baadhi ya wafanyabiashara wa bongo walioongozana na jk marekani. toka shoto ni issack mwamasika, gerald mongela, emily mwenewanda, mary malekia, elvis musiba, joachim lyimo, veronica lyimo na mulamu nghambi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Hii deligation yote imeenda kwa hela zao au za wavuja jasho?.
    Warioba kasema viongozi ni watu na wana makosa,hii ni wazi kwamba Dr Slaa ana ukweli.Warioba kakiri kwamba Mkapa&JK ni watu na wana makosa ila tusiwazonge.

    ReplyDelete
  2. WADAU; LEO AJABU KWELI. KATIKA WIKI HII UA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI, BLOG YANGU (MICHUZI) IMETIMIZA WATU MILIONI MBILI (2,000,000) NA NINADHANI HADI SIKU YA MWISHO WA RAMADHAN ITATIMIZA WATU MILIONI 3. (KWI KWI, KWI, KWI KWIIIIIIII, TEHE TEH TEHE TEHEEEE, AAAAAAA, WE MAMA MBAVU ZANGU, WE MAMA MBAVU WEEEEEE... A.) I WISH KILA ANAYETEMBELEA HUMU ANGECHANGIA DOLA MOJA KWA SIKU...TEH TEH TEH TEH SIJUI NINGEKUA MILIONEA WA DOLA NGAPI....TIH TIH TIH KWI KWI KWI KWI KWIWWWWWWWW.

    ReplyDelete
  3. Wafanya biashara,
    Mbona sioni picha za kina.
    Dewji,Mengi,Kishimba,Simba,Mohamed Enteprise na wengine wengi.
    Naomba mtu anisaidie kutaja bishara ya kila mmoja pichani kutoka kulia kwenda kushoto.
    Pamoja na jinsi ya kuwasiliana na hawa watu

    ReplyDelete
  4. Kuuliza si ujinga.
    Hawa waungwana wanafanya bashara gani? Kwangu itakuwa vizuri kama utanipa habari hii kwani wawekezaji sio lazima wawe weupe ati.
    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  5. Inabidi hawa jamaa wapewe darasa kuhusu habari ya suti. Piga ua kifungo cha chini huwa hakifungwi. Kwa jinsi walivyovaa wafanyabiasha/wawekezaji watakuwa na picha tofauti na biashara. Tunajua kuwa uvaaji ni pendeleo la mvaaji lakini unapotaka kumshawishi mtu awe m-bia inabidi uwe umevaa vizuri. Jinsi unavyovaa watu ndivyo watakavyo kuona kama wewe ni muhuni au mtu wa kutojali au mtu uliyepitwa na wakati na listi inaendelea.

    ReplyDelete
  6. Naamini kabisa kuwa wafanyabiashara wa Marekani na serikali yao imefurahi sana kuwapokea hawa wafanyabiashara muhimu sana wa Tanzania... inaonyesha jinsi walivyovaa kuwa wana mamilioni ya dola na wako tayari kusaidia uchumi wa Tanzania. New York Stock Exchange lazima iwaalike hawa wakapige kengele kwa heshima yao na ya Tanzania.

    Najitahidi nisife kwa kicheko. Tanzania tutafika lakini pole pole ni mwendo.

    ReplyDelete
  7. watuambie wameenda kuuza nini America?au wameenda shoping?
    au watalii wamekwenda kutembea US!
    ONLY IKNOW MOST OF THEM ARE GOVERNMENT OFFICIAL,LEADERS BUS ORG,AND SOME FRIENDS!

    ReplyDelete
  8. Misafara kama hii wangekuwa wanachukua na Makonda na madreva wa ya mabasi waje waone jinsi wenzetu wanavyofanya kazi yao.

    Sio vibaya japo akachukua na viongozi wa machinga pale mazenze na mchikichini maana wanavikundi vyao,hii inaweza kuwpa hamasa ya kufanya makubwa zaidi.

    Ni hayo tu

    ReplyDelete
  9. wadau me ninavyojua mary malekia ndiye agent wa sony hapa town, Elvic Msiba ndiye presidee wa TCCIA na Mulamu Nghabi naona kijana anatoka town ankampuni yake moja pale mavuno house inapublish magazine moja ya matangazo jina ckumbuki lkn waswahili wanasema mdogomdogo ndiyo mwendo big up wengine cwajui.

    ReplyDelete
  10. Huyo mmoja ni kijana wa mjini pale bongo(mishe town) anaitwa Mulamu sasa sijui jamaa amepata dili gani haya wee hongera inaelekea sasa bongo mambo swafi, ama JK ameanza kuwaona na vijana.

