naomba uje kanisani kwangu kesho ili unipe michapo yako hiyo (naamini una hakika na unachokisema). Nani anamlazimisha mwingine kuwa na dini isiyo yake?

    Naomba uje umejiaandaa unieleze kwa kirefu maana madai yako mazito sana!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 14, 2007

    ANON WA 4:13PM EAT

    Wewe kweli CCM Damu na jinsi UCCM ulivyokuathiri kifikra unashindwa hata kupambanua mambo halisi ya maisha, Hivi hapo Dar kuna nyumba ngapi za watu wasio waislam ukifika unavua viatu nyumba hizi ni misikiti???, Kama mtu kaweka Carpet la shs mill 2 ambalo ni nadhifu na safi kiasi kwamba wewe na matope yako ya kariakoo shimoni au Umeingia kwenye madimbi kwa kuua sungusungu sababu ya kutokuwa na nauli ya daladala unataka usivue viatu vyako vichafu. Loooh!!! Shame on you, usafi ni Tabia ya mtu kama wewe socks unavaa mwezi bila kufua lazima ulalamikie kuvua viatu kwa hofu ya kutoa "DONGO", Fikiria tena uje na sababu iliyoenda shule ya kusupport argument yako sio kuleta U-CCM wako hapa matokeo yake unatupaka matope wana-CCM wote tuone na mtazamo wa kuona kuvua viatu ni suala la waislam. Nakupa -100% marks kwa comments mbovu kama hiyo. Nachelea kusema Think again because you hadn,t thought as a sound human being!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...