jamaa akilipiga sop sop wanja letu jipya la neshno stedium. jana jk alilitembelea na kushauri kwamba endapo hautakamilika kabla ya siku ya mechi na msumbiji usifanyiwe haraka kufunguliwa hadi asilimia 15 zilizosalia za ujenzi zikamilike. jk pia alipiga mkwara kwamba matunzo na kuajiri kwa watu wenye ujuzi vipewe kipaumbele ama sivyo watu watatafutana ubaya. jina limebakia lile lile la tanzania national main stadium hadi itapoamuliwa vinginevyo. kuna waliopendekeza uitwe benjamin mkapa kumuenzi aliyewezesha ujengwe, wengine wamependekeza uitwe mwalimu nyerere kumuenzi baba wa taifa na wengine wametaka uitwe jina la rubani wa ndege za kivita alieanguka hapo miaka ya nyuma, kepteni karama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2007

    kweli uwanja wa taifa wa neshno stedium unatisha

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2007

    Uwanja poa sana huu lakini unatakiwa kuhifadhiwa vizuri, Sasa mtu unaenda kutazama mechi huna wasiwasi hongera wabongo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2007

    Wacha uitwe hivyo hivyo Tanzania National Stadium na SIO vinginevyooooooo !!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2007

    AISEE MICHUZI UWANJA HUU HAUNA HAJA YA KUPEWA JINA LA MKAPA WALA RAIS YOYOTE KAMA ILIVYO KAWAIDA YA WAAFRIKA. UKIZINGATIA KWAMBA NI UWANJA UNAOWEZA KUTUMIKA KWA MICHEZO MBALIMBALI JINA LITAKALOPENDEZA ZAIDI NI "THE NATIONAL SPORTS STADIUM" AU "THE NATIONAL SPORTS ARENA".
    MAJINA MENGINE NI VICHEKESHO TU KMA SIYO KIINGEREZA KIBOVU.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2007

    Uwanja wa taifa ungepewa jina tofauti kuliko kila kitu kuitwa majina ya watu na viongozi imeshapitwa nawakati.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2007

    tafadhali Michuzi watu waenziwe na ukweli wa Mambo, rubani aliyeanguka hapo kwa jina sikumbuki isipokuwa ni mtoto wa Chief Haroun Msabila Lugusha wa Sikonge, kwa jina la nyumbani Mazwazwa,sasa labda kama siasa zinaingilia lakini ukweli wa mambo ni huo!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 30, 2007

    sio siri dude linapendeza..yaani world class kabisa isipokuwa kuhusu jina sijui Karama ni nani lakini aliyeanguka hapo kama rubani wa Air Force ni Kapteni Mazwaza, mtoto wa Chifu Lugusha wa Sikonge, Unyanyembe, sasa sielewi kama siasa zimeingia hapa kupotesha ukweli, Michuzi saa nyingine inabidi ufanye homework kabla ya statement kama hizi, kuna wanaojua lakini tupo pembeni tu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 30, 2007

    jamani hiyo ni domestic MOA intatumika kukata majani ya uwanja wa taifa. serikali nunueni machine zinazotakiwa kutumika viko kama tractor but vidogo sana hata tfsc watakuwanazo,hiko kitaaribu uwanja tu.hata hivyo nawapa hongera kwa kazi nzuri iliyofanyika uwanja ni mzuri na unavutia cha kufanya sasa tafuteni wadhamini wakubwa ambao wataweza kuendesha stadium.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 30, 2007

    Wamekwisha anza tia aibu, hiyo mashine ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani---hata mtu ukitumia akili ya kawaida tu utagundua kuwa HP yake ni ndogo kukata wanja lote hilo---wabongo sijui tuko vipi?

    ReplyDelete
  10. Uwanja poa lkn huyu dereva mkokoteni mimi simuani hata kidogo ktk kutunza uwanja.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 30, 2007

    Trekta ni trekta tu, hata kama ni dogo!

    Mimi naona hicho ki-MOA kinafaa sana. Ila waongeze idadi yake, kama vitano hivi.

