jengo la yatakayokuwa makao makuu mapya ya jeshi la magereza lilo mtaa wa shaaban robert/sokoine drive karibu na ifm linakaribia kwisha kukarabatiwa na wenyewe kuingia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Michuzi hebu waambie hao wataalamu wa sirikali waache uvivu wa kufikiri.
    Hivi tuongee mara ngapi kuwa kujaza majengo yote muhimu katikati ya jiji kunaongeza msongamano wa watu na magari? Hivi hawa ni 'planners' wa namna gani ambao wana fikra duni za namna hii? Jengo hili na mengine yote mapya yaliyo katikati ya jiji ambayo huhudumia maelfu ya watu kwa siku yalitakiwa kuwa nje ya jiji kama vile Bunju, Boko, Bagamoyo, Kibamba, Kibaha, Chanika na Pugu, ili kupunguza msongamano katikati ya jiji.
    Ndio hiki kinachowafanya wawe wazito hata kuhamia Dodoma?
    Aaargh! Tushachoka kufundisha sasa!
    Wanatukanisha taaluma zao hawa.

    ReplyDelete
  2. yaani kuna sababu gani watu kama magereza kuwa hapo katikati ya mji huku wakihudumia maelfu ya watu kila siku na yale mafoleni yote...city planners wetu ni zerio nimeamini

    ReplyDelete
  3. Anonymous wa Monday, October 29, 2007 5:44:00 PM EAT, asante sana kwa maoni yako kuhusu Jiji la Dar es Salaam.

    Maoni yangu ni tofauti na yako ingawa yanalenga haja ya kupunguza msongamano hapo Jijini. Hii inawezekana kabisa. Mapesa ya kufanya hivyo yapo kwani Tanzania yetu si masikini; ni tajiri. Tunafuja mapesa yetu bure.

    Fikiria, hao mawaziri karibu sitini ni wa nini, kama sio ku-“exercebate the so-characterised” umasikini wetu? Hawa “mawaziri” na “wizara” zao wanamaliza mapesa kwa mishahara ya wafanyakazi, kuwapamba kwa magari ya fahari na majumba, marupurupu, ubadhirifu, ufisadi, na kurudufisha huduma.

    Tulishindana na Benki Kuu ya Dunia, washauri wetu wa uchumi, kututaka tupunguze sekta ya serikali (umma) ambayo ilikuwa imeota kitambi. Tukashauriwa kuipeleka “gym” ikafanye mazoezi ya kukonda; ikakonda! Lakini sasa tumerudia yale yale ya kuota kitambi, tena kikubwa zaidi! Ikiwa kitambi kwa binadamu leo hii ni “skandali”, basi hata kitambi cha serikali nacho ni “skandali”!

    Najua nchi kongwe (kama Uingereza, Ujerumani, Ufaransa) zilikuwa tayari na dola (the state) kabla vyama vya siasa kuanzishwa. Nchi changa (kama Tanzania) zilikuwa ni lazima ziunde vyama vya siasa ili zijenge “the state” ambayo ingejenga nchi. Matokeo ya kuota kitambi hicho yalikuwa ni mafanikio ya kujenga nchi.

    Leo hii eti tunaambiwa mambo yamebadilika. Kuna kuoana baina ya sekta ya serikali na ile ya binafsi. Ndoa hiyo ndio kitovu cha maendeleo ya kujenga nchi….bado tunajenga nchi mpaka leo!

    Kurudia ya Jiji la Dar, tunalipendelea sana jiji hili. Linazidi knawili. Wengine kati yetu wanalifananisha na New York au Shanghai kwa madhari yake. Tuliache Jiji hili lilivyo bila ya kulinyonga. Lakini Jiji la Dar limeshindwa kudhibiti wingi wa magari kwenye barabara zilizotengenezwa wakati wa Gavana akiwa ndiye mwenye gari, na wakati wa kutaka kutoka na gari hilo, barabara zilifungwa.

    Mpaka sasa, serikali imekataa kuhamia Dodoma; inazidi kujenga nyumba za mawaziri na maafisa wa serikali Dar! Nchi imetumia mapesa mengi kwa ajili ya hayo “Makao Makuu Dodoma” toka enzi za “Sir” George Clement Kahama! Na “over cost” yake inazidi kila mwaka, licha ya ufisadi wa wafanyakazi wake kukopa mapesa na kujijengea majumba yao. Hii inajulikana hata kwa TAKUKURU! Tuache kuhamia Dodoma!

    Itatubidi tuunde “our own format of decentralisation”, ambayo ni “home grown” ili kuendeleza baadhi ya miji yetu mingine na kupunguza msongamano wa magari jijini Dar na taabu nyinginezo.

    Lakini tuendeleze miji mingineyo kwa kuhamisha wizara fulani kutoka Dar es Salaam. Kila mwaka tuhamishe kundi moja la wizard. Baada ya miaka kama kumi hivi, Tanzania itakuwa imebadilika sana!

