prodyuza josiah kibira keshaanza kazi ya kushuti 'bongoland II' toka juzi. hapa yuko lokesheni na trupu lake

mpiga picha wa filamu ya bongoland II akiwa mzigoni


mama thecla mjata ambaye ni mmoja wa waigizaji akipata maelekezo
stelingi wa bongoland II peter omari atayecheza kama juma (shoto) akitambulishwa na gervas kasiga kwa maekta wa bongo. kazi ya kushuti filamu hiyo inayoonesha itakuwa moto wa kuotea mbali imepamba moto na prodyuza josiah kibira ametahadharisha wanaijeria wakae mkao wa kula kwani kaja kuwashika...
kwa habari zaidi nenda bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2007

    HAYA sasa wanasinema wa tanzania mungu atupe nini? wakati wa kuachana na takataka cheap za kinigeria umefika.huyu bwana ni mtengenezaji sinema serious japo ni ktk medium ya video
    kwa hakika hii ni baraka na ni nafasi kwa wanasinema watanzania hasa behind the camera KUJIFUNZA
    na ninasikitika sana kwa kweli sioni mashamsham ya wansinema wa kitanzania juu ya kaka yetu kibira ,wanasinema wa bongo mpo wapi au mlitaka awe mnigeria ?
    msione aibu jamani nendeni kumsapoti huyo bwana ,mpeni ushirikiano wenu,ulizeni maswali ya kiteknikali huyo bwana knows the best about film making
    msiache pia kununua sinema zake mziangalie critically mtaona tofauti ya melodrama,soap na feature film feature,
    brother kibira asante kwa kuleta production nyumbani ,fungua milango wakaribishe kwenye sets na locations zako ili tujifunze kutoka kwako
    great job kibira.
    Raceisnobar

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2007

    Ila naye asije akatumbukia katika ulimbukeni wa 'taito' ya sinema kuwa kiinglishi wakati sinema yenyewe ni ya kiswahili

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2007

    naunga mkono hoja za jamaa hapo juu. unajuwa wanigeria filamu zao zote mwisho wao ni mmoja ni KUOKOKA tu hata kama theme sio ya kidini itapelekwa huko kwa nguvu. suluhisho la tatizo fulani katika jamii huwa ni mtu KUOKOKA na kuwa MLOKOLE. kwa hilo filamu zao zinaboa sana.

    huyu mshikaji ni bora amekuja kuwaonesha watz kuwa nao wanaweza kutoa filamu zilizo bora na za kiwango cha kimataifa. big up kwa sana. ondoa takataka za kinigeria tz.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2007

    Michu,mimi naomba niulize kwa nia njema tu,hii movie itaektiwa kwa kiswahili ama king'eng'e?nauliza kwa sababu kama ni kwa ajili ya soko la afrika mashariki kiswahili is ok,lakini kama tunataka kula sahani moja na wanigeria basi hatuna njia itabidi tukubali picha zetu zichezwe kwa kiingereza kisha tuweke sub titles za kiswahili,au mnaonaje wadau?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 07, 2007

    Namtakia kazi njema ndugu yetu kibira. Kutengeneza filamu si kazi lelemama inahitaji kujituma haswa na kwa satili ya wasanii wetu na hao wanaojiita madirector /maproducer wasizanie ni mchezo mchezo inabidi wakaze mkanda kama wanataka wafikie tulipofikia sis wengine.Muhimu wajitahidi kupata elimu ya utengenezaji filamu na hizo video waende hata vikozi vifupi vifupi itasaidia kuwafungua macho. Hivi karibuni nilimpigia simu super star wa bongo nikitaka kujua kuhusu equipments walizonazo na timu ya watu wao kulikuwa na jamaa zangu wankuja kufilm huko kazi nzuri tu jamaa walishindwa hata kunielezea matokeo yake wanakata simu aibu kweli na hiyo ilikuwa nafasi nzuri kujifunza na kupata contact.

    Napenda kuuliza swali moja tu ni vipi Kibira amewashirikisha hao maproducer/ directors wa bongo? Ninavyojua mimi kila mtu anataka asikike yeye tu hawezi kukubali kusikia michuzi naye alishiriki kama director. Bado safari ndefu sana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 07, 2007

    kuna hilo dirisha la gesti haus lenye rangi ya kijivu. Nini kimewavutia kwenye hiko chumba? Namzungumzia huyo jaa anaeshuti kitanda kitupu.
    Labda dhamira ni kuonesha umaskini...hayaaaaaa!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 07, 2007

    anony wa Tarehe July 7, 2007 9:52:00 AM EAT

    Nimekusoma ila nafikiri si lazima kiingereza kwani kuna movie kama TSOTSI imeigizwa kwa kizulu na wameweka subtitle za kiingereza na imepewa mpaka osca award nadhani ni utengenezaji tu movie iliyopikwa hata ikiwa kijerumani utaelewa tu tafuta DVD ya TSOTSI angalia hadi mwisho yule director anaelezea kuwa alikuwa akitengeneza movie bila maneno kwa kuwa hakuwa na mtaji mwanzoni na zilinunuliwa sana na hata wewe ukiona utaona kwali zinaelewweka na baadae kaja na TSOTSI na amefanikiwa nadhani kinachohitajika ni kazi makini tu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 07, 2007