    ReplyDelete
  11. Sasa labda sielewi! sasa hao so called wafanyabiashara, wanakwenda na raisi Marekani ili iweje???? kuwatangaza? i dont reallly get it!kawa wanataka kwenda si waende kwa mida yao! individually??goin wit Mr president will change somethin???? or make any impact?? i doubt! they r clerly swallowing poor citizens doughz! itz sickening!

    ReplyDelete
  12. Jamani msiwasumbue hawa wafanya biashara maana ndio wanaoweka mafuta ndege ya ya raisi,au mnafikir ndege inakula mafuta ya elfu kumi nini?Hilo wese achana nalo babu hiyo sio RAV 4 eti.

    ReplyDelete
  13. Bwana Mithupu kuna tofauti kubwa kati ya mchezo wa checkers ambayo kwetu ni Draft na mchezo wa chess.Hawa wachumba wanaonekana wanacheza draft(checkers) angalia mpangilio wa kete utagunduwa.
    by Rubaman

    ReplyDelete
  14. Watanzania tuna safari ndefu, sijui ni kwanini mtanzania akionekana anafanya maendeleo maoni yanakua ni negative tu! Any way hawa ni wafanyabiashara ambao wanaenda kuitangaza Tanzania na kujitangaza biashara. Nawapongeza kwa wabantu asili kuonekana kwenye mishafara kama hii na naomba wengi wazidi kujitokeza na sio kulalamika tu. wabantu oyeeee

    ReplyDelete
  15. Big up wanyabishara wa Tanzani. tunataka wengi wajitokeze namna hii

    ReplyDelete
  16. Sasa mwenye jibu atuambie..hawa wanafanya biashara gani? na wameongozana na rais ili iweje? awatafutie wateja ama kitu gani? nani analipa gharama za hawa watu,wale watoa jasho wasiojua lini watafaidika na jasho lao au?
    Anaejua anifahamishe wajemeni.

    ReplyDelete
  17. Wabongo bwana we are still far....
    yaani hawa ndiyo wafanya biashara maarufu wa Ki-Tanzania wakuongozana na Raisi kwenda Marekani mbona nikichekesho sana..kwa mawazo ya Jk hawa watu wanaweza kuongea na nani biashara labda kuomba mkopo...mfanyabiashara huna angalau 1 million USD kwenye account alafu eti unaenda state kuongelea deal ni kichekesho na aibu kwa nchi... namna hii kweli Tanzania nisawa na kichwa cha mwendawazimu ambacho kila mtu ujifunzia kunyoa....(jamani mwenye details za kwamba Tanzania tuna millioner businessman naoma utufahamisha kupitia blog hii)

    Doctor....

    ReplyDelete
  18. Si mara ya kwanza rais kuambatana na jeshi la wafanyabiashara. hatujawahi kupewa ripoti ya mafanikio yao. Ila nakumbuka mwaka jana alikuwepo pia mwandishi dada Badra Masoud (Mtanzania) ambaye aliporudi aliwaumbua kwa kusema walikuwa busy wakifanya shopping zao na kurudi na makontena yao Kwisha. hakuna zaidi. Badra akaitwa na Ikulu na kuambiwa kuwa tripu kama hiyo haipati tena.

    ReplyDelete
  19. ETI WAFANYABIASHARA.HAWA WOTE MISHEN TAUNI TU HAWANA LOLOTE.WAJANJA WA BIZNES AKINA MO,DEWJI,ZAKARIA,BAKHRESA,ASKOFU WAPO WAPI HAWA WANA HATA 2 MILLION USD KTK ACCOUNT ZAO.HALAFU PESA KAMA NI BIBI NA BABU ZETU WAVUJA JASHO NDIO WAMETUMIA KWENDA USA SUBIRI TUNAENDA KWA FUNDI MITAMBO UTASIKIA MAMBO WAKIRUDI EBO.SAM-ATHENS

    ReplyDelete
  20. dah..wee DOCTOR weye..inaelekea upo very bitter na watu wenye fwetha sio? hivi wewe unakazi kweli ama masaa yote kwenye udaku kuwasema wenzio? sasa kwataarifa yako...hao wote pale ni matajiri...tena mpaka wakachaguliwa na rais- cheti cha juu..mbona wewe hatukuoni kwenye picha? manake umepinga kweli...na huna chochote cha kutuonyesha...midaaa..(wabongo ndo maana hatuendelei..) no suport...tunataka vya wenzetu..

    ReplyDelete
  21. huyo badra masoud, alikuwa anafanya nini, wakati wenzake wapo 'SHOPPING'?? manake sio lazima uwe kwenye kikundi kufanikiwa....ebu mtu aniambie..

    ReplyDelete
  22. INASIKITISHA SANA.

    RAIS WETU NAE AACHE KUFANYA KAZI YA TCCIA. ANAJISHUSHA SANA HADHI... SIJAONA RAISI WA NCHI ANASINDIKIZA WA-BUSINESSMEN KWENYE KUTANGAZA NCHI. KWA SIE TUNAOISHI MAREKANI TUNAHIMILI VICHEKO VYA MATAIFA MENGINE...

