mshiriki wetu katika bigi braza 2 richard akiwa na mai waifu wake siku ya harusi ilofanyika dar. sio vibaya tukaendelea kumpa saposti angalau kwa kujiunga na marafiki katika linki hiyo chini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Kuna namna ya kumdokeza ili aoshe nywele zake? Anatia aibu, na zile nywele zitakuwa zinanuka mpaka sasa kwani wenye rasta wote tunajua kama hazioshwi mara kwa mara zinatoa harufu!!

    ReplyDelete
  2. Kama zako zinanuka basi hata za wenzio? wewe labda ni wale rasta wa pwani wanaopara samaki LOL

    ReplyDelete
  3. Huyu Jamaa ana jina la kikaburu na vile vile ameoa mzungu, uraia wake kwa kweli unanipa wasiwasi.

    ReplyDelete
  4. Huyo anaesema haoshi nywele ana lake jambo! Sio rasta wote wachafu km wewe uliemponda mwenzako! Wapo wanaume ambao hawana rasta lakini wachafu kuanzia soksi akivua lazima upate flue na akiongea mdomo unanuka kuliko choo hapo bado kikwapa! Richard ni msafi nywele zake anazipa treatment zote za kidread sio mchafu mchafu km unavyoponda wewe! kama humjui na huna cha kutoa comment kwani lazima uandike? Watanzania bwana! ndio maana hatuendelei hatupendani ata kidogo! Wivu tu unawasumbua namfagilia vibaya waaa Richard keep it up! tuko pamoja! usituangushe, isiwe haire wakati unajichana nyama utapoteza point mwanawake! Wewe ni ndugu damu ya TZ ata km wanaponda kaza buti ndio mwendo binadamu wote hatufanani kuna watu kazi yao kuchafulia watu hawawajui na hawana kazi yakufanya nikuchaguachafua majina yawatu na kuponda kutumia blog hii! HAMIJEY

    ReplyDelete
  5. what a nice couple, they look lovely, bless, may there mariage last forever-mdau England

    ReplyDelete
  6. Huyo dada atanenepa kweli. Kapendeza lakini. Naona jamaa anaturinia mzungu wake. Haya.

    ReplyDelete
  7. Hongera Richard, nimeingia hapo Bro Michuzi alipotuambia tubofye, nimeona a lot of good comments, ila comment moja imenisikitisha sana, inayotoka kwa aliyejiita Dada mtu wa Richard, amesema kuwa marafiki zake yeye dadamtu anaoishi nao Marekani hawajamsaidia ktk kumpigia kura or so kaka yake, na akasema Hao marafiki zake wasimjue jue siku wakipata matatizo ya Misiba..well??? Was there a need for this?, hata kama watu hawajamuunga mkono kaka yake, dada huyu hatakiwi kulipiza kisasi especially wenzake hao wakipatwa na shida, yeye atumie ile methali isemayo TENDA WEMA UENDE ZAKO. Kwa kweli comment yake hiyo imenisikitisha sana.

    All in all, Tumpigie kura mwenzetu huyu siku za kupiga kura zikifika, comments za kijingajinga za dada yake zisitukwaze.

    NY nawakilisha

    ReplyDelete
  8. Wadau hebu nifahamisheni, hivi kwa wabongo kushiriki bb ni lazima uwe mulat? yule wa kwanza mlevi alikuwa mulat, na huyu tena anaonekana mchanganyiko.

    ReplyDelete
  9. jITANGAZE lAKINI lIKIKUKUMBA fAGIO LA uMASIKINI kAMA yULE bBA aLIYESHIKA nAFASI yA pILI, uSIJE kULIA kILIO cHA mBWA.
    mWENZIO aLIFANYA vIZURI nA aKASHIKA nAFASI yA pILI. aKAWA bONGE lA cELEBRITY. uLIZA aNAFANYA nINI hUKO kWAO mOROGORO. mUUZA cHIPS, mISHIKAKI nA mAYAI yA kUKAANGA kWA cHACHANDU yA nDIMU kALI nA pILIPILI yA mBILIMBI. cIAO.
    (sKAVENJA)

    ReplyDelete
  10. Misupu jiandae kupata visitors wengi hapa. Page hii ya Rich na Rikki imepaishwa kwenye blog ya Big Brother.

