jk akipokea zawadi ya mpira toka kwa zamunda, mbongo anaeishi marekani hivi majuzi.

Serikali yapania uraia wa nchi mbili

Na Mobhare Matinyi, New York

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, amesema serikali itahakikisha sheria ya uraia wa nchi mbili inapitishwa kwa manufaa ya Watanzania na taifa na si vinginevyo.

Akizungumza na baadhi ya Watanzania waliokutana naye mjini New York wiki iliyopita katika hoteli ya Grand Hyatt, Waziri Membe alisema lengo la serikali ni kuwasaidia Watanzania na si kugawa uraia wa Tanzania kwa wageni wenye uraia wa nchi zao.

Alisema haingii akilini ni kwa nini Mtanzania wa kuzaliwa anyang’anywe uraia wa Tanzania kwa kuwa amechukua uraia wa nchi nyingine kutafuta faida za kielimu, ajira au hata matibabu.

“Ni kwa nini tumuadhibu huyu Mtanzania wa kuzaliwa kwa kuwa tu amechukua uraia wa nchi nyingine ili apate elimu ama ajira na kusaidia ndugu zake waliobaki Tanzania?” alihoji Waziri Membe.

Waziri alisisitiza kuwa sheria hiyo itakapopitishwa haitatoa mwanya kwa kila mtu kuuvamia uraia wa Tanzania bali itawalinda Watanzania wanaotaka kuchukua uraia wa nchi za nje kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Akitoa mfano mmojawapo bila kutaja majina ya wahusika, Waziri Membe alisema anaifahamu familia moja ya Watanzania ambayo ililazimika kuchukua uraia wa Kanada kwa sababu za matibabu, na kwamba kuwanyang’anya uraia watu hawa ni kuwaadhibu bila kujali uhai wao.

Alieleza kuwa familia hiyo ina watoto wawili ambao matibabu yao hugharimu dola 2,000 kwa kila mmoja kwa mwezi, na kwamba kwa kuchukua uraia wa Kanada, matibabu hayo yanakuwa bure. Alihoji je, ni haki kuwanyang’anya uraia wao wa Tanzania?

Akitoa mfano wa manufaa yanayopatikana Ghana, Waziri Membe aliwaambia Watanzania hao kwamba ni muhimu kwa Tanzania kutumia raia wake walioko nje kwa manufaa ya taifa na siyo kuwabagua.

“Mwaka jana pekee wananchi wa Ghana walioko nje waliingiza dola bilioni 2.5 kwa njia mbalimbali halali,” na akaongeza: “Taifa dogo kama Komoro, mwaka jana lilipata dola milioni 89 kutoka kwa wananchi wake walioko Ufaransa pekee.

Akifafanua zaidi, Waziri Membe alisema wakati akiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kipindi kisichofikia miaka miwili, Tanzania ilitoa uraia kwa wageni 101 na kushangaa ni kwa nini Watanzania wa kuzaliwa wapoteze uraia wao.




Waziri Membe aliwataka Watanzania kujenga umoja thabiti na kuwahakikishia kwamba serikali itakuwa pamoja nao ili kuleta maendeleo kwa taifa, na kwamba mawazo kuwa usalama wa taifa utakuwa hatarini si la jambo kuhofia iwapo sheria itatungwa vizuri.

Tanzania ina raia wake waliosambaa nchi mbalimbali duniani huku idadi kubwa ikiwa katika nchi za Kiarabu za Ghuba ambako wakati serikali ikiongeza ofisi moja ya Ubalozi nchini Oman miaka michache iliyopita ilikadiria kuwa kuna Watanzania laki tano.

Nchi nyingine ambazo Watanzania wanakadiriwa kuwa wengi ni za Marekani Kaskazini na Ulaya Magharibi ambako wako kwa maelfu, ambao wengi wao hukabiliwa pia na utata wa uraia wa watoto wao wanaozaliwa ugenini.

Mjadala wa suala la uraia wa nchi mbili umekuwa ukiendelea nchini katika siku za karibuni ambako kumeibuka kambi za wanaopinga kwa madai ya kulinda maslahi ya nchi na wanaounga mkono kwa madai hayo hayo ya kulinda maslahi ya nchi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Weweeee! watu TULIOJILIPUA tutaula kishenzi..UK msomali tanzania mbongo.duuh siamani

    ReplyDelete
  2. Mwanzoni mbona walitukatalia iweje sasa wakati Dr. Slaa ameanza kuchachamaa ndio huyo MWEHU MEMBE aseme hivyo ???? Aende anakokujua na hiyo serikali yake ya AWAMU YA NNE !!!!!