    Trrekta, hata kama ni dogo, linaharibu turf!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 30, 2007

    Aisee Anon wa June 30, 2007 5:22:00 PM EAT

    Hata mimi nimeshangazwa na hiyo Domestic Lawn Mower inayotumika kwa kazi hiyo ya kukata majani uwanja wa kimataifa kama huo. Yaani ina maana serikali imeshindwa kununua better Lawn Mower ambayo inaweza kufanya kazi effectively?? au hadi nazo tupewe msaada na wachina?? Kweli waafrika tuna matatizo. Hii Lawn Mower hata kwa domestic ni ndogo sana na mara nyingi ukiitumia hata majani unakosea kuyakata.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 30, 2007

    "TANZANIA MAIN NATIONAL STADIUM"??? maana yake ndio nini jamani? kiingereza nacho kigumu kweli!!!!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 30, 2007

    Kweli kamashine kadogo sana kwa uwanja mkubwa kama huo . Wajitahidi wanunue vile kama vitrekta vitahifadhi hata nguvu za kiume za mkataji .Namna hiyo ukimaliza kufyeka wanja lote hilo namna hiyo ni kasheshe au wakagomboe yale majani bandarini na walipie ushuru kama alivyo agiza JK TFF bwana?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 30, 2007

    Hilo jina la uwanja ni zuri ILA kama kweli mamlaka husika ilikuwa inataka kutengeneza pesa ingeuza haki za jina la uwanja kama vile Aseno walivyofanya kule Uingereza. Mwenye uchache mkubwa ndiye angeweza kuweka jina lake katika uwanja huo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 30, 2007

    Namuunga mkono Raisi Jk kwa kuwaonya wanaoutunza uwanja waajiri watu na lazima wame na vifaa vya kisasa sio kama hicho domestic MOA kinacho katia majani hapo huo ni udhalilishaji.Tafuteni vifaa kama tractor ndogo na wanazijua.Kuweni na upendo na mali za wananchi nyie mlio pewa kumiliki kwa kuupa matunzo.Pia wabongo wame na uchungu na mali mamoja na maendeleo ya nchi kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa moyo ili tz iendelee.Mfano wanaonesha wachezaji wa taifa star.Basi na sisi wangine tuige mfano huu kwa kuongeza juudi katika shughuli zetu na sio kukalia mizinga na rushwa kila mtu.Nchi ni yetu na kila raiya anawajibu wa kujitolea muanga ktk kuijenga kwa hali na mali

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 30, 2007

    sasa hii noma huyu jamaa hadi amalize uwanja mzima huo mgongo utakuwa umepinda nusu mduara. uwanja mzuri sana next muhimbili.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 30, 2007

    Kwanini wasitangaze na zawadi ya watu wakuname huo uwanja wabongo bwana wanapenda sifa zao wenyewe. Huku tuliko kila siku kuna mashindano ya kuuchagua jina la kitu fulani. na watu wanapewa tarehe ya mwisho. wakipata majina wanachuja na kupata jina la maana

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 30, 2007

    ni raha kuona na sisi tumeanza kusababisha kashkash kwa wapinzani wetu kwa mfano b.faso. eti chama wamejiuzulu kutokana na kipigo kutoka kwa TZ!

    http://news.bbc.co.uk/sport1/hi/football/africa/default.stm

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 01, 2007

    kwa kweli kama tuko serious , hi lawm mower ya nyumbani haitakiwi kutumika kukatia huo uwanja, naomba muombe ushauri kwa hao wajenzi au nchi jirani ni machine gani itafaa, kama hiyo tractor etc na sio domestic one.
    lakini mambo yetu yakiwa kama ya siku zote haya tuendele na domestic lawn mower

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 01, 2007

    Kwa kweli hata mimi nadhani serikali na FAT wanatakiwa wanunue mashine ya kukatia majani.

    Domestic Lawn Tractor ina cost kati ya $1500 mpaka $3000, angalau tununue hiyo. Hi mashine ya kusukuma inatudhalilisha.

    Wanja poa sana, matunzo tu .

