BAADA YA KUTANGAZA ZAWADI YA $500 KWA MDAU ATAKAYEBAHATIKA KUWA MGENI WA MILIONI 2 KWENYE GLOBU HII, NIMEKUWA NAPATA MASWALI NA PIA MAWAZO KIBAO YA NAMNA YA KUMPATA HUYO MSHINDI IKIZINGATIWA KWAMBA WENGI WA WADAU HUJA KAMA MAANONI. NAFUNGUA MJADALA KUOMBA MSAADA WA KUJUA KIFANYIKE NINI ILI HAKI ITENDEKE. NAANZA KWA KUTUNDIKA WAZO LA MDAU HUYU CHINI:
Michuzi,
Sisi wanalibeneke, tuna maswali mawili matatu ya kukuuliza..
Je ni vipi utajua huyu mtu ni wa milioni 2 ? Kama utatumia ip address ambazo ziko logged on your Visitors counter, utakua wrong, kwa sababu watu wengi wanatumia internet cafe, na wadau wa bongo utawakosesha hili shindano, wengi hawana computer majumbani mwao, wadau wengie wanatumia proxy server, au hali kadhalika wengine wanatumia computer za makazini.. Je ni vipi utajua hilo. Na hata hivyo that remain IP address, ni vipi utahakikisha mwenye hiyo ip address ndio huyo ambaye anasema ndie..Fikiri juu ya hili Michuzi.

Shauri.Mimi nakushauri make it like a lottery syndicate, watu wasubmit email zao kupitia kwako, when the counter hits 1999999.. kwa muda wa siku 3 kutoka hapo...

And then you select them randomly using a probably special software. wadau mutamsaidia juu ya hili, Je software gani inaweza kutumika kwa hilo, lazima itakuwepo tu.

Halafu zawadi iwe 250Us dollar kwa mshindi wa kwanza, 150US dollar kwa mshindi wa pili na 100Us dollar kwa mshindi wa tatu.

Mimi mchango wangu kama nikishinda, nitawapatia Childrens ward muhimbili.

By Mchangiaji,
mmchangiaji@yahoo.com

Huo ni ushauri tu, wengi wa wadau watakua na mengi ya kuchangia,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Heeee-Heeee... ni hatari pale langoni mwa Issa Michuzi dakika ya 89 inaelekea dakika ya 90.

    Bwana Mchangiaji anapiga shuti kali lakini anapangua pale goal kipa Issa Michuzi, inakuwa ni kona.

    Naona wachezaji wote wanasogea golini kujaribu bahati yao katika dakika hii ya mwisho iliyosalia ...

    Kwa niaba ya Radio "somaulaya at gmail dot com" ni mtangazaji wako hapa naitwa Mnyatiaji wa Dola 500. Namkabidhi mwenzangu Anon aweze kumalizia ka-ngwe haka kalikosalia.

    Anon endelea ...

    ReplyDelete
  2. Ndugu Mchangiaji wazo ni zuri lakini kuna njia bora zaidi ya kumpata mshindi bila kutumia bahati nasibu.

    Pili bwana Issa hana kibali cha kuchezesha bahati nasibu kwa hiyo asije akaingia matatani bure.

    === Njia yenyewe ni hii ==

    1. Issa ongea na aliyekutengenezea hii blog aweke ka-application ka kugenerate random numbers pale chini kando kidogo au juu kidogo ya counter. (anaweza kutumia hata turing generator, ila hiyo namwachia yeye kwa kuwa ni mtaalamu wa IT)

    2. Hako kaapplication akaunganishe na counter kiasi kwamba kwa kila namba inayofikiwa na counter kuna corresponding random number inakuwa generated na inahifadhiwa katika log za hii website au hata kwenye kadatabase fulani hivi.

    3. Hii random namba itakuwa pia inaonekana kwetu sisi wasomaji.

    4. Kwa hiyo mtu atakayefungua hii blog na kukuta counter inasoma 2,000,000 achukue screen shot akutumie kwenye e-mail, au kama hawezi basi akutumie tu e-mail kukwambia kuwa yeye ndio mtu wa 2,000,000 na random namba aliyoikuta siku hiyo ni fulani.

    5. Then wewe unacheki kwa database yako kuthibitisha.

    6. In fact ili kuondoa mashaka yoyote unaweza ukaipublish hiyo log au database ya random numbers kwenye mtandao in real time. Yaani kila inapoupdate na sisi tunaweza kuona. Kupublish unaweza kuinsert ka-java application kwenye hiyo nafasi ya blue kwenye blog hii.

    Hitimisho,

    Kwa njia hii atapatikana mshindi mmoja tu wa halali. Hakuna mtu anayeweza kubahatisha random numbers.