    Sibonike _ Ontario (CANADA)

    ReplyDelete
  3. Hili jambo ukiliangalia kwa haraka haraka utadhani ni zuri sana lakini ukilitazama tena kwa mara mbili mbili utaona ya kwamba uraia wa nchi mbili ni mbaya sana kwa Tanzania, Nasema haya kwa sababu zifuatazo:

    1: Wewe kama raia ambaye unaye ipenda nchi yako ni nini haswa kilicho kufanya utafute uraia mwingine, je hapo unaonesha ni mtanzania halisi? Na ni nchi gani utakayo pigania?

    2: Tunaweza kuja kupata ma spy ambao watakao fanya kazi katika maeneo mbali mbali nyeti na ata yasiyo nyeti ndani ya Tanzania eti kisa uraia wa nchi mbili ambao watakao kuja kuiangusha au kurudisha nyuma ili Taifa zuri duniani na sio tu ma spy bali ata Viongozi wenye uraia wa nchi mbili ambao hawata simamia maendeleo na haki za mtanzania. Viongozi hawa hawa wataweza kuwa madarakani kwa kivuri cha utanzania na kutumikia matakwa ya taifa lingine.

    3: Mwisho, Ningeshauri Serikali waliangalie hili swala kwa makini na sio kwa juu juu tu kisa kuweza kupendwa na wananchi wachache au kuweza kufanya familia zao kuangukia katika kitengo hicho kisa tu wawe raia wa mataifa mawili.

    Itakuwa ni aibu kwa Mtanzania anaye lipenda Taifa lake la Tanzania kuunga mkono ili swala.

    Busara na hekima ziwe mbele ya Viongozi wetu na sisi wananchi katika kutafuta suluhisho la hili jambo kwa maana matokeo yake yataiweka Tanzania pabaya.

    2007 PeAcE

    ReplyDelete
  4. SAFI SANA WAKIPITISHA HIYO TUNARUDI HOME TENA INGAWA TUMESHAOA NA KUPATA WATOTO UGENINI.NASHANGAA SANA WATU WANASHINDWA KUELEWA MAMBO MADOGO.''DUAL CITIZENSHIP'' NI ''COMMON'' SANA KTK NCHI ZA ULAYA,AMERICA NA BAADHI YA NCHI ZA BALCAN.WABONGO WANAOPINGA NI WALE WAHAFIDHINA(CONSERVATIVE) WALIOISHI NA KUKULIA KATIKATI YA MAPORI YA SIMBA,AU KTK MIGOMBA TU HAWAJAONA WENZETU WANAFANYA NINI.POA SANA ITS TIME TO COME BACK TO OUR HOME LAND..SAMEER-ATHENS(GREECE)

    ReplyDelete
  5. Shukurani, tutafaidi sie watanzania tuliochukua uraia nje, karaha zakulipia visa nikija TZ kwa nchi yangu Tanzania niliyozaliwa itakwisha.
    Jambo zuri sana

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Waziri Membe!Mheshimiwa kweli uko kazini na sio mchezo kama baadhi ya wakuu.
    Yote uliyosema kuhusu kunyang'anywa uraia wa ki-Tanzania kwa waTanzania waliochukua uraia ugenini kwa faida zao na jumuia kwa jumla ni sawa kabisa.
    Wanaopinga swala hili wanapendelea kuona wageni wanagaiwa uraia wa kiTanzania kirahisi rahisi tu na wazawa wananyimwa eti kwa vile wamechukua uraia wa ugenini.Uraia huo huko ugenini haupatikani kirahisi, na mpaka mTanzania anafanya hayo anafanya ili kupunguza masumbuko ya hapa na pale(mojawapo ya sababu) kwa vile hajui lini atajaliwa kurudi nyumbani!
    Hongera sana Mh Membe!

    ReplyDelete
  7. Hongera Jk, walau wabeba maboksi huko mbele watarud home bila khofu ya visa...lkn wale mliojilipua muandike mmeumia

    ReplyDelete
  8. AH YAANI HAWAKULIONA HILI?? HIVI NI LINI JAMANI TUTAKUWA NA VIONGOZI WANAOELEWA MAMBO YANAVYOKWENDA KATIKA SOKO HURIA ???

