Hello vipi mjomba michuzi,
mimi ni mdau hapa uk. leo tupo kazini kuna jamaa wawili wa kimarekani wakawa wananiulizia kama nashekherekea `kwanzaa` nikashangaa kwani sijawahi kusikia sikukuu hiyo,ila baadae wakanionyesha web-site ya african-americans nikagundua ni sikukuu kubwa huko america.wanaaita kwanzaa,na pia wana nguzo (principle) zao ambazo ni pamoja na ujamaa,umoja nk maneno wanayotumia ni hayo hayo ya kiswahili. Nikaona nikujulishe ili wengine waelewa jinsi lugha yetu inavyotumika ulimwenguni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. kwanzaa ni sikukuu kubwa tu marekani inayotambulika hata kushinda eid.

    ReplyDelete
  2. Ahh...ati kwanzaa...ujinga wa aina gani huo? mseto huo yaani mchanganyiko wa choroko,dengu,maharagwe na sijui nini ndio linaleta upumbavu huo ambao unaitwa kwanzaaa,mamilioni ya kinigro wala hawana muda na upumbavu huo bali wametosheka na kuziiga mila za mabwana wao wa kizungu...sasa nyie waswahili msinyemelee meaningless shit like kwanzaaa

    ReplyDelete
  3. Mimi nilipo fika hapa US Miaka kadhaa iliyou pita nilishangaza kuona jinsi hawa wenzetu wanavyo jitengenezea sikukuu an kuharibu lugha yetu...eti "kwanzaa" ukuwauliza inamaana gani wanasema first fruit WTF

    Anyways... tumesha wazoea sikuhizi. Ila mi waonea huruma kwasababu wazungu husema ..." my great, great... parent came from German, Russia etc" lakini wenzangu na mie hawajui hata wametokea nchi gani.

    Wengi wao hawataki hata kuikubali asili yao.

    Lakini hii inatokana na wazungu pia wao wame wa "HYPNOTIZE" kwa kuwafanya waone kuwa mweuzi ni kama laana.

    Hii inadhihirika hata katita hii lugha yao, Black market, black hat technique, white collar job n.k

    Kila kitu kibaya huku ni BLACK (which fuck everything up)

    ReplyDelete
  4. Inasemekana kuwa kuna jamaa mmoja alikuja pale Tanzania miaka ya nyuma sana wakati siasa ya Ujamaa na Kujitegemea inapamba moto sana mwanzoni mwa miaka ya sabini; aliishi pale Tabora. Jamaa huyu alipenda sana maisha ya watanzania wakati huo chini ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hasa kwa vile ilikuwa inaonyesha matumaini makbuwa sana. Nakumbuka kuwa jamaa huyu alibadilisha jina lake na kujiita Maulana Kalenga.

    Bwana Kalenga aliporudi kwao Marekani, wakati huo bado kuna majeruhi ya ubaguzi, ndipo akaanzisha hii filosofia ya "Kuanza" mapambano dhidi ya umaskini. Kwa bahati mbaya kiswahili kilimpiga chenga kidogo akasema "Kwanzaa." Wote waliomrithi wakaishia kwenye mkumbo huo huo wa kufanya makosa hadi hapo neno "Kwanzaa" limebaki kama ndilo sahihi.

    ReplyDelete
  5. Muanzilishi wa Kwanzaa anaitwa Maulana Karenga kama alivyosema Kichuguu. Bado yupo hai na ni Professor wa Black Studies pale Cal State Long Beach, California.

    Organization yao inaitwa US, kwa maelezo zaidi angalia hapa chini: http://www.us-organization.org

    ReplyDelete
  6. ndio hivyo kwani hata hizo sikukuu za xmas,thanks giving,pasaka,eid etc zilianzishwa na watuu kama nyie na hakuna chochote cha kushangaa hapo na hata dini nazo ni hivyo tuu zilianzishwa na watu kwa mitazamo yao wenyewe wala hazikushushwa na mungu na baada ya miaka mingi ndio binadamu tumeamini sana mpaka tunaona kama ni kitu kimeshushwa na mungu

    ReplyDelete
  7. wehu hawa ni kweli hiyo sikukuu ipo.Hawa watumwa kweli huku hawajuwi hata historia yao.Waafrica wana akili kupita hawa jamaa huku,darasani tunawatwanga sana tunaokwendanao shule,vichwa vyao uji mtupu hasa weusi wehu sana.Wachache weusi wanaopandisha shuleni.Mimi huwa nacheka sana eti uwa wanachukua madarasa ya kijinga kama jinsi ya kujibu mitihani,huu si wehu kabisa yaani kweli huku kuna darasa za weusi hususani za jinsi ya kujibu mitihani,maswali yanawapiga chenga huwa wanakremu basi swali likizungushwa tu hola.Tujivunie sana waafrica tuna bongo sana lakini wengi hatuzitumii.Someni wadau msiwaogope hawa jamaa pumba tupu,blingbling nyingi vichani patupu.Ask= aksi

    ReplyDelete
  8. We anon wa Tuesday, November 27, 2007 2:30:00 PM EAT muongo kabisa. Labda hao wanugu wa vijijini kwenu. Hawa jamaa wakiamua kwenda shule wanafanya vizuri kweli. Sisi wote tuko kiwanjani na tunasoma nao. Usiwapotoshe watu na fikra zako za kibaguzi.