    KWANZA: HII NI KWA SABABU UBALOZI WETU HAUFANYI KAZI YAKE - HII INAJULIKANA WAZI

    PILI: SERIKALI NAYO HAIJUI KUONGOZA KWA KUTUMIA VYOMBO VYAKE TOFAUTI ..KAMA TCCIA (AMBAYO IMEOZA NA AKINA MUSIBA)

    TATU: UCHUMI WETU SIO SIRI UNALIWA NA WAJUAJI - WAHINDI, WAGENI ETC ETC -

    MENGI NINGESEMA.... ILA NIISHIE NA.. TANZANIA KWELI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU !!!- ALIBASHIRI BABA WA TAIFA, MWL. NYERERE...

    ReplyDelete
  23. Natumaini kuwa hawa so-called wafanyabiashara wamejilipia usafiri, malazi, kula nk!
    Mr Mengi, Mr Kishimba na wafanya biashara maarufu wa maana wako wapi?
    Huu msafara jamani si ulibidi uongozwe na waziri wa biashara?Au hatuna waziri,naibu waziri wa biashara au mwenyekiti wa bodi ya biashara?Sijui kwa nini msfara huu unaongozwa na Mh Rais Kikwete?!
    Halafu basi hawa wafanya biashara wenyewe hawatii moyo kwa mtazamo wa mwanzo,kimavazi nk;hivi ni vitu muhimu sio mtu unajiweka hivyo hivyo tu.Sio kwetu huko!
    Kweli tuna safari ndefu kama ilivyosemwa na anonymous hapo juu!

    ReplyDelete
  24. My dear Anonymous september30,2007 2:07:00 AM EAT .
    Fortunately i cant feel bitter for rich Tanzanian kama kweli wapo maana sijawahi kuwasikia wala kuwaona kwenye Forbes Journal.. hata kama wapo mie hawawezi kunitia wivu kwasababu mie siishi bongo nyie ndiyo mnawaabudu...kwa taarifa yako hao watu wana hela ya kula siyo status ya Tanzanian businessmen......
    Pili mie ni mtu educated ambaye kila siku lazima nisome blog hii ya nyumbani ,magazeti mbali mbali, journals e.t.c ili kupata information mbali mbali...wala siyo kupiga udaku wa kibongo
    hapo tunachangia hoja na kutoa maoni, in fact Tanzania is meaning much for me although iam not staying there thus why u see my views and remarks in this blog...
    Tryto see things in black and white not just in gray colour only....
    Doctor....

    ReplyDelete
  25. Tanzania Tanzania nakuppenda kwa moyo wote

    Hivi Bush ameshafika Bongo mara ngapi manake wawekezaji ni wengi sana ssijui walipelekwa na nani huko?

    Usanii tu..mbona wafanyabiashara wa kweli hatuwaoni hapa hata mmoja na kazi ya wazisri wa biashara ninini? Kweli hela ya walala hoi inaliwa na walala hai

    Hapo kula bure kulala bure tena NY City!!!!!! mama yangu vidola vyetu vinaisha vyote

    ReplyDelete
  26. Hao hapo pichani ni wafanya biashara kama walivyo wafanya biashara wengine.
    Nakumbuka moja kati ya majukumu ya serikali yeyote ile ni kuwawezesha wananchi wake, na hili limekuwa likifanyika katika serikali ya Tanzania katika ngazi mbalimbali.
    Mh rais amekwenda New york kwenye mkutano wa baraza la Umoja wa Mataifa, kuna ubaya gani kama akiombwa na wananchi wake afanye shughuli nyingine zaidi ya ile iliyompeleka?
    Ni lini tutajivunia mchango wa wafanya biashara wazalendo wa Tanzania?
    Wale wote wanaopinga jitihada za serikali bila ya kutoa mwelekeo mbadala wenye manufaa hawaitakii mema nchi yetu.
    Tubadilike wa-Tanzania tuache kupiga majungu tufanye kazi. Na kama kazi yako ni majungu na udaku nitavipiga vita wakati wote.
    Huu ni ukweli.

    ReplyDelete
  27. SERIKALI INAWAWEZESHA WATU WA MAKUNDI YOTE. SOMA HAPA CHINI
    Mkweli

    SIDO, TFSR wasaidia wajasiriamali wadogo
    Gurian Adolf, Sumbawanga
    HabariLeo; Thursday,September 27, 2007 @00:03

    SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Tools for Self Reliance (TFSR), wametoa msaada wa zana za kufanyia kazi kwa vikundi 40 vya wajasiriamali wadogo Rukwa.