    SOKO HURIA LINATAKA VIONGOZI KUWA KARIBU NA WANANCHI AMBAO NDIO WAJASIARAMALI WENYEWE ILI KUPATA MAWAZO YANAYOENDANA NA HALI HALISI WAKATI WANATENGENEZA HIZO SERA ZAO.

    WATANZANIA WENGI BADO WAKO KATIKA LEVEL YA BIASHARA NDOGO NDOGO KATIKA UJASIRIAMALI LAKINI ANGALIA MFANO SOKO LA HISA BONGO LINAKUBALI KAMPUNI ZA MTAJI WA KUANZIA TSHS. MILIONI MBILI? JE HAO WALIOKOPI HIYO SERA HAWAKUJIULIZA WAFANYABIASHARA WANAOHITAJI MITAJI MIDOGO WATARAISE VIPI MITAJI?? HUO NI MFANO TU.

    SASA ISHU YA URAIA, YAANI MPAKA WAKADESE GHANA NDIO WATOE TAMKO?? SHAME ON YOU FOR LACK OF FUTURE ORIENTED PLANNING??

    NA SASA HIVI KUNA ISHU YA EAST AFRICA FEDERATION?? YAANI JINSI VIONGOZI WETU WALIVYO GOI GOI MPAKA UGANDA NA KENYA WAMESHAWASHTUKIA WANATAKA KUWAPIGA CHINI NA WAO KUANZA KIVYAO. SIWEZI KUWALAUMU KWA SABABU SIDHANI KAMA MAONI WALIYOKUSANYA KUWA WATANZANIA HAWATAKI JUMUIA YAMECHUJWA VEMA. HIVI HAWAKUMBUKI KUWA MAREHEMU BABA WA TAIFA ALIKUBALI VYAMA VINGI JAPOKUWA NI 20% TU YA WATANZANIA WALIOKUBALI KUWE NA VYAMA VINGI?? MIMI SIDHANI KAMA MAONI YOTE YANATAKIWA KUPEWA UZITO SAWA. KUNA WATU WANAOELEWA WANACHOZUNGUMZA NA KUNA WATU WASIOELEWA VIZURI. SASA SIO SERIKALI INAKUBALI TU MAONI ETI KWA SABABU NI YA WENGI??

    YOU GUYS IN THE GOVT MNATAKIWA KUWA PRO-ACTIVE JAMANI SIO KILA SIKU TANZANIA TUNAKUWA NCHI YA KUFUATA NA KUIGA WENGINE WANACHOFANYA.

    ReplyDelete
  9. SORRY NINA MAANA SOKO LA HISA LINATAKA MTAJI WA CHINI KABISA UWE MILIONI MIA MBILI (TSHS. 200,000,000) SIO "MILIONI MBILI" KAMA NILIVYOANDIKA HAPO AWALI.

    JE HAWA WATU WAMEFANYA SURVEY KWELI YA SME's HAPA BONGO?? MI NASHAURI MTAJI UNGESHUSHWA HADI MINIMUM YA MILIONI ISHIRINI (TSHS. 20,000,000) TU. KWA SABABU WATU WENGI HUWA WANAANZA NA VIMTAJI VIDOGO DOGO ZAIDI YA HAPO, KWA HIYO BY THE TIME WANAPOFANIKIWA KUKUZA MTAJI MPAKA 20,000,000 WANAKUWA WAMESHAPATA UZOEFU FULANI NA SIO VIBAYA WAKIRUHUSIWA KUANDIKISHA BIASHARA ZAO KATIKA SOKO LA HISA ILI WAKUSANYE MTAJI ZAIDI TOKA KATIKA UMMA.

    ReplyDelete
  10. hebu nielewesheni... ufahamu wangu mdogo wa suala hili ni kwamba ili upewe pasport ya nchi unayoomba uraia yabidi uikabidhi ile uliyonayo, na ili upewe passport mpya hapa tz yabidi uirudishe yazamani sasa haya yanakwendaje?
    Na wale wanaozitupa passport zao wakajifanya warundi, wasomali nk.inakuaje?Wanaojilipua je?
    Hivi ni sawa kweli uikane nchi yako,mpaka kuamua kuitupa au kuchoma moto utambulisho wako,halafu kesho unadai passport nyingine?mh!!
    Nielewesheni plz,hili lanipa mkanganyiko

    ReplyDelete
  11. samahani natoka nje ya hoja,
    nimeona komasho moja hapa juzi inaonyesha Tanzania, inaanza na mlima kilimanjaro, then serengeti na vijiji then inasema tanzania land of kikimanjaro,and Zanzibar. Ni komesha nzuri na i was veri impresd.
    Je kuna anaefahamu ni nani mhusika na hiyo komasho? ni serikali ya Tanzania, au some travel agency, au wizara husika na utalii?
    Asante,
    Mtanzania in NY.

