SERIKALI imetoa taarifa kujibu shutuma za rushwa kwa viongozi na watendaji wakuu wa serikali zilizotolewa na Mbunge wa Karatu kwa kupitia CHADEMA Dk. Wilbrod Slaa hivi karibuni.

Taarifa hiyo iliyotolewa Ijumaa Sept. 28, 2007 na Waziri ya Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Muhammad Seif Khatib (pichani) imesema shutuma hizo hazina msingi wowote na zinastahili kupuuzwa.

"Tafsiri pekee na mantiki ya kutolewa kwa tuhuma hizi wakati huu ni kuwa hili ni jaribio la kuwavunja moyo wananchi kuhusu manufaa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005," imeeleza.

Imesema kwmba Serikali inapinga vitendo vya rushwa nchini "kwa nguvu zake zote" na kama Dk. Slaa na wenzake wana lengo la kupiga vita rushwa basi tuhuma hizo wangezifikisha katika vyombo vinavyohusika ili zishughulikiwe.

Dk. Slaa, akiwaongoza wanasiasa wenzake kadhaa wa kambi ya upinzani, walitoa tamko hadharani Septemba 15 mwaka huu kwenye viwanja vya Mwembeyanga, wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam, kuwatuhumu viongozi kadhaa wa umma kuwa wanashiriki vitendo vya rushwa.

Kufuatia tuhuma hizo, gazeti la kila wiki la MwanaHalisi linalotolewa jijini Dar es Salaam, limekuwa likisambaza tuhuma hizo bila ya kutafuta ukweli wake, taarifa imesema.

Taarika kamili ya Serikali inatarajiwa kuchapishwa ikiwa ni tangazo katika magazeti kadhaa ya kila siku Jumamosi Sept. 29, 2007.

Taarifa imesema Serikali ya Tanzania wakati wote imekuwa ikitekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kupambana na rushwa, awamu ya kwanza ya mwaka 1997/2004 na awamu ya pili mwaka 2005/2010.

Imenukuu Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005, Ibara ya 110, inayoelezea mapambano dhidi ya rushwa na tamko la Rais Jakaya Kikwete dhidi ya rushwa katika hotuba yake ya kuzindua Bunge Desemba 29, 2005.

Serikali imeanzisha Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye Wilaya zote nchini, imeshughulikia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na inashirikisha wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa, imesema.

"Serikali isingebuni na kutekeleza mikakati hii kama isingekuwa na nia ya dhati ya kupambana na tatizo la rushwa [WINDOWS-1252?]nchini…Serikali haikutarajia kwamba watakuwepo miongioni mwetu watakaotumia fursa hizi kuibua taarifa za uzushi kwa lengo la kuchafua majina ya wenzao ili kujipatia umaarufu wa kisiasa wasioustahili," imeongeza.

Taarifa imesema Serikali inaelewa kwamba Dk. Slaa na wenzake ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 wakitegemea kushinda lakini walishindwa na wananchi kuichagua CCM.

Imesema wananchi wanayaona mafanikio mengi katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba wanachokitafuta wale walioshindwa ni kile walichokikosa na hivyo wanajaribu kuwahadaa na kuwachanganya wananchi.

"Serikali ya Awamu ya Nne ni imara na iko makini kutekeleza ahadi zake zote ilizowaahidi wananchi wakati ilipokuwa inawaomba ridhaa ya kuingia madarakani.

"Hivyo ni vyema wananchi wakatambua kwamba wapinzani hawa hivi sasa wanatapatapa na wanataka kutuondoa katika lengo letu la kuwaletea maisha bora Watanzania," imeongeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Chonde JK rudi home!

    2007-09-28 18:46:27
    Na Mwandishi Wetu, Jijini


    Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Jakaya Kikwete akiendelea na ziara ya kikazi huko nchini Marekani, baadhi ya wananchi waliojitambulisha kama wakereketwa wa maendeleo, wamemlilia kiongozi huyo wa nchi wakitaka arudi nyumbani haraka kuokoa jahazi.

    Wamesema jahazi linaelekea kuzama kutokana na baadhi ya watendaji wake muhimu kuzidi kuumbuliwa laivu na wananchi kila wanapokwenda kwenye ziara vijijini, kitu kinachoonyesha wamechoshwa na utendaji wao.

    Kwa mujibu wa wakereketwa hao, kurudi kwa JK, kwa upande mmoja kutasaidia kwani atawakumbusha tena watendaji wake hao juu ya kile alichowafundisha katika semina elekezi kadhaa alizowahi kuwaandalia na hivyo kuwaepusha na aibu zaidi.

    Aidha, wananchi hao wamedai kuwa kwa kufanya hivyo, vigogo hao wa ngazi mbalimbali mikoani, wataweza kujirekebisha na hatimaye kuacha kuumbuka kutokana na zomea-zomea wanayokumbana nayo kila kukicha.

    ``Hali siyo nzuri kwakweli? aibu wanazopata baadhi ya vigogo wa mikoa katika ziara ya Waziri Mkuu Lowassa ni ushahidi kuwa baadhi yao wanastahili msasa zaidi kama si kuondolewa,``amesema mmoja wa wakereketwa hao, Mzee Dickson Kunambi, mkazi wa Ubungo Jijini.

    ``Licha ya umuhimu wa ziara anayofanya sasa kwa taifa, bado kuna haja ya kumtaka Rais Kikwete arejee ili kurekebisha mambo? wapo watendaji ambao wanamuangusha wazi na wakiendelea kuachwa, kasi mpya na nguvu mpya ya kusaka maendeleo itaendelea kukutana na vikwazo,`` akasema mkereketwa mwingine, aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mary.

    Matukio yanayotajwa na wananchi hao kuwa ni mfano wa kuumbuka kwa vigogo ni pamoja na yale yaliyojiri mkoani Mwanza.

    Mbunge wa Geita, Mhe. Ernest Mabina, CCM, ni miongoni mwa waliokumbwa na kibano cha wananchi.

    Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, ni kwamba mbunge huyo alizomewa Septemba 23 mwaka huu, mbele ya Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa alipokuwa ziarani wilayani humo.

    Kigogo mwingine aliyekutana na adha hiyo ni Waziri wa Miuondombinu, Bw. Andrew Chenge, ambaye alitolewa nishai na wananchi wa Ukerewe, huku wakiungwa mkono na Mbunge wao, Bi. Getrude Mongela, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Wilayani Ukerewe.

    Waziri Chenge alijikuta akiumbuka baada ya kujaribu kukanusha malalamiko ya wananchi waliyoyatoa kwa Waziri Mkuu Lowassa kuwa kivuko cha Kisorya kinachounganisha wilaya hiyo na mkoa wa Mara ni kibovu.

    Mwingine anayetajwa katika orodha ya vigogo walioumbuka hivi karibuni kwa kuzomewa na wananchi ni Afisa Kilimo wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Bw. Marco Nkilila.

    Afisa huyo alizomewa baada ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo kwa Waziri Mkuu kuhusiana na mfereji unaopeleka maji kwenye mashamba ya mpunga ambao wananchi waliulalamikia kuwa umeziba.

    ReplyDelete
  2. NA MWANDISHI WA WALALHOI KOKOTE PALE TULIPO.

