wachache, kama wapo, wameshawahi kumuona marehemu mzee kaduma akiwa amenuna

marehemu mzee kaduma akimkabidhi jk risala aliyosoma siku ya ufunguzi wa tamasha la utamaduni na sanaa chuo cha sanaa bagamoyo mwaka jana

popote palipokuwa na ngoma ama mambo ya sanaa sio tu alikuwa hakosekani bali alikuwa katikati ya eneo la tukio

aliheshimika na kila mtu, hasa kwa vile naye aliwaheshimu wote - wakubwa na wadogo

mzee kaduma daima alikuwa smati na anaondoka akituachia majonzi mazito ya kupotelewa na lulu ya sanaa na utamaduni iliyotukuka.

MSANII mkongwe wa sanaa za maonesho nchini, Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma, aliyefariki dunia jana mchana kwa maradhi ya kupooza (stroke) anatarajiwa kusafirishwa leo Ijumaa kuelekea nyumbani kwake Bagamoyo na baadaye kijijini kwake Itamba, Iringa, kwa Mazishi.
Enzi za uhai wake marehemu mzee Kaduma aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa la Lugha ambayo kwa sasa imebadilishwa na kuwa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni.
Baada ya kustaafu Serikalini marehemu mzee Kaduma aliendelea na shughuli za sanaa akiwa kama kiongozi na mtendaji katika sanaa za maonesho ikiwamo ngoma na maigizo.
Alikuwa mwanzilishi wa Kituo cha Sanaa za maonesho Tanzania (TzTC) na Taasisi ya sanaa za maonesho Mashariki mwa Afrika (EATI) ambapo pia alikuwa Katibu Mtendaji wa kwanza wa asasi hizo.
Aliamua kupumzika kuzitumikia asasi hizo mwaka 2003, ambapo aliendelea na shughuli zake za kawaida za kufundisha masuala ya sanaa katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo akiwa kama mkufunzi mwalikwa katika Idara ya tamthiliya ambapo alikuwa akifundisha somo ya uandishi wa michezo ya kuigiza kazi aliyokuwa anaedelea kuifanya hadi kifo kilipomkuta.
Marehemu Kaduma pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Hakimiliki (Cosota) hadi kufa kwake, kazi ambayo aliifanya kwa ufanisi na uelewa kiasi hata kuamsha wasanii katika kuona umuhimu wa chombo hicho na kujisajili wao na kazi zao kwa wingi kuliko wakati wowote wa uhai wa Cosota.
Kwa mara ya mwisho, marehemu mzee Kaduma alifanya onesho akiwa msanii wa kujitegemea mwezi Juni mwaka huu, wakati wa semina maalum ya kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, iliyoandaliwa na Mfuko wa Utamaduni Tanzania ambapo alitamba na shairi la 'Naililia Tanzania'.
*KWA MUJIBU WA RATIBA ILIYOTOLEWA USIKU HUU NA KAMATI YA MAZISHI INAONESHA MWILI WA MAREHEMU MZEE KADUMA UTAAGWA ASUBUHI SAA 4 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI, KABLA YA KUPELEKWA NYUMBANI KWAKE BAGAMOYO AMBAKO UTAAGWA NA WAKAZI WA HUKO NA SAA NANE SAFARI YA KUMSAFIRISHA ITAANZA SAA 8 MCHANA KUELEKEA KIJIJINI KWAKE ITAMBA, IRINGA, KWA MAZISHI
MOLA AILAZE PEMA PEPONI ROHO YA MPENDWA WETU MZEE KADUMA
AMINA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mwenyezi mungu ndio mtoaji na kwake yeye wote tutarejea R.I.P HON .G .KADUMA pole na salamu za rambirambi ziwafikie ndugu na jamaa wa mzee Kaduma.pole Zilaoneka Kaduma.G.Kaduma ni Msanii mtendaji cultural activist,actor poet,writer,instructer,Teacher and Cultural Guru of the United Rep of Tanzania, wanafunzi wa Chuo cha Sanaa kwa ujumla tutakumbuka na kuuenzi mchango wako msingi katika kuiendeleza Sanaa ya muafrika ulimwenguni.R.I.P

    ReplyDelete
  2. Kwa mpitio wa haraka haraka, wakati mwingine, unafikiria anafanana kidogo na Jaji Joseph Sinde Warioba, kasoro urefu!

    Tusisahau, miaka ya kumalizia 1960s alikuwa mwalimu Chuo Kikuu Mlimani! Wengine (wanafunzi) tulimwacha hapo chuoni mwaka 1970.

    Godwin Kaduma, thanks a million for the deserving and exemplary role model to many youngsters!

    ReplyDelete
  3. Mungu Amlaze mahali pema!Nasikitika sana wasanii hawa wanapoondoa dunia , hasa ya sanaa ya Tanzania. Hawa ndio watu waliokuwa pamoja na yote, hawa kuacha kusaidia kukuza sanaa ya Tanzania kama ya Kitanzania.

    Sasa hivi kuna watu wanafikiri kuwa Ngwasuma kwasababu maarufu, ndio sanaa asili ya Tanzania. Hukwe Zawose kaondoka ambaye alikuwa anacheza angaza Kaduma, Kaduma sasa kaondoka
    DUH!
    .....NAAACHA!
    Ni maskitiko tu....
    kama kuna Mtu hanielewi...

    ReplyDelete
  4. NI MAJONZI MAKUBWA KWA TUNAYEMFAHAMU KATIKA MAISHA HAPA DAR HASA KATIKA SANAA,MIMI BINAFSI NIMEPOKEA TAARIFA HII KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA KIFO CHAKE,MUNGU AWAPE NGUVU WANAFAMILIA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MSIBA WA NDUGU YETU KADUMA.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI,AMINA

    ReplyDelete
  5. Nami naungana na wadau wote kutoa pole kwa wale wote na watanzania kwa ujumla tulioguswa na msiba huu kwa karibu. Njia bora ya kumuenzi ni kuyaendeleza yote mema aliyoyasimamia na kuyafanya. Hii no njia ya kila mmoja nasi tujiandae.

    ReplyDelete
  6. Michuzi,
    Sikuwahi kumfahamu marehemu awali lakini hiyo picha ya Mwisho ya Mzee Kaduma "akiwa smart" akitembea imenigusa sana..

    Ni kweli amutuacha lakini siamini kama ametupa mgongo kama anavyoonekana ktk hiyo picha.

    Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi amen

    ReplyDelete
  7. Ni masikitiko makubwa kumpoteza mzalendo kama huyo, Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Hata hivyo ninavyofahamu mimi marehemu alikuwa na mke/wake na watoto lakini lolote halijasemwa juu ya hao waliobaki!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...