    ReplyDelete
  12. Hongera sana Mh. B. Membe wewe ni nyota pekee inayong'ara katika baraza la mawaziri la awamu ya nne. Pamoja na kuwa ulikaa kwa kipindi kifupi pale mambo ya ndani mafanikio uliyoyapata yalikuwa makubwa mno hasa katika kuharakisha utoaji wa pasi za kusafiria. Na hapo mambo ya nje umeanza vizuri sana. Kila la heri na uendelee na uzi huo huo.

    ReplyDelete
  13. Hii itasaidia sana watoto wa walalaheri...wengi ndio wapo nchi za nje.

    Wazazi wao wanataka kuzidi kutoroshea nchi za nje mapesa ya Tanzania kupitia ankara za watoto wao!

    Eti Membe anasema nchi nyingine, kama Djibouin zinaiingiza pesa nyingi kutoka kwa Wa-Djiboiti walioko Ufaransa!

    Lakini huyu huyu Membe hatuambii ni "walalaheri" wangapi walioko nchini Tanzania wanaoiba, wanaofanya vitendo vya rushwa na ufisadi, na kusafirisha mapesa ya Tanzania nchi za nje!!!

    Si makumbuka stori ya Gavana wa Benki miaka kama mitatu iliyopita aliseama kuwa Watanzania wamelimbikiza mapesa yao nchi za nje mengi zaidi kuliko yaliyoko kwenye benki zetu nchini. Lakini hakusema za kwake ni ngapi huko nje! Sasa yamemfikia shingoni!

    Eti waliko nje ya Tanzania walete mapesa yao nchini, na hali nyie wakubwa mlioko nchini Tanzania mhamishie nchi za nje mapesa mnayoiba, kama wakina Mobutu, Abacha na rafiki zenu wengine!

    Watoto wa walalahoi walioko nchi za nje wengi ni kwa ajili ya scholarships; wengine shauri ya kusitooawayi kwa meli za matapeli! Of course, kuna waliooa kwa ajili ya mapenzi na makaratasi ya uraia.

    Mimi nataka kuwa raia wa Burundi. Halafu nitakuwa raia wa Djibouti. Bado najifunza Kifaransa.

    Baadaye nitakuwa raia wa Amerika. Bado ni kijana wa miaka 19 kwa hiyo italazimika nijiunge na jeshi la Amerika, kabla ya kufikia miaka kama 26 hivi. Pengine ikiwezekana tuje tumtwange Mugabe! Na siku Tanzania ikifanya "nyoko nyoko" kwa nchi yangu mpya ya Amerika, nije niitwange Tanzania!

    What a crap! Dual citizenship sometimos goes around our behinds, like a diaper. But sometimes it smells shit!

    Anyway, hongera kwa kuwa na "VIONGOZI WANAOELEWA MAMBO YANAVYOKWENDA KATIKA SOKO HURIA." Ndio maana mimi sasa ni kapitalisti, pia!

    Capitalism has neither boarders nor social responsibility; kazi yetu sisi mabepari ni kutengeneza fweza, fweza kwa wingi! Kama unabisha soma kitabu chetu cha ubepari kiitwacho: In Defense of Global Capitalism by Johan Norberg.

    Sisi "VIONGOZI (mabepari) “tu”NAOELEWA MAMBO YANAVYOKWENDA KATIKA SOKO HURIA" tupo Tanzania. Ndio maana tuliwakaribisha wawekezaji kutoka nje, waliosema:

    "Asante kwa kutukaribisha bila ushuru wa forodha, bila kulipa kosi miaka mitatu...Wengine tunachimba dhahabu usiku na mchana. Tlisafirisha michanga mingiiiiiiiiiiii ya dhahabu, in the name of research feasibility (eti kama kuna dhahabu)…

    “Tunaacha mazingira yameharibika. Maji machafu yenye zebaki (mercury) kutoka migodini yanaingia aridhini na mitoni hadi mziwani! Zawadi yenu: 'pesa za njugu'...

    “Siku mtakayoanza kutuchokoza kwa makodi yenu, tutafunga hiyo migodi kwa kisingizio kuwa hakuna dhahabu ya kutosha... kama tulivyofanya huko Buhemba!"

    (CHEKA)!