    Kama ripoti iliyoandikwa na gazeti la Habari Leo ina ukweli basi kuna kitu kinachoendelea na ambacho bila ya shaka kimemsibu Jaji Warioba kuja na mawazo ya aina hii. Hebu soma na uamue mwenyewe au ni mimi ndiyo nimechanganyikiwa. [b]Mgaya Kingoba HabariLeo; Friday,September 28, 2007 @00:02[/b] WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema amekerwa na tabia ya wanasiasa kupakana matope na kuonya kuwa kisingizio cha utawala bora kisitumiwe kutaka kuangusha dola zilizopo madarakani. “Tukosoe lakini si kupata maslahi kisiasa… naona ndiyo tabia ya sasa kupakana matope kupata maslahi kisiasa. Tusiache kupambana na rushwa, lakini tusipakane matope kwa maslahi ya siasa,” Jaji Warioba aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake Oysterbay, Dar es Salaam jana. Sambamba na hilo, mwanasiasa huyo maarufu nchini alisema ameshitushwa na madai ya ufisadi yaliyoelekezwa kwa baadhi ya viongozi wa serikali, akiwamo Rais Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa. “Mengine yanashitusha. Umoja wa nchi hii unaweza kufika mahali pabaya. Yaani Rais anaitwa fisadi kwa sababu hizi na zile tu. Huyu ni mwanadamu kama wengine, lakini ndiyo symbol (alama) ya Taifa, ukishamwita fisadi na unakwenda unazungumzia hivyo hakuna uongozi wa Taifa. “Hata Mkapa aliyemtangulia anaitwa fisadi, hivi hivi tu, habari hizi zinaleta picha gani? Kwamba alijitajirisha yeye na ndugu zake katika miaka yake 10. “Mkapa kama binadamu alikuwa na weakness zake, lakini kwa nchi hii huwezi kufuta historia yake,” alisema Jaji Warioba katika mkutano ambao alizungumza kwa makini na kwa busara, huku akitumia mifano mbalimbali kujenga hoja zake mbele ya waandishi waliokuwa kimya wakimsikiliza. Alisema ameshangazwa na siasa iliyojitokeza katika miaka ya karibuni ya kupakana matope, ndani ya serikali na katika vyama vya siasa, akionya kuwa hiyo itaipeleka nchi pabaya. Lakini zaidi, akawataka viongozi wa serikali, wapinzani na waandishi wa habari, kujiuliza kama kweli habari hizo na mambo yanayoandikwa, ndivyo vipaumbele vya wananchi. “Rushwa imekuwa silaha ya kisiasa, watu wanatumia good governance (utawala bora) kutaka kuangusha utawala uliopo madarakani. “Siku hizi wakubwa wakizungumzia utawala bora, ujue wanazungumzia regime change (mabadiliko ya uongozi). Nia yao ni kutaka kuondoa utawala ule. Angalia Irak. Sababu ya Marekani ilikuwa kumuondoa Saddam. Simtetei Saddam, lakini nia yao ilikuwa kumuondoa. Leo hii mauaji ni ya kutisha kuliko wakati mwingine wowote. “Jana nimemwona Mugabe anazungumza UN. Wakubwa Zimbabwe wanazungumzia good governance, suluhisho ni Mugabe ang’oke, ardhi si issue, issue ni Mugabe. “Good governance inatumiwa kama silaha ya kisiasa, kubadili utawala. Watu wanaamini ukiondoa utawala, rushwa itakoma, Siamini,” alisema Jaji huyo aliyewahi kuwa pia Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Alisema rushwa nchini imekuwa ikiongezeka kiasi kuwa hata wananchi wa kawaida, sasa wanashiriki kwa kiasi kikubwa, lakini hiyo siyo sababu ya kuondoa utawala. “Unataka regime change au kuendeleza utawala. Kwa hiyo, mnawaambia wananchi hawa ndiyo wala rushwa, wakiondoka mambo safi, mimi inanipa taabu. “Watu wameacha kushughulikia matatizo ya wananchi, mambo ya msingi ya wananchi. Kwa mfano, mwaka jana, tumepata tatizo la chakula na umeme, lakini badala ya kuzungumzia jinsi ya kulikabili mwaka huu, watu wako busy kuzungumzia mambo ya uongozi. “Wanazungumzia nani fisadi, kutueleza mambo yao ya uongozi. Vipaumbele vyetu vinaanza kupotoshwa. Maendeleo hayawezi kuletwa na viongozi na serikali. Yataletwa na wananchi, serikali inatunga sera tu na kuzisimamia. Yanayokuja sasa ni lawama tu,” alisema na kuongeza: “Vyombo vya habari mtusaidie, utawala bora ni kitu muhimu, lakini watu wanahitaji msaada. Nimesikiliza Bunge hadi ikafika hoja ya Zitto, watu wanajadili masuala ya uongozi tu. Hoja inazungumzwa mazungumzo hayalengi hoja yenyewe. Hii concentration ya kulaumiana sijui inawasaidiaje wananchi.” Alisema ameiona orodha inayodaiwa kuwa ya mafisadi wanaoitafuna nchi, lakini akasema haina jipya kwa sababu imeshawahi kuandikwa, lakini akasema ina maswali mengi. “Hii si ilitoka katika miezi miwili mitatu iliyopita. Ilikuwa na wafanyabiashara wakubwa, ikaja nyingine kabla ya hii. Hii ndiyo current (ya sasa) ikipita, sijui itakuja nyingine. “Wengine wameisambaza, wanaizungumza wananchi hawana details (maelezo ya kina). Siyo kitu kipya, imefanywa issue (hoja). Msingi unawezekana upo, lakini ndivyo mambo yanavyopaswa kufanywa? Unatudanganya, unachotusaidia hakionekani. Ukitazama mahakamani hatashinda, lakini politically, amepata umaarufu,” alisema Jaji Warioba. Akizungumzia kuhusishwa kwa Rais Kikwete katika orodha hiyo, Jaji Warioba alisema: “Kwa kweli tu Rais alikuwa Waziri hapo kabla, anahusishwa kwa kusaini mikataba wakati huo”. Kuhusu Rais mstaafu Mkapa, huku akishika tama, Jaji Warioba alisema: “Huyu alikuta mfumko wa bei ukiwa zaidi ya asilimia 30, ameondoka uko chini ya asilimia tano. “Amekuta katika huduma ya afya tunategemea vipakiti vya dawa ya misaada kutoka nje, ameondoka hali ya sekta ya afya imeimarika kwa kiwango kikubwa. Amezikuta shule na vyuo katika hali mbaya, leo kuna mabadiliko makubwa katika elimu. Katika miundombinu, amejenga madaraja na barabara. “Mawasiliano yamekuwa mazuri. Hata vyombo vyenu vya habari vimeongezeka na mawasiliano ya simu leo unaweza kuzungumza hata ukiwa kijijini. Tumeshausahau uongozi wake.” Alisema alifikiri kipaumbele cha viongozi wa serikali na wa upinzani na vyombo vya habari, ingekuwa ni kuhimiza suala kama kilimo ambao huu ndiyo msimu wake, badala ya kukazania kulumbana kuhusu uongozi. “Jana (juzi) nimemwona Mhita anazungumzia suala la mvua, nilidhani hii ndiyo message (ujumbe) ungesambazwa, lakini wangapi wanamsikiliza. Tukiwaandama viongozi hatupati maendeleo. Jana Karamagi, leo Mgonja, kesho sijui nani anakwenda mahakamani. Tukiendelea hivi sijui…,” alisema. “Tunavyo-behave sisi inaweza kuwa burudani kwa wananchi, lakini isilete maendeleo. Tuache tabia ya kupakana matope, haitatusukuma mbele. Tusiache kupambana na rushwa, lakini tusifanye hivyo kwa maslahi ya siasa,” alisema. Alisema maisha ya wanaharakati na viongozi wanaopiga kelele juu ya wananchi ni bora kuliko ya wananchi, na kuonya kuwa kumeanza kujengwa tabaka miongoni mwa wanajamii. “Tubadilike, tuwe na vipaumbele vitakavyosaidia wengi, badala ya maslahi ya wakubwa ambayo hali zao ni nzuri,” alisema Jaji Warioba na kueleza kuwa mkutano wake huo na waandishi wa habari haukuwa na shikinizo la mtu ye yote. “Kawaida yangu najulikana kwa misimamo yangu. Sijatumwa na serikali wala chama. Nazungumza ninachoamini,” alisema Jaji Warioba katika mazungumzo ambayo kwa kiasi kikubwa yalijikita katika kuzungumzia madai yaliyotolewa na wapinzani hivi karibuni kuhusu viongozi yaliyodai wanaitafuna nchi. Note Yangu: Hivi tusipouliza na kufuatilia matendo na maneno ya viongozi wetu tufuatilie nini sasa?

    ReplyDelete
  3. Nyumbani ni nyumbani,na politics zetu just dont add up,as time is money,tunakuomba on behalf of wabeba maboxi wote duniani,hizi taarifa uwe unazifupisha

