ngekewa ya mdau wetu richard bado inamsaidia kubakia ndani ya jumba la big brother ambapo usiku huu kwa mara ya tano mfululizo kapona kuenguliwa na code wa malawi ambaye ndiyo mwanzo kuwekwa kwenye mkao wa kutoka kupigwa chini. kila mtu anaamini kwamba richard ndiye stelingi wa bba mwaka huu na kwa vile stelingi hauwawi huenda akalamba dume. wengi wana imani kwamba akitoka richard utamu wa jumba hilo utakufa kabisa....
habari kamili za kutolewa nishai kwa code bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Phew man that was close. Richard wewe ni kama Paka una maisha mengi manaake kila wiki unachaguliwa kuenguliwa lakini watazamaji tunakupenda sana tunakulinda.

    == OMBI KWA WABONGO ==

    WATANZANIA WENZANGU MIMI SIO MSHABIKI SAANA WA BIG BROTHER LAKINI NI MSHABIKI SANA WA USHINDANI.

    NAOMBA HILI GAME LA BIG BROTHER TULICHUKULIE KAMA MASHINDANO YOYOTE YALE. UKIPATA MUDA WA KUPITIA ONLINE FORUM YA WAPENZI WA BIG BROTHER (link ni: http://www.mnet.co.za/profiles/bba/ForumListing.aspx halafu select "Housemates") UTAGUNDUA KUWA RICHARD ANAREPRESENT TANZANIA KWA KIWANGO CHA JUU. YAANI AMEKUWA GUMZO AFRIKA NZIMA, NA TISHIO KWA NCHI NYINGI ZENYE WASHIRIKI WALIOSALIA (HUSUSANI NIGERIA)

    KWA UFUPI NI KWAMBA RICHARD AMEONESHA CHARACTER INAYOVUTIA NDIO MAANA AMEFIKA HAPA ALIPO. SASA HIVI WANAIJERIA WANAOGOPA KUWA MSHIRIKI WAO ATAPIGWA CHINI MANAAKE RICHARD AMEKUWA TISHIO FULANI KWA HIYO WAMEANZISHA MAJUNGU KUWA TABIA YA RICHARD INAHATARISHA NDOA YAKE NA UPUUZI MWINGINE TU (AS IF THEY REALLY CARE, KUMBE NI GAME PLAN TU)

    KWA HIYO NAOMBE MUINGIE PALE KWENYE FORUM MUWAJIBU WANAIJERIA WAACHE KUMSAKAMA MTU WETU.

    AKISHINDA ITALETA SIFA KUBWA SANA KWA TANZANIA. HAYA MAPUNGUFU YAKE YOTE HAYATAKUMBUKWA BALI ATAKUMBUKWA KAMA MSHINDI WA BIG BROTHER 2007.

    AFTER ALL, HISTORY REMEMBERSLY KINGS ONLY KINGS (WINNERS) ...

    ReplyDelete
  2. duuuuuh jamaa una akili saaaaana tena saaana yaani una akili za kuzaliwa sio wengine wakina sie mpaka tukariri. sasa subiri nikuunge mkono kweli yako kabisa kama tukiwa na umoja na huyo kijana akashinda sifa ni kwa taifa letu na sio kitu kingine.mara ohh mke wake mara ohh Salama Jabir kapiga siku hiyo kwenye mahojiano eti anakunywa pombe sana kwani anakunywa peke yake? kwani ni yeye peke yake amabaye yuko commited jamani huo ni mchezo tuuuu na una mwisho wake.cha msingi mimi naona kijana ananifurahisha saana ndani ya nyumba na bila yeye siangaliii tena nitakuja kusikia mshindi na kama mithupu ukikumbuka kumuweka mshindi.mimi niko huku ukerewe lakini darasani kutwa nzima wanafunzi wenzangu wasiojua kitu chochote kuhusu africa wanashabikia big brother kisa mie niliwaambia kuhusu kijana wetu. jamani tuwe na umoja na tumpesupport.