    ReplyDelete
  14. Leo itakua kicheko lakini kesho itakua kilio. Wahindi watakavyorudisha uraia wa kwao ndio hapo mtajiuliza ni nini kikosewa. Wahindi na dual citizenship wanainyonyoa USA lakini kwa vile ni big country wakla haitotoneshiki . Wakianza na kanchi hako yangu macho.

    Dual citizenship itawasaidia wachache sana. The rest of the people watakaonufaika ni wahamiaji wa nchi nyingi.

    Mtu akiukana uraia wa bongo na kuchukua wa nchi nyingine kinaeleweka faida zake..lakini hebu jiulize mtu aliyeukana uraia wake akachukua uraia wa TZ alikua anatafuta nini? Na siku akirruhusiwa kurudisha uraia wa nchi mbili atachukua nini kutoka nchini mwetu?

    Sijui wataweza kuandika law gani itakayomskubalia mzawa kuwa na uraia wa nchi mbili lakini mtu wakuhamia asiruhusiwe kukeep uraia wake na kumegua wa bongo pia. Easy said than done but I feel sorry for the poor people.

    ReplyDelete
  15. Ndio maana wengine wanyimwe tu uraia wa nchi mbili. Wewe unayesema kulipa visa yaani wewe dual citizenship yako ni kwa ajili ya visa tu. Visa yenyewe unaomba umeshanunua ticket.

    Wenzako ni kwa kuwekeza nchini na kufanya mambo ya maana sio kihela cha visa tu. Na wengine kuwa Senior citizen nchi za watu ni mwiko ndio maana two 2 nestings muhimu ndugu yangu.

    ReplyDelete
  16. Bepari kijana unaongea ukweli mtupu mwenye akili asome point zako.

    ReplyDelete
  17. Michuzi anzisha tena topic ya watanzania kurudi nyumbani kama ile ya 1/1/2006 itupe changamoto, hamasa na mzuka wakurudi nyumbani. Inaelkea wabongo bado kujiamini kwetu ni kudogo sana.

    ReplyDelete
  18. kwanza kabisa si nchi zote ambazo zinalazimisha kuukana uraia wako ukiomba upewe mpya.kwa hiyo kuna watanzania wengi ambao bado wana pass za tz japo wana uraia wa nchi nyingine.mf.wahindi wengi wana uraia wa canada na tz kwa vile canada wao hawalazamishi mtu kurudisha pass yake.hivyo hilo nalo litambuliwe vizuri sana.

    ReplyDelete
  19. Huyu Membe alisikia wapi kuwa ili upate matibabu nchini Kanada ni lazima uwe raia? Nijuavyo ni kuwa ukiwa mkaazi wa kusumu(landed) una haki ya matibabu, masomo nk Tusichanganye mambo

    ReplyDelete
  20. POOR TANZANIA!
    I see you depening into trouble day by day.I think this will be the bigest mistake ever!.If we pass this and slow East african; The rest will look at us as confused and contradictory. How can you pass dual citizenship and yet you are afraid of your own neighbor? How do u guarantee of those Giriki's and Wadachi wa Arusha and Tabora?.Kibaya ninachokiona ni Ndugu zetu wahindi ambao Membe mwenyewe ametumia Mfano wa familia yao. WATAIUA THAMANI YA PESA YETU AS LAWS TO REPATRIATE MONEY WILL BE MUCH MORE EASIER AND WILL LEAVE OUR ALREADY BROKEN BY "DALALI BALALI" FEDERAL RESERVE EMPY!!! Sio UTANI angalieni hili la pesa in first two years of Dual citizenship MTANIAMBIA.
    KILA LA KHERI TANGANYIKA NA ZANZIBAR!!

    MTANZANIA ASILI!!

    ReplyDelete
  21. KWA SERIKALI YA TANZANIA,
    SHUKRANI!!
    Hilo neno moja linatosha kusema yote yaliyo moyoni na ktk ubongo wangu.

    NYAKATAKULE!!