    ReplyDelete
  4. The world must know what is happening here…

    RESISTING CORRUPTION AND
    BREAKING RANKS –THE PRICE YOU
    PAY IN TANZANIA

    Edited By:
    M. M. Mwanakijiji

    The Experiences with Taking dissent in Tanzania and the
    Debacle around the Bank of Tanzania (BOT):
    Paper Presented at the Workshop for U4Workshop
    19th September 2007
    AT CORAL BEACH HOTEL, DAR-ES-SALAAM:
    By
    Dr. Willbrod Peter Slaa, MP (CHADEMA – KARATU)
    1 INTRODUCTION:
    This is the final presentation in our workshop. It looks analytically at the possibilities of
    Resisting Corruption within the framework of the abundant legal and policy instruments
    as well as the price one pays in breaking ranks with the system.
    This presentation also looks at experiences of taking dissent in Tanzania, their
    consequences and thus indicating what is actually happening on the ground despite the
    many constitutional, legal instruments and beautiful words and promises that are being
    made by the authorities.
    1.1 SUMMARY OF FACTS: The CASE of BOT:
    On the 25th of June, in my main Speech as Shadow Minister, Office of the Prime
    Minister, I demanded explanation from the Government concerning various obtaining
    and indeed widely circulated reports of misappropriation/misuse of public funds and or
    elements of corruption at the BOT. Immediately after My Speech, I was summoned by
    the Hon. Prime Minister, in the Speakers Lounge, and was requested not to pursue these
    matters as they would greatly tarnish the image of our Nation.
    My position was that to the contrary we would be more credible and trustworthy if these
    charges were properly and transparently investigated. The Parliament likewise would be a
    credible and independent Institution it deserves. However, after around 40 minutes we
    agreed to differ. The Government did not only give satisfactory answers, but came up
    with contradictory statements through ‘Statements” of the Minister for Finance as well as
    the Minister for Energy and Natural Resources, during the week, before the winding up
    of the Prime Minister’s Budget.
    Latter, during the week, at the Appropriation Committee of the Full House, I gave an oral
    notice that I intend to bring a private motion for the appointment of a Parliamentary
    Select Committee as per sect.104 (1) and (2) of the Standing Orders, to investigate the
    veracity of those reports, as well as to prove the accuracy of the statements made by the
    two Ministers. This is the only avenue open to a backbencher, in accordance with the
    Parliamentary procedures.
    On the 26th of June, I submitted my notice officially in writing as per requirement of
    section (2) of the Standing Orders. Detailed statement was submitted after thorough
    research to the Clerk of the National Assembly on the 8th of August 2007 as per the
    requirement of the same provision of the Standing Order.
    In the morning of the 13th of August a special seating of the Steering Committee of the
    CCM caucus consisting of Central Committee Members in the House was convened in
    the Office of the Speaker. Membership of this Committee Comprises of the Prime
    Minister, the Speaker, Secretary General of CCM (also an MP), the Public Relations
    Officer of CCM (also MP), and the Deputy Speaker. In other words, the Steering
    Committee is made up of members of the Central Committee of CCM.
    Reliable information from this meeting indicates that the two Private Motions, one of
    Zitto Kabwe, and the other of Dr. Slaa, were the subject of discussion. The meeting went
    on for over four hours.
    On the 13th of August, I received a letter from the Office of the Speaker, ref.
    CA.150/277/01/07 demanding that I submit evidence to ‘support my motion’ so that the
    Speaker ‘may satisfy himself’ before the motion is scheduled for debate. I submitted all
    the evidence in 1V volumes the same evening of the 13th of August, with a three- page
    summary indicating the source of the relevant documentary evidence.
    However, in the morning of the 15th of August, I was brought a copy of a letter dated
    30th of July 2007 to Intelligence Officer in Dodoma, purportedly from the Intelligence
    Head Office in Dar. I studied the letter and the attachments and was convinced that it is a
    trustworthy document. It had as an attachment an Audit Document from the CAG, which
    I am using to build my case on. The letter was meant to advice the PM to block my
    Motion from being presented in the House, as it raises issues that the Government has no
    satisfactory answers, since the basis of the allegations are the findings of CAG.
    From this, and with the background of the Steering Committee meeting that had taken
    place on the 13th I concluded that the letter of the Speaker on the 13th was in fact an
    implementation of this letter. I still decided to give the office of the Speaker benefit of
    doubt, but until morning of the 16th there was no indication that the motion would be
    scheduled at all. I therefore, on the 16th of August decided to withdraw my Motion in
    accordance with provisions of section 48 of the Standing Orders.
    With this background let us now look at a few issues in my Private Motion for which a
    Select Committee was to be established: -
    1:2 ALLEGATIONS OF MISUSE OF PUBLIC FUNDS/USE OF FUNDS
    CONTRARY TO FINANCIAL PROCEDURES:
    1:2.1 BOT PAYING TSHS 155 BILLION IN RESPECT OF
    DEBTS OF MEREMETA (GOLD) CO.LTD:
    Since 1998 we have been following up in Parliament various issues concerning this
    company, reported in the House to be a corporation sole, under the Tanzania Armed
    Forces, and the proceeds of which would be used to finance the mass production of the
    ‘Nyumbu’ (Buffalo) trucks manufactured by JWTZ (Tanzania People’s Defense Forces).
    However, since then there has been no transparency, and no reports concerning this
    company were ever presented to the House, despite the many questions we raised (vide
    Hansard Reports since 1998). During the Budget Session 2006/2007 the Government
    admitted this company was under liquidation. We needed more details and none was
    supplied.
    In short, the Government could not provide satisfactory answers as to that are the
    shareholders, the directors, where Meremeta is registered, where the accounts of
    Meremeta are audited, and where the income from Meremeta appears in the Revenue
    books of the Government!
    This 2007/2008 Budget session, in reply to my speech, the Minister for Energy and
    Minerals, reiterated that Meremeta has been under liquidation and all properties of
    Meremeta Transferred to another company, TANGOLD Ltd, a 100% Government owned
    company. Yet when we demanded where TANGOLD is registered, who are the directors,
    where are the accounts and why TANGOLD did not feature anywhere in the Budget
    speech of the Minister, still we did not get any response from the Government.
    My independent research uncovered the following:
    Meremeta Gold Co., Ltd was registered in the UK as an ‘Offshore Co.’ with Registration
    no. 3424504 being registered as a Private Co. It has a certificate of Registration issued by
    Registrar of Companies in London issued on the 19th August 1997. It was then registered
    in Tanzania as a branch of foreign company on the 3rd of October, 1997 obtaining
    ‘Certificate of Compliance no. 32755. My search further indicates that Registrar of
    Treasury holds only 50% of the shares in Meremeta and a South African Trienex (PTY)
    Co., Ltd owns the other 50%. The available documents further reveal that two London
    based companies i.e. London Law Services Ltd and London Law Secretarial Service Ltd
    have one share each.
    A number of serious issues are raised by these findings?
    (i) Why would the Government of Tanzania hide all this information from the
    Parliament?
    (ii) How many shares does Meremeta have? Simple mathematics indicates that
    there is something fishy about this whole affair particular with the number of
    shares.
    (iii) Why should Meremeta be registered as an ‘Offshore” company? Gold is in
    Tanzania; the JWTZ is a Tanzanian Defense Force what is being
    camouflaged? This is even more complex as the other main shareholder is
    South African (entity)
    (iv) Who exactly are these London Law Services and London Law Secretarial
    Services Ltd? What would a law firm have to do with gold mining?
    (v) Meremeta was registered in 1997. According to records it ought to be making
    its returns 30th September every year. No returns are available in Dar, and no
    official Audit has ever been conducted. In fact, Alex Stewart Evaluation
    reports that Meremeta “had refused to be audited” by them on the pretext that
    it is a Government company. How is this explained?
    (vi) Meremeta is registered as a Private Co. how much has it ever paid to the
    Government in Taxes?
    (vii) How much profit has been realized since the establishment of this company,
    and how much has Tanzania benefited as a country and/or NYUMBU directly.
    (viii) The Budget Speech 2006/7 indicates that in the Financial year 2006/2007
    Meremeta output was 2.7 Tons of Gold, if Meremeta was actually liquidated
    how then is this explained?
    (ix) After all is the Parliament no entitled to proper answers to all these legitimate
    questions on behalf of the People of Tanzania?
    Yet, with all these questions unanswered, the Controller and Auditor General’s (CAG)
    report (BOT audited Accounts) of ending 30th June, 2006 (after liquidation) that BOT
    paid Meremeta debts to the tune of Tshs 155 Billion as follows: US $ 118,396,460.36 to
    an unknown account of Nedbank Ltd of South Africa through HSB of New York. The
    Balance of US $ 13,736,628.73 was paid to TANGOLD account with NBC Corporate
    Branch Dar-Es-Salaam. This raises further questions: -
    a) How is it that such a huge sum could be paid without Parliament being
    notified, and or such important information being deliberated withheld
    from the people’s representatives?