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 01, 2007

    Anony wa June 30 @ 5:22 pm mie nakuunga mkono kuhusu issue ya kutafuta machine zilizoenda shule kuliko huo mkokoteni anaousukuma huyo mshikaji. Hizo tractor ndogo zinapatikana tena at a very reasonable price na zina range kati ya $1500 hadi $2500. Sasa jamaa wasije wakapiga bao kwa kusema wamenunua hizo trekta kwa $15,000, maana bongo kwa kupigana mabao hatujambo.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 01, 2007

    Walipewa picha ya lawn mower wakachagua the least expensive bila kujua ukweli. Huo ni utani na ndio kuharibu uwanja. na huyo mtu akitoka hapo mgogo umempinda...duh hapo mbeba box anaona kazi yake kama ni yke poa sana. Hat athe cheap tractor lawn mover could do the best job

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 01, 2007

    Isijekua mwenye tenda kapewa millioni 15 kununua profession one kaagiza hiyo.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 01, 2007

    Jamani hata kabla hawajakabizi hilo liwanja tuwaulize hela za lawn mower yetu tuliowapa ndio hiyo? Manual labor hatutaki tena.

    We need a good one

    Tusilaumu serikali hilo wanja bado hatujakabidhiwa hivyo wanatumia the cheap cheap one siku wakitupa tutawauliza the good good one iko wapi??? Nadhani ilikua included kwenye contract he he he ehe

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 01, 2007

    Kwanza hao wafanyakazi lazima wawe na uniform,lazima tuheshimu huo uwanja.Naunga mkono watu washindane kuchagua jina la kiwanja..sio lazima liwe la Kiongozi..kila kitu Tz kitakuwa na jina la kiongozi while kuna majina mengi mazuri

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 02, 2007

    Iangalieni kwa macho na akili hiyo lawn mower! Sio manual, jamani! Kwani hiyo mashini juu ya sehemu ya majembe ni ya nini? Hizo waya kutoka kwenye mashini hadi usukani wa mwendeshaji ni za nini?

    Mwendeshaji anaonekana kana kwamba anasukuma manually. labda hakufundishwa namna ya kuongoza mashini hiyo. Amezoea hizo za manual ndio maana simama ya namna hiyo.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 02, 2007

    Wengie mnaropoka ropoka tu.

    Nakubaliana na Uwanja wa Nyasi kuwa mashini hiyo si manual! Hiyo mashini ni sawa na hizo zitumikazo katika kula theluji huku kwenye nchi za theluji!

    kama alivyosema, trekta linaharibu the turf. Kwa hiyo walioleta hiyo mashini...natumaini ni hao hao waliojenga hilo wanja, walijua!

    Cha maana ni kuwa na mashini za namana hoyi kama tano hivi ili kufanya kazi upesi.

    Acheni kuropoka. Mwulizeni Michuzi, ambaye ameiona mashini hiyo, kama kweli ni manual!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 02, 2007

    Jamani Mliotoa maoni kuhusu hiyo mashine hata mimi nawaunga Mkono. Lakini hebu tusipende kulaumu Serikali kwa kila kitu. Ukweli Huu uwanja badoupo chini ya Mkandarasi na Serikali bado hata kukabidhiwa kiwanja. Kwa hiyo kama ni mashine ya Domextic use hilo bado lipomikononi mwa mkandarasi. Inaonyesha kuna wadau wao wanaugonjwa wa kukosoa serikali tuuuuuu. Bila hata ya kufikiria ukweli nani alaumiwe.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 02, 2007

    S.alaikum wadau pls. nijulisheni lini huu uwanja utafungulia rasmi na mimi nipate kuja Bongo, Naishi Muscat na hamu niwepo siku ya kufungua uwanja.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 03, 2007

    Mwahahaaaaaaaaaaa, sasa uwanja mkubwa wote huo atamaliza saa ngapi?
    Yaani wanatujengea uwanja kama huo lakini hawana kigari cha kuufyeka?
    Kweli tuko Afrika haahhaaaaaa

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 03, 2007

    daim!!! is he gonna finish kweli na usawa huu wa lawn mower ya kukatia back yards?? They better buy big equipment or something!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...