    Nakuunga mkono hapo juu, ulimbukeni wa watanzania kuwa ukitumia kiingereza ndio bora unachangia kurudisha maendeleo ya wasanii. Watu watapenda kuona sinema au muziki wa kitanzania ili kuona utanzania pamoja na lugha. Ndio maana sinema za kihindi zimeendelea kwa lugha zao mavazi yao nyimbo zao na subtitles za lugha nyingine. Wana muziki mashuhuri Africa,Miriam Makeba hugh masekela, Ladysmith, Salif keita, Fela, wanamuziki maarufu wa Congo na wengineo wengi walitumia lugha zao na mitindo yao. Hivyo tusiogope kuwa watanzania katika lugha na mitindo.wakati mwingine watu wanafurahia kitu tofauti katika ulimwengu uliofurika na vitu mbalimbali.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2007

    Anon wa hapo juu nakuunga mkono kabisa kitu muhimu ni hadithi yenye kuvutia.Picha si lazima iwe na sauti kwa mfano picha tunazoita experimental film hamna sauti kabisa ni sound na background music lakini ukiangalia unaelewa vizuri sana na ni mwanzo mzuri wa kuingia hatua ya pili ya utengenezaji filamu kubwa.
    Kwahiyo hata tukitumia kiswahili na hadithi ikawa nzuri basi tutauza tu hizo filamu zetu mfano angalia wafaransa, wajerumani, warusi, tena warusi wanadirector wao ambaye alichangia sana katika kuweka muelekeo wa filamu duni anaitwa Eisenstein na mwenzake wa Ufaransa Bazin wao walikuwa wanatumia lugha zao lakini mpaka leo watu wanasoma habari zao na staili za utengenezaji film walizozianzisha kwa sisi afrika tulikuwa naye Ousmane Sembene yeye katumia lugha ya kwao lakini filamu zake zimeshinda tuzo nyingi tu na kwa sasa karibu vyuo vikuu vyote duniani wankofundisha mambo ya filamu inapofika kwenye third cinema bazi wansoma na kuangalia za Ousmane sembene.
    Tutumie lugha yetu kiswahili na kuweka subtitles za kiingereza.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2007

    hyo anoni hapao juu amesema kweli nakuunga mkono watanzania lazima tukubali hataujui na tukubali kujifunza suala la utengenezaji sinema hata kama teknolojia inaruhusu yeyote yule kumiliki vifaa japao vya video jamani ni VIZURI TUZINGATIE kanuni husika za utengenezaji sinema
    ukiangalia sinema za tanzania hasa hizi za siku hizi (video)zinazotengezwa kila kukicha .hasa ukiangalia pasi na sauti utaona ni vigumu sana kupata hadithi ya hiyo sinema.tena actors wanafanya juhudi kweli kupayauka na kutuambia sisi watazamaji ni kitu ganai anachointend kufanya au anachofanya ili sisi tuelewe hii siyo sinema sababau sinema kimsingi ni sanaa ya kuelezea hadithi au tukio kwa kutumia mwanga
    hebu angalienieni sinema ya Totsi ya afrika ya kusini,Tusamehe-kibira films (mtanzania) Cape of good hope (south africa) pamoja na hizi za holiwud jaribu angalia bila sauti kwanza mara kadhaa kisha angalia ikiwa na sauti then angalia ni kiasi gani umeweza kuelewa kinchosinemiwa!
    maproducer na directors wa tanzania acheni mzaa wenu huo ni sinema zenu za nigeria kuwa eti ndo kipimo kipimo chenu sasa kimewasili nyumbani mwenzetu kaka yetu kibira anaujuzi wekeni misifa yenu chini unganeni naye awafundishe ni vigumu kila mmoja wenu kuwapo ktk set basi hata ka-workshop tuu kadogo ombeni huyo bwana ni mwansanaa haswa hana hiana atawafundisha au kuwapa siri muhimu za utengenezaji vipaji nyumbanai tunavyo lakini kipaji pekee hakitoshi na vema tuakapata kuwa refined ktk muelekeo au standard zinazokubalika ili siku kwa kutumia hivyo hivyo vipaji vyetu vya nyumbani
    akhsanteni

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 09, 2007

    hata kama tupo maskini, hivyo vyumba vingetiwa soap soap! kidigo,
    huko juu ya kabati ni nini??
    au hawakupata nyumba nzuri kidogo, hata Nigeria kuna nyumba mbaya but unachagua, hata kama unapotrait umaskini but sio urough

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 09, 2007

    Nafagilia movie za tanzania ziwe za kiingereza tukitaka masoko nje ya nchi.
    Movie za nigeria wote tunaangalia kwa vile tunaelewa wanachosema.

    Foreign movies zina wapenzi wengi lakini ni lazima iwe imesikika kikweli kweli na director awe ni maarufu ulimwenguni. Nina rafiki yangu ni mpenzi wa foreign movies sana tu. lakini zote zime ziko kwenye academy nomination kwanza ndio ataenda kuzirent.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 11, 2007

    THECLA MJATA!!! MAMA AMEANZA ZAMANI KWELI LAKINI HAZEEKI KEEP IT UP MAMA U R OUR TANZANIAN ELIZABETH TAYLOR

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 11, 2007

    Ni heri kutengeneza za kingereza na kuziuza. Huyo anayesema sijui movie gani ya kizaire ilikwenda kwenye osca sasa si herui ugamble na masoko kuliko kugamble osca award.

    kama unataka kuuza kwa wingi nenda na lugha ya kimataifa kama unajiamini kuwa itafika kwenye oscar basi nenda na lugha ya kiswahili

    ReplyDelete
  15. Hey Michuzi,

    Asante sana kwa kupoisti picha. Leo ndo nimeweza kuziona.

    Kujibu hoja za wasomaji, sinema inactiwa kwa kiswahili. Josiah mkali, mtu akitoa phrase ya inglishi inabidi washuti tena kwa kiswahili. Shooting inaendelea vizuri sana, tuko on schedule. Nadhani watazamaji watafurahia car chase Manzese.

    Mengine baadaye.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...