    b) From the shareholding, it is clear that Tanzania has only 50% of the
    shares, (if the mathematics is correct), why is it that the full amount of the
    Meremeta debt was to be carried only by BOT? Or otherwise, what
    percentage of this debt BOT actually covered on behalf of Tanzania?
    These issues need to be probed, and the only statutory authority for this work would be
    the Select Committee of the Parliament as per Section 104 (1) and (2). This is also in
    fulfillment of the Constitutional requirement of the powers of the Parliament, Art.63 (2)
    3ab.
    1:2:2: TANGOLD LTD:
    As stated above, The Parliament was given scanty information about TANGOLD. My
    investigation further revealed the following:
    a) That TANGOLD Ltd. is a foreign registered Co. It was registered again as an
    offshore co. in Mauritius with Registration no. C 205006121 dated 8th April 2005
    and subsequently registered in Tanzania as a branch of foreign company and got
    Certificate of Compliance no. 55661 dated 20th February 2006.
    b) That the Memorandum and Articles of Association do not show in any of the
    articles or even by implication, that TANGOLD is a Government owned
    company.
    c) Section 7 of the Memorandum and Articles is even more shocking. It indicates
    that the shares may be transferred to members of the Family of the Shareholders
    that is father, mother, wife, and children. This construction in a memorandum of a
    company belonging 100% to the Government seems not only odd but also
    strange.
    d) TANGOLD Co., Ltd was registered in 2005. No returns and or Audited accounts
    have been submitted to date. These raise serious issues of concern. We have seen
    above, that BOT already paid the sum of US $ 13,736,628.73 from Public coffers.
    The nation, through its representatives needs to know what this money was for.
    The Nation needs to know the activities of this company said to belong to the
    Government of Tanzania, if indeed it does belong to the Government. The
    Parliament needs to know to what extent this company has been of benefit to our
    country, and how much has been paid in taxes if any! If not why?
    e) My further investigation of the BRELA FORMS indicates that in all the relevant
    forms and returns, no where do the Directors register themselves as
    representatives of the Government, albeit, their directorship elsewhere is stated
    accordingly. This is very shocking for a company purported to belong 100% to
    the Government.
    f) The Registrar of Treasury, who owns in trust all Government property does not
    appear anywhere in the statutory documents of this Company, a matter raising
    serious concern.
    g)
    Hence, a solid ground motivating me to demand for the establishment of a Select
    Committee of the Parliament to probe on these pending and unresolved issues.
    1:2:3 BOT PAYMENTS TO MWANANCHI GOLD CO.LTD.
    (IRREGULAR PAYMENTS):
    Mwananchi Gold Company Ltd. (MGCL), unlike Meremeta and TANGOLD is a locally
    registered Private Company. In the Financial years 2004/2005 and 2006/2007 BOT
    effected total payment of US $ 5,512,398.55. I have no problem BOT making payments
    to private companies. I am concerned with the irregularities in the payments. CAG
    Management letter indicates that up to 21st December 2006, MGCL had an outstanding
    payment of US $ 62,847.91, equivalent to 78,753,459.in the form interest for loan
    advances. According to the auditors the interest was to have been paid in the first six
    months. Yet, 18 months later, no single cent had been paid and the BOT had not moved
    in to take any attachments or properties. This is a serious irregularity.
    Further a loan of US $, 2,807,920, appears as per CAG report to have been secured by
    raw gold purchased with the same loan funds. This transaction is nor usual.
    BRELA reports indicate that BOT holds 500 shares in MGCL and NDC- a Government
    parastatal holds 375 shares. Other Private companies by the names of Mwananchi Trust
    Company Ltd holds 1,123 and Chimera Company Ltd with 500 shares respectively.
    MGCL was registered and got certificate of Registration na.44962 dated 12th December
    2002 and was registered as a Private Company without authority to sell shares to the
    public.
    The Mwananchi Trust Company and Chimera Company raise lots of question marks in
    themselves too.
    The CAG report further indicates the following unsubstantiated BOT payments to
    MGCL:
    a) 17/7/2005 File 18003 Temp f/47 US $ 95,000 to MGCL.
    b) 29/0/7/2005 ‘Allowances’ US $ 7,500 to MGCL without explanation.
    c) 18/01/2006 Transfer to Tanzania Embassy, Kinshasa, US $, 1,500,000 without
    any explanation.
    It is therefore clear that there is a ‘thick cloud’ around these transactions within the BOT
    all of which needed to be probed in detail by a statutory body in a transparent procedure.
    The Select Committee would not be allowed, as stated earlier on.
    1:2:4: OTHER ALLEGATIONS CONCERNING BOT:
    Allegations concerning the EPA have been reported by the Papers and the Government
    has not denied these reports. This same concern is also reported by the CAG, with much
    higher figures. I would like to take note in particular the Story in the Government Paper,
    Daily News, Issue no. 0856-3812 and 9315 of 22nd June 2007. According to this report
    payments close to 30.8 billion was made to M/s Kagoda Agricultural Co. Ltd, a private
    Co. registered on the 29th of September, 2005 and within 8 weeks BOT had already
    made payments to the tune of 30.8 billion to foreign companies-through Kagoda, which
    companies the CAG could not identify even after contacts with their metropolitan
    companies in the USA, Italy, Germany, France, and Japan.
    I therefore needed an explanation from the Government in my Speech, and as I could not
    get any satisfactory reply from the Government, I this is one of the areas covered in my
    oral Notice for the Select Committee of the Parliament. The Government indicated that it
    would work in collaboration with the IMF on this matter. Yet, the Parliament is the sole
    Constitutional and statutory body and hence the Government reply was not satisfactory,
    particularly since the coverage of the Government ‘Special Audit’ was limited to EPA
    only.
    The total amount of misappropriation/loss of public funds/use of public office for corrupt
    purposes is said to amount to US $ 1,000,000. This is only from the identified sources
    and could be only a tip of the iceberg. It is therefore clear that there was need for a Select
    committee of the Parliament.
    2: REASONS FOR THE SELECT COMMITTEE:
    As it is clear, from the available records and documents the abuse, misappropriation and
    use of public funds contrary to Public financial Memoranda is very extensive. Secondly,
    any allegation against the Bank of Tanzania, involves, the Government by virtue of the
    nature of the Bank and its mandates. In most cases, allegations would touch on the
    personalities within the Government. In such a situation, no person can be a judge of
    himself.
    3: WITH THIS BACKGROUND IS IT POSSIBLE TO
    FIGHT CORRUPTION IN TANZANIA:
    Having stated what has transpired in practice in the case of the BOT let us now briefly
    look at the various instruments that theoretically make the fight against corruption in
    Tanzania look possible, and in fact makes Tanzania a model country, on the right track in
    the process of fighting corruption. I will only attempt to venture into a few areas for
    purposes elucidation.
    3.1: The Constitution as the basis:
    Indeed Tanzania’s Constitutional provisions, if properly implemented take us miles away.
    Art. 8(1)(a) of the Constitution, specifies that ‘The people are the source of all authority,
    and the government shall get all its authority from the people’ (literal translation). And
    8(1)(c) the ‘government shall be answerable to the people’.
    Article 18(b) each person has right to seek, receive and disseminate information without
    regard to territorial boundaries.
    Article 63(2) further stipulates that the ‘the Parliament shall be the supreme body in the
    United Republic of Tanzania, and shall have authority on behalf of the people to
    “oversee” and “advice” the Government and all its organs in the implementation of their
    respective responsibilities in accordance with the stipulations of this Constitutions’. In the
    implementation of its responsibilities, Parliament shall ‘demand from any minister any
    question under his responsibilities’Art. 63(3)(a).
    The Member of Parliament is then indemnified in the implementation of his
    responsibilities, and is guaranteed full freedom of speech and debate, and that this
    freedom shall not be questioned any where in the United Republic, and shall not be sued
    for anything said or submitted in the form of a motion, private members Bill, or any
    ‘other means’ (Article 100(1)(2).
    These provisions create the Constitutional basis of my demand for the Select Committee.
    3.2 THE PARLIAMETARY IMMUNITIES, POWERS AND PRIVILEGES ACT,
    1998 (RE)
    This act amplifies and puts into operation the stated Constitutional provisions in a
    number of ways.
    a) Sect.3 guarantees freedom of speech and debate, “There shall be freedom of
    speech and debate in the Assembly and such freedom of speech and debate shall
    not be liable to be questioned in any court of place outside the Assembly (vide
    also Art.100 (1)(2).
    b) That “subject to this act, and to any statutory or other provisions regulating the
    disclosure of information by public officers, a member may, on request by
    ‘himself’, be furnished with information by the public officer concerned”(Sect.10)
    c) The Act provides ample power for the Parliament to be able to oversee and
    indeed supervise the Government if properly implemented. It provide powers to
    the Assembly, Select Committee and or any such other Committee to ‘ …order
    any person to attend before the Assembly or before such committee and to give
    evidence or to produce any document in the possession or under the control of
