wadau kunradhi. eti mtu kuomba chumvi usiku ni mwiko?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Heheeeelo!!! michuzi bwana, mbn unajifanya km vile co mtoto wa uswahilini?!!! Ni ukweli mtupu (sina uhakika) ukisema chumvi ucku hupewi...ni imani tu!! sema NAOMBA DAWA YA MBOGA!!!

    ReplyDelete
  2. sio vibaya sema imetumika hili hiweze kukomesha kuomba omba vitu vidogo kama hivyo.tunatakiwa kununua vitu vya kutosha hili kukizi mahitaji yetu.nadhani niivyo labda mtu mwingine ana wazo zaidi.hii nachukulia tu kama kupiga mluzi usiku vibaya hahaha.

    ReplyDelete
  3. .. Ni mwiko wa kupikia nini?

    ReplyDelete
  4. Sheeee!! Mishusi sasa mesidisha hii shokosi, hifi we bila kuona watu nasungumusa sana kune hii bulok hufurahi. unashokosa tu wadau usikie file nasema sasa mi naambia wewe kwetu naomba chumfi saa yoyote, hapana nyima hii mambo ya ushoyo kwetu hamna kabisa. mesikia ambia na hiyo mutu ingine. Sheee! we nasemasema tu, mi hapana taka sikia tena

    ReplyDelete
  5. kuomba hata mchana ni mwiko huku tuliko... hamna kuomba nunua huna kula chukuchuku ili upate akili ya kutafuta kesho ya kwako...

    ReplyDelete
  6. kama kuomba ni mwiko,mbona nchi yetu ina mazoezi makali kupokea hiyo misaada, zakaa na fitra kutoka popote hivyo?wahenga wa benki ya dunia hawajatupachikia jina la 'one of the poorest country in the world'bila sababu!!!kweli sisi matajiri wa maneno tuu bali masikini wa kila kitu kingine...naam

    ReplyDelete
  7. Hapana, sio mwiko ni KIJIKO.

    Utajiju.

    ReplyDelete
  8. Nini kuomba chumvi usiku, hata mchana mwiko hasa maeneo ya Masaki, Osterbay, Upanga na uzunguni kwingine kwenye tabia za kizungu.

    Lakini uswahilini sema naomba dawa ya jiko, utapewa tena kwa shingo upande.

    Nafikiri kama mdau mmoja alivyosema hapo juu ni kupunguza kuomba omba kwa watu hasa usiku maana pengine mwenye nyumba kajirudia mapema anataka kupumzika nyie 'hodi, naomba chumvi!' sasa wazee wazamani walikuwa na busara waliweka miiko. Kwanini isiwe vibaya mchana.

    He lakini hata dukani ukienda kununua chumvi usiku ukamwambia mwenye duka nipe chumvi hakupi nakumbuka nilipokuwa mdogo mwenye duka alinitoa baru! Toka tokaa!!Tena basi ilikuwa kama saa moja hivi usiku. Nikarudi nyumbani natetemeka sikujua kosa langu, mamangu alijua tu nishalikoroga nimesema chumvi dukani ilibidi aende mwenyewe. Hapo ndipo nilipojifunza somo la kutoita chumvi 'chumvi' wakati wa usiku.

    Miiko mingine bwana! halafu wala hawakwambii maana yake!!

    ReplyDelete
  9. yaani wewe anon 29 nov 11:53 p
    umenifurahisha sana loh !!
    umenikumbusha kwetu nyumbani umasaini Arusha
    Love that town
    Home sweet home

    mdau nje ya nchi

    ReplyDelete
  10. Mkuu unazungumzia chumvi gani?

    ReplyDelete
  11. kaka Michuzi kuomba chumvi usiku si mwisko bali maneno unayotumia kuomba chumvi hiyo.Manake kuna kajiimani kazuri tu kanakohusisha lugha isiyoeleweka na madude ya ajabu kama majini nakadhalika.Inaaminika chumvi ina kazi nyingi sana hasa katika ulimwengu wa majini kwa hiyo hakuna mwanadamu anataka kusaidia uharabafu au unyamabaf wa majini hayo na wachawi wao lakini kama unahitaji kufanyia kazi halali ya jikoni basi utasema unaomba dawa ya jiko au dawa ya mboga na utapatiwa jini usiku au mchawi hawezi kusema dawa ya mboga atasema chumvi tu kwani ndivyo inavyostahili kuitwa kwa shughuli zao upo hapoooooo. La msingi wazee wa zamani walikuwa wanajua namna ya kubana mambo bila kutika hofu!!!!

    ReplyDelete
  12. Ni mwiko kaka michu inapandisha sodium mwilini,unaweza kupata heart failure.Kwahiyo ni mwiko kama hukula chumvi mchana basi usiku pumzika.Na iwe mwiko kabisa usumbufu sana na uzembe kuomba chumvi usiku.

    ReplyDelete
  13. uswazi hupewi ukisema unaomba chumvi, na pia ukienda hata dukani ukasema nataka sindano ya kushonea wanakunyima wanasehema hakuna kumbe ipo ila usiku hawauzi, pia ukiomba chenchi usiku upewi mara nyingine hata mchana wanaogopa chuma ulete yaani uswahi kazii kwelikweli

    ReplyDelete
  14. hii imenikumbusha chumvi chumvi , chumvi chumvi tutalamba ! dooooh by chuchu sounds

    ReplyDelete
  15. tumia jivu, ni sawa na chumvi, badala ya kusumbua watu na njaa zako usiku, ulikuwa wapi siku nzima!!!!

    ReplyDelete
  16. ISSA UNATUCHANGANYA CHUMVI YA KUOMBA "..USIKU.." UNAYO ZUNGUMZIA WEYE NI IPI..KUMRADHI

    ReplyDelete
  17. Duh, Anon 12:35 PM umedata. We kwani unaelewa chumzi zipi kama sio ipi na ipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...