    Kwa kasi ninayoiona sasa zimebaki siku 3 - 4 kufikia 2,000,000 kwa hiyo mwambie mtaalamu wako wa IT achangamke. Kuna script kibao tu anaweza kurekebisha hapa na pale.

    Ni mimi mdau wako dar.millionaire@gmail.com

    ReplyDelete
  3. Wazo langu:
    Mtu wa Milioni mbili anaweza kui"save" page kwenye computer na kumtumia Michuzi kwa Email as an Attachment na Michuzi akiifungua ataweza kuona kwamba huyo mtu ni wa Millioni 2...hilo ni wazi langu na nimefanya experiment na imekubali, nadhani hilo linaweza kufanikisha na mshindi atapata $500 bila kugawa....Asante

    ReplyDelete
  4. Hmm,I agree that IP addresses can indeed cause confusion...The main problem here is anonymity,'cause anyone can claim they're someone else and vice versa...

    I wouldn't advise you to use any sort of 3rd party software in picking the winner,I mean let's face it:Anything that's computer generated can be manipulated by anyone,including lottery type programs.

    With that said,here's my proposal:

    Since all competitions be it online or off-line have respective terms and conditions,I believe that there have to be some conditions present in order to have the right winner,and these could be such as:

    1)Frequent visitor of the blog(You can check this through your visitor log).

    2)Have a blogger account(Creating a blogger account is free so no one should complain about this lol)

    3)Have an active Email account with either MSN,Yahoo,or Google(You can verify a person's IP through their email,so this provides an extra measure of security)

    4)Be ready to answer a general question about Tanzania,e.g Who's the current President of TZ?(This eliminates the possibility of a Bot-That is,a computer and not an actual person-winning the money).

    Now,with all this said ^,the proper way of deciding a winner would be through the Comments feature on the blog,basically:You put up a post once the ticker hits 2 million,people comment on the post leaving nothing but their emails and or blogger id,and then you randomly pick a winner from the email addresses left on the post.

    In my opinion where the money goes is up to the person who wins it,i.e they can use it/donate it as they wish,and I also think that the persons choice shouldn't be made public until they have won the cash ;)

    ReplyDelete
  5. Candy,

    Wazo lako ni rahisi kutekeleza lakini sio salama kabisa. Unaposave hiyo website, counter inahifadhiwa tofauti kama picture. Kwa hiyo mtu anaweza kuirekebisha kirahisi tu ikasoma 2,000,000 kwa kutumia Photoshop au hata Painter.

    Nimelipenda wazo la bwana dar.millionaire (anon wa pili hapo juu). Hilo naona halitakuwa na nafasi kwa msomaji yoyote kufanya utapeli. Labda designer wa michuzi ashindwe mwenyewe kufanya huo utaalamu.

    ReplyDelete
  6. Naona milioni mbili itawafanya watu waweke camp kwenye blog ya michuzi.

    Mbona mi naona ni simple kama huna camera basi save the screen
    copy the screen na email kwa michuzi basi unajulikana ni wewe. sasa mambo ya IP yanatoka wapi?

    Wewe kama unafuatilia ushindi kila ukilog in check wewe ni wangapi ...if you are luck copy the screen email it to him......

    ReplyDelete
  7. Hamna cha kuchangisha lottery wala nini mshindi ni big 2 million that is it...mwenyewe michuzi kashasema watu wengine mnaongezea nini?

    Na ujue kuna watu wengine hawataki kujulikana humu kwenye blog...sasa kama michuzi angesema mshindi ni lazima kutanganzwa au..??

    Kwanza mimi nikishinda....I know I will nitamwambia michuzi hiyo hela amlipie school tuition mwanafunzi mmja humo bongo.....

    ReplyDelete
  8. nyie mambo ya IP ya nini ...Mimi natumia wireless internet...kwenye simu IP yangu inachange kila sekunde. Nikimove from ne building to another ni different ip. ssa hapo si kuwafanya wengine wasishinde.
    na mambo y akusema sijui fungua uwe member wengine hawataki kujulikana humu...

    Muachieni michuzi mwenye kumtumia screen sht ndio huyo mshindi....

    ReplyDelete
  9. Wadau ni kweli wengi tunapenda u-Anon ila kuchukua screen shot na kutuma kwa michuzi ni uzushi kwa sababu unaweza ukaiedit kabla ya kutuma.

    Kwa hiyo solution ambayo mpaka sasa naona imetulia ni ya mdau anon wa pili toka juu. Hiyo kama itatekelezwa itaondoa mawaa, na asiyetaka kujulikana hatajulikana pia. Lakini kwa ustaarabu atakayeshinda ni vema atambulishwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...