    such person...’(Sect.13 (1) (2). These are immense powers, and would have been
    the statutory authority for the Select Committee to probe the stated BOT alleged
    misappropriation/misuse of funds and elements of Corruption. In other words the
    Select Committee acquires Quasi-judicial powers.
    d) However, all these powers, are eroded by the subsequent provisions, "...The
    Speaker shall have the power, subject to the Standing Orders of the Assembly, to
    determine whether or not any act, matter or thing is one into which the Assembly
    may inquire, judge and pronounce upon. (Sect. 12(2).
    e) Further the “…Speaker shall, either of his own accord, or upon recommendation
    of a committee, report to the Attorney General all acts, matters or things
    amounting to offences under this act…" This provision, prima facie, looks an
    unconstitutional, taken into account the Freedoms granted above. But this is the
    situation, and hence, most Members of Parliament are automatically silenced for
    fear of being reported to the Attorney General and hence being charged for
    criminal offences.
    f) These provisions put too much power in the hands of the Speaker, and may
    arbitrarily decide either way, hence watering down the spirit and the freedoms,
    responsibilities provided by the Constitution. This is even more precarious when
    the Speaker is not only an active Member of the Ruling Party, but also a Member
    of the Central Committee, a member of the Caucus of the Members of the Ruling
    Party, and plays active partisanship.
    3.3 THE STANDING ORDERS 2004 EDITION:
    I wish to hasten that these are in the process of being amended. For the purpose of
    understanding the BOT debacle I will use the 2004 Edition, which is still current.
    a) One of the major weaknesses of the current Standing Orders is that they have
    concentrated too much power in the Hands of the Speaker. The Speaker has
    power to decide/rule on any matter and may not be questioned, albeit there is a
    procedure for complaint, but himself chairs the committee, and in this case the
    Deputy Speaker shall chair it. The report is still submitted to him though.
    b) The Select Committee is provided for under Sect.104 (1)(2). The provision does
    not require any censorship by the Speaker. In the case it was imposed, on the
    instruction of the Members of the Steering Committee of the CCM-the Ruling
    Party. The parliamentary matters were taken outside the realm of the Parliament
    and decided by Leadership of a Party. The Leadership and Authority of the
    Parliament were only implementers of decisions originating from another
    authority, which is of course mixed with that of the Executive as the Chairperson
    of the CCM Steering Committee is the Prime Minister. A blurred vision of the
    Doctrine of the Separation of Powers.
    c) The practice has been since this current Parliament; many decisions have been
    arbitrarily made by the Speaker, basing on the authority granted by Sect. 126 of
    the Standing Orders. However, strictly interpreted, the Speaker is only mandated
    by this section to make decision basing on parliamentary tradition, if and only if
    the matter has not been regulated by the Standing Orders. Such decisions have
    been the arbitrary change of Sect.81 (2)(b) during the budget Session. The
    arbitrariness leads to loss of confidence in the parliamentary system and authority,
    but also issues are compromised on the basis of political affiliation and the like.
    3.4 THE PREVENTION AND COMBATING OF CORRUPTION ACT,
    2007:
    When this Bill was first presented it raised hope among many people. The Preamble
    makes a very bold statement when it says, the ‘Government...to ensure that Tanzania
    remains a corruption free state adhering to principles of freedom, equality, justice,
    brotherhood, peace and wherein all people are equal and every person has a right to
    ownership and protection of property acquired by lawful means.’ It creates, a ‘Land of
    Promise!
    The Act has many good things. The best among them, which has been a big mousetrap
    for the International Community, is Sect.5 (2) “The Bureau shall be an independent
    public body”. Paradoxically, no other paragraph through all the 55 sections indicates or
    even alludes to this “independence”. At the time of drafting and passing this bill we
    protested vehemently against this dangerous game, but the majority made their way, the
    minority may ‘have been listened to’, of which I am not sure either.
    The PCCB can not be an independent organ when:
    a) The Director General is nominated/Appointed by the President, and no
    prerequisites for the appointment have been statutorily postulated. No transparent
    procedures at the very least have been postulated for this purpose either. Nothing
    at the end of the day can stop full and maximum loyalty to the sole appointing
    authority.
    b) The PCCB reports directly to the President. And the only two connections with
    the Parliament is (i) when funds are appropriated by the Parliament (Sect.47 (1)
    and (ii) when the Minister “lays’ the report before National Assembly. In
    accordance with the Standing Orders, the ‘Laying” is not followed by automatic
    debate of the report, except when so demanded by an MP and supported by at
    least 10 MP’s which is not always easy, as there is no prior notification as to the
    date of the laying down of the report. Most reports pass unnoticed on account of
    this bad regulation. According to the Minister responsible, ‘the PCCB is an arm of
    the Government just like the Police force”.
    c) This is an indication of the relationship between the Government and the PCCB,
    and hence directs contradiction with the Spirit of Section 5(2) of the ACT. The
    outcome is not difficult to imagine, under the circumstances. Indicators are
    always clear as in the case of the investigations concerning the RICHMOND Co.
    ltd, closed without the report being made public despite a public outcry and clear
    indicators of elements of corruption.
    d) Similarly in the case of the BOT debacle, the PCCB is alleged to have sent out a
    circular to all the electronic and Print media notifying them that the matter is
    under investigation, and that as per Sect.37 not even investigative journalism is
    allowed. As per this section it is even a criminal offence, bearing a fine of one
    hundred thousand, and or imprisonment for one year, and or both. This Circular
    has affected me as I was to make a Radio Presentation at one of the local Stations
    but the program was cancelled 30 minutes before the start of the program. We are
    indeed entering an even darker age in the fight against corruption.
    e) I had presented the BOT issue in Parliament, and thenceforth a public matter. I am
    surprised, PCCB undertaking any serious investigation, without having
    summoned me? Reading between the lines it is clear what this means and or leads
    to. The matter is up for a big cover, and this should be linked to what the Prime
    Minister told me on the 26th of June 2007.
    4: CHALLENGES FACED BY TANZANIAN
    PARLIAMENTARIANS:
    We have taken note of the legal framework its strength and weaknesses. Let us now look
    briefly at the challenges facing a Tanzania Member of Parliament, who seeks to expose
    cases of grand corruption.
    The legal framework and the parliamentary system structure are basically in place but are
    not basically user friendly. There are a number of reasons for this: -
    4.1: The Culture of docility:
    Tanzanians are just coming out of single party rule (we are just about 15 years into multi
    party system). The dominant culture of docility under the single party structure is still in
    the minds of many. When told to ‘shut-up’ in the ruling party caucus, normally the CCM
    Members will shut up sheepishly and for a motion in parliament to succeed you need
    coalitions.
    It is not possible to build coalitions under the current system. In the case of the BOT
    debacle only one CCM member openly and defiantly supported the call for ‘Select
    Committee’. He had actually been summoned by the authorities but says he obeyed his
    ‘conscience’ rather than the ‘party whip’. Many of these are of cause needed, but it takes
    a generation to make them. Courage is groomed and developed, is not only inborn.
    4.2: The un-supportive and user-unfriendly legal framework:
    As noted above, there are very good legal provisions, in the Constitution, the principle
    legislation, as well as in the subsidiary legislation (Standing Orders). But the wide use of
    the “Claw-back” provision-type render even the good provisions basically useless. These
    provisions are used to induce fear in the Members, and in the end they decide to shut up,
    quietly enjoy the luxurious benefits endowed to an MP, than the peril and tedious process
    of ‘self-defense’ whether in the House, or through the party caucus to Party Machinery as
    has happened so many times to a number of those who appeared to be vocal.
    4.3 The unwarranted use of the State Intelligence.
    The unwarranted use of State intelligence, in silencing such serious issues, as it happened
    in the case of the BOT debacle (advice to the Prime Minister) instead of the State
    Intelligence and the State Machinery supporting proper investigation and supporting
    committed Members in the fight against Corruption. Even such Institutions as PCCB
    which should have been in the forefront, are Government protective machineries rather
    than harbingers for the war against corruption for reasons explained above. I have
    incidences of PCCB involvement in petty issues on the Instruction of Government
    leaders-Regional Commissioners and District Commissioners, elsewhere rather than the
    real issues of corruption. And sometimes, PCCB is even instructed to cook up cases, as
    recently happened in Karatu. I can provide evidence if needed.
    4.4 The absence of clear separation of power between the Executive and the Parliament.
