24/11/1971: edda williams ngulukulu a.k.a edda sanga akiwa mzigoni studi za redio tanzania. huyu ni mmoja wa nguli wa habari bongo ambaye alikwea hadi kufikia ukurugenzi hapo rtd

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Aisee kweli alikuwa bomba. maana hapo hata mimi nilikuwa sijazaliwa. ila kweli nimeamini vumilivu hula mbivu. Hongera sana mama Sanga. Natumai wale wa makamo yako ambao hawakubahatika kupata shuguli za maana enzi hizo watakuwa wamechakaa sana na vikongwe kwa sasa.

    ReplyDelete
  2. Yaani nakumbuka huyu mama alivyokuwa akiendesha vipindi ilikuwa burudani tosha hasa akiwa external services akisoma habari kwa kiiengereza. Halafu na mtangazaji makini na mwenye sauti nzuri huchoki kumsikiliza.

    Sio watangazaji wa siku hizi utafikiri wako kwenye mkinda au gombe sugu pepere pepere hata huelewi wanasema nini wengine wanakohoa redioni wengine hawaongei kiswahili fasaha, kwenye r anaweka l kwenye l anaweka r, wengine sauti kama vyura, basi tafrani mtindo mmoja. Utangazaji ni fani ya kusomea na uwe na sauti na kipaji sio ukiamka unakurupukia kwenye redio!

    ReplyDelete
  3. Du alikuwa mzuri yaani mimi nilifikiri msichana wa mjini wa sasa maana hizi fashion zimerudi tunaomba picha zake za sasa michuzi

    ReplyDelete
  4. nilikuasijamuona kwa sura lakini sauti yake ilikua inanimaliza sana.

    Kumbe alikua ni mtu mzima sana '71 alishakua kwenye studio kweli lishe bora hauseeshi

    ReplyDelete
  5. Michu mama mkongwe wa RTD Nelly Kidela amefariki miezi michache iliyopita umechuna kimya? hivi mchango wake haufahamiki kwa jamii? hebu fatilia habari zake

    ReplyDelete
  6. Michu mama mkongwe wa RTD Nelly Kidela amefariki miezi michache iliyopita umechuna kimya? hivi mchango wake haufahamiki kwa jamii? hebu fatilia habari zake

    ReplyDelete
  7. Kweli bro Michu yani kweli mmekaa kimya kuhusu kifi cha mama Nelly kulikoni!leta habari kidogo

    ReplyDelete
  8. SANA EDDA! Huyu naye alikuwa si mchezo.
    Michuzi je una taarifa ya magwiji wengine Wahabarishaji utuletee hapa taarifa zao mfano:
    1. Mzee Japheti Mukama (Jogoo) aliyekuwa anawika enzi zake toka Idhaa ya Kiswahili-US mpaka nywele za watu zinasimama pote duniani hadi huko Murangi, Makojo, Butata n.k
    2. Mama wa shoka wa Idhaa ya Kiswahili Ujerumani (DW) yupo mpaka sasa na sauti yake ya kumtoa mtu pepo bila kufukiza ubani!Anajiita UMLIKHEIR? (Samahani nadhani nimekosea sp.za jina lake, sina jinsi naomba nisaidiwe). Jamani kuna sauti na sauti lakini ya huyu mama nasema libarike tumbo la aliyemzaa!

    Nyakatakule Unyilisya Echalo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...