    ReplyDelete
  22. HOJA YA URAIA WA DUAL CITIZENSHIP KWA JICHO LA KITAALAM

    HII NI NUKUU FUPI YA PAPER ILIYOCHARAZWA NA WANASHERIA WASOMI KUHUSU URAIA WA NCHI MBILI. NIMEWEKA NA ANWANI YAKE YA MTANDAO ILI KILA MTANZANIA ANAYETAKA KUFUATILIA HAYA MAMBO AISOME. NI HII:
    http://www.lrct-tz.org/PositionPaperOnDualCitizenship.doc

    ...It is alleged, without sufficient proof, that there are at least 600,000 Tanzanians abroad (the higher range is close to 1.2 million Tanzanians). These Tanzanians said to be remitting approximately 63% of all foreign exchange inflows into Tanzania annually, including aid-in-kind. This remission is in the form of monetary aid to family members, personal and other investments. These are some of the issues which the Commission will have to find out in the study to ascertain whether it is justifiable to introduce dual citizenship based on economic reasons.

    ...Tanzania could borrow a leaf from Ireland as there are millions of Irishmen who have become citizens in the U.S.A, Britain and Australia and yet they keep strong links with their country of origin. Their contribution, in patriotically driven investment, has made a substantial contribution to making the Republic of Ireland Europe's fastest-growing economy today.

    ReplyDelete
  23. NYIE MPAKA TUWASUMBUE NDIO MNAANZA KUFANYA MABO YA MAANA..SUBIRINI SASA MTATUKOMA..

    ReplyDelete
  24. MZEE MEMBE HAPO TUPO PAMOJA,WANAOPINGA DUAL CITIZENSHIP NI WATU WALIOPITWA NA WAKATI, NI WALE WASIOJIAMINI NA POINT ZAO NI ZA KINAFKI.

    ReplyDelete
  25. wewe unayesema wahindi wanauraia wa nchi mbili tz na canada sidhani kama unaelewa unachosema. Hata kama canada hawamlazimishi mtu kurudisha uraia wa nchi yake lakini kisheria Tz ukishachukua uraia wa nchi nyingine huna uraia wa bongo tena. Labda hao wahindi wako wanauraia wa canada na india. India ina dual citizenship ukitaka unalipa $5000 wanakeep uraia wako.

    ReplyDelete
  26. canada hata ukienda kutembea tu ukaugua wanakutibu bure. sio lazima uwe raia na kupata uraia wa canada sio vigumu kama usa au uk. Canada bado wanahitaji watu.

    ReplyDelete
  27. Viongozi wanataka tuwekeshe bongo wakati wao hela zao wanaweka nje ya nchi. Ajabu sana

    ReplyDelete
  28. Anony up there when you say there are 1.2 mil Tanzanians living abroad, do you know how many of them are Indians hold Tanzanian’s passport? Let be real... When I went to get a new passport I was amazed by how many Indians and Ethiopians holding Tanzanian passports there. We were hardly 10 real black Tanzanians and majorities were of Indian and Ethiopian origins. How many of these people do you see even bother meeting with the president while he is abroad? They don’t care…and they represent 90% of all so called "Tanzanians living abroad"

    See the reality check of those who meet with the president all the time. They are all black Tanzanians who are real wazawa and have greatly feelings of their country and a representing only 10%.

    Many real real Tanzanians abroad are students and will never benefit with this so-called "DUAL CITIZEN"

    The president needs to try harder to keep the economy strong to convince people to think twice before they abandon their citizenship. I wonder why he is even happily fine hearing that people ditch the citizenship because of economic factors. He should be ashamed of that because in many countries people abandon their citizenship from politics or war reasons.

    He should persuade people to go back home after finishing their education not rewarding them with the second citizen after they first dump it.

    We always see the comments from wabongo begging wabeba mabox to go back home after finishing skull but surprising the president is not.

    ReplyDelete
  29. Wewe anon 8:46 nani kakwambia ukienda Canada kutembea tuu,utatibiwa bure???????

    ReplyDelete
  30. We jamaa unayedai eti ukienda Kanada tu unatibiwa bure, mimi nilishindwa kutibiwa mafindofindo tu, bahati nzuri tulikuwa tumemaliza mkutano wa kimataifa, na Mganda mmoja akanipeleka kwa ndugu yake wakaniokoa kwa anti-biotics tu, homa ilishapanda mpaka nikaanza kutetemeka. Nilikwenda kliniki mbili na hospitali mbili na nikafikia mahali hata pa kwenda pharmacy nikiwa na pesa yangu ya dawa tu, lakini wapi. Nikaondoka siku hiyo jioni na nilipofika Uingereza mambo yakawa freshi nikarejea Bongo na kuendelea na matibabu Sinza. Acheni kujipendekeza, hakuna matibabu ya bure Kanada, msitake kumjibu Waziri hata kama hamna pointi, amewahi kufanya kazi Ubalozini Kanada kwa miaka minne, anajua anachosema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...