KUTOKANA NA MSIBA MZITO ULIOTUKUMBA WA KUONDOKEWA NA MPENDWA WETU HAYATI MZEE GODWIN KADUMA, KWA HESHIMA NA TAADHIMA NDUGU WADAU KWA MOYO MZITO NAOMBA KUSITISHA SHAMRA SHAMRA ZA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA MIWILI YA GLOBU HII NILIYOPANGA IDUMU KWA MUDA WA SIKU TANO KUANZIA SEPTEMBA 25, 2007.
HIVYO KWA UNYENYEKEVU NAOMBA KUSITISHA MVUA YA SALAMU ZA PONGEZI NYINGI ZIKIWA ZIMEAMBATANA NA PICHA TOKA KILA PEMBE YA DUNIA ZILIZONINYESHEA TOKA JUZI NA KUNIFANYA NIJISIKIE KUHEMEWA KWA FURAHA KUONA NAMNA WADAU MNAVYOUNGA MKONO GLOBU YENU HII YA JAMII.
HIVYO NAOMBA NIPOKEE HIZO SALAMU KWA PAMOJA NA KUSEMA AHSANTE KWENU NYOTE MLIOTUMA NA AMBAO MLIKUWA MNATAKA KUTUMA. MOYO MLIOUONESHA NI CHANGAMOTO KUBWA SANA KWANGU KUKAZA BUTI NA KUENDELEZA LIBENEKE ILI NIHITIMISHE MATARAJIO YENU. NAMI NAAHIDI KUFANYA HIVYO, INSHAALLAH, TUOMBE AFYA NA UZIMA.
NI IMANI YANGU MTANIELEWA NA KUKUBALI OMBI LANGU. KWA MARA INGINE NASEMA AHSANTE SANA WADAU WOTE, MUNGU AWAJAALIE KATIKA SHUGHULI ZENU ZA KILA SIKU.
MICHU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mungu amlaze mahali pema peponi

    Ni uchungu kupoteza mtu mwenye sifa zote hizo lakini tunatakiwa kushukuru Mungu kwa kila jambo.

    Kam unavyoonyesha picha za huyu mzee wetu akiwa na tabasamu basi na sisi tungemuenzi kwa kutabasamu tu....Honesty week hii toka salamu zinaze pande zote za dunia nimekua nikifungua blog yako zaidi ya mara tatu kwa siku...Ilikua inanipa tabasamu sana kuona picha mbalimbali za watu kote ulimwenguni....DON"T STOP your celebration.

    Haya ni maisha na tucelebrate maisha yake kwa tabasabu.....

    RIP

    ReplyDelete
  2. Ujumbe wako unaeleweka.

    Wengi twakukumbuka pale Mlimani miaka ya kumalizikia 1960s.

    Kazi aliyotenda popote pale Tanzania imezaa matunda mengi nchini!

    ___________________________________

    Michuzi, najua wewe ni "photo journalist".

    Tafadhali sana naomba urekebishe lifuatalo:

    "...KUONDOKEWA NA MPENDWA WETU HAYATI MZEE GODWIN KADUMA..."

    Kidogo limepindika. Hayati anawezaje kutuondokea? Aliyetuondokea ni Mzee Godwin Kaduma

    Naona lisomeke:

    "...KUONDOKEWA NA MPENDWA WETU MZEE GODWIN KADUMA..."

    ReplyDelete
  3. Pole Salenga na Neema. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  4. Tunatoa pole kwa jamaa na marafiki wa mzee Kaduma.

    Michu hata hivyo mbali na hii lililotupata, kila kitu lazima kiwe na kiasi tukiendelea kuleta wote picha kila siku nadhani mwishowe tutaitakia hii blogu dethidei badala ya bethidei yaani hata nafasi ya kuweka comments itakosekana maana watu wana mafilimu na mabuku na mimikanda na matepu na maslaidi na madividii na madijito yenye sauti na harufu ya masinepu kibao!

    Tunaendeleza mwendo majariwa!

    Cha msingi ni wewe kutokubinya maoni ya wadau;Isipokuwa kama kweli kuna sababu za msingi zilizo wazi.

    Nyakatakule unyilisya echalo.

    ReplyDelete
  5. Pole sana na msiba kaka Misupu

    ReplyDelete
  6. WE ''NAJIFUNZA'' KUMBE HUJUI MAANA HALISI YA HAYAT.HAYATI SIO MAREHEM KAMA ILIVYOTUMIWA AWALI.HAYATI NI NENO LENYE ASILI YA KIARABU NA LINA MAANA YA MAISHA,KUWAPO MAISHANI.KUMBUKA MAREHEM MZEE A.MWILIMA(MWENYEZI MUNGU AMREHEMU)NA WATAALAM WA KISWAHILI WALIKWISHA REKEBISHA HILI.REGARDS

    SAMEER

    ReplyDelete
  7. SAMEER,

    Kumbe ka-blogu kanaweza kuwa "chuo kikuu cha lugha yetu"!

    Kwa hiyo, neno "hayati", kama Michuzi alivyolitumia hapo juu, lina maana ya "maishani"; kwa mfano, "...KUONDOKEWA NA MPENDWA WETU HAYATI..."

    ReplyDelete
  8. Wanakijiji wote poleni na msiba huu mkubwa.Mimi binafsi nimeguswa sana na habari hizi.Tujifunze kwa aliyoyafanya marehemu,na tuwe na nguvu kuwa kifo kipo na kila mtu lazima atakufa.Tutiane moyo kwa kusema kuwa mpiganaji mwenzetu ametangulia mbele ya haki na sisi tutamfuata siku ikifika
    Majita

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...