    [url]http://www.mnet.co.za/profiles/bba/ForumListing.aspx?bid=10&tid=604[/url]

    ReplyDelete
  11. Anony wa kwanza katoa comment kwamba Richard aoshe nywele kwa sababu tangu "wapigane vita vya rangi" inaonekana hajaosha nywele. Anony wa pili karukia kuuliza/kikejeli eti kama rasta za anony wa kwanza zinanuka sio hata na za wengine. Anony wa tatu karukia eti "sio rasta wote wachafu" Sidhani kama anony wa kwanza alisema marasta ni wachafu.

    Jamani, hata kwenye yale maandishi yanayopita chini ya screen za TV watu kibao wamecomment kuhusu kuosha rasta zake zenye rangi, sio kwamba jamaa ni mchafu bali nywele zake bado zina rangi basi azioshe - sasa tatizo lipo wapi? Sio chuki wala nini ila tu kushauriana mimi nadhani.

    Asipo angalia hilo ndilo litakuwa downfall yake mule ndani. Isitoshe, alipewa jukumu na akashindwa na anakuwa mbishi.

    Eniwei, tuone itakuwaje - lakini nakubaliana na anony wa kwanza kwamba aoshe nywele zake kutokana na ile rangi. Nionavyo mimi, ati!

    ReplyDelete
  12. very Nice ........... M, Kenya

    ReplyDelete
  13. wabongo watu wa ajabu sana.kwanini hatupendani?always ni watu wakuongea negative about ur fellow tanzanians,nia aibu sana.hakuna mtu anyechemka kwenye big brother kama lerato lakini wa south africa wenzake wanamsupport sana no matter the criticism juu yake.kwa kumponda mwenzetu,tunajenga au tunabomoa?acheni ushamba kwanza wengi wanaoongea wanafuatilia mara mojamoja au kwa kuibia kama umeangalia diary session ya jana even big brother alimuuliza richard kama aletewe kitu cha kutoa rangi kichwani rangi haiwezi toka kwa shampoo na conditioher tu.hata Merly haijatoka kichwani na hata nguo hazijatoka rangi.its a shame my fellow tanzanianas.tuwe tunapeana support,acheni ushamba baadhi yenu.tuwe civilised kidogo.wivu tu

    ReplyDelete
  14. Mbongo atia aibu

    2007-08-15 18:59:22
    Na Amour Hassan


    Mwakilishi wa Tanzania katika jumba la Big Brother Africa II, Richard Bezuidenhout, 25, alivaa kimini na sidiria katika onyesho la vipaji na kuonywa na Big Brother kuwa ataadhibiwa vikali kama ataendelea kubishana na bosi wa jumba hilo (Big Brother mwenyewe) katika matukio mawili tofauti ya wiki ya kwanza ya shindano hilo.

    Richard, ambaye alianza ushiriki wake kwa kujitenga na wenzake hadi kuanza kuandamwa na `meseji za sms` za watazamaji zinazopitishwa kwenye TV, ambazo hata hivyo washiriki hawazioni wakidai kuwa `anaboa` na atolewe kwa vile anaonekana kummisi mkewe, alionywa na Big Brother katika siku ya tano ndani ya jumba hilo baada ya kuitwa katika chumba maalum cha maswali cha `Diary Room`.

    Katika siku za kwanza, Richard alikuwa akibishana na Big Brother kila alipoitwa katika chumba hicho, lakini siku hiyo Big Brother ambaye haonekani na husikika sauti tu, alimuonya akimwambia: ``Uko katika jumba la Big Brother, na Big Brother ndiye anayetunga sheria, hakuna maafikiano. Kama utaendelea na tabia yako utaadhibiwa vikali.``

    Awali, Richard alipoitwa katika chumba hicho aliambiwa na Big Brother kuwa ameitwa humo kwa habari mbili - moja njema na moja mbaya.

