MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo, litakalofunguliwa kesho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Mh. Kijakazi Mtengwa amesema kuwa Dkt. Shein amekubali kushiriki ufunguzi wa Tamasha hilo la 26 ambalo hufanyika kila mwaka mjini Bagamoyo na kuratibiwa na Tassisi ya Sanaa na Utamaduni ya Bagamoyo (TaSuBa) zamani Chuo cha Sanaa.
“Tamasha litafunguliwa Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt Shein, ambapo pamoja na mambo mengine atakagua maonesho ya sanaa za ufundi na pia kukagua ujenzi wa ukumbi mpya wa kisasa wa maonyesho unaojengwa Chuoni hapo,” alisema.
Amesema katika miaka 25 tamasha hilo limekuwa tukio muhimu la sanaa na Utamaduni hapa nchini ambapo limewezesha mkusanyiko mkubwa kila mwaka kwa wasanii na watazamaji kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“Hadi kufikia mwaka jana tamasha hili lilikuwa limeshirikisha vikundi 555 vya hapa nchini na 101 vya nje ya nchi. Tamasha la mwaka huu litashirikisha vikundi 45 vya ndani na nje ya nchi, vikundi kutoka nje ya nchi vitatoka nchi za Uholanzi, Japan na Italia,” alisema Mh. Kijakazi.
Amesema Tamasha la Mwaka huu litakuwa na kaulimbi isemayo Sanaa katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini ambapo litakuwa la aina yake kutokana na kuwa mbali na maonyesho ya sanaa za Jukwaani na za ufundi pia kutakuwa na michezo ya jadi kama vile Bao, Mieleka, kukimbia kwenye gunia, mashindano ya Ngalawa, warasha, makongamano na filamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mungu wangu kwa mara ya nne sijui kama sio ya tano richard kabaki ndani ya nyumba tena. jamani nina furaha kama vile mie ndie mmoja wa familia ya richard.mungu ibariki tanzania.

    ReplyDelete
  2. Mwaka huu jirani zetu hawapo mwaka huu? Nakumbuka 2006 waganda walikuja na ngoma ya ankole ilikua bomba. Tamasha lile ni zuri sana ila cha ajabu halijapata hadhi yake inayostahili. Labda kwa Tanzania halijapewa promosheni ya kutosha. Nahisi hata wadhamini wa kibiashara halina,sijui labda ni sera ya waandaaji. Kaka michuzi najua utajitolea kutupa taarifa zaidi kuhusu yatakayojili huko ila naomba uniulizie kwa waandaaji ni kwanini kitu kizuri kama kile hakipati mwitikio unaostahili. Natamani siku moja Bagamoyo ijae ifurike ili wananchi waishio jirani na eneo lile wanufaike zaidi na tamasha lile. Shime wadau mjitokeze kushuhudia urithi wetu wa sanaa. Sio kila siku buzuki,bongo fleva,taarabu. Tuelekee na huku.Tamasha letu liwe kama carribean carnival za london na matamasha mengine duniani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...