    Where the Prime Minister exerts excessive control over the Parliament, either through the
    ruling party caucus, or directly through instructions to the Speaker. On direct instructions
    by the Prime Minister, the Motion to create a Select Committee to carry investigation on
    BOT was withdrawn. This directive was aimed to ‘hide’ the truth from the parliament
    and hence the public, under the guise of ‘protecting the national image’. Which in my
    opinion is more damaging as truth is indivisible and will re-surface at some stage
    anyhow. But irreversible damage would have been done by then.
    4.5 The effects of the “Donor Praise” and the “ Bretton Woods System” of working only
    with the Government.
    The Parliament is completely in the dark when it comes to Donor or Partner funding. It is
    only now that some Friendly Partner countries contributing into the Direct Budget
    Support (DBS) are approaching the Parliament and access some information. Information
    is power. Parliamentarians fail in most cases to fight corruption, as the Funding
    arrangements, agreements, and whatever conditionality is not known to them. It is not
    possible let alone, easy to ‘Oversee” something you do not know. The Budgets in
    Tanzania are passed generally without much critique for lack of proper information, and
    in some cases, direct refusal of the government to provide such necessary information for
    the Parliament to perform its oversight function.
    Most donor countries, on visiting a few projects, come out even before a comprehensive
    evaluation, with ‘huge praises’ of the Government performance, to the effect that the
    Government would not subsequently accept any internal criticism. But to our experience,
    most of the missions, see only tip of the mountain, and do not experience what actually
    happens on the ground. A Partnership with Parliament is the only way to get a balanced,
    and true picture of how the funds are used on the ground.
    4:6 the dominance of a Single Party in Parliament:
    The sheer numbers of the ruling party in the House is a great obstacle to any serious fight
    against corruption. The Members of the ruling party are instructed to defend their
    Government. Most of them are aware they would not have gone through if not by direct
    support of funds obtained from the same Government, source of which they do not know,
    by such other indirect ways. In fact, the Kagoda case is a typical example, and reliable
    information says, that the money was taken from the Bank of Tanzania for campaign
    purposes (remember 29th of September, 2005 was right in the middle of campaign for the
    General Elections). Hence, allegations of CCM buying voters, CCM being able to
    provide nation wide T-Shirts and Caps as campaign material, things very attractive to
    rural peasants who are struggling to buy clothing –hence elements of corrupting voters).
    Indeed, this makes the statement by the Intelligence, that the Government would have no
    ‘satisfactory answers to these issues” more plausible. Yet even International Observer
    Missions, who come only for a few final days of the campaign eventually, declare the
    elections free and fair, but the process of election in Tanzania lasts about 70 days.
    Observing a few campaigns, actual voting in a number of stations out of over 35,000
    polling stations, and counting in about the same number does not make one to make such
    far reaching conclusions. Consequently, whatever is said by anybody else, the
    Government reply is ‘ we were elected by overwhelming majority’. The results are now
    visible. Things seem to be crumbling all over; shouts of corrupt practices abide within the
    CCM intra party elections. With clear evidence of what is happening within the Party,
    what would have prevented them from the same practice in the General Election? Once
    one gets in through a corrupt practice it is totally impossible to fight corruption.
    With 274 MP’s against 45 of the opposition, CCM is assured to pass any motion, whether
    for the good of the nation or otherwise, (as long as it is) important is to protect their
    regime.
    5: MY ORDEAL IN PARLIAMENT AND ITS CONSEQUENCES
    As stated above, on the 16th of August 2007 I withdrew my Motion by way of a letter to
    the Clerk of the Assembly, stating reasons for the same, and called a press Conference. I
    was worried of the similar consequences of what happened to Hon. Zitto on the 14th, of
    August, when he was suspended by a resolution of the Parliament.
    The real reasons are:
    a) Once a Motion is submitted to the Clerk of the National Assembly is not
    withdrawn, it is the property of the Parliament, and a Member, including the
    author may not debate it in any other forum until it becomes a public documentafter
    being tabled and debated in the House. This is in accordance with the
    Standing Order. In the circumstance, it was very clear, that the strategy adopted
    was to prevent it from getting into the House, and therefore, it would be
    permanently ‘dead’. The only solution was to withdraw and adopt other methods
    to continue with the fight against corruption. This is why I am now free to make
    this presentation. It would have been irregular, and I would have been charged for
    it.
    b) The allegations involved are very serious, and any delay in raising alarm would
    cause greater harm to this nation.
    c) Even if, it were to go into the House, ways and means would have been found to
    cover up the issues and facts and debate would go lop-sided as the Buzwagi issue
    was conducted, and the purposes intended would not have been achieved.
    6: THE POSSIBLE CONSEQUENCES PERSONALLY ON THE
    Immediately after the Press Conference I received three unidentified Telephone calls,
    threatening my life, for ‘poking my nose’ in peoples affairs. They all used hidden ‘cell
    numbers’ under “ private number’. When I reported to the police was asked if I had any
    suspect, but could not have imagined whom could that be. They refused even to open a
    police investigation file claiming they have no way of identifying suspects, as Tanzania
    has no control system as yet. I reported to my Party leaders, and they had also received
    similar calls asking them to warn me. The Chairman has since written a letter to the
    Inspector General of Police (IGP) to see to it that appropriate protections is provided, but
    we have not received any communication from the IGP to date. These are challenges one
    faces for standing for the Truth in a society where ‘values’ do not count.
    Could be taken to court, on made up charges, and the case would in practice never take
    off for years. This is a very effective means of covering up issues. It is good that the
    Judiciary is more and more becoming independent and is more likely to refuse such a buy
    out now than ever before. Yet it remains a challenge. I even received a threat from the
    Speaker, that I should expect a court actions should I dare to go public outside the
    Parliamentary system where I would have ‘some kind’ of immunity.
    7:0 WHAT COULD BE DONE TO KEEP THE FIGHT ON COURSE?
    This is of course the end purpose of this paper. The experiences are only meant to help
    solve the obtaining problem(s). In my opinion a number of things need to be urgently
    undertaken if the fight against grand corruption is to succeed.
    7:1 Harmonization of all Laws:
    The most important strategy is:
    a) First and foremost to make a review of all the laws, including the Prevention and
    Combating of corruption Act, 2007. The ‘claw-back’ clauses should be
    immediately and urgently removed to give greater effect to those positive
    provisions stated above. Once the claw back clauses are gone, I am sure
    courageous Members of Parliament will rise, and take up the challenge, as they
    will personally feel protected. The donor community may have an important
    influence in this area, albeit not a direct one.
    b) To make PCCB a truly Independent Institution, and accountable to the Parliament
    instead of the President. The Transparent system of appointing Director General
    of PCCB should be stated in the law, and Security of Tenure established
    statutorily. This will assure the Independence of the Institution, and subsequently
    PCCB shall no more be obliged to take instructions from the Government
    functionaries.
    c) The Letter of the Law, be it Constitution, Statutory laws, and or Standing Orders
    should be strictly observed and the current practice of interpreting laws according
    situations should cease forthwith.
    7:2: CREATING GREATER TRANSPARENCY IN FUNDING
    ARRANGEMENTS:
    Corruptions breeds where there is great secrecy. Current procedures and arrangements
    encourage corruption, It is my earnest appeal to all our Funding Partners, who are
    contributing to DBS, (around 42% of Recurrent Expenditure) and even higher percent of
    the Development Budget, to access all such information, if not to the Full House, at least
    to relevant Parliamentary Standing Committees. These will enhance the Oversight Role
    of the Parliament.
    Increased Sessions and Interaction with the Parliament will also greatly contribute to
    awareness on the side of Parliamentarians. The increased information will enable the
    Parliamentarians to critically analyze the Government reports, expenditure as well as
    performance.
    I believe if these basic interventions are undertaken, we shall be able to make significant
    step towards the fight against Corruption. The Funding Partners have a very significant
    role in this, and indeed have ability in pushing for these changes as a precondition for
    further support. The money you provide is Tax Payers money somewhere else, and I
    believe no Tax Payer would want his money misused. In some cases, the Donor money
    may not be used directly but the locally generated funds will be used for these clandestine
    operations, but since the donor does not know or even have full access to information on
    local funds would not reckon easily any misappropriation.
    E N D