    Akaanza kwa kumpa habari mbaya, ambayo ni onyo hilo na kisha akampa habari njema ambayo ni pongezi ya siku yake ya kuzaliwa ambapo alikuwa akitimiza umri wa miaka 25 na akampa na keki ya `bethidei` iliyopambwa kwa mishumaa ambayo alirejea kuizima na kufurahi pamoja na wenzake 11 ndani ya jumba hilo.

    Tukio la kuvaa sidiria na kimini, lilikuja katika siku ya saba ndani ya jumba hilo ambayo ilikuwa ni Jumamosi ambapo washiriki wote 12 walitakiwa kuandaa jambo la kuonyesha kipaji walichonacho.

    Mshiriki Jeff, 23, kutoka Kenya alielezea uwezo wake wa kutunga vitabu na kimwana mwakilishi wa Uganda Maureen, 27, alicheza ngoma ya asili na kupiga msamba wakati Mtanzania alitoa kituko kilichomuweka katika wakati mgumu kwa kupanda stejini akiwa na kimini na viatu vya mchuchumio.

    Akaanza kusema ``haijalishi nini mtu amevaa, daima atabaki kuwa vile alivyo.`` Kisha akavua shati alilokuwa amevaa akabaki na sidiria na kimini na akasema: ``Kwa mfano mimi nitabaki kuwa mwanaume hata kama nimevaa hivi. Najivunia kuvaa hivi niwapo nyumbani kwangu na mke wangu.``

    Jaji Randall aliyekuwa akitoa maoni pamoja na jaji wa kike Marlouw, alimwambia Richard: ``Ikiwa kwa wiki tatu tu umeshadata hivyo, sijui itakuwaje baada ya miezi mitatu.``

    Na jaji wa kike Marlouw alimwambia:``Nilikuwa nakuamini kuwa wewe ni mwanaume mwenye mvuto zaidi kwenye jumba hili lakini leo umeniangusha.``

    Mjadala huo haukuishia hapo kwani baadaye usiku wakati Richard akipiga stori za kawaida na memba wenzake wa jumba hilo alijikuta katika wakati mgumu na kulazimika kujitetea kuwa yeye si shoga.

    Mwakilishi wa Malawi Code Sangala, ambaye katika vipaji yeye aliimba wimbo wa kienyeji akipiga na gita lake ambalo hulitumia kuwaburisha wenzake katika jumba hilo, alimkomalia zaidi Richard ambaye hadi alianza kuwa mnyonge.

    Alimwambia: ?Usikitetee kitendo chako cha kuvaa sidiria, kimini na viatu vya mchuchumio kwamba ni cha kawaida? si cha kawaida kwa wengine kama mimi.

    Wewe unasema mkeo hakushangai nyumbani kwako ukivaa hivyo, lakini kama rafiki yangu wa kike angeniona mimi nimevaa hivyo, angeshangaa sana kwamba `he huyu amekuwaje tena?``.

    Jumapili ijayo washiriki wataanza kutajana wenyewe kwa wenyewe kupendekeza majina mawili ya watakaopigiwa kura ya kutoka katika jumba hilo ambalo linamulikwa kwa kamera 28 zilizotapakaa kila kona kwa saa 24 zote za siku.

    Mshindi atapatikana baada ya siku 98 na atajizolea kitita cha dola 100,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 130 za Kitanzania.

    Miaka minne iliyopita wakati shindano hilo lilipofanyika kwa mara ya kwanza, Tanzania iliwakilishwa na Mwisho Mwampamba aliyefikia hatua ya fainali kabla ya kuzidiwa kete kidogo na kimwana Mzambia Cherise Makubale.

    Richard, mzaliwa wa Ilala, ana mke mzungu raia wa Canada mwenye umri wa miaka 28 na ni mshiriki pekee miongoni mwa washiriki wa Big Brother II aliye katika ndoa.

    SOURCE: Alasiri

    ReplyDelete
  15. Wadanganyika kwa ushamba bwana wa kupenda foreigners bwana, sasa mwajigonga kwa richard na dada yake kwa vile richard kaoa mzungu, mnafikiri mtaamka siku moja mmebadilika kuwa wazungu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...