barabara za dar si magari tu yaliyo mengi bali pia madereva watemi. jamaa mwenye ki rav 4 alikatiza boda kukwepa foleni na kukutana na magari yanayoenda alikotoka. kuambiwa apishe akaleta utemi. na mwenye shangingi naye kumbe mtemi. ilikuwa raha ya aina yake na hadi naondoka sehemu ya tukio jamaa alikuwa bado kadindisha na mwenye shangingi akawa anakula naye sahani moja...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. bongo kwa utemi!watu hao nao hawana kazi?

    ReplyDelete
  2. Hahahaha Muchuzi Lugha hiyo usituharibie swaumu. Utemi muhimu na huwa unasaidia wakati mwingine.

    Hivi kumfanyia/unyesha utemi mwenzio si ndio bully....

    Usherekeaji mzuri wa kutimiza aka 2

    ReplyDelete
  3. Nisaidieni wajameni: "Kudindisha" ni tusi au msamiati wa kawaida tu?

    ReplyDelete
  4. kudindisha kwa kweli ni tusi!ni pale wewe unapotaka ''kuwasha'' kibiriti ili ''utie'' moto

    ReplyDelete
  5. ISSA KUMBE HUYO DADA MWENYE HIYO GARI NDOGO KUSHOTO MNAFAHAMIANA, NIPELEKEE SALAMU ZANGU.

    ReplyDelete
  6. "Kudindisha" siyo tusi,bali ni kusimamisha.Ukiona kitu kimesimama ujue kimedinda.Kama mtu ana hasira na zimemsimama ujue amedindisha na situation hiyo.Hahahahahaha

    Haya wewe mwenzetu Dinah unayesikia tu mtu kadindisha kwenye ugomvi wa Rav 4 na Shangingi unaharibikiwa swaumu yako kulikoni?????Yani ni kudinda tu au kuna lingine.Kaaaazi kwelikweli.Nakumbuka wakati fulani tukiwa shule Tanzania wanafunzi wa "Kiume" wa Msalato walikuwa wanapata ugonjwa wa kupiga kelele wasipopewa uji wa mgonjwa.Vipi Dinah mdogo wangu,unahitaji ji wa mgonjwa nini??Tunaogopa makelele.
    Majita

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...