haya tena, ni kipindi cha lala salama kwenye jumba la big brother africa II ambapo kwa mara ingine tena bongo inawakilishwa kwenye hatua hii ya fainali na kijana richard na utaratibu wa kupiga kura umeanza rasmi leo wa kuchagua mshindi wa dola 100,000 kwa siku saba zijazo.

shime wadau na tumpe tafu richard kwa kumpigia kura kwa wingi ili ashinde nasi tujidai. ni rahisi sana kupiga kura. we nenda tu http://www.mnetafrica.com/bigbrother/vote.asp na fanya vitu vyako. haya tena wadau, umoja ni nguvu na wenzetu wanalijua hilo na wanalitekeleza kwa vitendo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. sawa baba kura tapata ila tatizo ni kuwa kura zahesabiwa ki nchi, yaani kama wote tutapiga kura toka Tanzania itahesabiwa tu kuwa Tanzannia wamemchagua Richard, nafikiri tupige kura kama tunatoka nchi nyingine pia, kama ukipiga kwa internet ni rahisi tu kuchagua nchi unayoitaka. au nimekosea wadau mnisidie.
    Jirani wa Richard!!! LoL

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli sina shaka na watanzania pale mambo yanavokuwa tyt na serious! haya shime jamani. Hii 100,000$ inaleta favourable balance kwenye uchumi wetu! wewe na mimi in a way ambayo huwezi ku-trace directly, tutafaidika tu.

    Jamani hasa wale tulioko nchi za ki-Africa,tafadhalini sana tuoneshe ushirikiano.Mimi niko Zambia,namtoa kijana kutokea ZAmbia.

    ReplyDelete
  3. kumtendea haki mke wa Richard na maadili ya kibantu ni asishinde ili arudi kwa mke wake waanze maisha mapya ila kama tunataka amuache na aendeleze mapenzi na Tatiana basi itabidi tujitahidi aishinde kwa kumpigia kura nyingi Wantanzania wote walionje pia wampigie kama wanarepresent nchi hizo ili ashinde

    ReplyDelete
  4. Kaka Michu, mbona waibania comment yangu?? We haya weeeee!

    ReplyDelete
  5. Wewe Ano 10:06.
    Utabiri wako siyo sahihi:
    Kama Richard atashinda na akapata hilo fungu, amini usiamini mkewe atarudi na wataendelea vizuri.Kinyume cha hapo atakuwa ameliwa!!!!

    Kwa hiyo watanzania tulioko nje tunusuru ndoa ya Rick kwa kumpigia Richard Kura ashinde tafadhali!

    In fact these are the things that brings a name to a country, it doesnt matter ameharibu au amejenga, but our contry becomes a talk to many other african Countries.

    A vote from DRC guaranteed.

    ReplyDelete
  6. WAJAMENI!
    NIMEINGIA KWENYE BLOG YA WANAIGERIA (http://www.nairaland.com/nigeria/topic-49369.1632.html)YAANI HUKO NI HARAMBEE HASWA! UTASHANGAA OFUNEKA ANABEBA KITU HIVIHIVI TUKILAZA DAMU! TUACHENI UTANI BAJAMENI! TUPIGENI KURA BANA

    ReplyDelete
  7. Na Manigeria yalivyo matapeli utashangaa na michuzi kampigia kura ofuneka , jamani hata blogu nyingine tafadhali michuzi washawishi watu wapkapige kura kama walivyo jitokeza siku ya kutesti uwanja wa taifa mpya tumpgigie kura richard wetu. mmoja wenu arudie tena jinsi ya kupiga kura tafadhali. michuzi fanya kampeni humu ndani ktukumbusha kupiga kila siku

    ReplyDelete
  8. habari zetu watanzania wenzangu.
    najua na kuamini watanzania tumesambaa africa nzima kama sio dunia nzima umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Shime shime tupige kura kijana wetu arudi na pesa TZ. Hata kama hakuna ataezifaidid directly lakini ni wazi kabisa tutafaidika indirectly: mfano; anaweza kuinvest hapa kwetu watu kibao wakapata ajira, hata akienda bar kunywa bado ataingiza revenue ya nchi yetu, akijenga nyumba mafundi ujenzi watapata ajira, house girl, mlinzi wote hawa watapata ajira, najua wenzangu mliosoma uchumi mnajua hii cycle inaendaje na itatunufaishaje sote direct or indirectly, shime shime tupige kura.
    na kama anony wa hapo juu alichosema mwisho wa siku ni tanzania ndo itapata jina kwahiyo kila mmoja wetu popote alipo atafeel proud! pia tumsamehe kuhusu mahusiano yake na tatiana, labda asingefanya kama anavyofanya asingefika hapo alipofika...finally.. so it is a party of the game.Piga kura pliiiiiiiz. mimi nimeshapiga, wewe je?

    ReplyDelete
  9. Jamani tupigeni kura ya kuwarudisha baba zetu na kaka zetu pamoja na akina mama zetu na dada zetu kazini baada ya kutimuliwa na Barrick. Na kwa kufanya hivyo jina la nchi yetu litajulikana.

    ReplyDelete
  10. mimi ni mtanzania kabisaa, ila richard sitaki ashinde, sijaipenda tabia yake kabisa, na naamini he has a price to pay kwa alichomfanyia mkewe, naomba asishinde na akirudi huku aishie kama nanihii!

    ReplyDelete
  11. ee bwana michu mbona najaribu kuingia kwenye web ya mnet ili nimpigie kamanda wetu kura lakini inabana kichizi wanasema sijui the information you put is not complete.
    wadau nisaidieni, mimi nimeweka e mail adress yangu na password yangu ya hiyo mail adress yangu ya yahoo, halafu nimekubali maagreement yao, is there anything i am doing wrong or may be something i can do to do my vote?pliz offer a help IT hand!PJ

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...