    ReplyDelete
  3. na kweli kaka michuu hii ni ngekewaa ni mshindi huyu hilo halina mjadala...tuzidi kumpigia kura

    ReplyDelete
  4. Mpinzani mkubwa wa richard ni ofunneka Tatiana na maureen hakuna kitu. Na possibility safari hii richard akapona ni kwamba tatiana hawezi kumvote out, same as ofunneka unless aamue kumtoa but hat richard na maureen wakibakia richard hawezi kutoka.Katika wote ni yeye peke yake aliyekuwa mkweli na sio manfiki tangu mwanzo.Jamani tumpigieni kura kwa nguvu zote angalau basi apate kitita kama mai nanihii ndio amesha nanihii(naogopa michu atanibania)

    ReplyDelete
  5. NAFURAHI KUONA MWITIKIO MZURI.

    SASA STRATEGY NI HII. WATANZANIA TUMPIGIE KURA OFFUNEKA. MAUREEN SIO TISHIO KWA RICHARD KWA HIYO HAKUNA HAJA YA KUMTOA KWA SASA.

    TUFANYE JAMBO MOJA. KURA KWA OFFUNEKA. THEN MWENYE MUDA AINGIE KWA FORUM AMTETEE MAUREEN. JISAJILI KWA JINA LA NCHI NYINGINE LAKINI SIO UGANDA, AU TANZANIA AU NIGERIA. WANAIJERIA HAWAMPENDI RICHARD, WANAMUOGOPA, ILA KWA SASA WALIOKO KWENYE KITANZI NI OFFUNEKA NA MAUREEN. KWA HIYO WABONGO TUMPIGIE KURA OFFUNEKA ATOKE. WAGANDA NAO WATAFANYA HIVYO KUMSAIDIA MAUREEN. OFFUNEKA ANA SUPPORT KUBWA LAKINI KAMA UNA MUDA NAOMBA UWE UNAPOST MESEJI KWENYE FORUM KUMFAGILIA MAUREEN NA KUMPONDA OFFUNEKA. KUNA WATU WENGI HAWAMFAGILII OFFUNEKA ILA TATIZO FORUM IMEJAA WANAIJERIA WENGI KWA HIYO WANAMPAMBA SANA MTU WAO.

    OFFUNEKA AKITOKA BASI RICH ATAKUWA AMESHINDA. OTHERWISE ITAKUWA KIMBEMBE NEXT WEEK.

    KWA MIJADALA YA STRATEGY TUENDELEE KUKUTANA HAPA KWENYE HII THREAD YA MICHUZI. HAKIKISHA UNASOMA DISCUSSION ZA WADAU KWENYE FORUM YA BIGBROTHER MARA KWA MARA.

    PIA KWA WALE WENYE DSTV TUMENI SMS KIBAO TU ZA KUMFAGILIA MAUREEN, NA KUMPONDA OFFUNEKA.

    ReplyDelete
  6. ukishinda unapewa gari ya dube ila angalia usalama usije na wewe ukaua kabla haujavuka nchi.

    ReplyDelete
  7. jamani kwa atakayepata mda wa kumvote mtu out tafadhali mtoeni offuneka.

    ReplyDelete
  8. Jamani utabiri wangu hapo jana mmeuona lakini??? Richard hayuko kwenye eviction wiki ijayo sasa ni kuomba mungu na kumpigia kura ashinde maana hata wale panya watakao ingizwa wiki hii hawata mdhuru yuko stable kijana hawezi kuleta mchezo dakika za mwisho akitoka ofuneka wiki hii basi mchuzi(sio michuzi) unaenda kwa richard mind you wanigeria wako wengi sana watapiga kura mpaka wafe michu piga kampeni basi angalau mwaka huu wabongo tuwe kwenye ramani kwa sana. waosha vinywa vinywa vyenu vita haribu bahati ya kijana wetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...