mie na chemi tukipozi na reginald mhango, bosi wetu wa zamani deiliniuzi. huyu mzee ndiye aliyetufundisha a-e-i-o-u za uandishi mimi na wengi wengine kiasi ya kwamba yeye ni zaidi ya bosi; ni baba yetu na mchango wake hatuusahau kamwe. yeye ndiye aliyekaribisha trupu la watengeneza filamu ya 'bongoland II' kutumia nyumba yake magomeni mikumi. hatuna cha kumlipa ila kumuombea maisha mema na marefu na tutazidi kumghasi kwa kuchota ujuzi na busara zake, na yeye haoneshi kuchoka kufanya hayo. chemi yupo bongo kucheza katika hiyo filamu ambayo imeanza kushutiwa juzi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2007

    Michuzi,
    Vipi umepata nyepesinyepesi toka Sweden kuwa mshikaji wako mkuu Nyupi katiwa lupango akiwa na unga.
    Tuletee yote yote na kundi la mshikaji wako

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2007

    wewe anoy wa hapo juu vipi? mbona unakuwa su muungwana? mambo ya mshikaji kukamatwa na unga utayawekaje katika blog? hiyo ni ishu private huwezi kuianika ulimwengu mzima. michuzi achana nae huyo jamaa haelewi atendalo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2007

    hawa wazee walikuwa waadilifu sana,angalia sebule yake ilivyo simpo baada ya kufanya kazi ya umma iliyotukuka kwa miaka mingi.vijana wa leo wape ujiko kama wa huyu mzee kisha uone kazi,utashtukia ana baloon,nyumba mbezi,watoto inteneshno sku.... na kaza wa kaza,kumbe udokozi tu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2007

    We anony wa July 7, 2007 9:57:00 AM EAT sio kwamba vijana ndo wezi, tatizo viongozi wetu tena watu watu wazima ni wabinafsi sana, Sasa kutokana na hilo na kijana akipata nafasi anaitumia kupora awezavyo, sababu haina maana wewe kujifanya mtakatifu wakati viongozi wetu wanapola mali zote, wewe ukijifanya muadilifu utashangaa wenzako wanaishi kama wafalme wakati wewe ni omba omba hapo ndo utaijua Tanzani.

    Kwa hiyo na wewe ukipata upenyo utumie vinginevyo itabaki historia kuwa uliitumikia serikali muda mrefu lakini hukuvuna kitu.

    ANABEM

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2007

    Yaaani uungwana ni pale tunashabikia kubeba unga, sikuelewi hata kama rafiki yetu akifanya kitu kichafu ni lazime tuseme ili na wengine wasirudie.
    Hii ni aibu kwetu sis wote watanzania, juzi tu si uliona Michuzi ameka peupe uchafu wa washirika wa Jack Pemba?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...