Dully Sykes kaingia Holland kwa vishindo leo asubuhi tayari kwa show itakayo fanyika Delft ijumaa 30/11/2007 na kaahidi kufanya maajabu huku akitamba na kibao chake kipya BABY CANDY.
Pichani ni wakati Mr. Misifa alipowasili Amsterdam Airport (Schiphol) akiwa na Promoter wake Charles Gadi kushoto pamoja na Pascal na Bachalla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Haya promota fanya kazi, exposure ni muhimu kwa kijana. Sio kuimba kwenye klabu tuu, vyombo vya habari wanamhitaji pia!

    ReplyDelete
  2. jamani hicho kibao cha baby candy naweza kukisikiliza wapi?

    ReplyDelete
  3. Kweli mr misifa ana aibu du tabu tupu

    ReplyDelete
  4. E BWANA HII IMETULIA BABAAKE.
    FAGILIA FAGILIA MISSIFFAZZZ CAMP !!

    ReplyDelete
  5. Oyaah! Dogo acha utozi na baridi la ulaya. Wee acha kifua wazi uone kama shoo utaipiga na winter hili utaishia kukohoa badala ya kuimba.

    ReplyDelete
  6. karibu sana holland, ila usilete ziile za wenzako waliopita. zingatia muda na kuwapa watu vitu vya maana. unaweza kubadilisha watu ambao bado wanapinga mtu mmoja mmoja. ambao wanataka makundi. mie nitatia timu ila usinilet down.

    ReplyDelete
  7. kibao cha baby candy unaweza kukisikiliza kwenye site ya darhotwire, ingia kwenye bongomdundo utaukuta huko....

    ReplyDelete
  8. Anon ingia www.swahiliremix.com , unaweza kusikiliza na kuangalia nyimbo ya Baby Candy

    ReplyDelete
  9. wenyeji wa holland mtafutieni kibarua cha mabox huko ikea,dhl nk.Au anaweza kujiunga na waghana kusafisha hotel za amsterdam maana waghana kibao wamejaa kwenye hizo hotel hasa za karibu na schiphol

    ReplyDelete
  10. Karibu sana ndugu yetu Dully.
    Kwa mujibu wa utamaduni wa Wadachi na hata Watanzania basi tunakusisitizia kuwa hapa ujali muda, ufanye kweli na usubiri watu ndo wakusifu. Hapa hilo jina la Mr. Misifa lina negative impact kwako na kwa kampuni yako na kwa Promota wako na kwa yeyote anayekufagilia kwa jina hilo lenye utata!
    Usikonde, Familia nzima tutatinga ndani siku hiyo ya Ijumaa.
    Ili usipate usumbufu wa namna ya kuvaa siku hiyo (ingawa ndani kutakuwa na joto la kutosha) hapa chini nakupa utabiri wa kuaminika wa hali ya hewa wa siku ya IJUMAA katika mji wa DELFT utakapokuwa unaturushia nyuki na asali:
    JOTO (Sentigredi): Juu- Nyuzi 11, Chini-nyuzi 8;
    UPEPO: 46km SSW;
    MVUA: Kutakuwa na manyunyu ya hapa na pale.
    Mdau,
    Nyakarungu

    ReplyDelete
  11. yaani wewe uliyoweka hiyo link ya huo mziki hapo juu nakushukuru sana
    wengine tulikua hatujawahi kuuona wala kuusikia
    wimbo ni mzuri sana lakini kuusikiliza tu.
    lakini hiyo video siifagilii wala nini
    yaani haya mambo ya kuiga wamarekani yamezidi sana mpaka yanatia kichefuchefu
    sisi tulio nje hatutaki kuona hizo, tunaziona nzuri zaidi ya hizo.
    halafu mtu kama hauko fit, why are you taking your shirt off? huna six pack bora ujivalie zako shati lako la mikono mirefu
    lakini wimbo ni mzuri sana lazima tumpe credit kwa hilo.

    ReplyDelete
  12. BACHALA NINAKUTAFUTA MPENZI!!! NIANDIKIE KWENYE mtamumie@yahoo.co.uk
    PLEEEEEEEEEASE!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...