wadau, katika pekuapekua zangu kufuatia mchongo wa stori hiyo chini nimekutana na picha hii na stori moja ya ajabu kwamba bongo tumenyang'anywa haki ya kujiita tanzania na mahakama moja huko marekani. habari kamili bofya hapo chini. ni stori ya zamani ila inatisha! http://www.theonion.com/content/node/29405#email_this

baada ya hiyo soma hii ingine chini na anayejua undani wake atupatie maana hii ni kasheshe.....


Google, Yahoo Sued For Stealing Names From Tanzanian Tribes
If you liked our report on the bizarre handwritten lawsuit against Google from a guy worried that his social security number was too similar to Google's name, here's another one for you. Once again, special thanks to Eric Goldman for passing this one on.
This time, at least, most of the lawsuit is typed (there are some handwritten parts at the end), though, there are numerous typos.

The lawsuit is being filed against both Google and Yahoo by a guy who is apparently being detained by Immigration services in Houston.
He claims that both Google and Yahoo stole their names from Tanzanian tribes -- and now they should pay up. Specifically, he claims that Google took its name from the Gogo tribe and Yahoo took its name from the Yao tribe.


Conveniently, this guy happens to be a descendant of both tribes. He's merely asking for both companies to pay $10,000 each to every member of both tribes, going back three generations. Simple!


While it is true that many companies are using foreign words (Swahili is especially popular) in choosing company and product names (Kijiji, Joomla, Renkoo, Wiki, Tafiti, Jambo, etc.), both Google and Yahoo have pretty well-documented histories of their names, and the names of these Tanzanian tribes clearly have nothing to do with either one.
Not that the guy doesn't try: "The court is now been asked to answer a common sense question: Is "Google" much more related, semantically and lexically, with "Gogo" or with "Googol"?"
Once again, the chance of this lawsuit getting anywhere is basically nil (even if they had taken their names from the tribes, which they clearly did not), but as Goldman points out to us: "There is, of course, a serious problem here about the courts getting clogged up with lawsuits brought by prisoners/detainees with too much time on their hands and nothing to do but file lawsuits, and companies having to spend money to stomp out these lawsuits."

In the meantime, this seems mighty close to life imitating The Onion.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. WANAWAZIMU WANACHEZA MAKIDAKIDA HAO !!

    ReplyDelete
  2. Michuzi eeh,
    Hii ni ya zamani sana.Ni kweli kesi ilikuwepo na iliunguruma sana tena ilikuwa na mvuto wa aina yake.Hukumu ilivyotoka Tanzania ya wakati huo ikapendekezwa itumie jina la "REPBLIC OF KANDAMIZAJI" Kwa hiyo tangia siku hiyo sisi watanzania tukaitwa "WAKANDAMIZAJI" Ndo maana yule mchekeshaji anaitwa Masanja Mkandamizaji yani sawa na Masanja Mtanzania.Ni story ya kweli kabisa.Mlioko Kandamizaji mtafuteni Masanja atakuwa na full data kwani haiwezekani hivihivi ajue jina hilo.

    ReplyDelete
  3. Michuzi,
    The Onion ni gazeti la joke. So hizi habari sio za ukweli nichangamsha baraza tu.

    ReplyDelete
  4. Mhhh labda Mtikila alishajua ndio maana anakazania tutoke na jina la "Tanganyika".

    ReplyDelete
  5. This is rather silly and as ridiculous as it sounds. I can't even imagine somebody can win over a poor case like that. This is to show you how much Americans are dumb and naive about the rest of the world. If and only if this lawsuit existed.

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi kuweka kichwa cha habari "Duniani kuna mambo juu ya suala hili" ni sawa na kuridhika kwamba sisi tumekosea na mshenzi huyu ana haki kumiliki jina la nchi yetu. Haijuzu kama anaingiza mabilioni au trilioni ya dola kwa jina hilo sio lake na kihaki nchi yetu inapaswa kumfungulia mashtaka nayeye alipie matumizi ya jina hilo. Ni ghadhabu na hasira nyingi kuona kwamba tumezubaa mno kiasi cha kwamba watu wanatuchezea mpaka katika nchi yetu.

    Tanzania ni jina la nchi yetu yeye atuambie kalipata wapi na kama alikuwa hajasikia nchi inayoitwa Tanzania sio kisingizio cha yeye kuvunja sheria. Mimi naishi Marekani ambako wenzetu wa Ethiopia wamewapeleka mahakamani kampuni inayomiliki migahawa ya Starbucks kwa ajili ya kutumiwa. Je sisi tutakaa na kusema duniani kuna mambo tu?

    ReplyDelete
  7. Michuzi na wana-blogu wote, hakuna ukweli wowote...na hakuna cha kuhofia!

    Hayta hayo ya majina ya Google na Yahoo, pia ni "mere satrical news".

    Tazama walivyoandika Jumla (Joomla)!

    "Gazeti", labda niseme ki-gazeti cha wiki, la Onion huandika habari kwa njia ya "satire" tu; hutolewa bure! Lenyewe hupata pesa kutokana na matangazo ya biashara!

    Ni kati ya vijigazeti vingi hapa Amerika. Kinachapishwa hapa New York, lakini "states" nyinginezo, kama Florida, zina ofisi zake.

    "Satire" zake ni sawa, kwa mfano, siku ya Fools Day, IPPMEDIA online ilikuja na stori miaka, kama mitano, iliopita kwamba Iddi Amin Dada alionekana mjini Tabora!