    Niruhusu nifupishe orodha ya wizara zetu ziwe wizara 15 tu. Orodha iwe fupi kama mini-sketi lakini ndefu kiasi cha kusetri huduma za lazima, kama ifuatavyo:

    Dar es Salaam: Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Mipango (Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi); Habari, Utamaduni na Michezo; Nje (Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki); na Ulinzi na JKT.

    Dodoma: Uhusiano wa Ndani (Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge); Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; pamoja na kuwa Makao Makuu ya Vyama vya Siasa ili viwe karibu na Bunge “tukufu”.

    Arusha: Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto); Sheria (Katiba na Utawala Bora); Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa Nairobi na Kenya Kusini.

    Mwanza: Afya na Ustawi wa Jamii, na Mazingira Nishati, Madini na Miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuwa jiji la kuhudumia biashara ya Ziwa Victoria, Rwanda, Uganda, na sehemu za Kenya Magharibi. Mwanza iwe senta ya madini.

    Kigoma: Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa biashara ya Ziwa Tanganyika, na DCR Mashariki, Burundi na hata Rwanda.

    Mtwara: Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko). Mtwara hauna budi kupewa hadhi mpya kama senta ya huduma za mpango wa “Mtwara Corridor” – kwa ajili ya Malawi na Zambia na sehemu za Msumbiji Kasikazini. “Daraja la Umoja” kwenye Mto Ruvuma ili kuunganisha Tanzania na Msumbiji sasa linajengwa baada ya kulisubiri kwa miaka mingi tangu Awamu ya Kwanza – wakati Msumbiji inapata uhuru wake! Mtwara iwe senta ya gesi.

    Mbeya: Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa nchi za Malawi na Zambia. Ni kitu cha kutia shime kuona kuwa uwanja wa ndege wa kimatiafa unaendelea kujengwa mjini Mbeya. Uwanja huu utasaidia pia kuinua maendeleo kwa mikoa ya kusini, ikiwa ni pamoja na kuinua hali ya utalii kwa mikoa hiyo ya kusini.

    Miji hiyo iwe na wizara ambazo nimeziunganisha. Tuwe na Mawaziri Wadogo 15 tu wakisaidiwa na nyongeza ya Makatibu Wakuu, endapo italazimika. Wizara hizi zitagawanya katika mafungu matano.

    Kila fungu la wizara zilizotawanyika lisimamiwe na afisa mwenye sifa za nidhamu na uchapaji kazi (mwenya madaraka makubwa zaidi ya makatibu wakuu) ili kuweza kufuatililia maazimio na miradi mbali mbali ya serikali kulingana na manifesto ya chama tawala (na kudhibitiwa na “chama tawala kivuli” kikisaidiana na vyama vingine vya siasa.

    Naona kumekuwepo na kuteuliwa kwa maafisa wapya wa kumsaidia Waziri Mkuu katika kusimamia mipango ya sera za serikali.

    Hii itasaidia sana kuangalia ni vipi tunavyotekelza yale ya Hotuba Rais aliyotoa alipokifungua Bunge la Awamu ya Nne. Na itawasaidia sana Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuweza kufuatilia, kukagua na kudhibiti miradi na maazimio yaliyowekwa.

    ReplyDelete
  4. Born Again Pargan, mimi anony.. wa kwanza hapo juu!
    Ushauri wako ni wa maana sana, na nauheshimu, ni ushauri wa kitaalamu kabisa, lakini sina uhakika kama hawa vichwa ngumu (watawala) watakuelewa, sana sana watahisi unataka kuwaharibia ulaji wao wa kuwatoa Dar na kuwapeleka mikoani (kusiko na miundombinu na huduma nyingine bora).
    Wasomi wa Tanzania tunakuwa 'underutilized' mno, hatupewi kazi za taaluma zetu kama hizi, badala yake tunafanya kazi nyingine tu ilimradi maisha yaende. Tukuchukuliwa na wanaotuhitaji nje ya nchi, serikali inapiga kelele kuwa wataalamu wake wanatoroshwa, yaani 'Brain Drain', sasa kama hatutumiki ama hatutumiwi ipasavyo kwa nini tusiende pale tunapohitajika?
    CDA (Capital Development Authority)ulikuwa ni mpango mzuri sana, sema shida ilikuwa ni watekelezaji, wanataka wafanye mambo kwa pupa, hili HALIWEKANI!
    Decentralization uliyoongelea hapo juu ni muafaka sana, sema shida sasa hatuna utashi wa kisiasa kutekeleza dhana hiyo. Pesa pamoja na rasilimali nyingine (ikiwemo rasilimali watu) zipo, je tuna utashi wa kisiasa (political will)?
    Shida iko hapo tu!
    Ndio hapa ambapo siasa na utendaji vinapoachana!
    Tuendelee kuelimishana.
    mheshimiwa_2000(at)yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...