    ReplyDelete
  5. khatib khatib mkono huupendie? ama mbavu zako umezichoka? serikali imara ipi boss wewe?hii ya kufuata jezi ya NEW CASTLE kwa mafunfgu ya walala hoi? its better you keep mum.au na wewew tukuanike? kama tuhuma ni uongo achaeni ELEZENI9 UKWELI MUOGOPENI MUNGU JAMENI

    ReplyDelete
  6. bomani juzi katuambia tuhuma za silaa ziko "legelege"...next ndugu waziri anatuambia hazina msingi wowote na zinastahili kupuuzwa...vichwa vyetu siyo vya kujifunzia kunyoa

    ReplyDelete
  7. Tamko la serikali linanikumbusha wiimbo wa Ndanda Kosova akiwa na WAJERAJERA.

    Sasaaaaaaaaaa wanaanzaaaa kuliaaaaa eeeheeee Nuruuuuu utufunguliiiiee Safinaaaaa...tiiiii aaaaah kidedeaaaaa

    Wakuna nazi wanapenda kusema -Mnalo!

    ReplyDelete
  8. HAWA WATU WA CCM NI WATU WA LONGO LONGO SANA WANAPENDA SIFA HATA ZILE ZA KIJINGA. WEAMETUHUMIWA KWA KUTUMIA VIGEZO VYA KISHERIA NA USHAHIDI. SASA WANACHOPASWA NI KUJIBU TUHUMA KWA USHAHIDI NA VIGEZO VYA KISHERIA PIA.SIYO MAMBO YA KUJISIFIA PUMBA NA UHOZO MTUPU." VIONGOZI WETU NI WANAFIKI SANA WANASADIKI UZALENDO KWA MIDOMO YAO, LAKINI MIOYO YAO NA VITENDO VYAO NI VYA KISALITI".

    ReplyDelete
  9. Kama hii ndio taarifa ya serikali na majibu rasmi ya serikali kuhusu tuhuma za nguvu dhidi ya mafisadi basi tumekwisha. Serikali ilipaswa kueleza jinsi gani TAKUKURU ilivyofanikisha kupambana na rushwa za IPTL, VALAMBHIA, RICHMOND na mazagazaga mengine mengi kabla ya kuwaambia watu wapeleke tuhuma zao kwa vyombo vilivyokosa mantiki zaidi ya kuwatetea wezi.
    Lakini la zaidi hapo, naona wanamkanusha zaidi Warioba zaidi ya Slaa. Ikumbukwe kuwa Warioba ktk taarifa yake, amezungumza serikali haina nia ya kupambana na rushwa, na ktk kipindi cha miaka 10 rushwa imekuwa maradufu. Khatib atuambie kuwa Warioba ni muongo, kabla hajarukia wapinzani. Kuhusu suala la kuchafuana kisiasa, hawajaanza wapinzani, rejea mchakato wa kutafuta urais ndani ya CCM.

    ReplyDelete
  10. Hoja hujibiwa kwa hoja na siyo maneno ya kitoto

    ReplyDelete
  11. Closing statement ya mzee Seif Khatib,hakuna maisha bora ila mnatuletea umasikini.Your days are numbered.

    ReplyDelete
  12. Kama serikali ipo serious kuhusu kupambana na rushwa, mbona wameshindwa kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ufisadi dhidi ya mfisadi Mkapa na Yona yanayohusiana na uporaji wao wa mgodi wa Kiwira na ulazimishaji wao wa mkataba na Tanesco.

    Michuzi naomba uiposti hii comment yangu.

    ReplyDelete
  13. WAPINZANI WAMJIBU WARIOBA

    2007-09-29 08:40:57
    Na Restuta James


    Umoja wa vyama vya upinzani umejiingiza katika malumbano na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba kwa kudai kuwa hautishwi na utetezi uliotolewa na kiongozi huyo na kwamba wakigundua kuna ubadhirifu aliowahi kuufanya wakati akiwa kiongozi wa ngazi za juu serikalini watamshughulikia.

    Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Jaji Warioba kuzungumzia tuhuma zilizotolewa na wapinzani za kuwataja hadharani viongozi wa serikali na kuwahusisha na ubadhirifu wa mali za umma.

    Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za makuu ya CHADEMA, jijini Dar es Salaam, viongozi hao kutoka vyama vya TLP, NCCR-Mageuzi, CHADEMA na CUF, walisema wanashangazwa na kauli zinazoendelea kutolewa na watu waliowatuhumu pamoja na ile ya jaji Warioba na kueleza kuwa hawatambui Jaji Warioba alizungumza kwa kutumia utaratibu gani kwa kuwa hivi sasa hashikilii wadhifa wowote.

    Viongozi hao wa vyama walisema Jaji Warioba alipaswa kueleza juhudi zake za kupambana na ufisadi na kwamba baadhi ya majina ya watu wanaowatuhumu si mageni badala ya kukaa kimya na kuwashangaa wapinzani ambao wana nia ya dhati ya kutaka ukweli juu ya matumizi ya rasilimali za umma na fedha za walipakodi.

    `Sisi tunaamini kuwa Jaji Warioba ni miongoni mwa viongozi waadilifu lakini kauli yake ya juzi inatupa utata sana maana alitakiwa kuwashauri viongozi wa serikali juu ya kutoa tamko kuhusiana na tuhuma hizi kuliko ambavyo viongozi hao wanaanzisha malumbano kwenye vyombo vya habari hivi sasa,` alisema Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuza Taifa Bw. Sam Ruhuza.

    Katika hatua nyingine viongozi hao walisema wameahirisha kulipua `mabomu mengine kwa kuwa bado wanafanya uhakiki na uchunguzi zaidi wa `mabomu` wanayokusudia kuyalipua.

    Walifafanua kuwa kwa sasa wanashirikiana na wataalamu mbalimbali kukamilisha uhakiki wa jambo wanalotaka kuwaeleza wananchi.

    Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw. Victor Kimesera alisema bomu lililopangwa kulipuliwa ni jipya na kwamba halihusiani na yaliyotangulia akitaja Buzwagi na viongozi waliotuhumiwa kujihusika na ufisadi.

    `Hili jambo ni jipya hatutazungumzia uamuzi uliofikiwa na watuhumiwa wa kutaka kutuburuza mahakamani maana hilo litatatuliwa kimahakama kama ambavyo wanadai,` alisema.

    Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema viongozi wa vyama hivyo wanashirikiana na jopo la wataalam wa kada mbalimbali kujadili suala hilo kwa kina na kwamba siku chache zijazo watawaeleza wananchi.

    Naibu Katibu Mkuu wa CUF ? Zanzibar Bw. Juma Duni Haji , kwa upande wake alisema anashangazwa na watuhumiwa waliotajwa kutokwenda mahakamani hadi sasa, badala yake kuendelea kusema kuwa wamechafuliwa majina na kukashifiwa.

    `Wanajifanya kuwa wamechafuliwa majina lakini hawataki kwenda mahakamani. Hiyo janja yao ya kutaka kuwaathiri wananchi kisaikolojia tumeigundua hivyo tunawaomba wananchi wawe makini kwa kufuatilia mambo haya bila kukata tamaa hadi hapo ukweli utakapojulikana` alisisitiza Bw. Haji.

    Mjumbe wa Halmashauri Kuu NCCR-Mageuzi Taifa Bw. Ruhuza aliongeza kuwa wanasuburi kuburuzwa mahakamani ili watoe mambo yaliyotakiwa kuzungumzwa bungeni na viongozi waliotaka kuwasilisha hoja binafsi.

    Mkutano huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa TLP Bw. Mrema, Bw. Ruhuza wa NCCR-Mageuzi, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Bw. Haji pamoja na viongozi mbalimbali waandamizi wa vyama hivyo kutoka bara na visiwani.

    Aidha viongozi hao walisema wataitisha mkutano mapema pale kazi ya uhakiki wa nyaraka za `bomu` wanalotaka kuwaeleza wananchi itakapokamilika.

    ReplyDelete
  14. Polisi wafyatua risasi kutawanya wananchi

    2007-09-29 08:42:08
    Na Raymond Kaminyoge


    Polisi jijini Dar es Salaam, jana walilazimika kufyatua risasi hewani kuwatawanya wanakijiji zaidi ya 100 na kuwakamata wengine 10 katika Kiwanda cha Saruji cha Twiga (TPCC), Wazo.

    Wananchi hao, wakazi wa Madale wilayani Kinondoni, walikumbana na balaa hilo baada ya kuvamia hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa kiwanda hicho.

    Habari kutoka eneo la tukio zimesema kwamba wanakijiji hao walitaka kumuona Waziri Mkuu ili wamueleze mgogoro wao wa ardhi.

    Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa kiwanda hicho cha saruji.

    Hata hivyo, Waziri Mkuu hakuwepo katika hafla hiyo na badala yake aliwakilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Dk. Batilda Burian.

    Wakiwa umbali wa takriban mita 50 huku wakiimba wimbo wenye ujumbe wa kurejeshewa ardhi yao, polisi na walinzi wa kiwanda hicho, waliwazuia kuendelea kusonga mbele.

    Hata hivyo, wanakijiji hao waliendelea kwenda mbele, hali iliyowafanya polisi kufyatua risasi tano kwa lengo la kuwarudisha nyuma.

    Baada ya risasi hizo, wananchi hao walijikusanya pamoja na kuendelea kuimba lakini baada ya muda kidogo kupita, walivamiwa na polisi ambao walilazimika kutembeza virungu ili kuwaondoa katika eneo hilo.

    Polisi walifanya hivyo huku wakiwakamata baadhi ya wanakijiji hao wakiwemo wanawake.

    Mmoja wa wanakijiji hao, Bw. Abdallah Mlaponi alisema wameishi katika eneo hilo kwa muda mrefu lakini wameshangazwa na hatua ya kunyang?anywa maeneo yao na kupewa watu wengine.