    Kwa mujibu wa Meneja wa Sido Mkoa wa Rukwa, Martin Chang’a, msaada huo wa vitendea kazi kwa wajasiriamali hao wa wilaya za Sumbawanga na Nkasi, una thamani ya Sh milioni 25.

    Chang’a alisema SIDO kwa kushirikiana na TFSR walitoa mafunzo kwa vikundi 40 vya wajasiriamali hao wa fani za ushonaji, useremala, mafundi magari, mafundi baiskeli, mafundi pikipiki, mafundi uashi na mafundi bati.

    Alisema baada ya wajasiriamali hao kupatiwa mafunzo hayo, SIDO kwa kushirikiana na taasisi hiyo yenye makao yake makuu Uingereza waliamua kutafuta vifaa kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali hao, kwani ili wamudu kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.

    “Tuliona elimu pekee isingetosha kujikwamua kiuchumi kutokana na wajasiriamali wetu kukosa mitaji na vitendea kazi, hivyo tumejitahidi kwa kushirikiana na wenzetu tumepata vitendea kazi, naamini vitawasaidia sana,” alisema.

    Akikabidhi vifaa hivyo kwa wajasiriamali hao, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay, alilishukuru shirika hilo kwa kuwawezesha wajasiriamali hao, na aliwataka wajasiriamali hao kuthamini msaada waliopewa na kufanyia kazi kwa malengo yaliyokusudiwa.

    Njoolay alilitaka SIDO kuwafuatilia kwa wajasiriamali hao mara kwa mara ili kuangalia kama vifaa hivyo vinatumika kwa malengo kusudiwa na iwapo itabainika baadhi yao wanatumia isivyotarajiwa, wanyang’anywe mara moja.

    ReplyDelete
  28. Wewe unaejiita Doctor, je ni ule u-Doctor kama wa akina Dr. Remmy?

    Hebu nikunukuu:
    "Fortunately i cant feel bitter for rich Tanzanian kama kweli wapo maana sijawahi kuwasikia wala kuwaona kwenye Forbes Journal.. hata kama wapo mie hawawezi kunitia wivu kwasababu mie siishi bongo nyie ndiyo mnawaabudu...kwa taarifa yako hao watu wana hela ya kula siyo status ya Tanzanian businessmen......"

    UNAJIDAI HUNA WIVU LAKINI UNAONYESHA UNAWAONEA WIVU SANA TU HEBU SOMA SENTESI YAKO HII

    '...kwa taarifa yako hao watu wana hela ya kula siyo status ya Tanzanian businessmen......'

    KAMA HUU SIYO WIVU NI NINI?

    "Pili mie ni mtu educated ambaye kila siku lazima nisome blog hii ya nyumbani ,magazeti mbali mbali, journals e.t.c ili kupata information mbali mbali...wala siyo kupiga udaku wa kibongo"

    ARE REAL EDUCATED? UKISOMA MAONI YAKO YA AWALI HAIONESHI HATA CHEMBE YA KUELIMIKA KWAKO, WEWE HUJAELIMIKA KABISAAAA, TENA UNACHEFUA.


    'hapo tunachangia hoja na kutoa maoni, in fact Tanzania is meaning much for me although iam not staying there thus why u see my views and remarks in this blog...
    Tryto see things in black and white not just in gray colour only....'

    WEWE NDIYO UNAYEANGALIA MAMBO KWA NJIA FUPI, NAKUSHAURI 'DOCTOR' UANGALIE PIA IN 'THREE DIMENSIONS' AND IN TRUE COLORS, BLACK AND WHITE INAKUPOTOSHA KAMA ULIVYOZOEA KUANGALIA.

    ReplyDelete
  29. Ebwana mbona jibu sipati. Hawa waungwana wanafanya bashara gani? Au misheni tauni ni biashara siku hizi?
    kwikwikwi
    Labda wawarubuni vipofu ila kama wanatafuta wawekezaji kwa uvaaji huu hutompata hata mmoja.
    Hawaonekani kama wapo makini.

    ReplyDelete
  30. na Doctor, najuwa huishi tanzania, lakini wewe ni mtanzania....hao wenzio wana represent inchi zao, wewe, unasema tuna waabudu..mbona hueleweki mpwa? unafrkri kuwa u.k ndo deali, wakati watu wanabeba maboxi?

    ReplyDelete
  31. Nyie woooooote mnaokandia hao wafanyabiashara hamna lolote mnaona wivu tu!!!!....mnataka kuniambia mngeambiwa muende nyinyi mngekataa? Mngesema aende Mengi, Dewji, Bakheresa na wengine maarufu? Achane wivu....kutesa kwa zamu.....zamu yenu itafika nanyi mtaenda...kama isipofika bahati mbaya kwenu.....bahati ya mwenzio usilalie mlango waziiii!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...