    Siku ya Fools Day moja, gazeti la Nation (Kenya) liliwahi kuandika habari kuwa mafuta yamegunduliwa chini ya Jiji la Nairobi!

    Sanamu ya Mzee Jomo Kenyatta, iliyoko nje ya Jengo la Bunge, ilionyeshwa imeangushwa chini na kuvutwa, kutokana na mwanzo wa uchimbaji wa mafuta hayo!

    Hiyo stori ya Saloon ya Tanzania huko Tallahassee, Florida, iliandikwa tu kufanya "satire" ya madeni (foreign debts) ya Tanzania.

    ReplyDelete
  8. This is so funny...nani hao huko TX jamani? Is this for real?

    ReplyDelete
  9. The Onion is a Satire paper, ni utani huu

    ReplyDelete
  10. SISHANGAI .....LA AJABU LIPI NASIE WATZ TUMELALA ....KUAMKA HATUTAKI!LABDA HILI LITATUSHTUA...LAKINI NIJUAVYO - SISI ...TUTARUDI KUKOROMA NA KUWAACHIA WAJANJA ....

    ReplyDelete
  11. IS this some kind of APRIL FOOL joke.

    ReplyDelete
  12. Mambo ya The Onion. Hili gazeti linasifika kwa kuwa na habari za kutunga ile mbaya, Kila story inayoandikwa kwenye kigazeti hicho, amini 0% ya story, that's to say halijawahiandika kitu chochote cha ukweli na hilo linajulikana na watu wengi US

    ReplyDelete
  13. Huyu Dennis Maringo anamatatizo. Hizi degree zenu za Law kutoka mlimani mnadhani mnaweza kupractice every where zitawapeleka pabaya. Sasa anatakiwa alipe dolla 500 kama cost za mahakama.

    ReplyDelete
  14. The onions ni comedian news center. Hii story sio ya kweli, American hawana judiciary power ya kuhold case ya nchi nyingine Vs their citizen.

    hiiyo kesi ya pili ni kweli, huyu jamaa aliye sue ni attoney graduate from University of Dar-es-salaam school of Law. I think ali sue ili kupata media coverage, and he did get them.

    ReplyDelete
  15. Hiyo "The Onion" ni website maarufu - kazi yao ni kupost vioja vya kuchekesha. Kama sijakosea, asili yao ni sawa na Mzee Punch pale UDSM (Mlimani). Soma historia yao hapa http://en.wikipedia.org/wiki/The_Onion

    Stori zao nyingi ni za kutengeneza na sio za ukweli. Burudika na vioja vingine hapa http://www.theonion.com/content/index

    ReplyDelete
  16. meee wa masikini hazaijamani sasa naanza kuamini

    ReplyDelete
  17. Wishful thinking!!!

    Ama kweli,leo nimefurahi sana, kumbe kuna watu hawalali wakifikiri kuhusu Tanzania. Maana nina uhakika ya kuwa hilo gazeti si la Watanzania na Watanzania si wengi kiasi hicho huko NY kiasi cha wao kuweza kuwatania kama hivyo. Na wakati huo huo sisi Watanzania hatulali tunafikiri jinsi ya kuchukua pipa kwenda ukerewe... Tena hao waandishi wako up-to-date mpaka na jina la Rais wa wakati ule walilijua. Kuna watu wengi sana nje ya Tanzania wanaamini ya kuwa Rais wa Tanzania ni Late Mwl. J.K. Nyerere (RIP) mpaka leo.

    Mungu ibariki Tanzania(TANganyika na ZAnzibar zenye NIA), wabariki Watanzania wote waliopo ndani na nje ya nchi. Wabariki pia wageni wote waliopo ndani ya ardhi ya Tanzania. Pawepo na amani na umoja katika nchi yetu ya Tanzania.

    Tanzania Oyee!!!

    Lilly

    ReplyDelete
  18. Mnaochukia kwanini jina linatumika kwenye hiyo tan saloon sielewi ni kwanini?

    Kwa upande wangu mimi nampongeza huyo kwa kuzidi kulitangaza jina letu.

    Ni sehemu ngapi Manhataan zinaitwa Tonga nani anajua kuna nchi inaitwa hivyo. Hata mimi nilikua sijui mpaka nikaelezwa. Na jinsi walivyoweka hotel zao na saloon zao utatamani kwenda ukaione hiyo nchi. Na jinsi inavyopata watalii mojawapo ni jinsi watu wanavyoona kunavyoliwaza na watu wanataka kwenda kuona the real thing huko.

    Sasa mimi naona ni muhimu kuwafagilia watu wanao kubali hata kulitumia jina letu. Wanaliadvertise kwa free

    Kuna Ireland hotel, Ethiopian restaurant, Tonga saloon, tonga bar, tonga restaurant, Kenya Coffee house etc...

    ReplyDelete
  19. michuzi kwa taarifa yako hilo gazeti lililoandika hizo habari THE ONION ni gazeti la udaku so is just a bunch of bu.......!?

    ReplyDelete
  20. HIYO HABARI IMEANDIKWA TU..LAKINI UKWELI NI KWAMBA TULISHAUZWA KIUCHUMI NA HUWEZI AMINI KUNAWATU HAWAJUI MPAKA LEO.. KWASABABU BORA MKONO UENDE KINYWANI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...