waziri mkuu mh. el akiisifu kamati iliyoandaa kagera dei usiku kuamkia leo diamond jubilei. shoto ni profesa anna tibaijuka, akifuatiwa na waziri wa elimu mh. margareth sitta na kulia ni bosi wa kampuni ya simu ya nanihii na wa pili yake ni mkuu wa mkoa wa kagera

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mbwenu other regions nao wafanye donations kama hawa. Infwakt nagamba mikoa kama Mwanza,Kilimanjaro ,Iringa, Mbeya wakiamua kuchanga kwa moyo kwa ajili ya developments za mikoa yao kuliko kusuburia Kasi(yenye speed 5km per hr) wangekuwa mbali sana

    ReplyDelete
  2. kwa kweli ni vizuri sana iwapo watanzania tutabadilika nakuchangia maendeleo zaidi Tanzania Itasonga sana tu ,maana tupo nyuma sana ki elimu hasa sekondari na vyuo vikuu , Watanzania imefika pahala tuhamasishane ili tuwe na mtazamo wa kuchangia maendeleo !safi sana hivyo huu nimwanzo bado mikoa, wilaya kata hata vijiji kibao tunataka kila kona ya tanzania yote.

    ReplyDelete
  3. Jamani sina nia mbaya, ila naomba kuuliza sasa mnaposema kila mkoa ufanye haitakuwa kuhalalisha Ukabila au Umajimbo? Naomba kutoa hoja.

    ReplyDelete
  4. Ngoja nikueleweshe kidogo, inamaa kama unakaa mwanza na barabara ni mbovu kama wanamwanza wanauwezo wa kuchangia barabara wachangie.Serikali yetu haiwezi kutusaidia kila kitu ndio maana wananchi wanaweza kuisadia local government kwa maendeleo ya mkoa husika. Dar es salaam kuna watu mchanganyiko na mji wa wazaramo lakini unajengwa na kupata maendeleo kwa watanzania wote. Hao wana kagera wameamua kuchangia maendeleo ya mkoa wao ambao kuna watanzania wanaishi sio tu wazawa wa Kagera natumaini umeelewa.Watanzania wengi ni wakazi wa mikoa miwili wanakofanyia kazi na walikozaliwa ndio maana watu wakifa huenda kuzikwa kwao na sio dar es salaam usipoelewa tena basi ndugu yangu

    ReplyDelete
  5. Nani alituwakilisha sisi Wahangaza,wasubi,nk katika "so called KAGERA DAY".Inaelekea walikuwa wahaya tu walioshiriki,Jamani ee kagera kuna kabila zaidi ya moja.

    ReplyDelete
  6. Huyu anony anaeulizia waangaza amenifurahisha sana sababu wengi wetu tunajua Kagera kuna wahaya tu....

    ReplyDelete
  7. Huyu anateulizia uwakilishi wa waangaza, wasubi na wanyambo anashangaza. Mwaliko ulikuwa wa wanakagera wote...yeye kama yuko Dar hakwenda na waangaza wenzake hawakwenda...wahaya wakaenda, kwa nini isiwe hivyo? Hoja za namna hii zinalenga kuharibu mpango mzima kwa kubaguana. Suala halikuwa uwakilishi, bali kutunisha mfuko wa kujenga shule Kagera, ikiwemo ngara, Karagwe na Biharamulo. Basi.

    ReplyDelete
  8. HIVI KAGERA HAKUNA VIONGOZI WA VYAMA VINGINE VYA SIASA? AU ILIKUWA SIKU YA KAGERA YA WANA CCM TU! MBONA HATUWAONI KWENYE PICHA AU KAMERA ZILISHINDWA KUWANASA?

    ReplyDelete
  9. Nimeuliza hivyo ili nijuwe kina nani walikwenda.Pia nilitaka kuujulisha umma kuwa kagera kuna zaidi ya kabila moja.Kuuliza si ujinga.

    ReplyDelete
  10. mtu mzembe wa kuchangia hata fikra moja ya maendeleo ni hodari kwa fikra mbovu kila tamko lake.watu waende shule anakasirika,wachangie shule anakasirika,wahimize maendeleo anakasirika.inavyoonekana hujawahi hata kumpa mdogo wako nauli ya siku moja akatoe matongotongo shuleni.wana-kagera kuchangia maendeleo ya mkoa ni kuleta maendeleo kwa wote wanaoishi kagera hata akiwepo mdogo wako atafaidika.ubaya nini au kwakuwa ni mvivu wa kutoa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...