    `Tulitaka kumweleza Waziri Mkuu, Bw. Lowassa namna tunavyodhulumiwa haki zetu, lakini tunashangaa tunapigwa virungu,` alisema.

    Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kanali Fabian Massawe, alisema wanakijiji hao kama wana matatizo ya ardhi, walitakiwa kufuata taratibu zinazotakiwa na siyo kuvamia shughuli za watu.

    Akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Dk. Burian alisema kukua kwa sekta ya ujenzi kunategemea sana kuwepo kwa saruji ya kutosha.

    Alisema asilimia 40 ya sekta ya ujenzi hapa nchini, inategemea kiwanda cha TPCC.

    `Upanuzi wa kiwanda hicho utasaidia kupunguza upungufu wa saruji unaotokana na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo hapa nchini,` alisema.

    Waziri Mkuu alisema katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2005, uzalishaji wa saruji uliongezeka kutoka tani 833,092 hadi 1,375,222.

    Alisema mahitaji ya saruji yaliongezeka kutoka tani 809,992 mwaka 2000 hadi tani 1,454,992 mwaka 2005
    Katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Bw. Klaus Hvassing alikabidhi tani 100 za saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule wilayani Monduli mkoani Arusha, tani 50 kwa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro na tani 50 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mkoani Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  15. Wanajibiduabidua tu hao Chama cha Mafisadi hawana jipya. Hawajajibu chochote dhidi ya tuhuma za Mkapa kujitajirisha akiwa Ikulu, kashfa ya ununuzi wa rada ya $40 million ambazo kati ha hizo $12 million alilipwa mdosi aliyeletwa na Mkapa kama wakala. Mdosi huyo huyo alikuwa wakala katika kashfa nyingine ya ununuzi wa helicopters za jeshi, ndege ya Rais na magari ya jeshi. Hawajajibu chochote kuhusiana na upotevu wa $250 millioni pale BOT na gharama kubwa sana za ujenzi wa Twin Towers za BOT. Hawajajibu chochote kuhusiana na na Mkapa na Yona kujipatia Kiwira Coal Mining katika Mazingira ya kutatanisha na kuishinikiza TANESCO kusaini mkataba usiokuwa na maslahi kwa Watanzania wa shilingi 340 millioni.

    Hawajajibu chochote kuhusiana na mikataba siri ya uchimbaji wa rasilimali zetu na Buzwagi ambao hata kama bei ya ounce moja ya dhahabu ambayo sasa inauzwa kwa $743 ikipanda na kufikia $10,000 katika mwaka 2025 Tanzania tutaendelea kulipwa kama tunavyolipwa sasa. Si ajabu katika list ya Shareholders wa Barrick kuna majina mengi ya viongozi wa Tanzania ambao wameweka mbele maslahi yao badala ya Watanzania. Wanasaini mikataba kama vipofu au ngumbaru ambao hawajaenda shule.

    Hakuna cha ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya wala maisha bora kwa kila Mtanzania. Dawa ya mafisadi na majambazi iko jikoni 2010 watakuwa history.

    ReplyDelete
  16. dah!! mi nimesoma machozi yametaka kunitoka..hivi ni lini viongozi wetu wataamka na kujali maslahi ya umma na si chama? Mi nilitegemea aseme wanaunda tume yakuchunguza madai hayo.. hivi kweli kila hoja kutoka upinzani haina msingi? wanatupeleka wapi hawa?
    Ilani ya CCM wametekeleza lipi hadi sasa.
    Na wewe ka.michu Uccm umekuzidi mbona hukutuwekea hayo majina aliyoyataja Slaa..ama jamani mie sikuona?

    ReplyDelete
  17. Kuna usemi unasema (kila watu wanaongozwa na uongozi wanao ustaili)
    kwahiyo watanzania tunastaili hao hao viongozi wetu tulio nao , mlio wachagua wenyewe bila kuradhimishwa ,mkiwa na akili timamu...mie sijuhi mtu kama huyu sijuhi waziri wa ....nani anachagua watu kama hawa?????nchi ina watu wasomi wanaishia ulaya kwa kukosa kazi nyumbani halafu watu wababaishaji wanachukua posti kubwa sababu wana mapinduzi.
    hakuna aibu kama mtu mzima kutetea ujambazi na ubadhilifu mali ya umma yaani viongozi wa Tanzania hawana aibu kabisa yaani nchi kama Tanzania na umasikini wake still bado hata kile kidogo alichowabarikia mungu mnazidi kuwanyanganya(tuma madini kidogo)kwa kujitajirisha nyie na famili zenu milioni 34 watu wako hoi(details za world bank) halafu sijuhi waziri anaingia kwenye blog eti kukanusha.. .mwishoni anasema maisha bora kwa watanzania...muulizeni huyo mheshimiwa kama mke na watoto wake wanaamka saa 10usiku kwenda kwenye foleni ya maji au kwake wana kula milo mingapi..??///// Hao hao wanajaa makanisani na misikitini kuomba mungu..... haya bwana siye yetu macho poleni mlioko bongo(Things fall apart -Amukeni si shwari tena....)

    Doctor..

    ReplyDelete
  18. Wanapotoa madai wapinzani, serikali huwataka watoe vithibitisho! lakini serikali inapokanusha haitoi vithibitisho bali hutaka wananchi waamini tu kuwa serilikali inasema kweli, sijui hawa wasomi wanadhani kuwa watu wote walio nje ya mduara ni mbumbu tu!

    ReplyDelete
  19. Chadema ni wasanii! - Mtikila

    Mtikila adai Chadema inafanya usanii

    Stella Nyemenohi
    HabariLeo; Monday,October 01, 2007 @00:03


    Quote:

    --------------------------------------------------------------------------------
    MWENYEKITI wa Democratic Party (DP), Christopher Mtikila ameibuka na kukishutumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa kinafanya usanii wa kutumia majukwaa kujadili madai ya ufisadi dhidi ya viongozi wa Serikali kwa lengo la kufunika vyama vingine na kushika madaraka na siyo kuleta ukombozi kwa umma.

    Mtikila, ambaye hata hivyo anaunga mkono madai hayo ya Chadema, alisema kitendo cha viongozi wa chama hicho kuacha kwenda mahakamani kinadhihirisha hawana nia thabiti ya kukabili tatizo, bali wanapoteza muda katika majukwaa kujipatia umaarufu.

    “Hawa watu (Chadema) ni wasanii. Wanataka washangiliwe kwa gharama ya taifa. Mikataba ni suala la kisheria, haki ya kisheria haipatikani katika majukwaa. Wao hawataki mahakamani ambako ndiko wangepata haki?” Mtikila aliiambia HabariLeo jana.

    Alisema kitendo cha baadhi ya viongozi waliotuhumiwa kuwa mafisadi kwenda mahakamani, ni mwelekeo wa kuzimaliza hoja hizo ambazo kama zingeshughulikiwa katika mkondo unaostahili, umma wa Watanzania ungeshuhudia mabadiliko.

    Viongozi waliotangaza uamuzi wa kwenda mahakamani kumfungulia mashitaka Mbunge wa Karatu, Wilbrod Slaa, kwa madai ya kuitwa mafisadi ni Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Grey Mgonja na Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Patrick Rutabanzibwa.

    “Kitendo cha walioshutumiwa kwenda mahakamani, hapo ndipo wamewabana. Lazima waanguke. Hapa suala la kujiuliza ni kwa nini Chadema hawakwenda wakati walikuwa na haki na hoja ni za kweli?” alihoji.

    Kwa mujibu wa Mtikila, aliwashauri viongozi hao wa Chadema kufungua kesi kupitia mawakili watatu ambao kwa mujibu wake, walitaka walipwe Sh milioni 10 kwa kazi hiyo, lakini viongozi hao wakakataa.

    Katika kile anachosisitiza kuwa ni usanii wa kutaka kutumia hoja hizo kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao, Mtikila alisema ushauri wake ulilenga kufungua kesi itakayotoa suluhu la ufisadi kwa upana, ikiwa ni pamoja na kuondoa kipengele cha usiri katika mikataba.

    Mtikila aliendelea kukishutumu chama hicho cha upinzani kuwa kinafanya hivyo kujizoelea sifa kwa kutumia hoja ambazo siyo ngeni ili kukidhi matakwa ya wafadhili wao wanaowataka wahakikishe kinaingia madarakani katika uchaguzi ujao, na wala si kwa masilahi ya umma.

    “Wanaposema Karamagi kasaini mkataba Uingereza, Chadema nao hawana tofauti naye. Hawa wana Barrick, wao wana Conservative, wamewaambia lazima waingie madarakani,” alidai Mtikila.

    Akisisitiza kuwa shutuma hizo dhidi ya Chadema hazitokani na wivu wa siasa,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...