    Kwanza wewe kiingereza hujui na masomo yanafundishwa kwa kiingereza, utawashindaje?

    ReplyDelete
  9. 2:30 unadanganya tuuu. Hawa wenye nafasi ya kusoma wanaakili sana...ni mazingira yao wanayoishi ndio yanaowafanya wachache wasiwe na akili lakin na kama uko community college basi sitashangaa lakini kwenye vuo vikuu wanaakili kuliko hata wazungu...

    wazungu wote wanaishia sociology, pychology or education major lakini hawa wote mtakua nao kwenye major ambazo zinahitaji kichwa....

    ReplyDelete
  10. huyo pumba wa 230 hajui anaongea nini,limekuja nchi hii linaenjoy freedom utafikiri babu yake ndio alipigania na kuanza kuleta madharau yasiyo na mpango,amka wewe bila hawa ungekuwa kidampa tuu na usingeijua marekani wewe ya leo na ungeishia gheto tuu bila haki yeyote...respect kwa brothers & sisters tafadhari ni watu smart sana ndio maana America ipo ilivyo sasa la sivyo mtu mweusi asingekuwa na haki yeyote

    ReplyDelete
  11. we anon nov 27 2:30 pm
    are you normal? au umepungukiwa kidogo?
    jamani mnatakiwa muheshimu watu na culture na zao
    wewe utafurahia kama wakisema waafrica wote wanashida kama unavyoona kwenye TV na kipindi cha World vision ?
    so stop being ignorant
    kama sio wao leo usingeingia Marekani na kufanya mambo yako freely.
    mkulima mkubwa wewe!!bonge ya mshamba

    ReplyDelete
  12. Wacha hawa wenzetu washehereke Kwanza, ni kweli wanafikiri kwanza imetokea na inatabuliwa africa. hawa jamaa baada ya kufika Amerika miaka hiyo ya zamani pamoja na utumwa, hawakuipenda Christmass (wanaamini niyo ni sikuku ya wazungu waliowatesa) hivyo walitafuta siku nyingine ambayo itatofautiana na Christmass digodo, ndo wakapata hii Kwanzaa, na nikweli hata mimi nilishangaa kwamba mwanzishaji alitokea Tanzania. mimi nafikiri Tanzania haswa wakristo huwa tunasheherekea siku kuu ya mavuno kila mwisho wa mwaka, na hawa ni kama sikuu yao "kwanzaa" the first, na nikweli hata ukiwauliza watakushangaa weweuliyetoka africa huwafamu nini maana ya kwanza. Hii ni siku ambayo inawapa faraja hawa ndugu zetu kwa mateso makubwa sana babu zao waliyopitia huko nyuma na kwao ni sikuu ya kuheshimiwa vilivyo. Hivyo tuwaheshimu pamoja na sikukuu yao hiyo. Jamaa wanaakili pia sana tu ambao wamependa kwenda shule sio wote mbumbumku kama tunavyofikiria, na maisha huku ni magumu tu kama nyumbani!

    ReplyDelete
  13. Hallo mzazi mwenzangu-Michuzi (kumbuka mwanao ataka kuoa mwanangu! mitaa ya tabata, haha)
    Binafsi nimeisikia kwanza kwa miaka 14 sasa na karibu miaka 4 sasa nimekuwa nikihudhuria sherehe hizi hapa ukerewe, nawafahamu baadhi ya watu walio mstari wa mbele katika hili, tatizo langu kuhusu wao na nimekwisha wahi kujadili na viongozi wao, wapanue shughuli za kwanza na kujenga mitandao madhubuti moja kwa moja katika nchi za africa, kwa uzofue wangu wanakutana wanawasilisha mada wanapiga kele kuhusu ubaguzi na kadhalika ila sijaona hatua muafaka za kukabiliana na haya, na kiasi kama wamejitenga badala ya kuuunana na waafrika walioko afrika.Kuna dhana ya pan-africanism, Wanatajwa sana kina marcus garvey, wanawake wa shoka kina queen nzinga na kadhalika ila hawajafanikiwa kiutekelezaji.Wana radio wanajadili masuala mbalimbali.
    Okay my husband wake , salaam!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...